Serikali ianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa

Serikali ianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa

Ni vyema kuanzisha Makanisa kwa lengo la kusambaza Injili ila kinachosikitisha sasa hivi kuna kundi ambalo limevamia eneo hili nyeti kutokana na aidha ugumu wa Maisha,tamaa ya utajiri,uelewa mdogo,ukosefu wa ajira au kutumika na Shetani wanaanzisha Makanisa lakini ndani yake wanaharibu taswira nzima na heshima nzima ya Imani.

Kuna Wachungaji ukiangalia matendo yao,mienendo yao,mawazo yao,mavazi yao,maneno yao,mambo yao,mahubiri yao nk unapata kichefuchefu na mara ingine kama Mkristo unaona aibu,ni udhalilishaji mkubwa wa Ukristo kwakweli.

Kinachosikitisha Serikali imeendekeza kuchukua hatua baada ya Matatizo kukua sana na kutengeneza taharuki ambazo zingeweza kuepukika,mfano yaliyotokea kwa Zumaridi huko Mwanza.

Kwanini Serikali isianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa itakayoundwa na Viongozi wa Makanisa wenyewe kwa namna itakayoonekana inafaa, ikaandaa Vigezo vya kuwa Askofu,Mchungaji,Mwinjilisti nk,ikaandaa pia Vigezo vya kuanzisha Kanisa na pia Mamlaka hiyo ikawa na jukumu ya kuyasimia Makanisa na Viongozi wake ili kuondoa hii aibu inayokua kila siku na kulinda usalama wa nchi?

Mwongozo wa Mambo mengi uko kwenye Vitabu vya Mungu hata Mavazi ila wanaibuka makanjanja hawana Elimu yoyote ya kutosha ya theolojia wanafanya upotoshaji waziwazi na wote tunaangalia,kila Mchungaji akiibuka namna hii na Kanisa lake mwisho wake ni nini?

Angalizo uanzishwaji wa Mamlaka hizi utoe uhuru wa kutosha kwa Viongozi wa Dini kusimamia na kuamua mambo yao,serikali isimamie tu utekelezaji yasije kutokea ya BAKWATA.
Tangu lini shetani akamsimamia Mungu?Serikali yenyewe imeshindwa kujisimamia pamoja na kwamba ina mihimili mitatu

Wao wawe makini tu ili Imani yeyote itakayopelekea jinai ndio iwajibishwe sio kusimamia,kumbuka kuna waganga wanatoa watu kafara na hamsemi,kuna watu wanaabudu mizimu wananyweshwa hadi vinyesi ila hamongei au sababu hawainyeshwi kwenye TV?
 
Huduma Za Makanisa/Misikiti Zinapata Usajili/Kufutwa/Kuzuiwa
Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Kuna Kitengo Maalum
 
Sadaka sio jambo la lazima Ila wachungaji wenu wanawalazimisha lazima mtoe Sadaka tena mjimalize kabisa, waislamu hawalazimishwi kutoa Sadaka wao Ibada inatosha sana Ila wakina mitume wenu Sadaka lazima uwape tena sio ombi au hiari bali ni lazima umpe Sadaka yako
Usilinganishe Uislamu na Ukristo halafu ukadraw conclusion

Kwenye ukristo Ibada=Sadaka
 
Serikali Haina mamlaka kuingia Kanisani na kupanga taratibu za IBADA.

Isiwapangie namna ya kuabudu,

Mungu mwenyewe huwashughulikia waovu Kwa Muda wake.

Mkiingia Kanisani, mtakachokipata msijesema hamkuonywa.
 
Usilinganishe Uislamu na Ukristo halafu ukadraw conclusion

Kwenye ukristo Ibada=Sadaka
Sadaka MZEE yaan lazima ulipie maombi hawaombi bure wale wachungaji, ndicho wamekisomea kwenye falsafa na teolojia jinsi ya kuwakwangua kondoo wao sadaka
 
Ni vyema kuanzisha Makanisa kwa lengo la kusambaza Injili ila kinachosikitisha sasa hivi kuna kundi ambalo limevamia eneo hili nyeti kutokana na aidha ugumu wa Maisha,tamaa ya utajiri,uelewa mdogo,ukosefu wa ajira au kutumika na Shetani wanaanzisha Makanisa lakini ndani yake wanaharibu taswira nzima na heshima nzima ya Imani.

Kuna Wachungaji ukiangalia matendo yao,mienendo yao,mawazo yao,mavazi yao,maneno yao,mambo yao,mahubiri yao nk unapata kichefuchefu na mara ingine kama Mkristo unaona aibu,ni udhalilishaji mkubwa wa Ukristo kwakweli.

Kinachosikitisha Serikali imeendekeza kuchukua hatua baada ya Matatizo kukua sana na kutengeneza taharuki ambazo zingeweza kuepukika,mfano yaliyotokea kwa Zumaridi huko Mwanza.

Kwanini Serikali isianzishe Mamlaka ya Usimamizi wa Makanisa itakayoundwa na Viongozi wa Makanisa wenyewe kwa namna itakayoonekana inafaa, ikaandaa Vigezo vya kuwa Askofu,Mchungaji,Mwinjilisti nk,ikaandaa pia Vigezo vya kuanzisha Kanisa na pia Mamlaka hiyo ikawa na jukumu ya kuyasimia Makanisa na Viongozi wake ili kuondoa hii aibu inayokua kila siku na kulinda usalama wa nchi?

Mwongozo wa Mambo mengi uko kwenye Vitabu vya Mungu hata Mavazi ila wanaibuka makanjanja hawana Elimu yoyote ya kutosha ya theolojia wanafanya upotoshaji waziwazi na wote tunaangalia,kila Mchungaji akiibuka namna hii na Kanisa lake mwisho wake ni nini?

Angalizo uanzishwaji wa Mamlaka hizi utoe uhuru wa kutosha kwa Viongozi wa Dini kusimamia na kuamua mambo yao,serikali isimamie tu utekelezaji yasije kutokea

Ngumu sana kuianzisha, hiyo mamlaka itakuwa na kazi ngumu zaidi na unavyofikiria.
 
Ni vyema kuanzisha Makanisa kwa lengo la kusambaza Injili ila kinachosikitisha sasa hivi kuna kundi ambalo limevamia eneo hili nyeti kutokana na aidha ugumu wa Maisha,tamaa ya utajiri,uelewa mdogo,ukosefu wa ajira au kutumika na Shetani wanaanzisha Makanisa lakini ndani yake wanaharibu taswira nzima na heshima nzima ya Imani.
Wazo zuri

Juzi nimevamiwa na genge usiku likiniambia kwanini sijaonekana kwenye Jumuiya, jana jioni narudi toka safari nalikuta getini ati sijaonekana ibadani na nijiandae kutengwa, nikawajibu neno moja tu "hewala"
 
Ngumu sana kuianzisha, hiyo mamlaka itakuwa na kazi ngumu zaidi na unavyofikiria.
Jambo ukiliona gumu hutathubutu hata kulianza

Tozo zilisemekana kutowezekana lakini zimewezekana na zinatesa vibaya mno
 
Jambo ukiliona gumu hutathubutu hata kulianza

Tozo zilisemekana kutowezekana lakini zimewezekana na zinatesa vibaya mno
Dini ni nyanja ngumu hatari, ukizigatia katiba yetu imeruhusu uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Abudu chochote bila kuwa threat kwa sheria ya tz
 
Hili jambo ni muhimu na lazima. Serikali bila shaka itaogopa wanasiasa uchwara kama kina lissu wenye kujidai kutetea uhuru wa kila kitu wakati taifa linaangamia kwa watu kupotoshwa na kuibiwa na wajanja.
Mamlaka inatakiwa iwe ya usimamizi wa dini zote maana hata kwenye uislaam kuna upotoshaji sana na kwenye nchi zingine amani imepotea kabisa.
Mamlaka inaweza kua moja ila iwe na sehemu kwa kila dini zetu kubwa uislam na ukristo. Wasomi wa dini toka vyuo au taasisi zinazokubalika ndio wawe wajumbe ili kuwekwa taratibu ya kuendesha dini zetu bila kuruhusu wahuni wenye kujitafutia utajiri wa haraka kwenye dini zetu.

Punguza chuki, Lissu kaingiaje?
 
Wewe Kunguni utakuwa walewale,ina maana hujui uanzishwaji wa hayo unayoyataja kuna Mamlaka zinasimamia?Kama ndivyo basi unastahili kuandika unayoandika na nakusamehe bure tutaongea ujinga ukikupungukia.
Hahahahaha, we bwana mdogo hujui kuwa uanzishwaji na usajili wa Makanisa upo chini ya wizara ya mambo ya ndani? Nilikuelewa unamaanisha kiundwe chombo au mamlaka maalumu ya kusimamia makanisa na kimsingi hiyo ndio hoja yako na umezunguka zunguka na ndio maana nikakueleza hayo mengine vipi? Yenyewe yapo huru? Inaonekana we maamuma una mapepo au ni mzee wa kusafiri na ufagio usiku ndio maana unayapiga vita makanisa. Nimekudharau sana.
 
Back
Top Bottom