Serikali acheni kukurupuka, wajengeeni uwezo badala ya kuwakandamiza wakulima wa bangi

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
7,101
6,708
Naandika bila ya mpangilio au mtiririko maalum. Nimekurupuka na Jazba.

Nimeona ni muhimu kuendeleza mjadala huu.
Kuna ....
Uzi huu ambao umetoa hoja zinazofanana na yaliyonitatiza roho yangu leo
(Ukipata vidakika pitia huko) na
baada ya kukutana na Uzi huu hapa, hususani kuhusu operesheni ya Polisi iliyofanyika katika Kijiji cha Kisimiri Juu, kilichopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha

Nimekurupuka na Jazba yaani

Mahekari ya shamba yameteketezwa kwa sheria kandamizi na ya muendelezo ya ukoloni mamboleo! Sheria ambazo zilijengwa kwa mahususi kukandamiza Jamii za Watu tofauti wa kirangi kati ya 'Wazungu' (Ukweli mchungu).

Kwanza napinga kitendo hicho kwa dhana zote. Kwani naona hiyo mantra ya 'Usalama wa Kiafya wa Raia" umejaa utabaka yaani ni lugha ya Utenganishi baina ya wale "Wazungu" wenye wanaofikiri ndio wanayo 'Gods given rights'. na hivyo sheria kama hiyo itawatenganisha kupata madhara ya kiafya kutoka kwa wale ambao ni Dhaifu. Mtafuteni Dr. Samuel Cartwright wa Chuo Kikuu cha Lousiana ili uweze kudavua.

Nasema hivi, Sheria inayotumiwa kwa wavuta bangi, wauza bangi na Wakulima wa bangi itenganishwe na sheria zingine kandamizi, zilizo jaa ukimbari.

Tuwe na mbadala wa kujenga badala ya kutiana umasikini. Ingefaa Wizara ya Kilimo, Wizara ya Kazi, vijana wawe na Idara ziliozoungana na Wizara ya mambo ya Ndani (Wizara mama ya polisi) kutaarifiana pale kunapotokea operseheni kama hiyo Kishimiri. Arumeru, Arusha

Wizara ya Kilimo itafute mbadala wa mazao mbadala kwenye shamba litakalo fyekwa bangi (wakati tukisubiri bunge kuamua hatima ya Kilimo hicho) na mkulima apewe kitu cha kuotesha ili aweze kuendelea kujikimu na maisha, mfano Alizeti au Mahindi. Vilevile Wizara ya kazi imwezeshe kielimu na kumjengea uelewa wa kibiashara badala ya kutiana hasara ili tuweze kuondoa Umasikini wa kutungiwa na Wakoloni. Ukoloni mamboleo.

Tuwe wabunifu

Hasara tunayoipata ni kuwili, Kwanza tunapoteza fedha kuendesha operesheni kama hiyo, tunajenga chumba kingine magereza, tunaenda kumlisha bure huyo kijana/mzee na yote haya yanahitaji fedha za kutoka kwa walipa kodi.

Tunapata hasara kwenye jamii, kwani Familia zinazoondokwa na mleta sembe hayupo nao sasa wenza wanaanza kuhangaika na maisha! Halafu unaja sema kwa Ajili ya "Usalama wa Kiafya wa Raia" mfyonyooo

Kwa wale wanaopenda kusoma tafuteni neno Raia limetoka wapi (etymology)

Kwa wale wanaotaka kujua tumetoka wapi na Sheria kandamizi kama vile sheria ya mikusanyiko, sheria za madawa ya kulevya, matumizi yake, karaha zake, faida na hasara zake. Jitumbukize mitandaoni. Panua wigo la Ufikiri na Mawazo bila kusahau Tamaduni, mila na maadili ya Mwafrika.

Nawasii Serikali yangu Tukufu Wacheni kukurupuka. Wajengeeni uwezo Vijana na Wakulima badala ya kuwakandamiza.

Amani iwatandae

Aluta Continua.
 
Back
Top Bottom