Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Serikali imekurupuka na pengine sitafanya makosa kusema wana kiherehere kwa kuharakisha kuzima mfumo wa analogia wa Television, maana muda vifaa vya Digital vianze kupatikana ni mfupi mno na hivyo kushindwa kutoa nafasi ya kutosha kwa walio wengi kuingia kwenye mfumo huo mpya, ukitilia maana elimu, nafasi ya kutosha kuingia kwenye mfumo mpya, kiwango cha kuelewa na hali kadhali hali ya uchumi ya wananchi walio wengi haikutiliwa maanani.
Mabadiliko yanapotokea kutoka mfumo mmoja na kuingia mfumo mwingine huwa kunakuwepo kipindi cha kutosha ili wananchi wawe tayari kuingia kwenye mfumo mpya ikiwa ni pamoja na
- utoaji elimu,
- ufahamu wa watumiaji,
- upatikanaji wa vifaa vya mfumo mpya kuhodhiwa na idadi kubwa ya watumiaji,
- kupima uwezo wa walio wengi kiuchumi kuwa na muda wa kutosha kukusanya nguvu ya kupata vifaa vya mfumo mpya.
Kasumba inasababisha mateso kwa wananchi
Tunaiga nchi zilizoendelea, hata hivyo hazikuchukua hatua haraka hivyo licha ya kuwa na option nyingi kwa watumiaji wa analogia system nchi hizo ziliamua kugeukia upande wa Digital baada ya kuona wali wengi ni watumiaji wa kubwa wa mfumo wa digital kama ifuatavyo:
- Kuna watumiaji wa Cable TV network ambapo nchi nyingi za mataifa ya magharibi kila nyumba lazima iwe na: Installed Electric power, Installed Telephone line, Installed Cable TV kabla haijasajiliwa kupata kibali cha makazi.
- Watumiaji wa TV kupitia Telephone line
- Watumiaji wengi wa Dish Network
- Watumiaji wachache wa Analogia Network
Uingiaji kwenye mfumo wa Digital umechukuwa muda mrefu tangu utangazwe kama ilivyotokea nchini Marekani, imechukua si pungufu ya miaka mitano hadi kufikia kuzima mfumo wa analogia, hata hivyo kuna baadhi ya state zinatambua na kuendesha mfumo huo wa zamani kwa ajili ya kujali wachache ambao uwezo wao hauruhusu kugharamia mfumo mpya wa digital ikiwa ni pamoja na gharama za upatikanaji wa ving'amuzi, hali kadhalika kuhakikisha huduma hiyo ya television wananchi wahaikosi ni muhimu kwa maisha, uchumi na mawasiliano katima maisha ya kila mwananchi.
Jambo la kushangazi serikali ya Tanzania kuharakisha mfumo huo mpya wakati Tanzania nzima karibu watumiaji ni wale wa mfumo wa analogia na wachache sana pungufu ya 5% tu wenye uwezo ambao wana mfumo wa dish network ambao utaona katika mtaa mmoja ni wawili au mmoja na pengine hakuna. Hii ni kasoro kubwa kwani haiangalii uwezo, nafasi na mazingiara ya watumiaji katika nchi yetu, ila serikali inafikiria tu uwezo wa walicho nacho kama wanaoishi kule mbwa wanakofungiwa ndani ya gati.
Serikali itazame upya na kujali wananchi walio wengi
Pamoja na serikali kuwa na kiburi kutosikiliza kilio cha wananchi, bado nafasi ipo kujali maisha ya wananchi wa kawaida ambao wengi wao mfumo huu elimu yake haijakolea na pia pengine uwezo wao wa kupata ving'amuzi unahitaji kipindi kirefu kutosha ili kupanga matumizi yao pamoja na upatikanaji wa ving'amuzi. Ningeipongeza Tanzania kwa mazingira ya wananchi wengi yalivyo mfumo huo hadi uwafikie wengi ingechukua zaidi ya miaka mitano ili kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya Television inaendelea kuwafikia wengi.
Kinachoendelea ni sifa za kisiasa zaidi kuliko hali halisi ilivyo. Pamoja na chombo cha umoja wa wenye kumiliki vyombo vya habari vya Television kulalamikia athari ambazo zimeshaanza kujitokeza, bado serikali imekuwa na kiburi cha kutosikiliza, ingawa serikali inajua wazi imeshaanza kuonja joto la jiwe kwa Revenue Authority kuanza kupungua mapato toka vyombo vya Television kwa sababu ya matangazo ya biashara kupungua sababu ya mfumo mpya wa digital kutofikia wengi, inaelekea serikali yetu inaendelea na kiburi cha kujali zaidi sifa za kisiasa badala ya heshima wanayotakiwa kujijengea kwa wananchi kwa wananchi wanaowatumikia.