Mkandara ,
Naomba niweke kumbu kumbu sawa kwa faida ya wanajamvi.
1. Wewe umesimamia S2 siku zote ukisema hakuna sababu ya kurudisha serikali ya Tanganyika
a) Itua uzalendo wa nchi
b) Italeta mgawanyiko miongoni mwa Watanzania
c) Mambo yote yawe ya muungano chini ya Tanzania lakini znz ibaki kama ilivyo. (Si chini ya Tanganyika)
2. Upo katika rekodi ukisema kuzinduka kwa Tanganyika kutaongeza gharama. Hapa uliamini uwepo wa Tanzania muungano
3. Kwamba, Tanganyika imevaa koti la muungano na kuwanyima wznz misaada na mikopo.
Kwa maneno yako ya bandiko hapo juu, una maana Tanganyika inakopa na kuwanyima wznz misaada na mikopo yao.
4. Umeeleza kuwa, znz inaweza kuchangia muungano kama itapewa kipaumbele cha bandari na biashara n.k.
Kwa maneno yako ya juu, una maana ZNZ inaweza kuwachangia Watanganyika!!!!
5. Hakuna taifa la Tanganyika, ukiungana na Shivji katika hilo.
Leo unasema taifa ulilosema halipo, ndilo lililopo.
Mifano ni zaidi ya 10 ikionyesha jinsi unavyobailika na kubadilisha position yako kila alfajiri na magharibi.
Nadhani ni ngumu kwangu na wengine kukuelewa hasa unasimamia nini, unazungumza nini na una tetea nini.
Tunachokijua ni kubadili position na kama utahitajika ushahidi upo wa kutosha.
Tanganyika
Kusema kuwa Tanganyika ipo isiyokuwepo ni muungano, hilo ni tusi kubwa sana kwa Watanganyika.
Kwanza, nikukumbushe kuwa umeangalia mjadala kwabahati mbaya hukuelewa au umeelewa vibaya dhana zilizojadiliwa
Pili, unajaribu kupotosha umma kwa kucheza na maneno zaidi ya facts
Mfano, unapodai Tanganyika ipo, isiyokuwepo ni muungano, una maana madai ya wznz ni dhidi ya Watanganyika na si muungano.
Mfano, wznz wanadai asilimia 21 ya ajira za Tanganyika, wanagharamiwa mambo ya wizara nyeti kwa gharama za Mtanganyika n.k. Hili ni tusi kwa Watanganyika na linahimiza kuzinduka kwake
Mkandara, elewa kuwa kinachotakiwa hapa fiscal autonomy kwa Tanganyika.
Hiyo itapatikana Tanganyika ikiwa inatambulika rasimi na kuwa na mwongozo wake kama ilivyo znz.
Hatutaki kuwa na dude Tanzania ambalo znz inalitumia kumuumiza Mtanganyika.
Elewa dhana ya fiscal autonomy na identity.
Kuhusu tume, walichosema ni kuwa kwa hali ya S2 muungano sasa haupo.
Wazanzibar wameondoa mambo mengi, na tume wameona ni kujidanganya kama tuna Sumatra na Zanzibar Maritime.
Hapa uelewe znz ipo Tanzania ili kullipiwa ada kule IMO na wala si muungano.Kwa
Ni kwa msingi huo tume ikasema, kuendelea na muungano wa kujidanganya huku Tanganyika ikibeba mzigo na Wazanzibar wakiungana kwa jina si kutenda haki. Na ni kwa jina hilo hilo wznz wanawajibika kupitia ili kuweza kujikwamua kwa mambo yao.
Prof Kabudi aliposema Watanganyika wana yao mezani alimaanisha hili.
Gharama za S3
Huko nyuma ulisema JMT inabeba gharama za S2 na ni rahisi. Tulikuuliza mara nyingi kwani gharama hizo zinachangiwaje? Hukuwa na jibu. Leio unasema S3 zitakuwa na gharama ukisahau hukuweza kutueleza gharama za sasa analipia nani.
Hoja yangu hapa si kujibu hoja zako, ni kukutaka utueleze unasimamia nini ili tuweze kujadiliana vema.
Kwa sasa kila jibu litakuwa na position tofauti na hilo litakuwa gumu sana the least to say.
Hebu tueleze, wewe unadhani nini kifanyike katika mazingira unayoyasema.
Sitopenda kuendelea kubishana na mtu asoweza kusoma maelezo ya watu akayaelewa kwanza kabla ya kutoa hoja zake. Haya yote sii maswali yangu mimi bali maswali ya wananchi walokusanya tume ya Warioba na ndio chanzo cha kuandika rasimu hii. Tunaijadili rasimu ya warioba na sii mawazo ya Mkandara hapa ila kubaliana ama pingana name kwa kufuata utafiti wa tume ya warioba.Mkandara ,
Naomba niweke kumbu kumbu sawa kwa faida ya wanajamvi.
1. Wewe umesimamia S2 siku zote ukisema hakuna sababu ya kurudisha serikali ya Tanganyika
a) Itua uzalendo wa nchi
b) Italeta mgawanyiko miongoni mwa Watanzania
c) Mambo yote yawe ya muungano chini ya Tanzania lakini znz ibaki kama ilivyo. (Si chini ya Tanganyika)
2. Upo katika rekodi ukisema kuzinduka kwa Tanganyika kutaongeza gharama. Hapa uliamini uwepo wa Tanzania muungano
3. Kwamba, Tanganyika imevaa koti la muungano na kuwanyima wznz misaada na mikopo.
Kwa maneno yako ya bandiko hapo juu, una maana Tanganyika inakopa na kuwanyima wznz misaada na mikopo yao.
4. Umeeleza kuwa, znz inaweza kuchangia muungano kama itapewa kipaumbele cha bandari na biashara n.k.
Kwa maneno yako ya juu, una maana ZNZ inaweza kuwachangia Watanganyika!!!!
5. Hakuna taifa la Tanganyika, ukiungana na Shivji katika hilo.
Leo unasema taifa ulilosema halipo, ndilo lililopo.
Sasa sielewi wewe unaelewa vipi kuhusu hili neno Muungano na mambo yake kuwa ya Muungano?=>Jaji warioba anasema hakuna mawaziri wa muungano wanaotembelea Zanzibar kwa ajili ya mambo ya Muungano.
Mambo yote ya muungano ni ya bara.
=>Anasema Nchi mbili zimeunganika lakini moja haina Sovereignty, Tanganyika iko huru kufanya mambo yake ya maendeleo lakini Zanzibar mpaka iombe ridhaa ya Bara.
Mkuu samahani nilichanganya mada kidogo na ya mwandishi wa kwanza. Unajua mimi nautazama Muungano wetu kama ni wa WATU na NCHI kutokana na historia yetu na hivyo hatuungani kwa sababu za kiuchumi ama kisiasa kama inavyodaiwa na wengi ambao ni wanasiasa uchwara. Hawa wanajaribu kwa kila hila kulifanya swala hili la Muungano kuwa ni wa kisiasa kutokana na walivyolishwa ama maslahi ya nchi za nje kutugawa ili watutawale kiuchumi. It all start with UCHUMI kutokea kutoelewana na kugawana mali kwa nchi zenye muungano na bahati mbaya tunachochewa na nguvu za mataifa makubwa zaidi yetu.Mukandara;
Nimekusoma na kukuelewa na kwa hakika umekuja kwenye hoja yangu kwamba; Si ndiyo hayo mambo ambayo tunatakiwa kuyaweka sawa kama mapungufu katika Rasimu hii ya Tume ya Jaji Warioba ili ikae vizuri zaidi kisha tusonge mbele? Tatizo letu nini hasa?
Katika ishu ya Jeshi na ufalme wa King Msawati hata sijakuelewa na kama nimekuelewa basi ni wazi unafikiria vibaya. Nasema hivyo kwa sababu hata sasa Jeshi liko chini ya mamlaka ya Muungano na tuna Amiri Jeshi mmoja tu ambaye ndiye Rais wa JMT na katika Rasimu hii ndicho kinachopendekezwa. Vinginevyo unaweza kunielewesha katika lugha rahisi zaidi ili nikuelewe
Ndiyo, na kama tunaona kuwa ishu ni Rasimu kutokuweka mfumo na vyanzo thabiti vya mapato ya kuindesha serikali ya Muungano ni wakati wa kurekebisha sasa kwa sababu huu ni muungano wetu sisi wana wa nchi hizi mbili na kwa hakika tuliungana kwa hiari hatuna sababu yeyote ya kushindwa kukubalianana kuanza kufikiri kusalitiana huko mbeleni. Na hili ndilo tatizo lililopo sasa kutokuaminiana na kama ni hivyo hata walioko huko Dodoma kwa sasa na wakawa na fikra hizi, ni wazi hakuna watakachokitengeneza!!
Serikali 3 na gharama zake
Baada ya kuvunjika kwa bunge la katiba juu ya swala la muundo wa serikali, nachukua nafasi hii kutoa majibu ambayo kwa sababu zisizojulikana imeshindikana kabisa kuelezewa tofauti ya gharama baina ya serikali 2 na 3, gharama zipi zitaongozeka kulingana na mapendekezo ya rasimu ya tume ya Warioba.
Na sii lengo langu kujaribu kuukana ukweli kwamba Tanzania ya leo inahitaji serikali 3 isipokuwa kuwataarifu wananchi kuelewa jinsi gani muundo wa aina hii una mamlaka gani na unafanyaje kazi zake ktk utekelezaji wa majukumu wanayokabidhiwa kikatiba. Hii inatokana na mimi kuwasoma watu wengi kutofahamu Mamlaka ya tawala wa muundo huu ili serikali hizo ziweze kuwawakilisha wananchi wake haraka na kwa ufasaha zaidi. Hivyo lengo la kuzitaka serikali 3 linaonyesha wazi ni kutaka kutengenisha mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa bara kutokana na ukweli kwamba hadi sasa Mambo yote ya Muungano ni mambo ya bara sio ya Muungano badala ya kuziunda serikali ziwe karibu Zaidi na wananchi wake ktk utekelezaji wa matakwa yao.
Mara zote nimesikia wananchi wakidai kuwepo kwa seikali 2 hakuna tofauti ya gharama na serikali 3 na wakitumia sababu za mapngufu ya utawala uliopo ambao miaka yote baada yatangu 1984 tulipounda vyama vingi, kumekuwa na mkanganyika wa utawala ambao umewavuruga wananchi wasijue mamlaka ya vyombo vyao yana ukomo gani. Pia imewavuruga viongozi ambao kwa dhana wamekuwa wakiongeza mikoa wilaya na majibo kufikiria ndio njia rahisi ya kuwafikia wananchi wakati mamlaka bado yapo chini ya rais wa serikali kuu. Hivyo mitazamo yote hii imelenga zaidi hifadhi ya Utawala (kisiasa) kuliko sababu za ujenzi wa nyenzo za kuijenga nchi na wananchi wake ambao pia kw abahati mbaya wamevutwa katika zizi la Uchama na kupoteza Utaifa wao.
Ngoja niseme ukweli, Ukweli ni kwamba tunapoihitaji serikali ya 3 siyo serikali ya ya Tanganyika kama wanavyodai wanasiasa wengi ama wana taaluma wapambanaji isipokuwa tunaihitaji serikali ya Muungano ambayo haipo. Ukweli ni kwamba jina la Muungano lipo lakini hatuna seriikali ya Muungano toka mwaka 1984, niliwahi kulisema jhili na sasa limedhihirishwa ktk kongamano la jana. Imeelezwa katika kongamano la Mwl.Nyerere foundation ya kwamba hata hayo mambo tunayosema kuwa ni ya Muungano ni mambo ya serikali ya bara.
Hivyo mawaziri wote walioko ktk ushirika wa Muungano ni mawaziri wa serikali ya Tanganyika sio ya Muungano. Wajumbe hao walifikia hadi kuhoji ni lini wananchi wamewaona viongozi mawaziri wa Muungano wakitemebelea Zanzibar katika maswala ya Muungano?. Kwa hiyo tunazo serikali2 nazo ni serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika - Hatuna serikali ya Muungano!.. Ukweli ndio huo japo unauma.
Kwa hiyo basi ni muhimu tukubali kwamba tuchukulie kwamba hii serikali ya Muungano ni serikali ya bara, bunge lake, mahakama zake zote ni za bara, na ndio maana wapo wananchi wanahoji kuwepo kwa wabunge wa Zanzibar katika bunge la Muungano kujadili mambo yasokuwa ya Muungano bila kujua kwamba pale hakunamambo ya Muungano. Hivyo tunachokililia leo hii ni serikali ya Muungano sio Tanganyika maaa ipo.
Sasa swali linakuja - Tukiunda serikali ya 3 ya Muungano haitakuwa na gharama zake? Hizo ghrama zake ni nani atazihudumia? Na Je, bunge la serikali hii litakuwa na wajumbe wangapi, kutoka wapi na majimbo gani? Mishahara na posho zao zitagharamiwa na nani, watumishi wake watakuwa sehemu zote za Jamhuri au makao makuu tu na kadhalika… Hizi gharama za misafara ya rais ktk mialiko ya Kimataifa, mawaziri wake, mamlaka yake katika mipango ya maendeleo na kadhalika ndiyo maswala muhimu ya kujadili kuliko kuendelea kuidai Tanganyika ambayo ipo.
Je, nchi za wenzetu walokuwa na mfumo kama huu mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za serikali zake umejengwa vipi na nini nafasi ya serikali kuu ktk ujenzi wa Mataifa hayo. Nini ukomo wa mamlaka ya serikali za nchi kuendea mamlaka ya serikali kuu juu ya jambo hilo hilo. Ikiwa Nchi inahitaji uwekezaji katika Kilimo, serikali kuu itahusika vipi tofauti na hizo za kila nchi.
Nafikiri hii inatosha kwa leo tutaendelea inapobidi baada ya michango yenu.
Mkuu wangu ulisikiliza mdahalo wa Nyerere foundation hivi majuzi na maelezo aloyatoa Warioba? nakuomba msikilize tena chukua muda wako kumuelewa na inakuwaje tena leo mnakataa utafiti wake. https://www.youtube.com/watch?v=bDbUTYbPMc4Nilitegemea utakuja na jibu la hofu ya ccm juu ya gharama za serikali ya Muungano. Analysis yako kwa sehemu iko sawa na kwa sehemu haiko sawa kutokana na mfumo halisi ambao umekuwa ukiendesha nchi hii tangu 1964, na nchi hizi tangu 2010.
Falsafa ya uchambuzi wa majina utawala gani unaitwa serikali gani si jambo la msingi hapa. Hakuna mtu asiyefahamu kwamba kuna SMZ and Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo essentially inahusika na masuala ya Muungano na ya Tanzania bara ama Tanganyika.
Ukweli ni kwamba Serikali ya Tanganyika haipo. Iliyopo ni ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar. Kuchapatisha masuala ya tanzania bara kwenye muungano ndiyo mwanzo wa confusions hizi na uwajibikaji usio tija wa serikali ya Muungano kwa Zanzibar.
Kinachotakiwa ni kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ambayo haipo na kuimarisha serikali ya Muungano ili iweze kusimama kama nguzo ya uwepo wa hizi serikali mbili washirika.
Naungana na wewe katika hoja ya kujadili masuala muhimu ya uimarishaji wa serikali ya Muungano.
Gharama ya serikali ya muungano kwa mujibu wa data kutoka hazina ni 1.8b.
Mkuu wangu wewe unajua alisema nini unaona shida gani kuyaweka hapa. Wewe sii uliridhika na majibu yake ina maana unayajua sasa iweje mimi nikatafute majibu wakati wewe ulikubaliana na majibu yake hii ina maana unayajua,unachoficha hapa ni kipi.
Hayo ya Maccm na ufisadi wake ni mada nyingine sijasema nakubaliana nao isipokuwa nahoji serikali 3 kama mwananchi ambaye ni mlipa kodi na najua kodi zetu zitaongezeka kugharamia serikali hiyo.
Serikali 3 na gharama zake
...................... Sasa swali linakuja - Tukiunda serikali ya 3 ya Muungano haitakuwa na gharama zake? Hizo ghrama zake ni nani atazihudumia? Na Je, bunge la serikali hii litakuwa na wajumbe wangapi, kutoka wapi na majimbo gani? Mishahara na posho zao zitagharamiwa na nani, watumishi wake watakuwa sehemu zote za Jamhuri au makao makuu tu na kadhalika Hizi gharama za misafara ya rais ktk mialiko ya Kimataifa, mawaziri wake, mamlaka yake katika mipango ya maendeleo na kadhalika ndiyo maswala muhimu ya kujadili kuliko kuendelea kuidai Tanganyika ambayo ipo.
Je, nchi za wenzetu walokuwa na mfumo kama huu mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za serikali zake umejengwa vipi na nini nafasi ya serikali kuu ktk ujenzi wa Mataifa hayo. Nini ukomo wa mamlaka ya serikali za nchi kuendea mamlaka ya serikali kuu juu ya jambo hilo hilo. Ikiwa Nchi inahitaji uwekezaji katika Kilimo, serikali kuu itahusika vipi tofauti na hizo za kila nchi.
Nafikiri hii inatosha kwa leo tutaendelea inapobidi baada ya michango yenu.
1.8 trillion. Na sehemu kubwa ya gharama hizi zitakuwepo hata Kama muungano utavunjika na kila upande kubeba mbao zake.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu unazungumzia wao wenye serikali 50 lakini wao mambo yao yote ya muungano yanazinufaisha nchi zote 50 sio kwetu sisi na wao hawakuanza na muundo wa chama kimoja na Ujamaa, vyama viwili kuungana na kadhalika.Nimeondoa bla-bla zingine na kutaka kukuonyesha kwamba wewe hujafikilia kabla ya kutuuliza swali la kizembe kama hilo. Wengi tunadhani tunafikilia, lakini kumbe sivyo.
Hizo nchi za wenzetu unazotaka ziwe mfano hujui kwamba kuna nchi zina serikali zaidi ya 30? USA ina serikali ngapi ndani ya Federal?
Hapo unapoona serikali mbili ni gharama kubwa na kwamba ya tatu itaongeza gharama zaidi, yaani umeamini kwamba tutaendelea kuwa na marais waizi kama hawa tulionao ambao wanajichotea tuuu pesa ya safari bila hata audit? Hata kama utabakiza serikali moja kwa kuwa na rais wa aina hii ambaye haoni tofauti ya pesa yake na ya serikali, mzigo ni mkubwa kuliko hata serikali 10.
Mkuu wambo mengine tumnalaumu serikali 2 bure kabisa. Kwa nini tunashindwa kujenga hoja za msingi ili tuwe na serikali 3? Wakati tunajua kabisa kwamba hakuna mambo ya muungano hivi sasa isipokuwa msahafuni kama vile Muislaam/Mkristu nayebeba Quran/Biblia na asiifuate ibada tutalaumu Quran au Biblia? Utalaumu kuwepo kwa madhehebu mengi kuwa sababu ama kuongeza madhehebu zaidi ndio itasaidia? Jamani sisi hatufuati katiba yetu wenyewe ni watu wasokuwa na dira wala uzalendo.Heba sema kama kweli, kuna sababu yoyote ya kuendesha serikali kwa gharama kubwa kiasi hicho? Hizi ni nchi maskini, lazima Rais awe na matumizi yanayo angaliwa, siyo hali ya sasa hivi ambayo anaonekana hawezi tofautisha kipato chake na kile cha taifa. Anachota na kutumia kama kijiwe chake bila ukaguzi. Ni kama Mobutu!
Mawaziri nao wanachota watakavyo. kila wizara ina pesa za chai jumla yake ni kubwa kuliko bajeti ya Elimu. Hayo ndo matumizi makubwa ya serikali wanayotumia kutuogopesha. Nonsense!
Mkuu nakuomba sana wewe na Nguruvi3, kina jassu na wengine msikilizeni hotuba ya mwalimu kwa makini isha jifikirieni nyie mmesimama wapi..Hotuba1.8 trillion. Na sehemu kubwa ya gharama hizi zitakuwepo hata Kama muungano utavunjika na kila upande kubeba mbao zake.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Binafsi yangu hainishangazi hata kidogo kuona mchakato wa katiba umekwama na hakuna maelewano wala hayatakuwepo kwa sababu sisi wenyewe hapa JF ni reflection ya wajumbe wa baraza maalum la katiba, hatuelewani na wala hatutaelewana. Hivi Ndivyo Miafrika tulivyo na haishangazi hata kidogo kwa siku zote maisha yetu yapo katika majuto ni mjukuu. Hakuna swali hata moja lilopewa jibu, hakuna isipokuwa kuzungushana ati nenda kasome rasimu kana kwamba kule kuna majibu. Labda nyie wenyewe rudieni kuisoma rasimu kisha wekeni majibu mloyasoma maana mimi nimeuliza kutokana na rasimu yenyewe na kama unayajua majibu kuna tatizo gani kujibu.
Mimi nimechukua muda sana kutafakari swala hili na kukosa majibu ktk maswala ambayo nimeyaorodhesha hapo juu lakini badala ya watu kunipa majibu yamekuja maswali na maelezo ya kukebehi na kdhalika kwa sababu hata wao hawana majibu isipokuwa wanataka tu serikali 3 kwa sababu ya Ushabiki. Ni rahisi kabisa kujiuliza serikali yenye mambo 7 itakuwa ana bunge la aina gani? wabunge hao watatoka majimbo gani? na watazungumzia mambo yapi ktk maendeleo ya taifa zima.
Mimi sii mshabiki wa vyama wala sintokubali kuburuzwa na upande wowote isipokuwa kuelewa tunaingia ktk muundo ambao hautawagharimu wananchi walipa kodi. Hii habari ya kwamba fedha zipo hazina pasipo kujua hizo fedha ni kodi zenu na zipo pale kwa mautumizi ya mwaka huu ni upumbavu mkubwa kutumia sababu kama hizo kujenga hoja wakati leo hii hatuna serikali ya 3 wala fungu lilotengwa kwa minajiri hiyo. hata kama kuna surplus hazina bado haioneshi ni jinsi gani tutagharamia serikali hiyo kwa miaka 50 au 100 ijayo.
Wengine wamehoji kama nimeisoma rasimu ya katiba wakati wanajua fika kwamba rasimu hiyo haijakamilika, hata hiyo Sura ya sita ya rasimu inatoa tu mapendekezo ambayo ibara ya 2 na ya 3 zinazungumzia mihimili ya serikali hiyo pasipo namba za watumishi wake, muundo na madaraka ya serikali hiyo pia utategemea mamlaka ya serikali 2 za muungano (serikali ya Zanzibar na Ya Bara kufikia muafaka wake. Hakuna kikao chochote baina ya serikali ya bara wala visiwani (kwa sababu hazipo) walofikia kuanisha muundo na madaraka ya serikali hii ya 3 isipokuwa kuweka mambo 7 yatakayo kuwa na Muungano na rais ambaye hatakuwa na mamlaka juu ya mambo yasokuwa ya Muungano. Hivyo sio tu rais anaondolewa nguvu yake bali uanapunguziwa hata uwezo wa kuendesha nchi.
Ifahamike tu ya kwamba gharama za kuendesha serikali ni kodi za wananchi, huko hazina kuna makusanyo ya kodi kwa ajili ya matumizi ya serikali zilizopo na sii vinginevyo. Hata bajeti inaposomwa sio kwamba fedha hiz ziko hazina bali makadirio ya makusanyo na mapato ili kuweza kujenga matumizi ya mwaka unaofuata. Na kwa Zaidi ya miaka 20 serikali zetu hizi mbili zimekuwa zikitumia Zaidi ya makadirio, hivyo miaka yote kulikuwa na deficit iweje leo tuongeze serikali ya 3 ionekane rahisi kihivyo? Kwa gharama zozote zitakazo jitokeza ni kodi zenu wananchi ndizo zitaendesha serikali ya 3 hivyo ni muhimu wananchi wafahamu kwamba gharama za serikali ya 3 zitatoka mfukoni mwao na sii hazina maana kule hawavuni fedha.
Nitashukuru tu ikiwa kuna mmoja wenu ana majibu ya maswali nilouliza. Haya na Lipumba alisema nini ama Profesa Fulani hayajengi mjadala huu isipokuwa kuweka kiza zaidi. Maadam serikali ya Muungano itakuwa na serikali ya 3, itakuwa na bunge lake na mahakama yake ni lazima tujue kwanza muundo wa serikali hiyo na watumishi wake, gharama zake juu ya hizi zilizokuwepo. Kusema tu haitagharimu zaidi ni maneno tuloyazoea kwani misingi mingi ya mwalimu ilivunjwa huko nyuma na fikra kama hizi za ujuaji sana, lakini tumekuja kuyajutia na hatuwezi kurudi nyuma tena kusahihsiha. Hili ni moja kati ya hatari kubwa za sio tu kuuvunja muungano bali kuwepo maswali mengi yasiyokuwa na majibu sahihi lakini bado tunakazania iwe hivyo kwa sababu tu hatuipendi CCM. Sio kila alichokianzisha mwalimu kipigwe vita, hapana ni muhimu tuwe na majibu kamili kabla hatujachukua hatua zozote.
Kwa mfano Zanzibar ina watu mil.1.3 na bara tuna watu mil.45, ni kiasi gani cha kila serikali itachangia gharama za kuendesha serikali hii ya 3. Je, Tanzania bara itakuwa tayari kutoa asilimia 97.7 ya mchango wake kuendesha serikali hii ambayo kwa ujumla wake hawaihitaji? Tanzania bara na visiwani wakisha kuwa na serikali zao zenye mambo yoote makubwa isipokuwa saba ambayo wanaweza kuyaendesha wenyewe kwa nini kuwepo na Muungano? Kweli wananchi wa Tanzania bara wako tayari kugharamia asilimia hii ili kuuenzi muungano ambao ni gharama za ziada?
BAK, Ufafanuzi wa Lipumba ni maoni yake yeye ambayo sii rasimu hivyo kama wewe unayo mawazo hayo jenga hoja hapo nilipouliza kwa kuyajibu maswali yangu kupitia majibu yake. Jamani lini tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu wenyewe? Kwa nini tunajenga mazoea ya Ubishi na hatutaki ku face ukweli pale tunapoona hatuna majibu? wewe nambie ulieweza nini kiasi kwamba unakubaliana na mapendekezo ya Lipumba na kama huyajui leo ina maana hujui..