Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
- Thread starter
- #21
Mkuu,
Ni mikoa ipi ambayo umetembea na ukaona asilimia kubwa wanatumia analogy? Nimekupa mfano wa mikoa ambayo mimi nina uhakika nayo kuwa analogy huko haijawa succsesful. Mfano Iringa, Mbeya, Mwanza, Kagera na Mara. Huko watu wanatumia zaidi satellite dish na cable tv, wewe unachobisha ni nini. Iringa asilimia kubwa ni dish uwe mjini au kijijini. Mbeya nako vivyo hivyo. Mwanza wanatumia dish na cable tv. Kuna watu kama Mwanza Satellite, Barmedas Tv, Ghana Tv wanasupply sehemu kubwa ya jiji la Mwanza, halafu wewe unasema eti makubaliano ya watu watatu, si kweli mkuu hujafanya research na ndio maana nasema yawezekana wewe anaiangalia DSM ukahisi na mikoani ni hivyo hivyo.
Kigoma pekee sijatia mguu wala kunusa hewa yake, hali kadhalika Tanzania visiwani, lakini mikoa mingine yote iliyobaki hakuna pakunidanganya nimekoroga kote.
Kwa mtazamo wa huduma za jamii hatuhesabu mtaa au kitongoji fulani nani ana dish network au kutumia converter box, tunachoangalia huduma hiyo imesambaa kwa wananchi wote. Kinachoendelea hapa ni kuangalia huduma iliyofikiwa kwa wachache wakati walio wengi pengine uwezo huo hawana, na zaidi waliojitahidi kuanza kuitumia sasa mfumo huo mpya unafanya warudie maisha ya zamani kupata habari kwa kutumia redio tu.