Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 579
- 887
Ni vyema kuanzisha Makanisa kwa lengo la kusambaza Injili ila kinachosikitisha sasa hivi kuna kundi ambalo limevamia eneo hili nyeti kutokana na aidha ugumu wa Maisha, tamaa ya utajiri, uelewa mdogo, ukosefu wa ajira au kutumika na Shetani wanaanzisha Makanisa lakini ndani yake wanaharibu taswira nzima na heshima nzima ya Imani.
Kuna Wachungaji ukiangalia matendo yao, mienendo yao, mawazo yao,mavazi yao, maneno yao, mambo yao, mahubiri yao nk unapata kichefuchefu na mara ingine kama Mkristo unaona aibu, ni udhalilishaji mkubwa wa Ukristo kwakweli.
Kinachosikitisha Serikali imeendekeza kuchukua hatua baada ya Matatizo kukua sana na kutengeneza taharuki ambazo zingeweza kuepukika, mfano yaliyotokea kwa Zumaridi huko Mwanza.
Kwanini Serikali isianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa itakayoundwa na Viongozi wa Makanisa wenyewe kwa namna itakayoonekana inafaa, ikaandaa Vigezo vya kuwa Askofu, Mchungaji, Mwinjilisti nk, ikaandaa pia Vigezo vya kuanzisha Kanisa na pia Mamlaka hiyo ikawa na jukumu ya kuyasimia Makanisa na Viongozi wake ili kuondoa hii aibu inayokua kila siku na kulinda usalama wa nchi?
Mwongozo wa Mambo mengi uko kwenye Vitabu vya Mungu hata Mavazi ila wanaibuka makanjanja hawana Elimu yoyote ya kutosha ya theolojia wanafanya upotoshaji waziwazi na wote tunaangalia, kila Mchungaji akiibuka namna hii na Kanisa lake mwisho wake ni nini?
Angalizo uanzishwaji wa Mamlaka hizi utoe uhuru wa kutosha kwa Viongozi wa Dini kusimamia na kuamua mambo yao, Serikali isimamie tu utekelezaji yasije kutokea ya BAKWATA.