Serikali inamlipia matibabu Shekhe mkuu India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inamlipia matibabu Shekhe mkuu India

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Mar 14, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mindhali huyu shekhe mkuu ni wa BAKWATA na yuko close na wagalatia kule serikalini sitoshangaa kama kodi za wananchi zinatumika kumlipia matibabu kule India.

  Kama ambavyo serikali isiyo na dini ilivyowalipia mahujaji kwenda Makka basi na hili nalo msije shangaa

  Hii siyo fitna lakini kama kuna ukweli kwenye hili then tunalo la kujadili Ijuma ya leo.

  Kama mjuavyo watawala wanaongoza BAKWATA wanachaguliwa na serikali hivyo its very simple ku connect the dots

  By the way ni mvutaji sigara mkubwa sana huyu..sasa inavezekana sigara nazo zinammaliza

  na mwisho zaidi tunaomba C.V yake  wasalaam
   
 2. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  ....usinichekesha ndugu yangu, kwani wewe hujui ya kuwa kwamba sheikh mkuu ni gov official??! kama walimpeleka yule mwandishi aliyemwagiwa tindikali, ndio itakuwa sheikh ambaye ni kibaraka na wao ndio waliomchagua??

  sema unachotaka kusema sio kukatakata kona!!!
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Jamani Mtanzania Asitibiwe Na Serikali Yake?
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wangapi so far wamesha tibiwa ambao ni walala hoi tu ? Labda wanatibiwa baada ya kuwa ni issue iko connected lakini si la serikali yake .Nakataa huu uongo .

  Askofu alikufa Mjini Dar Kanisa likiwa linatafuta pesa za kumpeleka India Serikali haikuwepo ?
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  GT...Hii ngoma ni ya kudiscuss hapa? Wa-TZ wangapi wanatibiwa na serikali Huko India?....na sehem zingine? kaka naona unaanza kuwa LOW siku hizi. I told u ktk thread fulani hapa...Please kaa Jadili na nafsi yako na angaalia vitu sensitive !!!
  Tujifunze nini ktk Hii Habari yako bro???
   
 6. green29

  green29 JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Kama wanamlipia Sheikh kwa nafasi yake katika dini ni suala la kujadiliwa; Si vibaya kukiwa na policy ya kuwatibia viongozi wa dini mradi iwe ni policy inayowahudumia viongozi wa dini zote na wote bila ubaguzi wala upendeleo.

  Kama Sheikh mkuu anatibiwa kama mtanzania haina shida tunamtakia afya njema. Japo sijui ni vigezo gani huwa vinatumika kuamua mtanzania gani ana haki zaidi ya wengine kutibiwa nje pale matibabu ya hapa nchini yanaposhindikana.

  Na kama anavuta na sigara ni vizuri pia kama mtanzania akishauriwa apunguze kuvuta sigara kwa faida yake, taifa, na wafuasi wa dini anaoaongoza.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0

  well ndio uzuri wa JF! we dare talk openly hata zile topics ambazo wengine mnaziona sensitive

  Ugomvi wangu uko na serikali ambayo inapiga Propaganda kuwa haina DINI ila wanachi wake wana uhuru wa dini

  sasa cha kujiuliza kama serikali ni ya Secular kwa nini iko biased?

  kwa nini nyimbo ya Tifa Mungu anaimbwa wakati kuna watu wengine hawamwamini Mungu?

  This is suppoed to be a government for all lakini contrary to popular belief ni kuwa serikali yetu imejaa udini wa kila namna na kama huamini tembelea ofisi za serikali isiyo na dini wakati wa Krisimasi...yaani hawa wapuuzi (wa serikali) wanaspend pesa za walipa kodi ku organise christmass parties, na kama kama hiyo haitoshi mahujaji wakikwama basi serikali isiyo na dini ya Tanzania iko tayari kwenda EXTRA MILE kuwaacomodate...na watawala wetu kama vile waziri mkuu kila kukicha anajitwisha mashughuli ya kwenda kufugua makongamano ya ma padre at a capacity kama PM...hayo ya kufuturisha ndio usiseme

  sasa huyu Shekhe wa BAKWATA kama alikuwa ni mvuta sigara na keshapata hilo gonjwa sasa kuna ubaya gani akatibiwa pale Muhimbili ? kwani Muhimbili ina matatizo gani?


  Haya ndio mambo yanayoniboa na hii serikali yetu ambao tunajidanganya kuwa iko far ehind na mambo ya Propaganda lakini ndio wenyewe kwa kuspin

   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0  wewe umeamka na si mfuata mkumbo

  tukishamliza hili la viongozi wa serikali kuingilia mambo ya dini tutamove on kwenye kuangalia gharama za sherehe za dini kwenye ofisi za serikali

  maana tatizo langu kubwa ni tuna produce quite big army of lawyers of recent na hawa jamaa wengi hawana nafasi za kushindana na akina IMMA au MNKONO sasa wataanza kutafyta zile kesi za NO WIN NO FEE na najua atatokea tu aliyekuwa frustrated mfano pale FOREIGN au HAZINA ambaye ataamua kufungua mashitaka dhidi ya Jamhuri on the grounds kuwa wizara husika imekuwa insensitive towards his/her belief na yuko offended na kadi za Krismas au Iddi

  Na of course najua atashinda tuu kesi na of course serikali itabidi ilipe kwa kuwa insensitive towards other faiths

  Tukishamaliza hilo itabidi tupush nyimbo ya Taifa iondolewe neno MUNGU but we have to start somewhere
   
 9. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapa sio kweli hata kidogo
  Kwani watanzania kibao wanamatatizo, tena ya ajabu na wanaomba msaada mpaka kwenye maTV na magazeti lakini Serikali hata haitoi hata chembe ya kuwasaidi.
  Kumbuka niliweka Picha ya kuomba msaada ya dada mmoja hapo Lugalo, lakini wamejitokeza wasamalia wema, ila serikali haijatoa hata kidogo, Pamoja na hali mbaya aliyonayo huyo dada.
  Hivyo sio kwamba anasaidiwa kama Mtanzania, bali kama kiongozi wa dini!
  Na sijui kama Serikali hii, inawasaidia Viongozi wote wa dini zote mbalimbali tulizonazo Tanzania? Kwa sababu tuna madhehebu kibao Bongo, Je serikali inasaidia Viongozi wote, Kama jibu ni hapana, Basi huu ni Ufisadi
   
 10. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi sina neno endapo kodi yangu inatumika kuokoa maisha ya muislam mwenzangu.(maoni Binafsi)
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tena ambaye ni mlalahoi.....?
   
 12. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya ni maoni binafsi, lakini sio ya Kitanzania (Labda wewe sio Mtanzania)
  Kwa sababu Kodi inayotumika sio ya Waislam tu hapa, bali ni ya watanzania ambao wana dini mbalimbali, sasa ikisema huna neno kwasababu kodi inamuokoa Muislam mwenzi, hii sio nzuri hata kidogo, Jamii ya watanzania hatuna matatizo ya Udini, labda kama unataka kuyapandiki!!
  Unadhani Kodi yako wewe(Binafsi) inaweza kumpeleka huyo Sheikh Kutibiwa India? Kama ni hapana basi jua unaitaji kodi ya Watanzania.

  Na tafadhali usitake kuwa chanzo cha kuchochea mapambano katika dini zetu, please, tumia busara zako na kuwasaidia watanzania kwa ujumla na si watanzania wa dini fulani.
   
 13. M

  Msavila JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni haki ya kila Mtanzania kupewa matibabu yanayostahili hapa nchini na ikibidi nje ya nchi. Tatizo lilijitokeza ni haya matabaka,e.g. Kapuya alikimbizwa India , wenzie wakabaki nasikia wengine walibaki tabora wakaendelea kudhoofu hatimaye kufa, kisa Kapuya ni waziri. Mimi naamini kwamba, kama hii serikali yetu ukiamua kuboresha medical facilities zetu, tunao wataalamu wengi na wenye uzoefu. Referal cases zingepungua sana au kubaki zile za kweli kweli. Hivi mtu una kisukari, leo unaenda medical checkup UK, watakueleza kipi ambacho hujasikia toka kwa madakitari wetu. Nauli ya mgonjwa, wasidikizaji na posho zao, consultancy/unnecessary investigations zinaotolewa kwa mgonjwa mmoja nje ya nchi zingeweza kununua vifaa vya kuhudumia wagonjwa wengi tu.
   
 14. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Swali la kwanza , Kwanza mna uhakika ya kuwa Sheikh mkuu analipiwa na hela ya serikali ? Kama jibu ni ndiyo basi tunaweza kuwa na debate. Mimi nadhani we must draw a line .....
   
 15. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sijui kama ni kweli huyo Sheikh Mkuu (Mufti) anatibiwa India na kwa gharama za nani, lakini kuna jambo nataka kuliweka wazi hapa kwani inaelekea wengi hawalijui ndio maana wanauliza maswali mengi na kulalamika.

  Utaratibu ama mfumo wa ngazi ya rufaa (referral hierarchy) wa utoaji wa huduma za tiba nchini Tanzania uko hivi: Inatarajiwa mgonjwa aanze katika zahanati, ikishindikana anapelekwa kituo cha afya, ikishindikana hapo anaenda hospitali ya wilaya, vivyo hivyo ya mkoa, rufaa na ya taifa (Muhimbili). Yeyote anaeshindikana kutibiwa Muhimbili kwa maoni ya mabingwa wetu, anaandikiwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, na hii hufanywa kwa gharama za serikali kwa mwananchi yeyote bila kujali cheo chake. Tatizo kubwa lililopo ni kuwa wanaoandikiwa rufaa hizo ni wengi kuliko uwezo (ndivyo tunavyoambiwa), ndio maana unaona wengine wakiomba msaada kupitia magazeti na vyombo vingine vya habari ili wawahi matibabu (maana unaweza kukuta mtu amewekwa kwenye foleni ya kwenda mwaka ujao wakati ugonjwa unaendelea kumtafuna!) Na taasisi kama Lions Club imekuwa ikisaidia sana kupunguza mzigo huu kwa kuwafadhili hasa wagonjwa wa moyo walioko kwenye orodha ya kupelekwa nje. Haya nayasema kwa uzoefu, mdogo wangu mmoja alipata mtoto mwenye tatizo la moyo (aliambiwa moyo una tundu), kwa hiyo baada ya kutibiwa Mt Meru Arusha na KCMC alipelekwa Muhimbili ambako walimwandikia rufaa ya kwenda India. Kipindi hicho mtoto alikuwa na umri wa miezi 9 tu, lakini aliwekwa kwenye foleni hadi alipokuja kufanikiwa kupelekwa akiwa na umri wa miaka 2, na bado ilibidi tuchange hela za kumsaidia mama yake gharama za kujikimu huko India maana serikali ilimlipia tu nauli ya ndege ya kwenda na kurudi na gharama za matibabu ya mtoto ambazo zililipwa moja kwa moja hospitali. Bahati nzuri mtoto alipona na sasa yuko shule ya msingi.

  Kwa hiyo kulipia wananchi matibabu nje ya nchi ni sera ya serikali, hasa pale ambapo matibabu husika hayapatikani nchini. Kwa mantiki hiyo, Mufti kama raia wa Tanzania, ana haki hiyo ya kutibiwa nje na serikali kama madaktari walishauri hivyo. Labda tunachoweza kujadili ni mambo kama hayo ya wananchi wengine kucheleweshwa (kama huyo mwanangu aliyesubiri zaidi ya mwaka), na kuwa je kungekuwa na busara gani labda kumweka Mufti kwenye waiting list kama wengine wanavyosubiri nk? Na je mnajua Mufti alisubiri kwa muda gani hadi kufanikiwa kupata nafasi hiyo? Mimi sijui, lakini kwa uzoefu najua kuna uwezekano naye pia kasubiri sana tu (kama analipiwa na serikali). Wakati tunafuatilia shida ya mtoto wetu kipindi hicho, kulikuwa na waziri mmoja mstaafu nae alikuwa kwenye listi, alisubirishwa hadi ndugu zake wakakasirika wakaamua kumpeleka South Africa kwa hela yao. Nilikuja kusikia baadae kuwa serikali iliwarudishia zile hela. Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu serikali kumlipia Mufti matibabu, gharama hizo serikali ingelipa tu hata kama asingekuwa Mufti, wapo wanaolipiwa hata leo, tatizo ni usumbufu uliopo hadi mgonjwa kufanikiwa kupata hiyo huduma.​
   
 16. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nilijua kuwa maoni yangu ni yakitatanishi na yanaweza yakatafsiriwa vibaya ndio maana nikaweka mabano mwisho nikisema ni binafsi.

  Nimesikia Mheshmiwa kweli uko sahihi. Kweli hayo maoni si ya kitanzania. Sentensi yangu sasa nataka isomeke hivi.

  Mimi sina neno endapo kodi yangu inatumika kuokoa maisha ya MTANZANIA mwenzangu.
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  hiyo ya mungu kwenye nyimbo ya Taifa na kadi za krisimasi mbona hamsemi au ndio sensitive?
   
 18. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mmhh watu wa mafia bwana.....

  nnakubali kwa nn mkaitwa mafia
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni kitendo cha ajabu sana. Hata wakati wa mahujajji nadhani Lowassa alifanya jambo la kijing sana kwenda kujihusisha na suala la mahujaji, na this time serikali inazidi kujiingiza kwenye mambo ambayo ni kinyume cha katiba. So what will happen kama viongozi wa anglican, RC, Lutheran au hata wa dini nyingie Hindu, na hata viongozi wa wapagani wakiumwa serikaliitawalipia?
  NI kifungu gani cha katiba ya Tanzania kinachomtambua Mufti Mkuu or Muadhama Pengo kama ni Governmet official? Isi this kujipendekeza kwa serikali kwa waislamu au kujaribu kuwahonga waislamu. Huku ni kutiana aibu tu. Waislamu wanauwezo mkubwa sana wa kuweza kumlipia Mufti matibabu, hata hivyo yeye alitakiwa kwenda kutibiwa Saudia na sio India, kwani yeye Kubenea?
   
 20. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,609
  Likes Received: 6,774
  Trophy Points: 280
  Wimbo wa taifa ni mali ya Taifa, siyo mali ya serikali. katiba inasema serikali haina dini haisemi Taifa halina dini. na katika taifa Majority ndo wanashika mpini, kwa hiyo katika Tanzania wanaomwamini Mwenyezi Mungu ambao ni wengi wana haki ya kuonyesha misimamo yao kwa dhahiri.

  Isitoshe serikali ni mali ya Taifa na Taifa siyo mali ya serikali, serikali kutokuwa na dini tuliamua sisi kama taifa iwe hivyo.Hakuna mahali serikali itaamua kuubadili wimbo wetu wa taifa bila ridhaa yetu sisi ambao ni wamiliki halali wa wimbo huo tena ambao ni majority katika nchi hii.
   
Loading...