Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,841
- 21,079
Dini ni sehemu ambayo mtu anaruhusiwa kuwa kichaa bila kunyanyapaliwa. Ni safe place. Mnataka kunyanganya watu na hiyo?
Wewe Kunguni utakuwa walewale,ina maana hujui uanzishwaji wa hayo unayoyataja kuna Mamlaka zinasimamia?Kama ndivyo basi unastahili kuandika unayoandika na nakusamehe bure tutaongea ujinga ukikupungukia.Misikiti, Vikongwe vya Uganga na Ulozi, Vilabu vya Pombe, Makasino, Makampuni ya betting na madanguro yenyewe ni sawa tu yaanzishwe mahali popote bila usimamizi wowote. Pumbavu kabisa wewe. Kuna mtu kaenda kuripoti kaibiwa au kunyanyasika huko makanisani. Hovyo kabisa umeamka kwenye danguro unaandika uharo huku.
Kwani wewe huwa hutoi sadaka kwenye hiyo imani yako? Shida yako ni ninj watu wakitoa sadaka kwenye imani zao?Muda wa Sadaka sasa ukifika utaona Mchungaji anavyowakoromea Wana kondoo wake watoe Sadaka kwa lazima yaani wajimalize mpaka nauli ya kurudia nyumbani, na Malofa wanatoa yaan Malofa wanazidi kua masikini huku mchungaji na timu yake ya upigaji wanazidi kutajirika
Haya tupatie hitimisho je ni nani basi akituambia kristo yuko hapa au yuko pale huyo tumwamini?Yesu alisema: "Na ikiwa mtu yeyote atawaambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa,’ au, ‘Yuko pale!’ msiamini. 24 Kwa maana Kristo wengi wa uwongo na manabii wa uwongo watatokea na kufanya ishara kubwa na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale waliochaguliwa. 25 Tazama! Nimewaonya mapema. 26 Basi, watu wakiwaambia, ‘Tazama! Yuko nyikani,’ msiende; ‘Tazama! Yumo katika vyumba vya ndani,’ msiamini." Mathayo 24:23-26.
Mambo unayoona ni utimizo wa unabii wa Yesu mwenyewe. Hizi ni siku za Mwisho. Lazima yaliyotabiriwa yatokee.
Sadaka sio jambo la lazima Ila wachungaji wenu wanawalazimisha lazima mtoe Sadaka tena mjimalize kabisa, waislamu hawalazimishwi kutoa Sadaka wao Ibada inatosha sana Ila wakina mitume wenu Sadaka lazima uwape tena sio ombi au hiari bali ni lazima umpe Sadaka yakoKwani wewe huwa hutoi sadaka kwenye hiyo imani yako? Shida yako ni ninj watu wakitoa sadaka kwenye imani zao?
Ugumu wa Maisha na mauzauza ya Maisha ndio hupelekea watu kufanya hivyo, wanaokesha kanisani masaa zaidi ya 12 unafikiri wanawaza nini cha zaidi?Wananchi wakipata maarifa ya kutosha, manabii uchwara na matapeli watakosa wateja.
Na ikiwa mtu yeyote atawaambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa,’ au, ‘Yuko pale!’ msiamini. Matthew 24:23Haya tupatie hitimisho je ni nani basi akituambia kristo yuko hapa au yuko pale huyo tumwamini?
Mkuu kama wenyewe hawalalamiki na wewe hawajakudhuru kwa lolote basi ni vema tuwaache wawe huru kama sisi wengine tulivyo huru.Nawasilisha.Sadaka sio jambo la lazima Ila wachungaji wenu wanawalazimisha lazima mtoe Sadaka tena mjimalize kabisa, waislamu hawalazimishwi kutoa Sadaka wao Ibada inatosha sana Ila wakina mitume wenu Sadaka lazima uwape tena sio ombi au hiari bali ni lazima umpe Sadaka yako
Ndio wanazidi kua makapuku huku Mchungaji akiwa anatajirika,Mkuu kama wenyewe hawalalamiki na wewe hawajakudhuru kwa lolote basi ni vema tuwaache wawe huru kama sisi wengine tulivyo huru.Nawasilisha.
Sadaka sio jambo la lazima Ila wachungaji wenu wanawalazimisha lazima mtoe Sadaka tena mjimalize kabisa, waislamu hawalazimishwi kutoa Sadaka wao Ibada inatosha sana Ila wakina mitume wenu Sadaka lazima uwape tena sio ombi au hiari bali ni lazima umpe Sadaka yako
Huujaenda kuhudhulia ibada zao hata Radio husikilizi Tv huangalii? Unatumia kingambuzi gani? Radio moja nilikua nasikiliza kuna mpangaji wetu hapa anaendaga huko Mchungaji analazimisha watoe Sadaka, acha ubishi ningekua nimerekodi ningeweka sauti hapa umsikieHakuna mtu anayelazimishwa kutoa sadaka nchi hii, wote wanatoa kwa hiyari yao kwa ufahamu timamu au kwa kupumbazwa.
Pakiuma watasema tu,huenda kuna faida wanayoipata ambayo mimi na wewe hatuioni na ndio maana hawaachi kwenda na zaidi ya hayo wanazidi kuongezeka.Ndio wanazidi kua makapuku huku Mchungaji akiwa anatajirika,
Huujaenda kuhudhulia ibada zao hata Radio husikilizi Tv huangalii? Unatumia kingambuzi gani?
Na wanazidi kua makapuku kila kukicha afadhari ya Jana huku mchungaji ananeemeka kweli dini ni biasharaPakiuma watasema tu,huenda kuna faida wanayoipata ambayo mimi na wewe hatuioni na ndio maana hawaachi kwenda na zaidi ya hayo wanazidi kuongezeka.
Mzee nmekwambia nmesikiliza leo baada ya Sala ya Toba mchungaji akaanza kulazimisha watoe Sadaka, wewe Tv huangalii Radio husikilizi kanisani kwao kwenye ibada huendi utajulia wapi?Hakuna mtu mzima anayelezamishwa kwenda kwenye hizo ibada, wote wanaenda kwa hiyari yao.
Kuna Card ya kiingilio ipo wanachaji 10,000 kwa kichwa unaandika matatizo yako yote yanayokusumbua, kuna package ya kuonana na mchungaji ana kwa ana kumueleza matatizo yako unalipia sio bureTanzania tunakoelekea hawa Watumishi wataamuru watu wale vinyesi kabisa. Na kinachotisha ni kiingilio cha kumuona Mtumishi kama Nabii Musa, Suguye na wengine wengi. Hatari Sana hii