Serikali ianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa

Serikali ianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa

Ni vyema kuanzisha Makanisa kwa lengo la kusambaza Injili ila kinachosikitisha sasa hivi kuna kundi ambalo limevamia eneo hili nyeti kutokana na aidha ugumu wa Maisha, tamaa ya utajiri, uelewa mdogo, ukosefu wa ajira au kutumika na Shetani wanaanzisha Makanisa lakini ndani yake wanaharibu taswira nzima na heshima nzima ya Imani.

Kuna Wachungaji ukiangalia matendo yao, mienendo yao, mawazo yao,mavazi yao, maneno yao, mambo yao, mahubiri yao nk unapata kichefuchefu na mara ingine kama Mkristo unaona aibu, ni udhalilishaji mkubwa wa Ukristo kwakweli.

Kinachosikitisha Serikali imeendekeza kuchukua hatua baada ya Matatizo kukua sana na kutengeneza taharuki ambazo zingeweza kuepukika, mfano yaliyotokea kwa Zumaridi huko Mwanza.

Kwanini Serikali isianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa itakayoundwa na Viongozi wa Makanisa wenyewe kwa namna itakayoonekana inafaa, ikaandaa Vigezo vya kuwa Askofu, Mchungaji, Mwinjilisti nk, ikaandaa pia Vigezo vya kuanzisha Kanisa na pia Mamlaka hiyo ikawa na jukumu ya kuyasimia Makanisa na Viongozi wake ili kuondoa hii aibu inayokua kila siku na kulinda usalama wa nchi?

Mwongozo wa Mambo mengi uko kwenye Vitabu vya Mungu hata Mavazi ila wanaibuka makanjanja hawana Elimu yoyote ya kutosha ya theolojia wanafanya upotoshaji waziwazi na wote tunaangalia, kila Mchungaji akiibuka namna hii na Kanisa lake mwisho wake ni nini?

Angalizo uanzishwaji wa Mamlaka hizi utoe uhuru wa kutosha kwa Viongozi wa Dini kusimamia na kuamua mambo yao, Serikali isimamie tu utekelezaji yasije kutokea ya BAKWATA.
Hilo linahitaji mchakato katiba ibadilishwe ya sasa isomeke serikali ina dini na raisi ni Ayatollah kiongozi mkuu wa Dini Tanzania ilivyo Iran,Rwanda nk au itamke Raisi ndie mwenyezi mungu anayetakiwa kuelekeza watu waabudu nini na waabudu vipi

Wimbo wa taifa wa Tanzania mfano kila mtu huimba Mungu ibariki Afrika na huimbwa na kila mtu akiimba huimba kwa hamasa kuwa mungu wake awe mhindu muabudu ng'ombe huomba ng'ombe aabuyo aibariki Tanza'mwingine mzimu wa babu yake mwingine mungu wake mwamposya mwingine mungu wake mavi yake au mwabudu joka.huimba kwa hamasa akiomba joka analoabudu libariki Afrika na Tanzania kila mtu huimba Mungu ibariki Afrika, mungu ibariki Tanzania kwa li mungu lake alijualo mwenyewe analoabudu na analiabuduje kavaa nguo au uchi anajijua mwenyewe

Dini ndizo zina watu tena loyal hasa hata wakiambiwa wale mavi ya kiongozi wao watabarikiwa wanakula mwanasiasa hana.Hivyo sio vizuri Serikali kujitumbukiza mambo ya dini.Katiba yetu iko vizuri mno kuhusu mambo ya dini kuliko nchi nyingi duniani ikiwemo Rwanda ambako Raisi ni kiongozi wa dini anayejua watu waabudu wapi,kiongoxi wao wa dini awweje nk

Serikali sio Mungu wa kusema.mtu anatakiwa asali hivi aamini hiki au asali kanisa au msikiti au dini ipi na kuvipi sio kazi ya serikali ndio maana katiba yetu imetamka wazi maswala ya imani za dini ya binafsi .Huridhiki na Bakwata au katoliki au dini yeyote sali ujuavyo abudu hata hawara yako cha msingi usifanye makosa ya jinai yaliyoko sheria za makosa ya jinai
Unaabudu nani,unaabudu nini na namna gani mambo yako binafsi na ibada zako ziwe za uongo au kweli mradi hazizalishi jinai Jinai ikiwepo sheria zipo utaburuzwa mahakamani wewe kama wewe sio dini unasali au unasalisha

Kusali kuhusishe kula mavi au majani ni imani yako kibinafsi

Sio.kazi ya serikali kusema usile majani ukisali
 
Kanisa lolote ikidhibitika mchungaji au padri kala vitoto vya kiume lifutwe
 
Back
Top Bottom