Serikali haina uzalendo, inajiibia yenyewe; ushahidi huu hapa!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,852
18,264
Habari za leo ndugu wakuu! Nawasalimu kwa jina la JMT. Baada ya salamu naomba niingie kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Nafahamu wengi wenu hampendi kusoma habari ndefu. Nitajitahidi kufupisha kadri nitakavyoweza.

Imenichukua muda kutafakari kwa kina juu ya ufisadi wa kutisha unaofanywa na watu waliopewa dhamana ya kulinda amana za taifa unaojidhihirisha sio tu kwa serikali ya mama Samia bali serikali zilizotangulia chini ya utawala wa CCM.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa taarifa zilizojaa ufisadi wa kutisha lakini sio wananchi wanaokemea wala serikali inayochukua hatua kuziba mianya hii ya ufisadi bali imebaki kuwa business as usual na mijizi imeendelea kupiga hela za umma bila kumuogopa mtu yeyote. CAG amekuwa kama mbwa anayebweka tu bila kuuma.
1680974426849.png

Mwandishi wa habari nguli, Jenerali Ulimwengu, aliwahi kusema kuwa CCM ni ukoo wa panya; yaani babu mwizi, baba mwizi, mtoto mwizi, mjukuu mwizi, kining’ina mwizi, kilembwe mwizi, na kilembwelezi naye mwizi sawia! Sasa nimeanza kuamini bila kusita kuwa CCM ni kama kansa inayolitafuna taifa kimyakimya huku watanzania, kama kawaida yetu, tukichekelea kama mazuzu tuliobadilisha dhahabu kwa kipande cha cha chupa. Hivi nchi hii imerogwa na nani hasa? Mbona tunaibiana kijinga kiasi hiki? Wananchi mnatuonaje lakini?

Nakumbuka Rais Jomo Kenyatta aliwahi kumwambia Mwalimu Nyerere kuwa yeye (Nyerere) anaongoza kwa raha kwa kuwa anaongoza watu wenye akili kama za maiti. Hili linaweza kuchukuliwa kama tusi na baadhi ya watu lakini huu ndio ukweli ambao hauwezi kupingwa na mtu yeyote mwenye akili timilifu. Watanzania ndivyo tulivyo kama anavyopenda kusema mwanaJF Nyani Ngabu kwamba “mitanzania ndivyo ilivyo”. Tumerogwa.

Kwa ufupi, ufasaha na bila kuwachosha, baada ya kutafakari kwa kina kuhusu jambo hili la ufisadi nimegundua kuwa mwenendo wa serikali usipobadilika, ufisadi hauwezi kuisha kamwe. Wizi mwingi unaofanyika unachochewa na serikali kwa namna moja au nyingine. Nitaeleza kwa ufupi kama ifuatavyo:

1. Matamshi ya Serikali
Sote tunafahamu kuwa Rais wa nchi anapotamka jambo au kutoa kauli yoyote, kauli hiyo huchukuliwa kama sheria. Mtakumbuka siku za karibuni Rais Samia alisema “kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake”, hivyo matamshi haya, kwa kiasi kikubwa, yalichochea vitendo vya ufisadi hapa nchini. Ndio maana ripoti ya CAG safari hii imekuwa na ufisadi mwingi kuliko mwaka wowote katika historia ya nchi. Ni kwa sababu ya kauli hii ya Rais Samia kuwaruhusu wezi kuiba rasilimali za taifa kadri wanavyotaka.

Ukimsikiliza vizuri mama, anasema yeye anajua watu wanakula fedha za umma lakini amewaacha wale kulingana na urefu wa kamba yao. Hawachukuliii hatua yoyote. Na kibaya zaidi hajawawekea kiwango cha ulaji wanachotakiwa kula.

Afadhali Magufuli yeye aliweka kiwango cha Tsh 5000 kwa askari kula rushwa ya kung’arishia viatu kuliko mama alivyowaruhusu mafisadi watafune wanavyojisikia bila kuwawekea kima cha chini.

2. Unyonyaji wa wafanyakazi kupitia kikokotoo cha kishetani
Wafanyakazi, hasa katika sekta ya umma, wanajua fika kuwa mafao yao yameporwa na serikali kupitia kuanzishwa kwa sheria ya kikokotoo inayoipa serikali jeuri ya kuchota mafao ya wafanyakazi kwa 67% huku wafanyakazi wawakiambulia 33% kipindi wanapostaafu.

Sote tulishuhudia jinsi wafanyakazi walivyoangua vilio kipindi Bunge tukufu la JMT linapitisha uporaji huu kuwa sheria mpaka Magufuli akaingilia kati kwa kusitisha utekelezaji wa sheria hii ya kishetani hadi 2023 lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Samia akaamua kupuuzia agizo la Magufuli na kuanza utekelezaji wake kwa kukandamiza haki za wafanyakazi mnamno mwaka 2021.

Kutekelezwa kwa sheria hii kumeitia serikali kitanzini kwa namna mbili:

(i) Laana kwa serikali na nchi. Nchi hii imelaaniwa kwa sababu ya kupora jasho la wafanyakazi wanyonge wanaoitumikia nchi kwa moyo mkunjufu bila kuchoka. Fikiria mtu anaitumikia nchi kwa zaidi ya miaka 30 lakini akistaafu hana mafao. Hii ni laana kubwa sana ambayo itaendelea kuitafuna nchi hadi Yesu atakaporudi.

(ii) Kwa kuwa wafanyakazi hawana mafao ndio maana wanaamua kujichotea mafao yao kwa njia ya ufisadi na kuwekeza ili watakapostaafu wawe na miradi ya kufanya, kama ilivyokuwa kabla mafao yao kuporwa na serikali tukufu ya CCM. Na ufisadi huu utaendelea daima dawamu hadi serikali itakapogundua ilipojikwa na kufanya matengenezo yatakayotibu majeraha ya wafanyakazi wanaoishi kama watumwa.

Tukumuke sababu ya serikali kutunga sheria hii ya kishetani ni kutokana mifuko ya hifadhi ya jamii kufilisika kwa sababu ya serikali kutolipa madeni ya nyuma na kutopeleka michango ya wafanyakazi inayopaswa kuchangia.

Pia serikali imekopa matrilioni ya fedha kutoka kwenye mifuko kwa muda mrefu bila kuzirejesha. Kwani mifuko hii ni mabenki hadi serikali ije kukopa huku badala ya kukopa benki? Ni kwa sababu ni rahisi serikali kuchota fedha hizi za wastaafu bila kuhojiwa na mtu yeyote ndio maana wanakimbilia huku. Basi kwa maana hiyo serikali itaendelea kuibiwa na wafanyakazi kwa kulipiza kisasi hadi itakapochukua uamuzi wa kufanya matengenezo. Tit fo tat is a fair play.

3. NHIF
Ufisadi kwenye mfuko wa matibabu wa NHIF kwa 90% umesababishwa na serikali ya CCM. Kuna namna 3 ambazo serikali imehusika hapa:

(i) Katika kuchangia huduma za matibabu, serikali inapaswa kuchangia 3% na mtumishi wa umma 3%. Kwa miaka zaidi ya 5, serikali imesitisha uchangiaji huu wa kisheria bila sababu za msingi hivyo kupelekea NHIF kujiendesha kwa naksi. Na endapo serikali itaendelea na ukaidi wake wa kutochangia, miaka sio mingi NHIF itakufa kifo cha mende hivyo kupelekea wananchama wanaotegemea mfuko huu kufa kwa wingi kutokana na maradhi yanayoweza kutibika.

(ii) Serikali ililazimisha wananchi watibiwe kwa Tsh 40,000 kwa mwaka (CHF iliyoboreshwa) na wanafunzi kutibiwa kwa Tsh 54,000 kwa mwaka huku wakijua fika kwamba kiasi hiki hakiwezi kukidhi kugharamia huduma za matibabu kwa mwanachama kwa mwaka mmoja. Matokeo yake watu wanatibiwa kwa pesa nyingi kuliko michango inayoingia.

(iii) Ni muda mrefu sasa serikali imekuwa ikichota matrilioni ya pesa kutoka mfuko huu pasipo kurejesha, kwa kisingizio cha kukopa. Wanakopaje fedha za michango ya wagonjwa badala ya kukopa benki? Yakhe hawana khaya? Serikali inafanya ujinga mkubwa sana kukopa fedha za wagonjwa badala ya kwenda kukopa benki. Hii ni sawa na kuchukua damu kutoka kwa mtu mwenye upungufu wa damu. hatimaye watamuua kabisa.

Ufisadi huu uliofanywa na serikali katika mfuko wa NHIF umepelekea mfuko kuwa na naksi kubwa kwenye matumizi yake hivyo kuonekana kuwa fedha nyingi zinapotea na kushindwa kujiendesha kwa faida. Chanzo kikuuu cha ufisadi huu ni serikali tukufu ya CCM.

4. Kuingilia kazi na utendaji wa vyama vya wafanyakazi
Ni muda mrefu sasa serikali imekuwa ikichomekea makada kwenye vyama vya wafanyakazi ili kuwavurugia wafanyakazi michakato ya kudai maslahi yao ya msingi. Humu ndani kuna uzi niliowahi kuandika kinagaubaga kuhusu suala hili. Hebu jisomee mwenyewe hapa

Ushahidi wa pili kuhusu serikali kuingilia vyama vya wafanyakazi kwa maslahi ya kuvikandamiza na kuvidumaza umejidhihirisha hivi karibuni ambapo Rais aliwateua kuwa wakuu wa wilaya makada watatu wa CCM waliokuwa wamewachomekwa kwenye chama cha walimu (CWT). Makada hao ni Rais wa CWT, Leah Ulaya na Katibu Mkuu Japhet Maganga ambao waligomea uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi za Ukuu wa wilaya wakitaja kuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho. Kada wa tatu alikubali uteuzi na hivi sasa anatumikia cheo chake kipya.

Makada hawa hawakuingia CWT kwa bahati mbaya bali walichomekwa kwa makusudi na serikali ya CCM ili kuleta migogoro ndani ya chama na kuwagawanya wafanyakazi washindwe kutetea maslahi yao ya msingi.

Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hizi ndizo baadhi ya namna ambazo serikali ya CCM imekuwa ikijiibia yenyewe kwa makusudi bila kujua madhara yanayosababishwa na huu mwenendo.

Nawasilisha.
 
Hapana serikali haijiibi bali inaiba hela ya wananchi. Serikali ikiiba kimyaaa, mwananchi akiiba mwizi(si mzalendo). Leo mkuu wa polisi kakimbia na mabillioni sasa nikiimbiwa kwangu nimwite nani kwa kunipa msaada wa kumkamata mwizi??
 
Habari za leo ndugu wakuu! Nawasalimu kwa jina la JMT. Baada ya salamu naomba niingie kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Nafahamu wengi wenu hampendi kusoma habari ndefu. Nitajitahidi kufupisha kadri nitakavyoweza.

Imenichukua muda kutafakari kwa kina juu ya ufisadi wa kutisha unaofanywa na watu waliopewa dhamana ya kulinda amana za taifa unaojidhihirisha sio tu kwa serikali ya mama Samia bali serikali zilizotangulia chini ya utawala wa CCM.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa taarifa zilizojaa ufisadi wa kutisha lakini sio wananchi wanaokemea wala serikali inayochukua hatua kuziba mianya hii ya ufisadi bali imebaki kuwa business as usual na mijizi imeendelea kupiga hela za umma bila kumuogopa mtu yeyote. CAG amekuwa kama mbwa anayebweka tu bila kuuma.
View attachment 2581332
Mwandishi wa habari nguli, Jenerali Ulimwengu, aliwahi kusema kuwa CCM ni ukoo wa panya; yaani babu mwizi, baba mwizi, mtoto mwizi, mjukuu mwizi, kining’ina mwizi, kilembwe mwizi, na kilembwelezi naye mwizi sawia! Sasa nimeanza kuamini bila kusita kuwa CCM ni kama kansa inayolitafuna taifa kimyakimya huku watanzania, kama kawaida yetu, tukichekelea kama mazuzu tuliobadilisha dhahabu kwa kipande cha cha chupa. Hivi nchi hii imerogwa na nani hasa? Mbona tunaibiana kijinga kiasi hiki? Wananchi mnatuonaje lakini?

Nakumbuka Rais Jomo Kenyatta aliwahi kumwambia Mwalimu Nyerere kuwa yeye (Nyerere) anaongoza kwa raha kwa kuwa anaongoza watu wenye akili kama za maiti. Hili linaweza kuchukuliwa kama tusi na baadhi ya watu lakini huu ndio ukweli ambao hauwezi kupingwa na mtu yeyote mwenye akili timilifu. Watanzania ndivyo tulivyo kama anavyopenda kusema mwanaJF Nyani Ngabu kwamba “mitanzania ndivyo ilivyo”. Tumerogwa.

Kwa ufupi, ufasaha na bila kuwachosha, baada ya kutafakari kwa kina kuhusu jambo hili la ufisadi nimegundua kuwa mwenendo wa serikali usipobadilika, ufisadi hauwezi kuisha kamwe. Wizi mwingi unaofanyika unachochewa na serikali kwa namna moja au nyingine. Nitaeleza kwa ufupi kama ifuatavyo:

1. Matamshi ya Serikali
Sote tunafahamu kuwa Rais wa nchi anapotamka jambo au kutoa kauli yoyote, kauli hiyo huchukuliwa kama sheria. Mtakumbuka siku za karibuni Rais Samia alisema “kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake”, hivyo matamshi haya, kwa kiasi kikubwa, yalichochea vitendo vya ufisadi hapa nchini. Ndio maana ripoti ya CAG safari hii imekuwa na ufisadi mwingi kuliko mwaka wowote katika historia ya nchi. Ni kwa sababu ya kauli hii ya Rais Samia kuwaruhusu wezi kuiba rasilimali za taifa kadri wanavyotaka.

Ukimsikiliza vizuri mama, anasema yeye anajua watu wanakula fedha za umma lakini amewaacha wale kulingana na urefu wa kamba yao. Hawachukuliii hatua yoyote. Na kibaya zaidi hajawawekea kiwango cha ulaji wanachotakiwa kula.

Afadhali Magufuli yeye aliweka kiwango cha Tsh 5000 kwa askari kula rushwa ya kung’arishia viatu kuliko mama alivyowaruhusu mafisadi watafune wanavyojisikia bila kuwawekea kima cha chini.

2. Unyonyaji wa wafanyakazi kupitia kikokotoo cha kishetani
Wafanyakazi, hasa katika sekta ya umma, wanajua fika kuwa mafao yao yameporwa na serikali kupitia kuanzishwa kwa sheria ya kikokotoo inayoipa serikali jeuri ya kuchota mafao ya wafanyakazi kwa 67% huku wafanyakazi wawakiambulia 33% kipindi wanapostaafu.

Sote tulishuhudia jinsi wafanyakazi walivyoangua vilio kipindi Bunge tukufu la JMT linapitisha uporaji huu kuwa sheria mpaka Magufuli akaingilia kati kwa kusitisha utekelezaji wa sheria hii ya kishetani hadi 2023 lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Samia akaamua kupuuzia agizo la Magufuli na kuanza utekelezaji wake kwa kukandamiza haki za wafanyakazi mnamno mwaka 2021.

Kutekelezwa kwa sheria hii kumeitia serikali kitanzini kwa namna mbili:

(i) Laana kwa serikali na nchi. Nchi hii imelaaniwa kwa sababu ya kupora jasho la wafanyakazi wanyonge wanaoitumikia nchi kwa moyo mkunjufu bila kuchoka. Fikiria mtu anaitumikia nchi kwa zaidi ya miaka 30 lakini akistaafu hana mafao. Hii ni laana kubwa sana ambayo itaendelea kuitafuna nchi hadi Yesu atakaporudi.

(ii) Kwa kuwa wafanyakazi hawana mafao ndio maana wanaamua kujichotea mafao yao kwa njia ya ufisadi na kuwekeza ili watakapostaafu wawe na miradi ya kufanya, kama ilivyokuwa kabla mafao yao kuporwa na serikali tukufu ya CCM. Na ufisadi huu utaendelea daima dawamu hadi serikali itakapogundua ilipojikwa na kufanya matengenezo yatakayotibu majeraha ya wafanyakazi wanaoishi kama watumwa.

Tukumuke sababu ya serikali kutunga sheria hii ya kishetani ni kutokana mifuko ya hifadhi ya jamii kufilisika kwa sababu ya serikali kutolipa madeni ya nyuma na kutopeleka michango ya wafanyakazi inayopaswa kuchangia.

Pia serikali imekopa matrilioni ya fedha kutoka kwenye mifuko kwa muda mrefu bila kuzirejesha. Kwani mifuko hii ni mabenki hadi serikali ije kukopa huku badala ya kukopa benki? Ni kwa sababu ni rahisi serikali kuchota fedha hizi za wastaafu bila kuhojiwa na mtu yeyote ndio maana wanakimbilia huku. Basi kwa maana hiyo serikali itaendelea kuibiwa na wafanyakazi kwa kulipiza kisasi hadi itakapochukua uamuzi wa kufanya matengenezo. Tit fo tat is a fair play.

3. NHIF
Ufisadi kwenye mfuko wa matibabu wa NHIF kwa 90% umesababishwa na serikali ya CCM. Kuna namna 3 ambazo serikali imehusika hapa:

(i) Katika kuchangia huduma za matibabu, serikali inapaswa kuchangia 3% na mtumishi wa umma 3%. Kwa miaka zaidi ya 5, serikali imesitisha uchangiaji huu wa kisheria bila sababu za msingi hivyo kupelekea NHIF kujiendesha kwa naksi. Na endapo serikali itaendelea na ukaidi wake wa kutochangia, miaka sio mingi NHIF itakufa kifo cha mende hivyo kupelekea wananchama wanaotegemea mfuko huu kufa kwa wingi kutokana na maradhi yanayoweza kutibika.

(ii) Serikali ililazimisha wananchi watibiwe kwa Tsh 40,000 kwa mwaka (CHF iliyoboreshwa) na wanafunzi kutibiwa kwa Tsh 54,000 kwa mwaka huku wakijua fika kwamba kiasi hiki hakiwezi kukidhi kugharamia huduma za matibabu kwa mwanachama kwa mwaka mmoja. Matokeo yake watu wanatibiwa kwa pesa nyingi kuliko michango inayoingia.

(iii) Ni muda mrefu sasa serikali imekuwa ikichota matrilioni ya pesa kutoka mfuko huu pasipo kurejesha, kwa kisingizio cha kukopa. Wanakopaje fedha za michango ya wagonjwa badala ya kukopa benki? Yakhe hawana khaya? Serikali inafanya ujinga mkubwa sana kukopa fedha za wagonjwa badala ya kwenda kukopa benki. Hii ni sawa na kuchukua damu kutoka kwa mtu mwenye upungufu wa damu. hatimaye watamuua kabisa.

Ufisadi huu uliofanywa na serikali katika mfuko wa NHIF umepelekea mfuko kuwa na naksi kubwa kwenye matumizi yake hivyo kuonekana kuwa fedha nyingi zinapotea na kushindwa kujiendesha kwa faida. Chanzo kikuuu cha ufisadi huu ni serikali tukufu ya CCM.

4. Kuingilia kazi na utendaji wa vyama vya wafanyakazi
Ni muda mrefu sasa serikali imekuwa ikichomekea makada kwenye vyama vya wafanyakazi ili kuwavurugia wafanyakazi michakato ya kudai maslahi yao ya msingi. Humu ndani kuna uzi niliowahi kuandika kinagaubaga kuhusu suala hili. Hebu jisomee mwenyewe hapa

Ushahidi wa pili kuhusu serikali kuingilia vyama vya wafanyakazi kwa maslahi ya kuvikandamiza na kuvidumaza umejidhihirisha hivi karibuni ambapo Rais aliwateua kuwa wakuu wa wilaya makada watatu wa CCM waliokuwa wamewachomekwa kwenye chama cha walimu (CWT). Makada hao ni Rais wa CWT, Leah Ulaya na Katibu Mkuu Japhet Maganga ambao waligomea uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi za Ukuu wa wilaya wakitaja kuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho. Kada wa tatu alikubali uteuzi na hivi sasa anatumikia cheo chake kipya.

Makada hawa hawakuingia CWT kwa bahati mbaya bali walichomekwa kwa makusudi na serikali ya CCM ili kuleta migogoro ndani ya chama na kuwagawanya wafanyakazi washindwe kutetea maslahi yao ya msingi.

Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hizi ndizo baadhi ya namna ambazo serikali ya CCM imekuwa ikijiibia yenyewe kwa makusudi bila kujua madhara yanayosababishwa na huu mwenendo.

Nawasilisha.
Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hizi ndizo baadhi ya namna ambazo serikali ya CCM imekuwa ikijiibia yenyewe kwa makusudi bila kujua madhara yanayosababishwa na huu mwenendo.
 
Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hizi ndizo baadhi ya namna ambazo serikali ya CCM imekuwa ikijiibia yenyewe kwa makusudi bila kujua madhara yanayosababishwa na huu mwenendo.
Unadhani Fedha ya kampeni wanapata wapi?kampeni za ccm ni very expensive
 
Tatizo hapo ni udhaifu wa kiongozi tuliyenaye, huo mfano wa hiyo kauli yake aliyoitoa ya kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, naamini hapo ndipo alipofungulia mbwa rasmi, sasa tunaumizwa tu.

Rais anayejidai kukomaa na wapinzani kwa kusema wakimpara atawaparua, huku akiwaacha wenzie ndani ya chama waendelee kujigeuza mbwa mwitu, watutafune watanzania bila aibu, huku akitoa kauli nyepesi kwa wezi kama "stupid" au "watupishe", huyu hatoshi kukalia ikulu yetu, vyema atupishe yeye.
 
Kweli kabisa mkuu. Hili nalo tatizo.
 
Back
Top Bottom