Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Kutokamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na kufikishwa kortini, kumemtia hofu Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, kwamba serikali inamuogopa.
Hakimu Simba ameielezea hofu hiyo leo mchana wakati akiendelea kusikiliza kesi inayomkabili Lissu na mmiliki na mhariri mtendaji wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, mhariri wake Jabir Idrissa na mchapishaji wa gazeti hilo Ismail Mahbood.
"Hivi Lissu hapa ameletwa chini ya Polisi au kajileta mwenyewe? Mbona hamjamkamata au mnataka mie nitoe uamuzi wa kumfutia dhamana wakati hamjatekeleza wajibu wenu? Simfutii," alisema Hakimu Simba.
Serikali, kupitia Polisi haikumkamata Lissu kama ilivyokuwa imeamuriwa na mahakama baada ya kusindwa kufika mahakamani hapo kwa kesi inayomkabili.
Akaongeza, mahakama kamwe haimuogopi Lissu, lakini inaonekana serikali inamuogopo mbunge huyo na mwanasheria mkuu wa Chadema.
Lissu, Mkina na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uchochezi ambayo ilifunguliwa na serikali tangu Juni, mwaka huu. Gazeti la Mawio lilifutwa na serikali kwa tamko la waziri wenye dhamana ya habari, Nape Nnauye, Januari, mwaka huu, baada ya 'kuchongewa' kwa muda mrefu na aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya habari, Maelezo, Assah Mwambene.