Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Tukitaka kupunguza gharama tuelekee serikali moja baasi vinginevyo serikali tatu na mbili zote ni gharama kuziendesha
 
Mkuu serikali Ni 1 tu, Hakuna 2 wala 3 mtumish aliyetukuka mh. Hayat Mwl nyerere(namheshm sana mi mwenzenu)alikosea sana tena sana wkt wamakubaliano Na Mh. Karume.Wazo la karume kuwa tuunde serikali moko Na yy angekuwwa makamu Wa rais lilikuwa sahihi kabisa. Ewe Nyerere kuteleza kwako Leo umetuachia msala Na Kansa ya maslahi Na ubnafs.Hata wkt Karume anakufa Ni jukum la serkali ya Nyerere kuipora kabisa Znz kwa gharama yoyote Na mwisho Wa cku ya Leo ZNZ ingebak mikoa tu ya Tanganyika ya Tnzania.yaani Mkoa Wa Unguja Na Mkoa Wa Pemba.Yeyote angejiinua tungemleta ale bata huku Dsm hatak tungemjumbe... Huyo Jamaa Nyla maada amejiona ana akili lkn akubali serkali 3 Ni gharama... Hakuweka gharama za bunge la tanganyka wala SMZ.Na baraza Lao.
 
Unachokizungumzia hapa ni gharama za mishahara ya Wabunge na Mawaziri wa Serikali ya Muungano pekee na nawashangaa hawa watu wengine wanaokusifia kwa Uchambuzi Wako Goigoi, kweli watu wengine hapa ni rahisi kupelekwa pelekwa tu, yaani hoja ikitolewa tu nyinyi kazi yenu kupiga makofi na kushangilia bila ya kuhoji. Sasa hapo inabidi uongezee na gharama za mishaahara ya Mawaziri na Wabunge wa serikali ya Tanganyika na Zanzibar.

Unakuja na mbwembwe na mikogo kibao halafu unaishia kutuandikia uchambuzi pumba, na hii iende kwenu wote mliounga mkono uchambuzi wake.
 
Unaijua serikali ya Tanganyika itakuwa na mawaziri wangapi?
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Vema, ila naomba tuletee pia gharama za uendeshaji wa serikali za nchi washirika yaani Tanganyika na Zanzibar. tukipata hizo hesabu tutaweza kuamua vizuri. Vinginevyo 2 au 3 ni siasa tu.
 
Mkuu hapo cjakuelewa. Ila jua kitu kimoja hapo.kwamba Hao wabunge 70 ujue ni wa muungano so huwezi kulinganisha na wabunge399 kwa7bu hao wote ni mchanganyiko wa tz bara na visiwani.

Mkuu, hao 399 ni wa JMT (Tanganyika na Zanzibar). Niko sahihi.
 
Chambua serikali ya Tanganyika na Zanzibar pia. Umechukua serikali ya Shirikisho kisha unaita gharama ya s3!!
 
Hizo takwimu zina kasoro. Rudi shule kidogo. Hapo Tanganyika haijawekwa.

Suala la Tanganyika lisikupe hofu. Tanganyika ina rasilimali za kutosha kujiendesha hata bila kutegemea misaada. Tatizo ni usimamizi mbovu wa rasilimali zilizopo nchini ndio linaloleta shida.
 
Unachokizungumzia hapa ni gharama za mishahara ya Wabunge na Mawaziri wa Serikali ya Muungano pekee na nawashangaa hawa watu wengine wanaokusifia kwa Uchambuzi Wako Goigoi, kweli watu wengine hapa ni rahisi kupelekwa pelekwa tu, yaani hoja ikitolewa tu nyinyi kazi yenu kupiga makofi na kushangilia bila ya kuhoji. Sasa hapo inabidi uongezee na gharama za mishaahara ya Mawaziri na Wabunge wa serikali ya Tanganyika na Zanzibar.

Unakuja na mbwembwe na mikogo kibao halafu unaishia kutuandikia uchambuzi pumba, na hii iende kwenu wote mliounga mkono uchambuzi wake.

Nipinge kwa kutumia facts and figures kama ambavyo mimi nimeweka figures. Vinginevyo hutaeleweka. Ubishi wa kizombi na usiokuwa na mantiki kama huu wako ndio unapelekea mnaitwa majina ya ajabu ajabu kama vile Intarahamwe, nk.
 
Ndani ya Muundo wa Serikali Mbili haiwezekani kuwa na baraza la mawaziri wasiozidi 10? kwani haiwezekani kuwa na wabunge 30 tukitaka ndani ya serikali 2?..Bado wenye kung'ang'ania serikali 2 au 3 hawajaweza kunishawishi vya kutosha kuwa mifumo yao itatatua kero zilizoko na kutuletea maendeleoa ambayo wananchi wanayatamani...
 
Mkuu hao mawaziri 60 ni wa muungano+Tanganyika na hao 15 wanaozungumziwa kwenye rasmu ni wa Muungano peke yake hizo gharama ulizokokotoa ni za kuendesha serikali ya muungano peke yake hapo hujaelezea gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika kama utaweza hebu jaribu kutuwekea idadi ya wabunge na mawaziri wa Tanganyika na pesa itayotumika kuwalipa usisahau kama kuna mahakama pia ya Tanganyika na ya Muungano

Mkumbuke hatuna katiba ya Tanganyika inaweza ikawa na mawaziri wachache kama wa muungano. Huu ndio ukweli lakini ma ccm yanaimba kama kasuku tu bila kuwa na facts.
 
Tundu Lissu aliwaambia. Ila hapo umezungumzia bajeti ya muungano. Bajeti ya Tanganyika na Unguja je?

unguja wanabajeti yao hadi hivi sasa,Tanganyika tutaunda katiba yenye ukomo wa wizara si kama uholela tulionao.
 
Kwa kukusaidia ili uelewe watu wanakuambia nini, chambua haraka za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na gharama zitakazokuwepo za kuendesha serikali 3
 
Huo uchambuzi haujaenda shule. Unaelewa maana ya Serikali tatu?

Wewe unayeelewa unashindwa nini kufafanua na kutuletea takwimu tuzione hapa? Acha ubishi wa kizombi!
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Hapo Mkuu bado hujakamilisha kazi ya kushawishi watu kuwa serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2. Kumbuka kuwa umepigia serikali ya Muungano tu bado hujazungumzia Tanganyika na Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka kamili kama nchi washirika kwenye shirikisho. Kila nchi itakuwa na bunge lake ambao majimbo huenda yakabaki kama yalivyo kwa sasa. Hivyo basi, kama hivyo ndivyo, tutakuwa tumeongeza gharama za wabunge 75 ambao mwanzoni hawakuwapo. Labda kwa upande wa mawaziri hapo tutakuwa tumewahamisha waliokuwa wakihudumia kwenye serikali ya sasa ya muungano na hivyo baadhi ya wizara hazitakuwapo kwenye nchi washirika (zile zitakazoshughulikia mambo ya muungano), mfano wizara ya mambo ya nchi za nje; Ulinzi na JKT; Fedha, uchumi na mipango; Elimu na mafunzo ya ufundi; Afrika Mashariki, n.k.

Suala hapa ni kusema fedha ya kugharamia hao wabunge wapya 75 zitatoka wapi? Hapo ndipo wachumi wanatakiwa wapafanyie kazi maana magamba ndipo yaliposimamia! Ila ukiyasikiliza haya majamaa ni kama mataahira fulani vile, kuna moja liliibuka mle bungeni eti linahoji, ardhi ya kujenga hizo ikulu 3 (serikali ya muungano, Tanganyika na Zanzibar) itatoka wapi?

Hivyo tusikimbilie kusema tu serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2 bali tuainishe gharama zote na vyanzo vya mapato vya kugharamia hizo serikali (iwe 2 au 3), hapo ndiposa tutakuwa tumeweza kushawishiana!! Lakini kwa hili bandiko lako mheshimiwa, bado hujanishawishi (ingawa mimi naitaka Tanganyika yangu!!)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom