Serikali inamuogopa Lissu?

Serikali inamuogopa Lissu?

Mada zingine muangalie mahali pa kuandika.

Serikali yoyote Duniani huwa haimuogopi yoyote yule akiwa amevunja sheria.

Avunje sheria aone Serikali mnayosema inamuogopa itakapo mshughulikia
Lugumiiiiiii!!?
Hapo veepe?
 
Kumbuka Mahakama ilitoa amri Lissu akamatwe.

..Ndiyo.

..lakini hajakamatwa na amefika mahakamani mwenyewe.

..hakimu alitakiwa ku-move on, na siyo kuhangaika na mambo yasiyokuwa na msingi wowote.

..kesi hii ni siasa-siasa tu. Hakimu anatakiwa aelewe hivyo.
 
Ni ujinga na upuuzi mtupu, eti Serikali kumuogopa Lissu,!!, Lisu ni nani ktk Taifa hili hadi ijishughulishe na ka lisu tu? Iache kushughulika na masuala muhimu yanagusa mstakabali wa maisha ya watanzania. Kujadili habari za Lisu ni sawa na kujadili tabia za mwendawazimu kushinda jalalani.
Mambo gani muhimu inashughulika nayo hii serikali ya mwendekasi ?
 
Kwa hakika aliyevurugwa na akavurugika ni wewe ambaye unahangaika na kajitu kadogo kama lisu. Mtu ambaye hata sifa za kutumbuliwa hana, kiboko yake ni Tulia Ackson tu.
Kamuulize rais wako mstaafu wa awamu ya NNE kila hotuba za mwisho wa mwezi alizokuwa anatoa kwa wazee wa kijani D,salaam kila baada ya maneno kumi, mawili lazima amtaje Lissu...... Kwa ufupi waulize hao mabos wako unaowaramba miguu yao ili uishi mjini watakwambie ukweli kuwa Lissu ni nani katika nchi hii
 
KISUTU YAMUONYA LISSU, YASEMA HAIMWOGOPI

Habari na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema haimuogopi kumwadhibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na imemuonya tabia yake ya kushindwa kufuata taratibu za kisheria anapokuwa na udhuru siku kesi yake inapopangwa kusikilizwa.

Kadhalika imesema Lissu anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii, mshtakiwa huyo alishindwa kufika mahakamani mara tatu mfululizo kusikilizwa kesi yake na wenzake watatu dhidi ya mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.

Onyo hilo lilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mahakama yake kutoa amri ya kukamatwa Lissu Novemba 3, mwaka huu.

"Pamoja na nafasi yako uliyonayo kwa jamii lakini ujue kwamba mahakama hatukuogopi labda upande wa Jamhuri ulioshindwa kuja kukukamata ... mahakamani hakuna kuoneana bali taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake" alisema Hakimu Simba.

ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya hakimu na Lissu:
Hakimu Simba ; Awali ulikwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani unadhani tunakuogopa?


Lissu; Sina nia mbaya mheshimiwa hakimu nilipelekwa Ujerumani kwa dharula.

Hakimu Simba ; Je, kesi ya Uchaguzi wa Jimbo la Bunda nayo ilikuwa ni dharula?

Lissu; Mheshimiwa hakimu nilipotoka Ujerumani nilikuta kesi ya Bunda imepangwa kusikilizwa na ilikuwa na muda maalumu, niliandika barua Hakimu Mfawidhi wa mahakama hii ya Kisutu na nakala nilielekeza kwa upande wa Jamhuri sina nia ya kuidharau mahakama.
Hakimu; Kutokana na nafasi yako katika jamii ujue kwamba mahakama hatukuogopi labda upande wa Jamhuri ulioshindwa kukukamata na kukuweka chini ya ulinzi.


Kabla ya majibishano hayo, upande wa utetezi ukiongozwa na Mawakili, Peter Kibatala, John Mallya na Rwekama Rweikiza ulidai kuwa mshtakiwa wa nne Lissu, ametii amri ya mahakama amejisalimisha mwenyewe.

Kibatala alidai kuwa Lissu alikuwa na anaendesha kesi ya Uchaguzi wa Jimbo la Bunda na kwamba pamoja na kuwa mshtakiwa pia ni wakili wa kujitegemea.

Akijibu hoja za utetezi, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita alidai kuwa, Lissu ni ofisa wa mahakama kama wakili na kwamba anajua taratibu za kufuata anapokuwa na udhuru wa kufika mahakamani lakini ameonyesha dharau kuondoka bila kibadi cha mahakama hiyo.

Hakimu Simba alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 20, mwaka huu na dhamana za washtakiwa wote zinaendelea.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine ni, Wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu, Dar es Salaam, Lisu na wenzake walikula njama ya kuchapisha
chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.


Pia Lissu na wenzake walidaiwa Januari 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa nia ya kuleta chuki na uchochezi kati ya wananchi na mamlaka halali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye uchochezi.

Aidha, Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo kwa nyakati tofauti.
 
Siyo kwamba ilitakiwa wahusika wa RICHMOND, IPTL, ESCROW, LUGUMI nk 'waone' kwa sababu walikiuka na kuvunja sheria? Kwa nini tuwe na matazamio hewa eti Lissu avunje sheria aone wakati wapo wavunja sheria kibao hawaguswi?!
Tatizo ni mleta mada na kichwa cha mada yake.

Elewa kuwa Serikali haigopi MTU yoyote yule.
 
Kutokamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na kufikishwa kortini, kumemtia hofu Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, kwamba serikali inamuogopa.

Hakimu Simba ameielezea hofu hiyo leo mchana wakati akiendelea kusikiliza kesi inayomkabili Lissu na mmiliki na mhariri mtendaji wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, mhariri wake Jabir Idrissa na mchapishaji wa gazeti hilo Ismail Mahbood.

"Hivi Lissu hapa ameletwa chini ya Polisi au kajileta mwenyewe? Mbona hamjamkamata au mnataka mie nitoe uamuzi wa kumfutia dhamana wakati hamjatekeleza wajibu wenu? Simfutii," alisema Hakimu Simba.

Serikali, kupitia Polisi haikumkamata Lissu kama ilivyokuwa imeamuriwa na mahakama baada ya kusindwa kufika mahakamani hapo kwa kesi inayomkabili.

Akaongeza, mahakama kamwe haimuogopi Lissu, lakini inaonekana serikali inamuogopo mbunge huyo na mwanasheria mkuu wa Chadema.

Lissu, Mkina na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uchochezi ambayo ilifunguliwa na serikali tangu Juni, mwaka huu. Gazeti la Mawio lilifutwa na serikali kwa tamko la waziri wenye dhamana ya habari, Nape Nnauye, Januari, mwaka huu, baada ya 'kuchongewa' kwa muda mrefu na aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya habari, Maelezo, Assah Mwambene.
Sidhani kama serikali inamuogopa Lissu. Nafikiri hata yeye mwenyewe Lissu anatambua fika kuwa Serikali haimuogopi. Yeye ni nani mpaka aogopwe? Nafikiri hajaingia bado kwenye 18 za Serikali kama mwenzake Lema, na siku akiingia ndio utajua kama anaogopwa au la.
 
Screenshot_2016-11-22-02-01-43.png
 
Serikali inafanya kazi kwa kufuata sheria.

Mh Lissu alishaandika barua ya udhuru ya kutofika mahakamani kutokana na kuugua na kwenda Ujeruman na pia kuhudhuria kesi huko Bunda na ana Haki kisheria.

Nalala zipo.

Sioni hoja ya mleta mada kuwa Serikali inamuogopa Mh Lissu
 
Hizi ni akili za kitoto sana eti serikali inamuogopa Lisu. Kweli vijana siasa zinawauwa kufikiri na sasa sio tena great thinkers maybe mmekuwa stupid thinkers. Leteni hoja za msingi hizi za kipuuzi wanazungumza watu amboa sio great thinkers.
Wewe ndio sio great thinker, mleta hoja kasema ni kauli ya Hakimu akiiuliza serikali na wewe unamlaumu yeye.
Ukiangalia utagundua kuwa walioomba Lissu akamatwe ni serikali ila walijua sababu zao hazina mashiko hivyo wakaitegea mahakama ndio imfutie dhamana wakati wanajua kuwa alikuwa kwenye kesi ya mahakama ya juu zaidi.
Kesi hizi za uchochezi wameshajua haziwafikishi popote hivyo bora wakomoe kwa dhamana tuu
 
..Ndiyo.

..lakini hajakamatwa na amefika mahakamani mwenyewe.

..hakimu alitakiwa ku-move on, na siyo kuhangaika na mambo yasiyokuwa na msingi wowote.

..kesi hii ni siasa-siasa tu. Hakimu anatakiwa aelewe hivyo.
Sawa kabisa.
 
Mada zingine muangalie mahali pa kuandika.

Serikali yoyote Duniani huwa haimuogopi yoyote yule akiwa amevunja sheria.

Avunje sheria aone Serikali mnayosema inamuogopa itakapo mshughulikia
Hujamwelewa hakimu?
 
Back
Top Bottom