Serikali iangalie namna ya kuwasaidia Wagonjwa wa Dialysis MNH

heavenlight M

New Member
Nov 6, 2023
1
2
Wagonjwa wa figo hawana msaada. Gharama ni kubwa sana dialysis kwa session moja ni Shs 180,000. Mgonjwa anatakiwa kufanyiwa angalau mara tatu kwa wiki.

Ikimaanisha Shs 540,000 kwa wiki. Wenye bima ya NHIF ya individuals kama Timiza haikubaliki. Dawa nyingi za kutibu figo hazikubaliki kwenye NHIF.

Serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia wagonjwa we figo.
 
Daah poleni sana,naamini wahusika wamesikia kilio chenu, pia nivyema muwe na chama cha kuwasemea itapendeza zaidi na itakua na nguvu.
 
Aisee!, tusingekuwa tunaenda Hosp mkuu, una gugo dariri unajitibu...JF forums kubwa iliyojaa wataalam wa kila aina.
Hospitalini tunaenda kutafuta matibabu. Lakini kujua chanzo cha ugonjwa ni juhudi zako binafsi. Hivi kweli unaweza kuuliza chanzo cha ugonjwa wa Malaria, Kipindupindu, HIV?

Ni rahisi sana kuvijua karne hii ya utandawazi kama hukuvijua darasani
 
Back
Top Bottom