Hii ndio hoja ya Mkandara kuwa znz haiwezi kupewa misaada na mikopo .Between:
1. trade
2. Foreign direct investment
3. Aid
Kipi ni bora kwa taifa? Katika yote haya, aid ni kitu cha mwisho kukipigania, unachohitaji ni more trade and investments. Sijui kwanini Watu wanapoteza muda kujadili AID kitu ambacho hakuna case study in Africa Kwamba ilisaidia taifa kujikwamua kiuchumi. Aid is beneficial only to tyrants na ndicho Wanasiasa ZnZ wanachotaka.
Swali ambalo Kobello huwa halijibu ni hili hapa,kwani kwasasa hivi nani analipaia gharama za S2?.
..lakini wa-Znz wenyewe wanasema wanataka madaraka makubwa na mapana zaidi ili wasiwe tegemezi kwa wa-Tanganyika.
Yes.Swali ambalo Kobello huwa halijibu ni hili hapa,kwani kwasasa hivi nani analipaia gharama za S2?
Yaani Kobello anaamini ukiwa na jina Tanzania, basi gharama zinapungua kwa Mtanganyika. Ukitenganisha S3 gharama zinaongezeka na znz inashindwa kulipa. Kwamba, inaweza kulipa ikiwa ndani ya Tanzania na inashindwa kulipa ikiwa nje ya Tanzania.
Serikali 3 na gharama zake
Baada ya kuvunjika kwa bunge la katiba juu ya swala la muundo wa serikali, nachukua nafasi hii kutoa majibu ambayo kwa sababu zisizojulikana imeshindikana kabisa kuelezewa tofauti ya gharama baina ya serikali 2 na 3, gharama zipi zitaongozeka kulingana na mapendekezo ya rasimu ya tume ya Warioba.
Na sii lengo langu kujaribu kuukana ukweli kwamba Tanzania ya leo inahitaji serikali 3 isipokuwa kuwataarifu wananchi kuelewa jinsi gani muundo wa aina hii una mamlaka gani na unafanyaje kazi zake ktk utekelezaji wa majukumu wanayokabidhiwa kikatiba. Hii inatokana na mimi kuwasoma watu wengi kutofahamu Mamlaka ya tawala wa muundo huu ili serikali hizo ziweze kuwawakilisha wananchi wake haraka na kwa ufasaha zaidi. Hivyo lengo la kuzitaka serikali 3 linaonyesha wazi ni kutaka kutengenisha mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa bara kutokana na ukweli kwamba hadi sasa Mambo yote ya Muungano ni mambo ya bara sio ya Muungano badala ya kuziunda serikali ziwe karibu Zaidi na wananchi wake ktk utekelezaji wa matakwa yao.
Mara zote nimesikia wananchi wakidai kuwepo kwa seikali 2 hakuna tofauti ya gharama na serikali 3 na wakitumia sababu za mapngufu ya utawala uliopo ambao miaka yote baada yatangu 1984 tulipounda vyama vingi, kumekuwa na mkanganyika wa utawala ambao umewavuruga wananchi wasijue mamlaka ya vyombo vyao yana ukomo gani. Pia imewavuruga viongozi ambao kwa dhana wamekuwa wakiongeza mikoa wilaya na majibo kufikiria ndio njia rahisi ya kuwafikia wananchi wakati mamlaka bado yapo chini ya rais wa serikali kuu. Hivyo mitazamo yote hii imelenga zaidi hifadhi ya Utawala (kisiasa) kuliko sababu za ujenzi wa nyenzo za kuijenga nchi na wananchi wake ambao pia kw abahati mbaya wamevutwa katika zizi la Uchama na kupoteza Utaifa wao.
Ngoja niseme ukweli, Ukweli ni kwamba tunapoihitaji serikali ya 3 siyo serikali ya ya Tanganyika kama wanavyodai wanasiasa wengi ama wana taaluma wapambanaji isipokuwa tunaihitaji serikali ya Muungano ambayo haipo. Ukweli ni kwamba jina la Muungano lipo lakini hatuna seriikali ya Muungano toka mwaka 1984, niliwahi kulisema jhili na sasa limedhihirishwa ktk kongamano la jana. Imeelezwa katika kongamano la Mwl.Nyerere foundation ya kwamba hata hayo mambo tunayosema kuwa ni ya Muungano ni mambo ya serikali ya bara.
Hivyo mawaziri wote walioko ktk ushirika wa Muungano ni mawaziri wa serikali ya Tanganyika sio ya Muungano. Wajumbe hao walifikia hadi kuhoji ni lini wananchi wamewaona viongozi mawaziri wa Muungano wakitemebelea Zanzibar katika maswala ya Muungano?. Kwa hiyo tunazo serikali2 nazo ni serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika - Hatuna serikali ya Muungano!.. Ukweli ndio huo japo unauma.
Kwa hiyo basi ni muhimu tukubali kwamba tuchukulie kwamba hii serikali ya Muungano ni serikali ya bara, bunge lake, mahakama zake zote ni za bara, na ndio maana wapo wananchi wanahoji kuwepo kwa wabunge wa Zanzibar katika bunge la Muungano kujadili mambo yasokuwa ya Muungano bila kujua kwamba pale hakunamambo ya Muungano. Hivyo tunachokililia leo hii ni serikali ya Muungano sio Tanganyika maaa ipo.
Sasa swali linakuja - Tukiunda serikali ya 3 ya Muungano haitakuwa na gharama zake? Hizo ghrama zake ni nani atazihudumia? Na Je, bunge la serikali hii litakuwa na wajumbe wangapi, kutoka wapi na majimbo gani? Mishahara na posho zao zitagharamiwa na nani, watumishi wake watakuwa sehemu zote za Jamhuri au makao makuu tu na kadhalika… Hizi gharama za misafara ya rais ktk mialiko ya Kimataifa, mawaziri wake, mamlaka yake katika mipango ya maendeleo na kadhalika ndiyo maswala muhimu ya kujadili kuliko kuendelea kuidai Tanganyika ambayo ipo.
Je, nchi za wenzetu walokuwa na mfumo kama huu mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za serikali zake umejengwa vipi na nini nafasi ya serikali kuu ktk ujenzi wa Mataifa hayo. Nini ukomo wa mamlaka ya serikali za nchi kuendea mamlaka ya serikali kuu juu ya jambo hilo hilo. Ikiwa Nchi inahitaji uwekezaji katika Kilimo, serikali kuu itahusika vipi tofauti na hizo za kila nchi.
Nafikiri hii inatosha kwa leo tutaendelea inapobidi baada ya michango yenu.
Kukopa kwa ajili ya maendeleo, siyo kukopa kwa ajili ya administration.Hapana rasimu imesema nchi washirika zitaruhusiwa kukopa na kuingia mikataba na mashirika au taasisi za kimataifa. Endapo JMT itahitaji basi itasaidia kwa hilo.
Kilio cha znz cha muda mrefu ni kuziwa kukopa au kukopa kupitia JMT.
Kusema hawataweza kulipa gharama za shirikisho si kweli. Wataruhusiwa kukopa hata Mkandara atathibitisha hili.
Kukopa ndio kilio chao cha muda mrefu sana, na rasimu imewapa nafasi hiyo
Swali ni kuwa, kwani sasa gharama hizo analipa nani katika muundo wa S2?Yes.
Kwa sababu serikali ya T anganyika itakuja na gharama zake mpya.
Wacha kukopa kwa maendeleo, mimi hata kuongelea kukopa naona aibu.Kukopa kwa ajili ya maendeleo, siyo kukopa kwa ajili ya administration.
Tuwe tunaona aibu jamani.
Kwa sasa gharama hizo zinalipwa na JMT/Tanganyika.Swali ni kuwa, kwani sasa gharama hizo analipa nani katika muundo wa S2?
Pili, Tanganyika haiwezi kuongeza gharama. Hivi ukiwa na mambo 22 au 7 yapi ni mengi na yenye gharama?
Hapana rasimu imesema nchi washirika zitaruhusiwa kukopa na kuingia mikataba na mashirika au taasisi za kimataifa. Endapo JMT itahitaji basi itasaidia kwa hilo.
Kilio cha znz cha muda mrefu ni kuziwa kukopa au kukopa kupitia JMT.
Kusema hawataweza kulipa gharama za shirikisho si kweli. Wataruhusiwa kukopa hata Mkandara atathibitisha hili.
Kukopa ndio kilio chao cha muda mrefu sana, na rasimu imewapa nafasi hiyo
Serikali ya muungano lazima itashughulikia International trade, Statistics,Climate, Research,Industrial licensing, Environmental Protection (Mimi ningependekeza ipewe National Parks na Game Reserves zote), Kilimo na mifugo, Uvuvi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sheria, Hazina (meaning fedha apart from currency, yaani taxation,mikopo na madeni etc), Social Welfare, Elimu etc....
Msiwasikilize hao wajumbe wa Tume ya Katiba, hawawaambii ukweli na wameficha mambo fulani. I can sense that.
Hapa mnasahau ukweli kuwa ndivyo ilivyokuwa hadi tukawa na mambo 22.Kwa maoni yako kuongezeka kwa "mambo ya muungano" ni kujenga muungano au kudhoofisha muungano?
Mimi naamini mambo yakiongezeka maana yake ni kuwa washirika wanaukaribia zaidi muungano wa kweli, kwani mwisho wa siku taasisi zinazoshughulikia masuala ya muungano nazo inatakiwa ziungane!
What do others think? Mchambuzi, Mkandara and Nguruvi3 especially!
Polisi, jeshi, currency, uhamiaji, vyama vya siasa na katiba havitaongeza wala kupunguza gharama zake za uendeshaji kwa sababu vyombo hivi vitakuwa chini ya serikali moja.Kobello,
Kuhusiana na hoja kwamba serikali ya Tatu itaongeza gharama, tuliangalie kwa mfano jeshi la polisi, utaratibu na allocations ya kimataifa ni Askari mmoja kwa kila Watu, raia au wananchi Mia nne; serikali tatu zitaongeza gharama gani Katika suala hili?
katiba ya sasa ya JMT Inasema wazi Kwamba serikali ya muungano ndiyo inasimamia pia mamlaka ya Tanganyika/Tanzania bara, kwa maana hii, gharama za Tanganyika Zipo na zinatambulika kikatiba, sasa cha ajabu nini kuhusiana na gharama za Tanganyika Kwamba kutakuwa na gharama Wakati katiba inaweka wazi Kwamba kuna gharama za Tanzania bara za kusimamia? Gharama hizi Zipo tu...
Na Isitoshe, kwa Mujibu wa rasimu, wizara za muungano zitakuwa ni nne tu tofauti na Hali ya sasa chini ya serikali Mbili ambapo Zipo za muungano, zipo mchanganyiko baina ya Tanganyika na muungano, na Zipo za Zanzibar...
Sent from my iPhone using JamiiForums
..naunga mkono hoja zako kwa asilimia 100.
..imetokea mara nyingi wa-Znz kushindwa kuendesha mambo yao na Tanganyika ikalazimika kuwasaidia.
..lakini wa-Znz wenyewe wanasema wanataka madaraka makubwa na mapana zaidi ili wasiwe tegemezi kwa wa-Tanganyika.
Polisi, jeshi, currency, uhamiaji, vyama vya siasa na katiba havitaongeza wala kupunguza gharama zake za uendeshaji kwa sababu vyombo hivi vitakuwa chini ya serikali moja.
Lakini katika mfumo wa Federation, serikali kuu itakuwa na Treasury yake na Serikali ya Tanganyika pia. Simaanishi kuwa Treasury ya Union itasimamia currency tu (yaani itasimamia Central Bank na Monetary Policy tu) bali itabidi isimamie Fiscal Policies zake na lazima itakuwa na departments na wafanyakazi wake tofauti na Tanganyika. Tanganyika itakuwa na Fiscal autonomy yake kwa hiyo nayo itahitaji vyombo vyake na wafanyakazi wake. Kwa sasa hivi, monetary policies zipo chini ya BOT na Fiscal policies zipo chini ya Hazina. Tukianzisha serikali ya Tanganyika, itabidi tuwe na Hazina ya Tanganyika ambayo itasimamia fiscal policies za Tanganyika independent of and under the jurisdiction of both Zanzibar and Union governments respectively. Kwa hiyo utahitaji chombo kipya chenye wafanyakazi wake na administration costs mpya kwa mwananchi wa Tanganyika.
Kuna Suala la International Trade, hili suala lazima nalo lisifichwefichwe kwa sababu huwezi kuondoa International trade kwenye Union. Lazima Union itakuwa na international trade kwa hivyo hilo ni la nane tayari panga pangua.For example,
Tanganyika ikiamua kujenga bomba la mafuta kwenda Mombasa kupitia Tanga, hiyo tayari ni international trade ambayo ipo chini ya jurisdiction ya Mipaka ya Serikali kuu ya Muungano, yaani mipaka ya Tanzania na Serikali ya muungano lazima ihusike. hata biashara za binafsi zinazovuka mipaka lazima ziwe controlled na Union government chini ya uhamiaji na customs. Kwa hiyo international trade itakuwa na chombo chake Tanganyika na Muungano (sizungumzii mambo ya mabalozi, kwa sababu hawa ni constant kwa union peke yake).
Mambo ya kilimo na mifugo, lazima kuwe na department yake kwenye Muungano na Tanganyika. Hasa kwenye issue ya Ghala la Taifa (food security), kwenye stabilization ya bei, emergencies, disease and pest control etc .. lazima Union iwe na chombo cha kusimamia haya mambo, haiwezi kuziachia Tanganyika na Zanzibar ziwe too independent kwenye masuala haya. They have to be harmonized.
Hapo bado kuna kupangua na kupanga court system ili kukabili changamota za Federal systems. Especially constitutionality issues na Inter-state trade na arbitrations nyingine kwa sababu migongano itakuwa mingi na efficiency ya mahakama zetu sidhani kama ipo tayari. Mfumo wa Federation (hasa tunaoutaka sisi ambao ni tofauti na federations kama za Nigeria etc...) ni mfumo unaotokana na nchi mbili zilizokwisha kuwa huru na wala siyo Kano na Biafra au Kivu na Katanga.
Costs zitaongezeka, tena sana na tusipende kukariri talking points za idadi ya Polisi na idadi za mawaziri. Waziri mmoja hata akilipwa milioni 200 kwa mwaka wakiwa kumi ni bilioni 2 kwa mwaka. Hatuzungumzii bilioni mbili kwa mwaka, tunazungumzia trilions.
Talking points zingine ni kukopa. Hivi watu wazima wanaweza kukaa chini na KUSEMA KUWA TUKISHINDWA TUTAPEWA MISAADA?? Mimi sioni kama ni jambo linalofaa hata kuzungumzwa na kiongozi yeyote yule.
Hapa ndipo sikubaliani na Watanganyika wengi. JMT ni Tanganyika na Zanzibar. Gharama za sasa zinalipwa na Mtanganyika 100%. Hakuna mahali wala mtu anayekataa ukweli huu.Kwa sasa gharama hizo zinalipwa na JMT/Tanganyika.
Ingekuwa swali lako la pili lipo based on such a simple logic, labda ungepata jibu unalotarajia. Na ndivyo inavyozungumzwa huko mjini. Kuwa mambo ya muungano yamepungua kwa hiyo mambo ya muungano yatapunguza gharama. Huo ni uongo mtakatifu!!
Serikali ya muungano lazima itashughulikia International trade, Statistics,Climate, Research,Industrial licensing, Environmental Protection (Mimi ningependekeza ipewe National Parks na Game Reserves zote), Kilimo na mifugo, Uvuvi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sheria, Hazina (meaning fedha apart from currency, yaani taxation,mikopo na madeni etc), Social Welfare, Elimu etc....
Msiwasikilize hao wajumbe wa Tume ya Katiba, hawawaambii ukweli na wameficha mambo fulani. I can sense that.
Kabla ya kukujibu maswali yako matatu, itabidi niweke mambo fulani sawa,Pili, Zanzibar wanataka mamlaka yao ya International trade. Znz wana bureau of statistic, wana climate depart, research institute zao, industrial license, environ protection, kilimo na mifugo, mawasiliano na uchukuzi, ZRA, baraza la mitihani, Bandari, Anga, utalii n.k. Tayari wanazo.
Unaposema eti hayo ni sehemu ya mambo ya muungano, unachotaka kusema ni kuwa uwepo wake ni kwa faida ya wote lakini gharama zake abebe Mtanganyika. Na kwamba znz ina haki ya kuwa na mambo yake, yale ya Watanganyika yawe ya wote.
Huu uzezeta wa Watanganyika utaisha lini?
Huwezi kuwa na muungano wa mambo yote huku sehemu moja ikiwa na mambo yake. Hili halipo popote duniani.
Ukiataka hivyo ni lazima uwe na ya Tanganyika ili baadaye kuwe na chombo cha pamoja.
Wazanzibar hawataki sasa ninyi mnalazimisha. Hivi hamuoni manaleta tatizo?
Nimekuuliza, mambo 22 sasa ni 7 (rasimu). Ni yapi yaliyoondolewa(15 ) ambayo Tanganyika inaona yameongeza gharama?
Katika mambo 22 ambayo kiidara ni 47 naomba uniambie kuhusu hili.
1. Zanzibar ilipoondoa bandari, anga, statistic, baraza la mitihani, ZBS n.k. gharama gani zimeongezeka kwa Tanganyika?
2, Hoja ya msingi hapa ni kuwa yalipopunguzwa mambo 22 a kubaki 7, kwa maana yaliondolewa 15, Tanganyika imeingia vipi gharama. I mean sasa tuna mambo ya Tanganyika na znz katika maeneo fulani, Tanganyika imeingia vipi gharama za ziada?
3. Katika mambo 7 ya tume, tunaomba utuonyeshe kuwa yanapokuwa ya ushirika Tanganyika itaingia gharama zaidi.
Hapa tuna ulinzi na usalama, mambo ya ndani, mambo ya nje, katiba, uraia na uhamiaji
Hapa tunataka utueleze, mambo hayo yanapokuwa ya shirikisho Tanganyika inaongeza vipi gharama.