Serikali iache kiburi kulazimisha mfumo wa Digital

Serikali iache kiburi kulazimisha mfumo wa Digital

Ukiingalia kwa undani unakuta ni dili ya watu wachache...ili wapige pesa chap chap, hii ingeachwa iwe katika hali ya soko hulia, chagua unachotaka kutumia. digital/analogia
INVOLVEMENT YA RZ1 KUMESABABISHA HATA WELEDI WA PROF. JOHN nKOMA UPOTEZE MUELEKEO. MZEE HATACONSIOUSNES YAKE INAMPINGA LAKINI AMEKOMAA. HIYO ANALOGUE ALILETA YEYE. HUU UCHURO TUTAWASHUHUDIA HAPHAPA BONGO WAKIHAHA KUMALIZA KESI SI MUDA MRFEU MAMBO YAO YATAKPOKUWA HADHARANI. HII SI BONGO YETU TUNAIJUA
 
INVOLVEMENT YA RZ1 KUMESABABISHA HATA WELEDI WA PROF. JOHN nKOMA UPOTEZE MUELEKEO. MZEE HATACONSIOUSNES YAKE INAMPINGA LAKINI AMEKOMAA. HIYO ANALOGUE ALILETA YEYE. HUU UCHURO TUTAWASHUHUDIA HAPHAPA BONGO WAKIHAHA KUMALIZA KESI SI MUDA MRFEU MAMBO YAO YATAKPOKUWA HADHARANI. HII SI BONGO YETU TUNAIJUA
Nimekusoma Mkuu, nitabu sana!
 
Wakuu mikoa mingi walikuwa hawapati hizi Tv local hadi watumie cable tv au ungo sasa mnasemaje wananchi wengi hawaangalii tena Tv?

Effect kubwa ni Dar lakini mikoani hata hawajui mnalalamika nini!

Twendeni hivi hivi hukutukiboresha huo mfumo mpya na TCRA wajitahidi kuwasimamia vizuri
 
Wakuu mikoa mingi walikuwa hawapati hizi Tv local hadi watumie cable tv au ungo sasa mnasemaje wananchi wengi hawaangalii tena Tv?

Effect kubwa ni Dar lakini mikoani hata hawajui mnalalamika nini!

Twendeni hivi hivi hukutukiboresha huo mfumo mpya na TCRA wajitahidi kuwasimamia vizuri

wewe unasema nini?
Vingamuzi vyenyewe havipo frsh matangazo yanakwamakwama tu ni bora ya analogia
 
Mkuu Candid Scope, hii ni deal ya watu, umesahau ile deal ya vizibiti mwendo wa mabasi? Watu walipiga hela viko wapi sasa? Na kati ya sasa na mwakani tutarajie deal mpya kama mbili au tatu hivi, hizo za mikataba ya wachina sijaziingiza. Watu wanafanya last collection before they quit the office. Na utamu ni kuwa deal zote hizi zinamkono wa magogoni
 
Jambo moja ambalo hujamwelewa mleta mada ni maana nchi kuwa na mfumo wa cable TV, sehemu chache sana zipo kama majaribio lakini si mfumo wa Cable at all. Kwa ambao hawajatembea na kufanya ulinganifu wa maana ya cable TV wataelewa tu kwamba unachosema ndio mfumo.

Kwa Taarifa Cable TV unayosema ni mfumo wa kivigongoji kama
kwenye mada hii hapo juu. Unaweza nionyesha nyaya za Cable TM ambazo zimetandazwa miji yote hata miji uliyoitaja kwamba kila anayetaka ni kuinua simu kuita wamwunganishie? Kama ni huduma ya kitongoji fulani kama ilivyo Kariakoo, magomeni na Ilala jijini Dar huwezi kusema tuna mfumo wa Cable TV. Tunaweza kusema tuna mfumo wa simu na umeme kwa vile kila sehemu mijini na baadhi ya vijiji huduma huyo imetandazwa eneo karibu lote. Hapa ndipo tunaposhindwa kuelewana.

Dish nalo ni la vibosile wachache wenye uwezo hivyo huwezi kusema wote wanatumia wakati ni wachache.

Wewe jamaa hujitambui na hujui unachokiongea. Halafu una ubishi usiokuwa na tija hata kidogo. Sijui kichwa chako kikoje wewe ndugu yangu maana unabishana hata na ukweli, au ndio kujifanya unafahamu sana kuliko wengine. Nimekupa hata hiyo mifano ya kampuni zinazotoa cable transmission bado unabisha. Au unadhani watu hatuzijui cable tv? Eti dish ni la vibosile nani kasema? Acha ubishi usio na manufaa. Jifunze kuelimishwa ndugu yangu usijione kama wewe ndio mjuaji wa kila kitu, unajiaibisha mkuu.
 
Wewe jamaa hujitambui na hujui unachokiongea. Halafu una ubishi usiokuwa na tija hata kidogo. Sijui kichwa chako kikoje wewe ndugu yangu maana unabishana hata na ukweli, au ndio kujifanya unafahamu sana kuliko wengine. Nimekupa hata hiyo mifano ya kampuni zinazotoa cable transmission bado unabisha. Au unadhani watu hatuzijui cable tv? Eti dish ni la vibosile nani kasema? Acha ubishi usio na manufaa. Jifunze kuelimishwa ndugu yangu usijione kama wewe ndio mjuaji wa kila kitu, unajiaibisha mkuu.

800px-HFC_Network_Diagram.svg.png


  • Jaribu tena kusoma kielelezo hicho hapo juu unaweza kuona hoja ninaposimamia, huduma hiyo imesambaa kila kaya mlangoni ambako nguzo za zimesheheni nyaya za huduma za umeme, simu na cable television. Mfumo ninaouonyesha hapa si ya mtaa au kitongoji ila ni mfumo wa nchi nzima unatakiwa uwe na mpango wa namna hiyo ndivyo tunaweza kujiridhisha kwamba tunao mfumo huo.

Kama una uzoefu katika debate hutanirushia madongo. Kuna watu wanaotaka kujifunza mambo kadhaa hapa wanapitia kusoma na kujifunza. Kusipokuwa na haja ya pande mbili kujenga mabishano ya hoja elimu hiyo haitawafikiwa walengwa na walio wengi. Mabishano ya hoja hizi ni elimu kubwa, na pale unapoona hoja inaelekea kupingwa na upande mwingine jua kuna mahala anaposimamia kujenga hoja si shauri ya ubishi tu unaofikiria.

Ukiandaa tesisi yako na kubaki kuiacha mikononi mwa jopo la maprofesa bila kujenga hoja za utetezi halitakuwa kosa la maprofesa to under-credit your performance education, ni tatizo lako mwenyewe kutojizatiti kuitetea. Hivyo kuna kitu ninachokiona kwamba hakija kamilika kuwa na mfumo kamili wa unachosema, ila ni watu au makampuni yanayojaribu kuingiza mfumo usiokamilika.

Ndio maana nilikuuliza kama mfumo huo upo rasmi
  • ye yote anaweza kutuma maombi ya kuunganishiwa huduma hiyo nyumbani kwake?
Hujanijibu hio.
Maana yake ni mtaa fulani au kitongoji fulani jamaa kaweka dishi lake na kusambaza kwa majirani. Kama huduma hiyo ingekuwa rasmi nyaya za cable talevision zingesambaa kila kuliko sambazwa nyaya za umeme na simu kwenye milingoti na kila atakaye angeunganishiwa bila kuambiwa hiyo huduma inapatikana masaki tu, maana yake ni kitongoji fulani kule si jiji lote.

Tusidanganyane huduma hiyo bado na kinachofanyika ni kama majaribu ya kiwango kidogo sana ambacho si huduma iliyosambazwa kwa wananchi walio wengi. Ni sawa na wale wanaoshare network ya dish lake kwa majirani kadhaa kwa masikilizano, hivyo hizo kampuni hazijaweka huduma hiyo kwa kiwango rasmi cha kufanya Cable Television network nchini, bali ni kama majaribio tu.

Kuweka network ya Cable Television kwa nchi nzima si kazi ndogo, ni sawa na gharama za kusafirisha nyaya za umeme au simu nchi nzima au tusema tu hata mijini. Kazi bado ndugu yangu
Maboso.
 
Kuna mambo yanayoshawishi watu kuamini kuwa kuna mazingira ya ufisadi wa kutisha katika Tanzania kukimbilia (na kulazimisha) mfumo wa digitali. Kwa mfano, ni kwanini watu wanalazimishwa kununua decoders (ni ving'amuzi au?) kutoka makampuni yanayouza matangazo ya televisheni badala ya serikali kuacha wafanyabiashara waagize digital converter boxes na kuwauzia watu? Hapa mambo mawili yalitakiwa kufanyika. Serikali aidha ingeondoa kodi kwa hizo converter boxes au ingetoa ruzuku kwa njia ya kuponi (vouchers) ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanamudu kununua vifaa hivyo. Ni kweli mfumo wa digitali ni bora zaidi ya ule wa analogia, lakini una faida gani kama asilimia 80 ya watu wenye televisheni Dar es Salaam hawapati matangazo kwa wakati huu?
 
Tatizo la hivi ving'amuzi si wananchi bali TCRA hawakuwa wamrjiandaa na hiyo digitali yao. Sasa hivi mimi sipati stesheni za ndani napata za nje. Nataka nifuatilie habari za nyumbani lakini nimenyimwa hii fursa. Bora turudi analogi hadi TCRA watakapokuwa tayari.
images
ANALOGIA VS DIGITAL
clip_installconverterbox.jpg

Serikali imekurupuka na pengine sitafanya makosa kusema wana kiherehere kwa kuharakisha kuzima mfumo wa analogia wa Television, maana muda vifaa vya Digital vianze kupatikana ni mfupi mno na hivyo kushindwa kutoa nafasi ya kutosha kwa walio wengi kuingia kwenye mfumo huo mpya, ukitilia maana elimu, nafasi ya kutosha kuingia kwenye mfumo mpya, kiwango cha kuelewa na hali kadhali hali ya uchumi ya wananchi walio wengi haikutiliwa maanani.
Mabadiliko yanapotokea kutoka mfumo mmoja na kuingia mfumo mwingine huwa kunakuwepo kipindi cha kutosha ili wananchi wawe tayari kuingia kwenye mfumo mpya ikiwa ni pamoja na
  • utoaji elimu,
  • ufahamu wa watumiaji,
  • upatikanaji wa vifaa vya mfumo mpya kuhodhiwa na idadi kubwa ya watumiaji,
  • kupima uwezo wa walio wengi kiuchumi kuwa na muda wa kutosha kukusanya nguvu ya kupata vifaa vya mfumo mpya.

Kasumba inasababisha mateso kwa wananchi
Tunaiga nchi zilizoendelea, hata hivyo hazikuchukua hatua haraka hivyo licha ya kuwa na option nyingi kwa watumiaji wa analogia system nchi hizo ziliamua kugeukia upande wa Digital baada ya kuona wali wengi ni watumiaji wa kubwa wa mfumo wa digital kama ifuatavyo:

  1. Kuna watumiaji wa Cable TV network ambapo nchi nyingi za mataifa ya magharibi kila nyumba lazima iwe na: Installed Electric power, Installed Telephone line, Installed Cable TV kabla haijasajiliwa kupata kibali cha makazi.
  2. Watumiaji wa TV kupitia Telephone line
  3. Watumiaji wengi wa Dish Network
  4. Watumiaji wachache wa Analogia Network
Imefikia wakati watumiaji wa analogia Network ni wachache sana, hilo likafanya kubadili mfumo huo na kuingia mfumo wa Digital hata hivyo ulipewa kipindi kirefu hadi wananchi wawe tayari kuingia kwenye mfumo huo kipindi ambacho minimum ni miaka mitano.

Uingiaji kwenye mfumo wa Digital umechukuwa muda mrefu tangu utangazwe kama ilivyotokea nchini Marekani, imechukua si pungufu ya miaka mitano hadi kufikia kuzima mfumo wa analogia, hata hivyo kuna baadhi ya state zinatambua na kuendesha mfumo huo wa zamani kwa ajili ya kujali wachache ambao uwezo wao hauruhusu kugharamia mfumo mpya wa digital ikiwa ni pamoja na gharama za upatikanaji wa ving'amuzi, hali kadhalika kuhakikisha huduma hiyo ya television wananchi wahaikosi ni muhimu kwa maisha, uchumi na mawasiliano katima maisha ya kila mwananchi.

Jambo la kushangazi serikali ya Tanzania kuharakisha mfumo huo mpya wakati Tanzania nzima karibu watumiaji ni wale wa mfumo wa analogia na wachache sana pungufu ya 5% tu wenye uwezo ambao wana mfumo wa dish network ambao utaona katika mtaa mmoja ni wawili au mmoja na pengine hakuna. Hii ni kasoro kubwa kwani haiangalii uwezo, nafasi na mazingiara ya watumiaji katika nchi yetu, ila serikali inafikiria tu uwezo wa walicho nacho kama wanaoishi kule mbwa wanakofungiwa ndani ya gati.

Serikali itazame upya na kujali wananchi walio wengi
Pamoja na serikali kuwa na kiburi kutosikiliza kilio cha wananchi, bado nafasi ipo kujali maisha ya wananchi wa kawaida ambao wengi wao mfumo huu elimu yake haijakolea na pia pengine uwezo wao wa kupata ving'amuzi unahitaji kipindi kirefu kutosha ili kupanga matumizi yao pamoja na upatikanaji wa ving'amuzi. Ningeipongeza Tanzania kwa mazingira ya wananchi wengi yalivyo mfumo huo hadi uwafikie wengi ingechukua zaidi ya miaka mitano ili kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya Television inaendelea kuwafikia wengi.

Kinachoendelea ni sifa za kisiasa zaidi kuliko hali halisi ilivyo. Pamoja na chombo cha umoja wa wenye kumiliki vyombo vya habari vya Television kulalamikia athari ambazo zimeshaanza kujitokeza, bado serikali imekuwa na kiburi cha kutosikiliza, ingawa serikali inajua wazi imeshaanza kuonja joto la jiwe kwa Revenue Authority kuanza kupungua mapato toka vyombo vya Television kwa sababu ya matangazo ya biashara kupungua sababu ya mfumo mpya wa digital kutofikia wengi, inaelekea serikali yetu inaendelea na kiburi cha kujali zaidi sifa za kisiasa badala ya heshima wanayotakiwa kujijengea kwa wananchi kwa wananchi wanaowatumikia.
 
Si tunataka kuona Mjengoni live, huenda huu ndio mpango. Kipofu usimpige mnyang'anye fimbo!!!!!!
 
Back
Top Bottom