Serikali Inaendelea Kuangalia Fursa kwa ajili ya Kuwawezesha Wanawake Kuanzisha Vituo Mahususi vya Uwekezaji na Masoko kwa Wanawake katika Kata

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945

NAIBU WAZIRI EXAUD KIGAHE - SERIKALI INAANGALIA FURSA KUWAWEZESHA WANAWAKE KUWEKEZA KATIKA KATA

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Serikali inaendelea kuangalia fursa mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kuanzisha vituo mahususi vya uwekezaji na masoko kwa wanawake katika kata.

Kigahe amesema hayo Mei 29, 2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Janeth Elias Mahawanga (Mb) katika swali lake lini Serikali itaanzisha vituo maalum vya kata kwenye uwekezaji na masoko kwa wanawake

Akijibu swali hilo Kigahe amesema Serikali imeanzisha majukwaa ya kiuchumi mahususi kwa ajili ya wanawake kupata fursa za uwekezaji na biashara na kuzitumia ikiwemo masoko ya bidhaa wanazozalisha.

Amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2021/2022, Mikoa yote 26 imezindua Majukwaa ya wanawake, Halmashauri 140 kati ya Halmashauri 184, Kata 1,149, kati ya Kata 2,404, Mitaa/Vijiji 1,776, kati ya Mitaa/ vijiji 7,613

Kigahe amesema Wizara kupitia Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO), yenye ofisi katika mikoa yote nchini hadi kufikia Februari, 2023, imeratibu na kutoa mafunzo na ujuzi kwa wajasiriamali wanawake 7,009 kupitia kozi 519 katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na uendelezaji wa biashara na shughuli za uzalishaji

Aidha amesema mafunzo ya huduma za ushauri wa kibiashara na ufundi yalitolewa kwa wajasiriamali wanawake 8,898. Mafunzo hayo yalitolewa katika nyanja za ufundi, uchumi, uongozi, masoko, ubora wa bidhaa, teknolojia, kubuni, kusanifu na kutayarisha uchambuzi yakinifu wa miradi ya viwanda na biashara.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-30 at 18.33.51.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-30 at 18.33.51.jpeg
    35.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom