Serikali-Bima ya Afya kwa wote inawezekana kwa kila mwananchi kutoa shilingi 5,000 kwa mwaka

Kwa nini wasitumie tozo kama kigezo cha kukusanya pesa kwa ajili ya bima ya mtu. Hizi tozo wanazotukata kikifika kiasi cha pesa kutosha kukata bima unatumiwa ujumbe ukafate bima yako ofisi fulani. Itaongeza ushawishi kwa watu kuendelea kutumia mobile financial service.
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Kila mtu ni mhanga wa ughali wa gharama za matibabu,tumeshuhudia jamii zikipata mgonjwa wa mda mrefu zinavyofirisika kwa kuuza kila mali yao Ili kugharamia matibabu ya mgonjwa na pengine asipone.

Kwa muktadha huo,wananchi wako tayari kuchangia walau sh.4,000-5,000 kwa kichwa kwa kila mwaka Ili kupata pesa za kuwa na bima.

Kwa kuwa wananchi wako tayari kulipa Serikali iandae sheria ya bima ya Afya kwa wote yaani universal healthcare act na Mfuko wa bima ya Afya ndio uratibu moja kwa moja jambo hili.

Ikiwa kila mwananchi au kichwa kitatoa sh.4,000 kwa mwaka kwa watu 60,000 serikali itapata wastani wa Trilioni 3 Kwa mwaka pesa ambazo ni mara mbili ya bajeti ya Wizara ya Afya.

5,000*60,000=3.E8.

Ikiwa watu walilipishwa sh.20,000 kwa kununua vile viliitwa vitambulisho vya ujasiliamali na pesa ikapatikana ni dhahiri kwa wazo kama hili wananchi wataliunga mkono maana kila mtu atalipa kwa idadi ya watoto alionao.

Kila una watoto 6 utalipia hivyo hivyo,kama wako 10 utalipia watoto kumi.Lakini makundi maalumu kama walemavu, watoto wa mitaani,wazee na watu wengine maskini Sana watalipiwa na Serikali kuu na makundi mengine kama vile wafanyakazi ambao hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi ambao wao wataendelea kukatwa kila mwezi ila viwango vitashushwa kutoka 3% to 1% .

Aidha pesa ziwe ni mahsusi kwa ajili ya dawa,vitenganishi na vifaa tiba vya kisasa wakati huo huo bajeti ya Wizara ya kawaida itaendelea kuwepo kama kawaida Ili kuzalisha wataalamu,maslahi Bora kwa watumishi,utawala na kugharamia ujenzi wa miundombinu mipya.

Utaratibu huu ukianzishwa hatutegemei tena kusikia eti ugonjwa fulani ni gharama sana na hivyo watu wachangie.Kila ugonjwa utakuwa ndani ya bima.Kama Til.1.5 ya covid imejenga madarasa 15,000 nchi nzima,imejenga majengo ya emergency,imejenga masoko ya machinga,imeleta maji,imenunua ambulance,x-rays,MRI nk ni wazi zikipatikana japo til.2.5 zitaleta mapinduzi kwenye sekta ya Afya Nchini.

Ni vyema serikali iamue sasa kuleta mjadala huu kwa umma na iweke utaratibu mzuri wa kulipa hizo pesa kwa njia ya mitandao ya simu na Benki Ili tuanze rasmi kuwa na bima ya Afya kwa wote.

Kiukweli gharama za matibabu zinaumiza na zinafukarisha Sana,tunaomba serikali ichukue hili wazo kwa sababu halihitaji pesa ya serikali bali pesa itatoka kwa sisi wananchi moja kwa moja.
Umeshakosea hesabu... hiyo hesabu yako ni milioni 300, kwa hiyo jipange kuweka hoja vizuri, aidha kuongeza gharama ili ifike Trilioni 3 au kuongeza watu
 
The Sunk Cost Fallacy
Wazo lako zuri, lakini hebu Cross check hizo hesabu zako hapo...

Trillion tatu haiwezi kupatikana kutoka katika watu elfu 60 wanaochanga elfu 5 kila mmoja kwa mwaka.
60,000 * 5,000 = 300,000,000 (M 300)

Ili kupata Trillion 3 kwa mwaka kwa michango ya shilingi 5,000 unahitaji watu milioni mia sita.
Watu mil.60 multiplied by tsh.5,000 Unapata Trilioni 3.
 
Kwa nini wasitumie tozo kama kigezo cha kukusanya pesa kwa ajili ya bima ya mtu. Hizi tozo wanazotukata kikifika kiasi cha pesa kutosha kukata bima unatumiwa ujumbe ukafate bima yako ofisi fulani. Itaongeza ushawishi kwa watu kuendelea kutumia mobile financial service.
Ndio maana tumesema serikali itaangalia namna nzuri ya kukusanya hiyo pesa.

Kwenye tozo kelele zitakuwa nyingi gharama zikienda juu tofauti na mtu kulipa at once.

Pia kwenye tozo itachukua mda kupata hizo pesa na uhakika utakuwa mdogo kwa sababu sio kila mtu atalipa tofauti na kuweka fixed amount kwa kila mtu .
 
Kwanini msitoe kwenye hayo makato ya simu au muongeze hata mia kwenye mafuta.

Elfu tano juu ya hayo makato,
 
Wewe makato ya simu yako mahsusi kwa ajili ya barabara,afya,maji na elimu .

Pia ni vihela vidogo hata Trilioni moja havifiki kwa mwaka,Afya haihitaji kudunduliza.

Wewe unaeongea hapa ukute ni muajitiwa na una bima ndio maana unachukulia simple tuu.

Lakini pamoja na hiyo bima yako ,magonjwa makubwa haitakusaidia.
 
Watu mil.60 multiplied by tsh.5,000 Unapata Trilioni 3.
Sasa mkuu umeanza kuipanda kichwani Mathematics.

60,000,000 * 5,000 = 300,000,000,000/=
Kwa mujibu wa Hisabati jibu hilo ni sahihi na linasomeka kama BILIONI MIATATU.

Ili upate Trilioni tatu yaani 3,000,000,000,000 unapaswa kuzidisha 600,000,000 * 5,000 au pengine 60,000,000 * 50,000.

Sijui kwanini tunafanya argument kwenye hili, sijui kwa kweli.
 
5000*60,000,000= 300,000,000,000 ni bilion 300 tu siyo trilion 3

Ila ni wazo zuri.

CHF tulichangaia 10% na 90% serikali ikamalizia.

Mkapa alikuwa noma.
 
Mkuu watu wote hawawezi kuwa serious ndio maana ya serikali kuingilia.

Unakuta anatembeza kibarua cha kuomba achangiwe ugonjwa na unakuta mtu anaenda kuomba msaada kwenye vyombo vya habari watu wamchangie.

Case kama ya Prof angekuwa na bima tusingefika huko na ashukuru alikuwa anafahanika sasa maskini wa kijijini si angeshajifia?

Kuchanga sio tatizo bali watu waaminifu wa kuhakikisha huzo Pesa zinatumika kwenye lengo husika. Sio pesa zinaingia kisha rais na genge lake wanaamua kuchota hiyo pesa na kuingiza kwenye miradi ya kusaka political millage, na fedha hizo kubatizwa ni fedha za rais na upuuzi mwingine kama huo. Mfano mifuko ya fedha za mafao ya wafanyakazi, hizo zimechotwa na kuingizwa kwenye miradi ya kusaka sifa za kisiasa, matokeo yake walengwa wanaishia kusotea mafao yao. Una wazo zuri lakini utapeli ni mwingi huko serikalini. Hivyo hakuna mtu kutoa pesa zake kwa majizi ya kura.
 
Muhimu hum badala ya kulipia bando 10000 kwasiku basi jibane usichati kwa wiki 5 mkatie mwanao bima ya afya ya 50,400/= halafu wewe mkeo baba na mama katehi ile ya 30,000/= au 50,000/= kwa familia utakuja kushukuru siku moja utapouguliwa ukiwa huna kitu

Huu ni utapeli mwingine wa kimachomacho. Nina mtoto wa kaka yangu anasoma chuo. Nimemlipia bima ya afya ya 50,400/, juzi ameugua na hakuna bima yoyote imemtibu. Nimeishia kutoa zaidi ya 60,000 kumtibia binafsi. Huo ni utapeli wa wazi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Moja kwa moja kwenye mada.

Kila mtu ni mhanga wa ughali wa gharama za matibabu,tumeshuhudia jamii zikipata mgonjwa wa mda mrefu zinavyofirisika kwa kuuza kila mali yao Ili kugharamia matibabu ya mgonjwa na pengine asipone.

Kwa muktadha huo,wananchi wako tayari kuchangia walau sh.4,000-5,000 kwa kichwa kwa kila mwaka Ili kupata pesa za kuwa na bima.

Kwa kuwa wananchi wako tayari kulipa Serikali iandae sheria ya bima ya Afya kwa wote yaani universal healthcare act na Mfuko wa bima ya Afya ndio uratibu moja kwa moja jambo hili.

Ikiwa kila mwananchi au kichwa kitatoa sh.4,000 kwa mwaka kwa watu 60,000 serikali itapata wastani wa Trilioni 3 Kwa mwaka pesa ambazo ni mara mbili ya bajeti ya Wizara ya Afya.

5,000*60,000,000=3.E11.

Ikiwa watu walilipishwa sh.20,000 kwa kununua vile viliitwa vitambulisho vya ujasiliamali na pesa ikapatikana ni dhahiri kwa wazo kama hili wananchi wataliunga mkono maana kila mtu atalipa kwa idadi ya watoto alionao.

Kila una watoto 6 utalipia hivyo hivyo,kama wako 10 utalipia watoto kumi.Lakini makundi maalumu kama walemavu, watoto wa mitaani,wazee na watu wengine maskini Sana watalipiwa na Serikali kuu na makundi mengine kama vile wafanyakazi ambao hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi ambao wao wataendelea kukatwa kila mwezi ila viwango vitashushwa kutoka 3% to 1% .

Aidha pesa ziwe ni mahsusi kwa ajili ya dawa,vitenganishi na vifaa tiba vya kisasa wakati huo huo bajeti ya Wizara ya kawaida itaendelea kuwepo kama kawaida Ili kuzalisha wataalamu,maslahi Bora kwa watumishi,utawala na kugharamia ujenzi wa miundombinu mipya.

Utaratibu huu ukianzishwa hatutegemei tena kusikia eti ugonjwa fulani ni gharama sana na hivyo watu wachangie.Kila ugonjwa utakuwa ndani ya bima.Kama Til.1.5 ya covid imejenga madarasa 15,000 nchi nzima,imejenga majengo ya emergency,imejenga masoko ya machinga,imeleta maji,imenunua ambulance,x-rays,MRI nk ni wazi zikipatikana japo til.2.5 zitaleta mapinduzi kwenye sekta ya Afya Nchini.

Ni vyema serikali iamue sasa kuleta mjadala huu kwa umma na iweke utaratibu mzuri wa kulipa hizo pesa kwa njia ya mitandao ya simu na Benki Ili tuanze rasmi kuwa na bima ya Afya kwa wote.

Kiukweli gharama za matibabu zinaumiza na zinafukarisha Sana,tunaomba serikali ichukue hili wazo kwa sababu halihitaji pesa ya serikali bali pesa itatoka kwa sisi wananchi moja kwa moja.
Kwa kuongeza tu zitakuwa ni T.25 kila mwaka au zaidi ya hio hela. Malipo yawe kwa control number tu.
 
Ndio maana tumesema serikali itaangalia namna nzuri ya kukusanya hiyo pesa.

Kwenye tozo kelele zitakuwa nyingi gharama zikienda juu tofauti na mtu kulipa at once.

Pia kwenye tozo itachukua mda kupata hizo pesa na uhakika utakuwa mdogo kwa sababu sio kila mtu atalipa tofauti na kuweka fixed amount kwa kila mtu .

Kwanini msiuze hizo raslimali mnazojifanya wazungu wanazionea wivu ili mtoe huduma ya afya bure? Au hizo raslimali huwa mnazitumia kwenye propaganda tu? Acha mawazo ya kutaka wananchi waingizwe mjini. Kauzeni raslimali mnazosema tunazo fullstop.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Muhimu hum badala ya kulipia bando 10000 kwasiku basi jibane usichati kwa wiki 5 mkatie mwanao bima ya afya ya 50,400/= halafu wewe mkeo baba na mama katehi ile ya 30,000/= au 50,000/= kwa familia utakuja kushukuru siku moja utapouguliwa ukiwa huna kitu
Nina swali mkuuu kwa mfano mie nipo huku ukerewe nikikata bima huku mf ya 50400 je nikisema nimehama mie na familia yangu kwenda SONGEA NAMTUMBO JE nitatumia kma kawaida au mpka ndio itakuwa ime kwisha nikajiunge tena songea mkuuu cjui naomba kujuzwa bro
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Kila mtu ni mhanga wa ughali wa gharama za matibabu,tumeshuhudia jamii zikipata mgonjwa wa mda mrefu zinavyofirisika kwa kuuza kila mali yao Ili kugharamia matibabu ya mgonjwa na pengine asipone.

Kwa muktadha huo,wananchi wako tayari kuchangia walau sh.4,000-5,000 kwa kichwa kwa kila mwaka Ili kupata pesa za kuwa na bima.

Kwa kuwa wananchi wako tayari kulipa Serikali iandae sheria ya bima ya Afya kwa wote yaani universal healthcare act na Mfuko wa bima ya Afya ndio uratibu moja kwa moja jambo hili.

Ikiwa kila mwananchi au kichwa kitatoa sh.4,000 kwa mwaka kwa watu 60,000 serikali itapata wastani wa Trilioni 3 Kwa mwaka pesa ambazo ni mara mbili ya bajeti ya Wizara ya Afya.

5,000*60,000,000=3.E11.

Ikiwa watu walilipishwa sh.20,000 kwa kununua vile viliitwa vitambulisho vya ujasiliamali na pesa ikapatikana ni dhahiri kwa wazo kama hili wananchi wataliunga mkono maana kila mtu atalipa kwa idadi ya watoto alionao.

Kila una watoto 6 utalipia hivyo hivyo,kama wako 10 utalipia watoto kumi.Lakini makundi maalumu kama walemavu, watoto wa mitaani,wazee na watu wengine maskini Sana watalipiwa na Serikali kuu na makundi mengine kama vile wafanyakazi ambao hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi ambao wao wataendelea kukatwa kila mwezi ila viwango vitashushwa kutoka 3% to 1% .

Aidha pesa ziwe ni mahsusi kwa ajili ya dawa,vitenganishi na vifaa tiba vya kisasa wakati huo huo bajeti ya Wizara ya kawaida itaendelea kuwepo kama kawaida Ili kuzalisha wataalamu,maslahi Bora kwa watumishi,utawala na kugharamia ujenzi wa miundombinu mipya.

Utaratibu huu ukianzishwa hatutegemei tena kusikia eti ugonjwa fulani ni gharama sana na hivyo watu wachangie.Kila ugonjwa utakuwa ndani ya bima.Kama Til.1.5 ya covid imejenga madarasa 15,000 nchi nzima,imejenga majengo ya emergency,imejenga masoko ya machinga,imeleta maji,imenunua ambulance,x-rays,MRI nk ni wazi zikipatikana japo til.2.5 zitaleta mapinduzi kwenye sekta ya Afya Nchini.

Ni vyema serikali iamue sasa kuleta mjadala huu kwa umma na iweke utaratibu mzuri wa kulipa hizo pesa kwa njia ya mitandao ya simu na Benki Ili tuanze rasmi kuwa na bima ya Afya kwa wote.

Kiukweli gharama za matibabu zinaumiza na zinafukarisha Sana,tunaomba serikali ichukue hili wazo kwa sababu halihitaji pesa ya serikali bali pesa itatoka kwa sisi wananchi moja kwa moja.
Hesabu zako zimekwenda mrama, rudia kujisoma taratibu ujirekebishe.
 
Wazo lako ni zuri ilifaa uweke na no. Ya simu,

Lakini unafahamu kuwa hela ya bima ya afya haitumiki kwa kazi iliyokusudiwa? Mfano Mtumishi wa serikali anachangia sh 30,000 kila mwezi na amechangia pengine miaka 15 bila kuugua magonjwa makubwa makubwa lakn ikitokea akaumwa magonjwa makubwa makubwa anaambiwa huu ugonjwa wako hauko kwenye bima ya afya au bima ya afya yako haitoshi uongezee kiasi ndipo upate matibabu, jiulize miaka 15 nachangia sh30,000 kila mwezi bado wanasema bima yako haitoshi je ni lini itatosha??
 
Back
Top Bottom