Serikali inamlipia matibabu Shekhe mkuu India

Halafu kumbe mzee wa watu huyu alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya private iitwayo KAM huko Arusha kwa karibu wiki mbili, na leo ndio ameondoka kwenda India kwa matibabu. Amefuatana na kiongozi mmoja wa BAKWATA na daktari anayemtibu (Dr Peter Mhando wa hospitali hiyo ya KAM), na bila shaka ni kwa gharama zake au za BAKWATA. Sasa sijui huu udaku wa kuwa kuwa yuko India na anatibiwa na serikali (na watu wakazua malalamiko kibao yasiyo na msingi) umetoka wapi?

Ingawa amechagua kutibiwa kwenye hospitali binafsi huko Arusha na baadae kwenda nje ya nchi kwa gharama zake, bado ikumbukwe ni wajibu wa serikali kugharamia matibabu ya wananchi wake wanaopewa rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi(ikiwa rufaa hiyo imetokana na maoni ya kitaalamu na si matashi binafsi ya mgonjwa kwenda kutibiwa nje).

Na ushauri kwa wanachama wenzangu hapa JF, habari zenye mwelekeo wa kizushi ziwe zinakemewa inapogundulika kuwa habari hiyo ni uzushi. Wahusika wa habari kama hizo pia wanaweza kuomba radhi wenyewe (ikiwa walipotoshwa/walipotoka), la sivyo moderators muwe mnawakemea maana mambo kama haya ndio yanayoathiri hadhi ya jukwaa letu hili tukufu.
 
..ngugu Zangu Waislamu Na Bakwata Kwa Ujumla Mmefedhehesha Kwa Kutomsitiri Kiongozi Wenu Mkuu Hadi Wiki Mbili Mzima Ahangaike Kahospitali Ka Mtaani....kanakoitwa Sijui Kam...kweli Si Halali Kabisa..hata Kama Kuna Tofauti Fulani Fulani..yule Ni Kiongozi ..hakutakiwa Kutelekezwa....waislamu Nchi Hii Wanakaribia Asilimia 40% ..kwa Hiyo Yeyote Anayetambulishwa Kama Kiongozi Wao Kidini Anastahili Matuzo Kutoka Kwa Waumini.....

Katika Hali Ya Kawaida Viongozi Wa Kikiristo Wengi Wakiwa Wanaumwa Huhudumiwa Na Makanisa Yao ...na Hata Kupelekwa Ulaya Haraka Kama Matibabu Yameshindikana Bila Kusubiri Huruma Ya Serikali.......hata Kama Ni Haki Yake Kama Raia....
 
1. Kwani BAKWATA hawana pesa kumlipia shehe Mkuu wao? Kama hawana pesa basi kama Mtz yoyote ana haki kuomba msaada wa serikali!

2. Ila kweli sijui kwa nini leo hii 40 years Tz hatuwezi kuwatibu viongozi wetu hapa hapa nyumbani..kwa nini Hospitali moja mashuhuri isitumike kuwatibu viongoz wetu?
 
Mimi sioni Chakujadili ikwa hakuna Ushahidi ktk hili.Tusije kwenda mbali zaidi na kusema kuwa kwakuwa Rais ni Muislamu basi ndio maana Shekh mkuu anapelekwa India matibabu.

Lamsingi waulizwe wenyewe Bakwata Wadisclose chanzo chao cha mapato na pesa za kumpeleka shekh Mkuu India.Wakipata toka nje ya nchi mtasema za Osama,zikitoka ktk shule zao za Kinondoni na Alharamain mtasema waongo.

Tuongee tukiwa na ushaidi wa kutosha.

Nawasilisha.
 
Afadhali aibiwe huyo ni mtu mhimu sana kwani ni mtu ambaye atasaidia kuwashawishi kutokana na cheo na mamlaka yake hao mafisadi yakaweza kuturudishia pesa zetu. Inshallah tumuombee apone. Amin
 
tuache unafiki na hoja zisizo na maana. kwani Shekhe kulipiwa matibabu kuna kosa gani jamaniii? mbona watoto kibao hupelekwa india kufanyiwa upasuaji wa moyo na magonjwa mengine?

na huyo askofu aliyekuwa kwa kukosa matibabu Dar ni yupi?
 
Mindhali huyu shekhe mkuu ni wa BAKWATA na yuko close na wagalatia kule serikalini sitoshangaa kama kodi za wananchi zinatumika kumlipia matibabu kule India.

Kama ambavyo serikali isiyo na dini ilivyowalipia mahujaji kwenda Makka basi na hili nalo msije shangaa

Hii siyo fitna lakini kama kuna ukweli kwenye hili then tunalo la kujadili Ijuma ya leo.

Kama mjuavyo watawala wanaongoza BAKWATA wanachaguliwa na serikali hivyo its very simple ku connect the dots
By the way ni mvutaji sigara mkubwa sana huyu..sasa inavezekana sigara nazo zinammaliza

na mwisho zaidi tunaomba C.V yake

wasalaam

GT,
Kama utakuwa umesoma postings za Kithuku please do the needful. Kwani pamoja na mtundiko wako kuwa hauna ushahidi wa kutosha pia na nadhani nia hasa ni kuidhalilisha BAKWATA na waislam wa Tanzania kwa ujumla hasa ukirejea maneno yako hapo juu niliyopiga rangi nyekundu.

Ni matumaini yangu kuwa utaonesha kiwango cha juu kabisa cha ustaarabu na wala si vinginevyo.

Natanguliza shukrani zangu za awali.

Kithuku,
Ninakushukuru kwa kuwaelimisha na kutoa taarifa sahihi kwa wana-JF.
 
Hivi unajua waislam wangapi wanaikubali BAKWATA?

Hivi unajua kama waislam wanajua kama BAKWATA ni BRAZA KUU LA KUWAKANDAMIZA WAISLAM TANZANIA?

Hebu nitajie mazuri 10 waliyofanya BAKWATA tangu iundwe

Shekhe mkuu ni mvuta sigara mkubwa na alikuwa anajua madhara ya sigara sasa he is just reaping what he sow

Nakuomba uache kutwist mambo hapa, kuicriticise BAKWATA haimaanishi kuwa waislam wa Tanzania ndio wanaokuwa criticized

Mimi sina neno endapo kodi yangu inatumika kuokoa maisha ya muislam mwenzangu.(maoni Binafsi)

Angekuwa ni mpagani, Mkristo, mbuda nk ungekuwa na neno (wewe ni mbaguzi kwelikweli. Hivi unadhani pesa zinazotumika kumtibia huyu kiongozi wa dini ni za Waislam tu? fedha ya serikali hana dini Mtumwa Alla.

Ninawasiwasi juu ya uzalendo wako kwa Taifa kutokana na falsa yako kama inavyoonekana katika post zako zote.
 
GT,

Victim blaming..sasa sigara kwani ni shehe tu anavuta? Hekima muhimu hapa..tumwobee atibiwe na apone haraka!

Mtu akinyoosha kidole kimoja kumhukumu mmwingine ajue vidole vitatu vinakuhukumu yeye!

Hakuna mwandamu mkamilifu! Acha tu atibiwe -kwa gharama za serikali au wasamaria..ili mradi apone!

GT unasemaje? Mbona ndugu yangu kwa hili unakosa ubinadamu?
 
Wala hii siyo victim blaming bali tunaweka facts wazi

Huyu anawakilisha chombo ambacho waislam wanakiona kama chombo kilichowekwa pale strategically na serikali ili kuwaonea

Huyu jamaa alitakiwa kuwa kiongozi wa hao waislam wa BAKWATA lakini kama kiongozi one would expect atakuwa anaishi by the morals na mojawapo ni kutokuvuta sigara sasa huu ni mfano gani?

Umezungumzia kuwa aonewe huruma kama mwanadamu lakini je kuna wanadamu wangapi wako hospitali ya Mafia hawajalipiwa matibabu ya nje kama anayopewa huyu mvuta sigara?

Keshaambiwa sigara in cause lung cancer lakini yeye bado anaendelea sasa sijui mnataka nini tena

Actually huyu akifa there wont be nothing to lose zaidi ya baadhi ya waislam kumzika kisha watamsahau tuuu

In short Shekhe mkuu huyu is not al Marhum Sheikh Nurdin al Shadly. Yaani anitia kichefu chefu sema ndio hivyo keshakuwa binadamu tuu.

Unazungumzia Ubinadamu lakini je huyu shekhe mkuu alikuwa na ubinadamu na nani? an please dont tell me mzee Chifupa!

Aliambiwa aache sigara yeye kaendelea na ubishi sasa mwenyezi Mungu anamuadhibu on daily basis achlia mbali zile dua za ansar sunna kule Tanga
 
Jamani Mtanzania Asitibiwe Na Serikali Yake?

mimi naona hii ni aibu kwa BAKWATA na wote walio chini yake haiwezekani kwa taasisi yenye waumini wengi karibia nusu ya watanzania kushindwa kumuhudumia kiongozi wake.
this is shame
 
mimi naona hii ni aibu kwa BAKWATA na wote walio chini yake haiwezekani kwa taasisi yenye waumini wengi karibia nusu ya watanzania kushindwa kumuhudumia kiongozi wake.
this is shame

BAKWATA haiwakilishi nusu ya waumini wa kiislam Tanzania bali you can be right kuwa BAKWATA na CCM ni dam dam

unless unataka kuamini propaganda kuwa BAKWATA=WAISLAM TANZANIA
 
Sikubaliani na serikali kwa kisingizio chochote kile kumlipia matibabu Shekh mkuu kwani wangesubiria kwanza waruhusu mahakama ya kadhi ndipo waweke vipengele kama hivyo.

Hapa tunatengeneza ubaguzi mmbaya sana na haswa ikizingatiwa kuwa taifa hili kwa sasa lina dini nyingi sana na viongozi wengi sana wa kidini kama tutaanza kukubaliana na mtindo huu kuna siku nchi itawaka moto kwani ila dini itataka kiongozi wao atibiwe na serikali hiyo hiyo

BAKWATA wana pesa walipaswa kuchukua jukumu hilo na kama wangeshindwa wangeonana na watanzania wenzao ambao naamini kuwa wangekuwa tayari kuchangia gharama za matibabu hayo.
 
Taabu hapa JF tunaongea tu hovyo hata ktk hali ya ugonjwa!

Katika hali kama hii ni hekima zaidi inahitajika zaidi ya sheria na taratibu!

Ubinadamu kwanza JF!!!!! Hivi kati yetu hakuna aliwahi kuugua na kulazwa mda mrefu? Mnadhani Shehe mkuu atajiskiaje akisoma hii thread?

Ktk yote sisi ni binadamu..then ndo mengine yanafuata..nadhani mnanielewa!
 
Kwanza ubinadamu ungeanza kwenye KODI ZA WATU na yo ufujaji wa pesa kama huuu

Shekhe mkuu ni expandable na kama aliendelea kuvuta sigara huku akijua madhara yake then he is getting what what he always wanted: GONJWA

na lingine inawezekana kabisa kuwa Mungu anamuadhibu kwa kuwa karibu na mafisadi wa CCM (kwa wale wanaomwamini Mungu
 
..........waislamu fuateni ushauri wa muheshimiwa rais..aliwataka wawe na umoja ..ikiwemo kuheshimu chombo chao watakachokiamua....sasa midhali bado hamjakubali kuunda chombo kipya ni vema mkamtii sheikh mkuu...matatizo ya ndani mnamalizana wenyewe.....NI AIBU KUBWA KIONGOZI MKUU WA KIDINI WA JAMII INAYOHESHIMIKA KULAZWA VICHOCHORONI.......MNGEMTIBU BILA KUSUBIRI MAGAZETI NA VYOMBO VINGINE VIWAKUMBUSHE....

NADHANI HATA WAKRISTO WANA MATATIZO YAO YA NDANI NA MAASKOFU WAO..LAKINI HAIJATOKEA MMOJA AKAUGUA AKALAZWA VICHOCHORONI.....UKISIKIA HIVYO UJUE ATAKUWE NI SELF PROCLAIMED ASKOFU....AMBAO SIKATAI WAPO WENGI ......WANAOHUBIRI AKIFIKISHA WAUMINI 50....ANAJIITA ASKOFU
 
CCM waliwaundia waislam chombo
kinaitwa BAKWATA

Huyo shekhe mkuu kulazwa vichochoroni ni saizi yake tu
 
Ikiwa Bakwata wana uwezo wa kumpeleka Makkah Sheikh mkuu, wakeze na viongozi wasio pungua 10 kila mwaka, iweje leo wakose fedha za kumpeleka ( kwa matibabu) India?

Fedha za umma zitumike vyema sio shamba la bibi lile tafadhali jamani
 
Back
Top Bottom