Serikali inatuona Watanzania kama kuku wa mgeni

HUSSEN KAMBI

Senior Member
Dec 4, 2023
174
211
Kwasababu gani nimesema inatuona kuku wa mgeni kuku wa mgeni yani inatufananisha akili zetu na kuku wa mgeni mfano kuku kama sio wa mgeni ukianika mpunga au mahindi akija kula unamfukuza kama sio wako lakini kuku huyohuyo uliomfukuza asile mahindi yako au mpunga wako kuku huyo huyo ukitaka kumchinja kwa ajili ya mgeni hata kama alikua mbali utamuekea mpunga hule hule au mahindi yale yale nakumuita aje ale hili umkamate kirahisi upate kumchinjia mgeni na yule kuku atakuja mbio mbio kuja kula bila ya kujiuliza mbona mwanzo nilivyoenda kula alinifukuza kwanini sasa hivi ananita nikale.

Hua ajiulzi hayo maswali anakwenda kula anaona kama anapendwa kumbe k andaliwa kisu ili achinjwe kwa ajili ya mgeni ndio maana nimesema serikali inatuona Watanzania kama kuku wa mgeni na mgeni mwenyewe wa serikali ni uchaguzi.

Yani kila kikifika kipindi cha uchaguzi serikali inajifanya inajali sana raia wake sehemu ambayo maji yalikua hayatoki yatatoka kodi zenye kuumiza watazipunguza yani vitu watavifanya kwa unafuu kidogo ili kutuhadaa ili tuwaone wanatujali na sisi wananchi hatujiulizi kama ilivyokua kwa kuku akujiuliza kwanini sasa hivi anaitwa wakati mwanzo alifukuzwa.

Tutawaona wanatujali n akuwapigia debe wanafaa kumbe wana tuhadaa hili wapate kutuchinja vizuri kwa miaka mitano atukuwaona majimboni wala kwenye kata lakini kikikaribia kipindi cha mgeni yani uchaguzi uta anza kuwaona majumbani mitaani wataonyesha huruma mapenzi hili tupate kusogea karibu yao wapate kutuchinja vizuri kwa ya mgeni wao ambaye ni uchaguzi.

Baada yatuchinja atutowaona tena mpaka miaka mitano ijayo ndio maana nimesema serikali na chama chao wanatuona watanzania kama kuku wa mgeni asiyejua kufikiri kwanini juzi nilifukuzwa lakini leo naitwa
 
Back
Top Bottom