Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Sasa hiyo uliyoleta ni ya Serikali moja katika tatu, halafu tuwekee na gharama za hizo Serikali mbili ulizoacha kukokotoa.
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Unajua umeipngelea tanzania afu kwenye kufanania unafanisha na tanzania bara na zanzibar pili kumbuka hapo hatuna katiba ya tanganyika alaf zanzibar pia ana katiba yake na mawaziri wake ambayo na tanganyika itakua nayo wakitengeneza yao pengine isimbane mtawala wake kama ilivo ya zanzibar tatu kuna kuichangia serikali ya tatu n mzigo kwa zanzibar ndogo nne kwann usishauri serikali mbili na ya tanzania isizidishe hao mawazir 15 na hao wabunge 70 kama kweli unaipenda tanzania
 
hivi kumbe watanzania wengi wanapumbazika na hayo machura ya CCM!! UKWELI ULIO WAZI Ni kwamba Hayo
maviumbe yanapigania ulaji wa vizazi vitano
mbele..kwa sababu wanatambua serekali tatu
hazitawapa mwanya mkubwa wa kula kwa mrija
au kwa lugha nyepesi kula vya KUNYONGWA!! But
I believe the will of their Devils shall never persist
this time around na Hawatoamini macho wala
masikio yao...NGOJA KITAMBO
TUU..YATATAFUTA PA KUJIFICHA HAYO
MAMBWEHA
 
Tunapoambiwa au kusikia kuwa wa Tanzania tu wavivu wa kusoma wengi tunadhani ni wanafunzi peke yao!Leo imejidhihirisha katika kambi ya wale wanaojiita wengi!Wao ni mabingwa wa wakuchonga na maadui wa maandishi!Hebu fikirini,Kila mjumbe ana kopi yake ya Rasimu na maandishi hayo yamo ndani ya rasimu lakini wengi wao wakisimama kuchangia wanasema serikali 3 ni gharama bila kutoa mchanganuo!Sasa hapa wamebanwa,tusaidiane kutoa kopi kwa ajili ya Wa Tz wenzetu ambao wapo kwenye vijiwe na hawana uwezo wa kuifikia mitandao,waweze kubaini propaganda chafu!
 
Mkuu nafikri bado hujatuelewa tunachokipinga katika uchambuzi wako, na bado unafanya kosa lile lile la kuonesha kwamba upande wa Tanganyika hakutakuwa na wabunge kabisa! Hapa tukubaliane kwanza kuwa serikali 3 inaongeza gharama ya kuhudumia wabunge 75 ambao hawakuwapo kabisa katika bunge la sasa la muungano. Ili kujua kama hawa wabunge walikuwapo au hawakuwapo hapo mwanzo lazima ujue majimbo ya muungano yamekaaje? Kwa mujibu wa rasmu ya katiba mpya, majimbo ya bunge la muungano ni mikoa yote ya Tanganyika (25) na Zanzibar (5), hivyo kila mkoa utatoa wabunge wawili (kwa uwiano wa 1:1 - me:ke). Kwa upande wa serikali ya Tanganyika majimbo yatabaki yale yale yaliyopo sasa hivi, maana hapo mwanzo hatukuwa na majimbo ya mikoa. Mtu mvivu kufikiria anaweza kusema sasa kama mkoa umetoa mbunge kuna haja gani tena kwa wilaya ile ile ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa (mfano Geita, Shinyanga, Arusha, Singida, Tabora n.k.) kutoa mbunge wa Tanganyika? Hii itakuwa ni upotoshaji, mbunge wa muungano ni wa jimbo la mkoa na atapigiwa kura na wakazi wote wa mkoa husika, wakati yule wa Tanganyika atapigiwa kura na wakazi wa jimbo husika. Hivyo sisi wapenzi wa serikali 3 tusikurupuke kusema itakuwa nafuu kuliko serikali 2, huu utakuwa upotishaji, bali tukubali kwamba kuna gharama mpya zitazaliwa lakini tutaweza kuzimudu (je! utatumia mbinu gani kuzikabili?). Hata UKAWA walipaswa kutengeneza partial budget ambayo ingeonesha mchanganuo wote wa gharama mpya na zile zinazojifuta, hapo wa-TZ wengi wangewaelewa, lakini sasa hivi wanapiga kelele kwa maelezo ya kufikirika kuliko uhalisia wake.

BADO TUNA KAZI YA KUFANYA WAKUU!!!

Mtu akiwa na akili kama za mbuni wa jangwani, ambaye huchimbia kichwa mchanagni akidhani amejificha, ni vigumu sana kuuona ukweli. Hebu jaribu kupitia michango yangu yote kabla ya kubisha.

Nimesema hivi: kwa sasa kuna wabunge 54 wa kutoka Zanzibar ndani ya JMT ambao hugharamiwa na serikali ya Tanganyika ( kwa kivuli cha Tanzania). Tukiingia kwenye shirikisho, hawa wabunge watapaswa warudi kwao. Hizi pesa tutakazookoa hapa tutazitumia kugharamia wabunge wetu 30 waliomo kwenye JMT ya Shirikisho. Pesa zitazosalia zitarudi serikali ya Tanganyika kwa ajili ya matumizi mengine.

Vyeo vya anasa kama vile wakuu mikoa, wakuu wa wilaya na wakuu wa tarafa vitafutwa. Tutabakiwa na wakurugenzi watendaji, makatibu tawala na maafisa utumishi wa majiji, manispaa na halmshauri. Hebu niambie tuna wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa wangapi katika nchi hii. Je, vyeo vyote hivi vikifutwa hatupati fedha za kuendesha nchi yetu ya Tanganyika na tukabakiwa na chenji ya kuchangia kwenye shirikisho?

Pamoja na haya yote, nchi ya Tanganyika itaongeza jitihada za kukusanya kodi, kupiga vita ufisadi na usafirishaji wa twiga kwenda uarabuni na ulaya. Hivyo nchi itakuwa na mapato ya kutosha kujiendesha. Hivi vyote ni vyanzao vya mapato. Sijui watu mnataka tuendelee kubebeshwa gharama za kipumbavu hadi lini. Serikali ikipunguza matumizi yake ya kipumbavu, kwa kutumia katiba mpya tutakayoitunga, nchi itapata pesa za kujiendesha na chenji itabaki.

Gharama za kuendesha serikali zitapunguzwa. Hakutakuwa na matumizi ya kipuuzi kama vile kununua samani na magari ya kifahari kutoka nje. Mawaziri watakuwa wanatumia magari ya kawaida kabisa—mashangingi na maV8 yatapigwa mnada wa hadhara na pesa zitakazopatikana zitatumika kununulia magari ya bei ndogo kwa ajili ya viongozi na chenji inayobaki tutaingiza kwenye matumizi mengine ya serikali.

Idadi ya wizara itapunguzwa hadi kufikia chini ya wizara 8 kutoka 29 za sasa na hakukutakuwa na uongezaji holela wa wizara kama ilivyo sasa. Mnadhani kwamba mawaziri kama Mwandosya wataendelea kuwepo katika serikali ya Tanganyika? Thubutu! Uongezaji wa kishikaji wa wizara kwa ajili ya kuwazawadia vyeo marafiki kwa gharama za wananchi utapigwa marufuku. Idadi ya wizara zinazotakiwa kuundwa zitaingizwa kwenye katiba. Kwa hiyo, rasi akiongeza wizara au akateua mawaziri zaidi ya wawili kusimamia wizara moja (kama ilivyo sasa) atakuwa wamevunja katiba. Marekani, pamoja na ukubwa wake wote ule, ina wizara 15 tu. Kwanini sisi tuwe na utitiri wa wizara wakati tungali masikini na ombaomba?

Haya makatazo yote yakiingia kwenye katiba, yatatusaidia kupata fedha za kutosha kuendesha nchi yetu hata bila kutegemea misaada ya masharti na masimango kutoka kwa wazungu. Tunapotafakari kuwa na serikali yetu ya Tanganyika inayojitegemea ni sharti tufikiri nje ya boksi. Tusikae tu kuimbishwa nyimbo za gharama bila kuchanganua mambo kwa kutumia vichwa vyetu wenyewe.
 
soma tena rasmu utapata picha ya serikali 3 hapa umeelezea serikali ya JMT. gharama ziko kwenye serikali za nchi washirika kwa kuwa watakuwa na mabunge yao na serikali zao pia.
 
Unachokizungumzia hapa ni gharama za mishahara ya Wabunge na Mawaziri wa Serikali ya Muungano pekee na nawashangaa hawa watu wengine wanaokusifia kwa Uchambuzi Wako Goigoi, kweli watu wengine hapa ni rahisi kupelekwa pelekwa tu, yaani hoja ikitolewa tu nyinyi kazi yenu kupiga makofi na kushangilia bila ya kuhoji. Sasa hapo inabidi uongezee na gharama za mishaahara ya Mawaziri na Wabunge wa serikali ya Tanganyika na Zanzibar.

Unakuja na mbwembwe na mikogo kibao halafu unaishia kutuandikia uchambuzi pumba, na hii iende kwenu wote mliounga mkono uchambuzi wake.

Naunga mkono hoja
 
Kwl kuna watu ni wagum kuelewa na ni hawa wakiingia mjengoni kwa khanga na kofia hubaki kushangilia kila kitu. Ni kipi hakieleweki hapa juu ya serikal mbl au tatu? Kwa mwenye hekima atafikiria, je, tumepata uhuru lini? Na je tulipata nafuu kupitia serikali mbili? Sasa unafuu utatoka wap sasa kwa serikal mbl? Mmesahau mikoa inaongezeka na wilaya kila cku? Vyeo hivi vya kisela vinatutafuna tu hamwoni? Mh, Mungu ibariki tz
 
Hapo Mkuu bado hujakamilisha kazi ya kushawishi watu kuwa serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2. Kumbuka kuwa umepigia serikali ya Muungano tu bado hujazungumzia Tanganyika na Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka kamili kama nchi washirika kwenye shirikisho. Kila nchi itakuwa na bunge lake ambao majimbo huenda yakabaki kama yalivyo kwa sasa. Hivyo basi, kama hivyo ndivyo, tutakuwa tumeongeza gharama za wabunge 75 ambao mwanzoni hawakuwapo. Labda kwa upande wa mawaziri hapo tutakuwa tumewahamisha waliokuwa wakihudumia kwenye serikali ya sasa ya muungano na hivyo baadhi ya wizara hazitakuwapo kwenye nchi washirika (zile zitakazoshughulikia mambo ya muungano), mfano wizara ya mambo ya nchi za nje; Ulinzi na JKT; Fedha, uchumi na mipango; Elimu na mafunzo ya ufundi; Afrika Mashariki, n.k.

Suala hapa ni kusema fedha ya kugharamia hao wabunge wapya 75 zitatoka wapi? Hapo ndipo wachumi wanatakiwa wapafanyie kazi maana magamba ndipo yaliposimamia! Ila ukiyasikiliza haya majamaa ni kama mataahira fulani vile, kuna moja liliibuka mle bungeni eti linahoji, ardhi ya kujenga hizo ikulu 3 (serikali ya muungano, Tanganyika na Zanzibar) itatoka wapi?

Hivyo tusikimbilie kusema tu serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2 bali tuainishe gharama zote na vyanzo vya mapato vya kugharamia hizo serikali (iwe 2 au 3), hapo ndiposa tutakuwa tumeweza kushawishiana!! Lakini kwa hili bandiko lako mheshimiwa, bado hujanishawishi (ingawa mimi naitaka Tanganyika yangu!!)

Link Warioba: Serikali ya Muungano haitakopa fedha - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Naomba sasa uzungumzie uwezo wa kila nchi yaani Tanganyika na Zanzibar, je kila mwanachama anaweza kumudu hizo gharama?
Hapa namaanisha wazanzibar wanaweza kugaramia serikali ya muungano na watanganyika vivo hivyo. Hivi kwa sasa wanachangiaje muungano nani anatoa asilimia ngapi na kwa mapato yapi?

Mkuu PESA zote za ulaya munachukua Tanganyika sasa unataka sisi wazanzibar tuwachangie nini?. Pesa muchukue nyinyi,kodi muchukue nyinyi na bado munataka Zanzibar iwachangie kwa lipi?
 
Unajua umeipngelea tanzania afu kwenye kufanania unafanisha na tanzania bara na zanzibar pili kumbuka hapo hatuna katiba ya tanganyika alaf zanzibar pia ana katiba yake na mawaziri wake ambayo na tanganyika itakua nayo wakitengeneza yao pengine isimbane mtawala wake kama ilivo ya zanzibar tatu kuna kuichangia serikali ya tatu n mzigo kwa zanzibar ndogo nne kwann usishauri serikali mbili na ya tanzania isizidishe hao mawazir 15 na hao wabunge 70 kama kweli unaipenda tanzania

Muungano mawaziri15. Tanganyika 16. Zanzibar 10. Jumla 41. Kwa sasa tuna 60. hahahah... naota tu mkuu sina data mie.
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Acha kupotosha watu , usidhani wote waliopo humu ni mapoyoyo wa hesabu kama wewe. Hebu mtaje waziri ambae anaelipwa milioni 20 kwa sasa? waziri mkuu mwenyewe mshahara wake hauzidi hata milioni 6.
 
Mkuu nakubalian nawe ila fahamu k2 kimoja (mm sio muumini wa serikali 2 au 3) ila naangalia uhalisia!

1. Baada ya kuunda serikali ya Tanganyika, kutakuwa na mawaziri ambao hawatakuwa wa muungano watakao shighulikia mambo ya Tanganyika (hawa watakuwa wangapi!!!!? katiba ta Tanganyika itaamua ---Hizi ni gharama za ziada ambazo utaziweka pale ulisema utasev kuhusu mawaziri...kupata ni sh ngapi unatakiwa kujua Tanganyika itakuwa na mawaziri wangapi!

2. Wabunge hali kadhalika watapungua ni sawa kusema tutasev bil 62 kama ilivyocema, je Tanganyika itakuwa na wabunge wangapi! hakuna ajuaye hadi katiba ya Tangayika itakapo tungwa.

My Take>
Kimsingi wote wanaosema gaharama za muungano zitapungua nikweli ila tunapojadili masuala haya nilazima tuakaangalia kwa mapana yake (sisi wananchi ni lazima tuwe na muono huo) kwani watawala wataangalia sehemu yao tu ya kiutawaka (mfani waziri wa MUungano atakwambia ni kweli gharama zimepungua) hawatakuwa na majibu halisi ya haya ila kwa wananchi tutakuwa tunafund project zote tutakwambia gharama zimeongezeka kwa kuunda serikali nyingine au zimepunguka au zimebaki kama zilivyokuwa in totality

Nakubaliana nawe kuwa Mwisho wa siku gaharama (kwa kuongeza Serikali ya Tanganyika) zinaweza kupungua au zikabaki kama zilivyo au zikazidi! so work done ikawa ni ZERO!
 
Mimi nilisema na nitaendelea kusema, kama maamuzi ya hatima ya MUUNGANO wetu, kigezo kikubwa ni GHARAMA za uendeshaji wa serikali, i.e. S2 v S3, kwanini basi tusiende kwenye S1? Kwanini hili CCM au CDM hata wale 201 hawalisemi? Maana yake ni kwamba gharama sio kigezo kikubwa cha maamuzi ya MUUNDO wa MUUNGANO. Kuna vigezo vingine MUHIMU zaidi vitakavyoamua aina ya muundo wa muungano wetu. Hivyo CCM wasijifiche kwenye KICHAKA cha gharama kukataa S3, Waje na sababu nyingine nzuri ambazo ni tangible. Mimi wakiniambia gharama, nitawaambia basi twende kwenye S1.
 
Sasa hiyo uliyoleta ni ya Serikali moja katika tatu, halafu tuwekee na gharama za hizo Serikali mbili ulizoacha kukokotoa.

Ni ngumu sana kujua gharama za uendeshaji wa Serikali ya Tanganyika, kwasababu haipo(?) in the first place. Mbaya ni kwamba Watanzania hatujiulizi haya maswali magumu, tumebakia na mipasho na light touch story hadi huko kwenye BMK. Lakini kwakuwa rasimu ya S3 tunayo, na pili kwa kuwa SMZ tayari ipo. Hii inaweza ikawa reference nzuri ya kufanya comparative analysis ya uendeshaji wa S2 v S3 kwa kutumia SMZ as a reference point. Wachambuzi watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani ya S2 zikoje. Na pia watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani S3 zitakuwaje kwa kutumia rasimu ya katiba. Hata kama sasa SMZ haichangii SMT is not excuse. To be fair kwa akili ya kawaida tu kwa mtu yeyote aliyesoma algebra. Kama tutakwenda kwenye S3, SMZ itagharamikia zaidi kuendesha serikali SMZ na Serikali ya Muungano), but at the same time Tanganyika itagharamikia kidogo/itapunguza gharama za kuendesha serikali Serikali ya Tangayika na muungano). Kama tutaamua kuendelea S2, SMZ itagharamikia kidogo kuendesha serikali (SMZ na Muungano) kwasababu gharama zote na Muungano atazibeba Tanganyika ambaye amejivisha KOTI la Muungano. Huo ndiyo UKWELI wenyewe.
 
Back
Top Bottom