The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,589
- 14,135
Moja kwa moja kwenye mada.
Kila mtu ni mhanga wa ughali wa gharama za matibabu,tumeshuhudia jamii zikipata mgonjwa wa mda mrefu zinavyofirisika kwa kuuza kila mali yao Ili kugharamia matibabu ya mgonjwa na pengine asipone.
Kwa muktadha huo,wananchi wako tayari kuchangia walau sh.5,000 kwa kichwa kwa kila mwaka Ili kupata pesa za kuwa na bima.
Kwa kuwa wananchi wako tayari kulipa Serikali iandae sheria ya bima ya Afya kwa wote yaani universal healthcare act na Mfuko wa bima ya Afya ndio uratibu moja kwa moja jambo hili.
Ikiwa kila mwananchi au kichwa kitatoa sh.5,000 kwa mwaka kwa watu 60,000 serikali itapata wastani wa Bilion 300 Kwa mwaka pesa ambazo ni robo ya bajeti ya Wizara ya Afya.
5,000*60,000,000=3.E11
Ikiwa watu walilipishwa sh.20,000 kwa kununua vile viliitwa vitambulisho vya ujasiliamali na pesa ikapatikana ni dhahiri kwa wazo kama hili wananchi wataliunga mkono maana kila mtu atalipa kwa idadi ya watoto alionao.
Kila una watoto 6 utalipia hivyo hivyo,kama wako 10 utalipia watoto kumi.Lakini makundi maalumu kama walemavu, watoto wa mitaani,wazee na watu wengine maskini Sana watalipiwa na Serikali kuu na makundi mengine kama vile wafanyakazi ambao hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi ambao wao wataendelea kukatwa kila mwezi ila viwango vitashushwa kutoka 3% to 2% .
Aidha pesa ziwe ni mahsusi kwa ajili ya dawa,vitenganishi na vifaa tiba vya kisasa wakati huo huo bajeti ya Wizara ya kawaida itaendelea kuwepo kama kawaida Ili kuzalisha wataalamu,maslahi Bora kwa watumishi,utawala na kugharamia ujenzi wa miundombinu mipya.
Utaratibu huu ukianzishwa hatutegemei tena kusikia eti ugonjwa fulani ni gharama sana na hivyo watu wachangie.Kila ugonjwa utakuwa ndani ya bima.Kama Til.1.5 ya covid imejenga madarasa 15,000 nchi nzima,imejenga majengo ya emergency,imejenga masoko ya machinga,imeleta maji,imenunua ambulance,x-rays,MRI nk ni wazi zikipatikana japo til.Bil.300 zitaleta mapinduzi kwenye sekta ya Afya Nchini.
Ni vyema serikali iamue sasa kuleta mjadala huu kwa umma na iweke utaratibu mzuri wa kulipa hizo pesa kwa njia ya mitandao ya simu na Benki Ili tuanze rasmi kuwa na bima ya Afya kwa wote.
Kiukweli gharama za matibabu zinaumiza na zinafukarisha Sana,tunaomba serikali ichukue hili wazo kwa sababu halihitaji pesa ya serikali bali pesa itatoka kwa sisi wananchi moja kwa moja.
Kwa mujibu wa Utafiti,73% wako tayari kulipa Bima ya Afya.Ni wakati sasa wa Serikali kuchukua hatua za utekelezaji.