Fursa ya Kuanzisha Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Karanga, Ufuta na Alizeti - Kata ya Likokona, Nanyumbu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Fursa ya Kuanzisha Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Karanga, Ufuta na Alizeti - Kata ya Likokona, Nanyumbu

Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) inaendelea kutangaza fursa za uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ikiwemo mazao ya karanga, ufuta na alizeti.

Haya yamebainishwa bungeni Februari 12,2024 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Nanyumbu, Ally Yahya Mhata.

Katika swali lake Mhata alitaka kujua mikakati ya Serikali wa kuhakikisha kiwanda cha kuchakata mazao ya karanga, ufuta na alizeti kinajengwa katika Kata ya Likokona, Nanyumbu.

Akijibu swali hilo, Kigahe amesema kwa kuzingatia mahitaji ya viwanda vya kuchakata mazao ya karanga, ufuta na alizeti katika Wilaya ya Nanyumbu, hususani Kata ya Likokona, Serikali kupitia SIDO, TEMDO na CARMATEC inaendelea kubuni mashine za bei nafuu za kuchakata mazao hayo.

"Aidha, Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) inaendelea kutangaza fursa za uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ikiwemo mazao ya karanga, ufuta na alizeti yanayopatikana Kata ya Likokona, Nanyumbu."

maxresdefaultnbvgytr.jpg
GGMA2nqXcAAFdqH.jpg
 
Back
Top Bottom