Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,253
Hali ya maisha imewachanganya vijana wengi, mazingira na hali sio rafiki kwa biashara, Ajira na zenyewe hakuna.
Vijana wamesoma na sasa wameishia mitaani, nguvu ya wazazi nayo imeishia hapo, serikali nayo imeishia hapo, kwanini kijana asichanganyikiwe.
Ongezeko la watoto wa mtaani nao ni zao la vijana ambao wapo kwenye kundi hili hapo juu kutokana na Kukosekana kwa maadili pamoja na familia bora yenye uchumi thabiti.
Ulevi wa kupindukia, wizi, utapeli, kubeti, kamari na michezo mingine michafu limekuwa kimbilio la vijana wengi wasomi kama njia mojawapo ya kujipa furaha na kuondoa msongo wa mawazo.
Pamoja na mambo mengine mengi kukosekana kwa mfumo rasmi wa maisha juu ya vijana wetu ndio chanzo kikuu cha uovu unaendelea hivi sasa, kama vile ulawiti, ubakaji, mauaji pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili.
Ukipita mitaani unaona vijana wasomi wanavyolewa pombe, mataptap, na kufanya vituko mitaani unabaki kusikitika tu!