Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

kama ya tanganyika itapunguza gharama basi tuvunje muungano kwani ulazima wa kuungana ni upi
 
Kwa hiki ulichokiandika naomba uelewe katika hili suala la kutaka serikali 2 linapiganiwa sana na hawa wabunge wa CCM Bara na Zanzibar kuanzia Wabunge wao na Raia wengi hawaitaki hiyo Serikali 2 ila hawa wa CCM kule Zanzibari wanalazimishwa na MFUMO. sasa kama hoja ni TANGANYIKA ndio inayoumia kuchangia hii serikali ya Muungano kwa nini hawa wabunge wa CCM Bara wanashabikia sana Serikali 2 ambazo kwa mtazamo wako sisi waBara ndio tunaoumia na Muungano huu wa Serikali 2?

Wadau;

CCM bara wanahangaika kulinda muundo wa sasa maana ndio mkondo na mtaro wao wa kupitishia ufisadi, uhujumu wa mali ya umma ili kuneemesha matumbo yao. Wameshahamasishana kuwa Rasimu ya 2, na ktk Serikali 3 zinapunguza madaraka, ukubwa wa serikali, mgawanyiko wa mali (equal sharing of resources), na kuweka tunu za taifa ambazo zinawaadabisha ccm ambao wanakula mno bila kunawa ktk mfumo wa sasa...lazima waogope kupindukia na wafanye wawezavyo kuulinda ufidhuli huo. Hakuna hoja nyingine, ndio maana wanahaha na kutangaza kuingia msituni kama mtaro wao huo utaonekana kuzibwa! Je watu kama hawa ni binadamu wenye akili au ni kusanyiko la majuha wahuni wanaoongozwa na kufikiria kwa njia ya matumbo yao? Kuna hoja hapo? naomba majibu kama yupo mwenye nayo..!
 
Mtu akiwa na akili kama za mbuni wa jangwani, ambaye huchimbia kichwa mchanagni akidhani amejificha, ni vigumu sana kuuona ukweli. Hebu jaribu kupitia michango yangu yote kabla ya kubisha.

Nimesema hivi: kwa sasa kuna wabunge 54 wa kutoka Zanzibar ndani ya JMT ambao hugharamiwa na serikali ya Tanganyika ( kwa kivuli cha Tanzania). Tukiingia kwenye shirikisho, hawa wabunge watapaswa warudi kwao. Hizi pesa tutakazookoa hapa tutazitumia kugharamia wabunge wetu 30 waliomo kwenye JMT ya Shirikisho. Pesa zitazosalia zitarudi serikali ya Tanganyika kwa ajili ya matumizi mengine.

Vyeo vya anasa kama vile wakuu mikoa, wakuu wa wilaya na wakuu wa tarafa vitafutwa. Tutabakiwa na wakurugenzi watendaji, makatibu tawala na maafisa utumishi wa majiji, manispaa na halmshauri. Hebu niambie tuna wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa wangapi katika nchi hii. Je, vyeo vyote hivi vikifutwa hatupati fedha za kuendesha nchi yetu ya Tanganyika na tukabakiwa na chenji ya kuchangia kwenye shirikisho?

Pamoja na haya yote, nchi ya Tanganyika itaongeza jitihada za kukusanya kodi, kupiga vita ufisadi na usafirishaji wa twiga kwenda uarabuni na ulaya. Hivyo nchi itakuwa na mapato ya kutosha kujiendesha. Hivi vyote ni vyanzao vya mapato. Sijui watu mnataka tuendelee kubebeshwa gharama za kipumbavu hadi lini. Serikali ikipunguza matumizi yake ya kipumbavu, kwa kutumia katiba mpya tutakayoitunga, nchi itapata pesa za kujiendesha na chenji itabaki.

Gharama za kuendesha serikali zitapunguzwa. Hakutakuwa na matumizi ya kipuuzi kama vile kununua samani na magari ya kifahari kutoka nje. Mawaziri watakuwa wanatumia magari ya kawaida kabisa—mashangingi na maV8 yatapigwa mnada wa hadhara na pesa zitakazopatikana zitatumika kununulia magari ya bei ndogo kwa ajili ya viongozi na chenji inayobaki tutaingiza kwenye matumizi mengine ya serikali.

Idadi ya wizara itapunguzwa hadi kufikia chini ya wizara 8 kutoka 29 za sasa na hakukutakuwa na uongezaji holela wa wizara kama ilivyo sasa. Mnadhani kwamba mawaziri kama Mwandosya wataendelea kuwepo katika serikali ya Tanganyika? Thubutu! Uongezaji wa kishikaji wa wizara kwa ajili ya kuwazawadia vyeo marafiki kwa gharama za wananchi utapigwa marufuku. Idadi ya wizara zinazotakiwa kuundwa zitaingizwa kwenye katiba. Kwa hiyo, rasi akiongeza wizara au akateua mawaziri zaidi ya wawili kusimamia wizara moja (kama ilivyo sasa) atakuwa wamevunja katiba. Marekani, pamoja na ukubwa wake wote ule, ina wizara 15 tu. Kwanini sisi tuwe na utitiri wa wizara wakati tungali masikini na ombaomba?

Haya makatazo yote yakiingia kwenye katiba, yatatusaidia kupata fedha za kutosha kuendesha nchi yetu hata bila kutegemea misaada ya masharti na masimango kutoka kwa wazungu. Tunapotafakari kuwa na serikali yetu ya Tanganyika inayojitegemea ni sharti tufikiri nje ya boksi. Tusikae tu kuimbishwa nyimbo za gharama bila kuchanganua mambo kwa kutumia vichwa vyetu wenyewe.

Uchambuzi wako ni hafifu sana! Sasa hivi umekuja na wabunge 30 wa muungano umewapata wapi? Kaisome tena rasmu ili ujue bunge la muungano litakuwa na wabunge wangapi? Unazungumzia Tanganyika ambayo haipo, una uhakika gani katiba itasema kama unavyofikria? Tuache kupotosha S3 ni ghari kuliko S2. Ila kuwa na S3 it is doer able! Umezungumza kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya, kwa katiba ipi? Je, tujadili kitu cha kufikirika? GT we can not do that!!
 
Maajabu ni kuwa wazanzibar wanataka S3

MWEN. Hapo ndiyo ninashindwa kuwashangaa kabisa Watanganyika na Wazanzibari! Wazanzibari WANATAKA S3 zitakazo waongezea gharama za kuendesha serikali (SMZ na Shirikisho). Lakini upande mwingine Watanganyika WANATAKA S2 zinazo waongezea gharama za kuendesha serikali, kwasababu Tanganyika imevaa KOTI la muungano. Sisi Watanzania ni VIUMBE wa ajabu sana.
 
Uchambuzi wako ni hafifu sana! Sasa hivi umekuja na wabunge 30 wa muungano umewapata wapi? Kaisome tena rasmu ili ujue bunge la muungano litakuwa na wabunge wangapi? Unazungumzia Tanganyika ambayo haipo, una uhakika gani katiba itasema kama unavyofikria? Tuache kupotosha S3 ni ghari kuliko S2. Ila kuwa na S3 it is doer able! Umezungumza kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya, kwa katiba ipi? Je, tujadili kitu cha kufikirika? GT we can not do that!!

Tuliza akili utanielewa. nimesema kwamba serikali ya Tanganyika itachangia wabunge 30 kwenye bunge la JMT. Sasa Tanganyika ya leo iliyovaa koti la muungano (Tanzania) inaweza kugharamia wabunge 54 kutoka Zanzibar itashindwaje kugharamia wabunge wake 30 ndani ya bunge la JMT? Huoni kwamba kuna unafuu wa gharama za wabunge 24 ambazo tutazitumia ktk matumizi mengine ya nchi yetu ya Tanganyika? Na je serikali yetu itakapofuta vyeo vya kifalme huoni tutaokoa fedha nyingi za umma zinazoteketea bila sababu?
 
Tena hatujaweka mshara anaolipwa kama mbunge, paendekezo ya Katiba Mpya noi kuwaondoa wabunge wasiwe Mawaziri

Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:
 
Kwa uelewa wako katiba ya Tanganyika ilishatebgenezwa? Je inasemaje katika muundo wa serikali?
Kama jibu ni bado basi ujue na hiyo itatengenezwa kulingana na uhitaji na uwezo wa kibajeti wa watanzania.

Amka na jitambue, Tizama jinsi maisha yako yanavyomuathiri jirani yako. Je ungefanyiwa wewe unfelikubali?

Mkuu Pengine umechanganya mafaili mimi nimesema alichoeleza mleta mada ni gharama za kuendesha Serikali ya muungano hauwezi ukasema serikali tatu ni nafuu kuliko Serikali mbili wakati hujui ya kuendesha hizo serikali mbili Zilizobaki angekuwa amechanganua gharama za kuendesha serikali zote tatu againist Serikali mbili hapo kusingekuwa na Shida

Halafu hapa mleta mada kaongelea Wabunge na Mawaziri tu Hajazungumzia Mahakama Taasisi nyingine
Nimesema muungano wa kweli ni wa Serikali Moja
 
Kuna wachangangiaji wengine humu ambao wao wanachofahamu ni kubisha tu, lakini ukiwauliza huo ubishi wao wanaupata wapi, hawawezi kukujibu. Inawezekana hasa hao wanaobisha sana huenda hawajawahi kuisoma rasimu yenyewe na kuchambua kilichomo. Kwa makusudi kabisa, nimeambatanisha nakala ya rasimu kwenye barua hii ili wale ambao hawajapata kuiona waisome na kuichambua ili wanapobisha wabishe kwa kutumia reference badala ya kupiga kelele tupu kama madebe shinda.

TUNAENDELEA NA MJADALA WETU WA KUTETEA URAHISI WA SERIKALI 3:

Uchambuzi wa Rasimu yenyewe unaonyesha kwamba gharama za kuendeshea muundo wa shirikisho lenye serikali tatu zinaweza kuwa hata ndogo kuliko gharama za kuendeshea muundo wa Muungano wa serikali mbili za sasa:

(i) Hadi sasa hakuna mtu yeyote au taasisi iliyofanya uchambuzi wa ulinganifu wa gharama za kuendesha serikali – iwe moja, mbili au tatu – katika nchi yetu. Kwa sababu hiyo, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba kuendesha serikali tatu ni ghali zaidi kuliko kuendesha serikali mbili;

(ii) Kama suala la gharama za kuendeshea serikali ndio jambo muhimu zaidi katika kuamua muundo wa Muungano, wanaopinga shirikisho la serikali tatu wangeeleweka kama wangependekeza muundo wa serikali moja tu, badala ya serikali mbili za sasa wanazoziunga mkono, au tatu zilizopendekezwa na Rasimu;

(iii) Kama mapendekezo ya Rasimu juu ya Mambo ya Muungano yakichukuliwa kuwa kigezo cha kupima ukubwa wa serikali – na kwa hiyo gharama za kuiendeshea – basi gharama za serikali ya Muungano zinaweza kuwa ndogo sana:

a. Kwa mambo saba ya Muungano yanayopendekezwa na Rasimu, hakutakuwa na zaidi ya wizara nne za Serikali ya Muungano. Hivyo, kwa mfano, kutakuwa na wizara ya katiba na sheria itakayoshughulikia masuala ya Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano; wizara ya ulinzi itakayokuwa na majukumu ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano; wizara ya fedha itakayoshughulikia masuala ya sarafu na benki kuu, na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano; na wizara ya mambo ya nje. Masuala yaliyobaki, yaani uraia na uhamiaji na usajili wa vyama vya siasa hayastahili kuwa na wizara zinazojitegemea kwa hiyo yanaweza kuwekwa chini ya mojawapo ya wizara zilizotajwa hapo juu;

b. Aya ya 93(2) ya Rasimu inapendekeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano kuwa mawaziri wasiozidi kumi na tano. Hata hivyo, aya ya 93(3) inaelekeza kwamba “Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na Wizara kwa kuzingatia mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii.” Kwa maana nyingine ukubwa wa Serikali lazima uzingatie Mambo saba ya Muungano. Kwa sababu hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano haiwezi kuwa na mawaziri wengi kuliko Mambo saba ya Muungano;

c. Kwa mtazamo huo huo wa aya ya 93(3) na orodha ya Mambo ya Muungano kama kipimo cha ukubwa wa Serikali ya Muungano, haiwezekani Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu wanaopendekezwa katika aya za 98 na 99 za Rasimu kuwa zaidi ya wanne;

d. Kwa kuzingatia idadi ya Makatibu Wakuu wenyewe, Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu inayoelezwa katika aya ya 100 na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inayotajwa katika aya ya 101, hazina maana wala umuhimu wowote kikatiba;

e. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu kuhusu Bunge la Jamhuri ya Muungano katika aya ya 105, kwa idadi ya sasa ya mikoa ya Tanzania Bara na wilaya za Zanzibar, Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa na wabunge 75. Kwa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, endapo Bunge la Zanzibar litakuwa na Wabunge hamsini wa majimbo ya sasa ya uchaguzi, wakati bunge la Tanganyika litakuwa na wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi ya sasa. Kwa maana hiyo, muundo wa Muungano wa serikali tatu utakuwa na mabunge matatu yenye jumla ya wabunge 314;

f. Kwa kulinganisha, Bunge la Jamhuri ya Muungano la sasa lina idadi ya wabunge 399. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kuna jumla ya Wawakilishi 91. Kwa maana hiyo, kwa muundo wa sasa wa Muungano, mabunge mawili tuliyonayo yana idadi ya wabunge 490. Idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu kwa wabunge 124! Hapa kuna unafuu wa gharama za kulipa wabunge 366 (sawa na unafuu wa Tsh 5.9 bilion). Hizi pesa zinatosha kabisa kuendesha serikali ndogo ya muungano na tukabakiwa na chenji tukafanyia mambo mengine.

g. Taasisi nyingine za Muungano zinazopendekezwa kama vile Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali (aya ya 102); Tume ya Utumishi wa Mahakama (aya ya 172); na Tume ya Utumishi wa Umma (aya ya 178) haziwezi kuwa kubwa sana kwa kuzingatia ukubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Rasimu;

h. Taasisi nyingine kama vile Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji (aya ya 188) na Tume ya Haki za Binadamu (aya ya 194) hazipo kwenye orodha ya Mambo ya Muungano na uwepo wao kwenye Rasimu unakinzana na matakwa ya aya za 59(1) na 60 za Rasimu. Kama majukumu ya taasisi hizo hayahusu Mambo ya Muungano, Tume hizo haziwezi kugharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

i. Majukumu ya utekelezaji wa Mambo mengine ya Muungano kama uchaguzi na usajili wa vyama vya siasa yanaweza kutekelezwa na taasisi husika za Washirika wa Muungano kwa makubaliano na masharti maalumu chini ya aya ya 59(3) ya Rasimu. Hii nayo itapunguza gharama za kuendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
View attachment 153735
 
Lakini pia mkumbuke kwamba kuna pesa nyingi sana ambazo zinapotea kupitia misamaha ya kodi, mikataba hewa ya uwekezaji na ufisadi. Hizi tukijumlisha na zile fedha ambazo tutaziokoa kwa kufuta vyeo vya kisultani vya wakuu wa mikoa na wilaya, hakika tutapata pesa za kutosha kuendeshea serikali ya muungano. Imagine pia mkuu akikubali kutoa zile bilioni 60 za EPA zikajumlishwa kwenye haya mahesabu...mnadhani tutakuwa na pesa ngapi? Obviously, tuatakuwa na mabilioni ya fedha. Pamoja na hayo kuna pesa nyingi sana zinapotea kupitia misamaha ya kodi na kutosimamia vizuri mapato ya serikali.

Bado najaribu kuwaonyesha mahali zilipo fedha za kuendeshea serikali lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watu hawataki kuelewa. Tena gharama za kuwahudumia wakuu wa wilaya na mikoa ni kubwa maradufu ya gharama za kumhudumia waziri. Wakuu wa mikoa na wilaya wanaishi maisha ya anasa sana hata kuliko mawaziri wa serikali. Sema tu watu wengi huwa mna-overlook gharama kama hizi.
 
Kwa mengine umesema kweli, ila hapo kwenye red napingana na wewe. Serikali ya Tanganyika haitakuwa na mawaziri kwa idadi kama hii tuliyo nayo maana wizara za muungano zitahama na mawaziri wake, hivyo nchi washirika hazitakuwa na mawaziri kama wale wa wizara za muungano. Mfano, wizara ya mambo ya nchi za nje; wizara ya ulinzi na JKT n.k nchi washirika hawatakuwa na wizara ya mambo ya nchi za nje n.k. Hivyo nchi washirika watapunguza idadi ya mawaziri. Upotoshaji mwingine unaofanywa na wale waumini wa serikali 2 ni kuhusu majeshi, kwamba serikali ya muungano itapata wapi fedha za kuwalipa? Ukweli ni kwamba majeshi yote yatakuwa chini ya serikali ya muungano na nchi washirika hazitakuwa na majeshi yake, bali kazi ya ulinzi na usalama itafanywa na majeshi ambayo yatakuwa chini ya muungano.

Sawa ukweli ni kuwa serikali 3 zitakuwa na gharama za ziada lakini zinaweza kukabilika!!!

Mkuu haakuna gharama za ziada kwa serikali tatu! Kumbuka kama ni wabunge hao 50 ndo hao hoo sasa hivi tuna wabunge nadhani 50+ kutokaa visiwani kwenye bunge la sasa. Kwenye serikali tatu gharama za hawa wabunge zitahamia kwenye serikali ya muungano kugharimia wabunge 50+ kutoka Tanganyika na visiwani watawagharimia hao 20 wanotoka kwao. Hivyo kuhusu wabunge na mawaziri wa muungano hamna gharama ya ziada!
 
. .

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:
tpaul
serikali ya Tanganyika itakuwa na ukubwa gani?
bunge la Tanganyika litakuwa na ukubwa gani?
isijakuwa linarithi umbile la hili la Muungano.....!!!
Total cost= Tanganyika + Zenji + Shirikisho.
 
tpaul
serikali ya Tanganyika itakuwa na ukubwa gani?
bunge la Tanganyika litakuwa na ukubwa gani?
isijakuwa linarithi umbile la hili la Muungano.....!!!
Total cost= Tanganyika + Zenji + Shirikisho.

Mkuu, ukubwa wa serikali ya muungano umeelezwa kwenye rasimu. Hebu fungua hiyo rasimu niliyoambatanisha hapo juu uisome. Kwa ufupi ni kwamba, serikali ya muungano itakuwa ndogo sana kuliko watu wengi wasnavyoogopeshwa kwa kukaririshwa majawabu bila kutumia uchanganuzi yakinifu.
 
Rasimu imeainisha ukubwa wa serkali na bunge la Muungano.
Kweli ni remarkably ndogo.
Ya Zanzibar tunajua ipo na ukubwa wake unajulikana.
Ya Tanganyika imeainisha kwenye Rasimu?
 
Kuna wachangangiaji wengine humu ambao wao wanachofahamu ni kubisha tu, lakini ukiwauliza huo ubishi wao wanaupata wapi, hawawezi kukujibu. Inawezekana hasa hao wanaobisha sana huenda hawajawahi kuisoma rasimu yenyewe na kuchambua kilichomo. Kwa makusudi kabisa, nimeambatanisha nakala ya rasimu kwenye barua hii ili wale ambao hawajapata kuiona waisome na kuichambua ili wanapobisha wabishe kwa kutumia reference badala ya kupiga kelele tupu kama madebe shinda.

TUNAENDELEA NA MJADALA WETU WA KUTETEA URAHISI WA SERIKALI 3:

Uchambuzi wa Rasimu yenyewe unaonyesha kwamba gharama za kuendeshea muundo wa shirikisho lenye serikali tatu zinaweza kuwa hata ndogo kuliko gharama za kuendeshea muundo wa Muungano wa serikali mbili za sasa:

(i) Hadi sasa hakuna mtu yeyote au taasisi iliyofanya uchambuzi wa ulinganifu wa gharama za kuendesha serikali – iwe moja, mbili au tatu – katika nchi yetu. Kwa sababu hiyo, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba kuendesha serikali tatu ni ghali zaidi kuliko kuendesha serikali mbili;

(ii) Kama suala la gharama za kuendeshea serikali ndio jambo muhimu zaidi katika kuamua muundo wa Muungano, wanaopinga shirikisho la serikali tatu wangeeleweka kama wangependekeza muundo wa serikali moja tu, badala ya serikali mbili za sasa wanazoziunga mkono, au tatu zilizopendekezwa na Rasimu;

(iii) Kama mapendekezo ya Rasimu juu ya Mambo ya Muungano yakichukuliwa kuwa kigezo cha kupima ukubwa wa serikali – na kwa hiyo gharama za kuiendeshea – basi gharama za serikali ya Muungano zinaweza kuwa ndogo sana:

a. Kwa mambo saba ya Muungano yanayopendekezwa na Rasimu, hakutakuwa na zaidi ya wizara nne za Serikali ya Muungano. Hivyo, kwa mfano, kutakuwa na wizara ya katiba na sheria itakayoshughulikia masuala ya Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano; wizara ya ulinzi itakayokuwa na majukumu ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano; wizara ya fedha itakayoshughulikia masuala ya sarafu na benki kuu, na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano; na wizara ya mambo ya nje. Masuala yaliyobaki, yaani uraia na uhamiaji na usajili wa vyama vya siasa hayastahili kuwa na wizara zinazojitegemea kwa hiyo yanaweza kuwekwa chini ya mojawapo ya wizara zilizotajwa hapo juu;

b. Aya ya 93(2) ya Rasimu inapendekeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano kuwa mawaziri wasiozidi kumi na tano. Hata hivyo, aya ya 93(3) inaelekeza kwamba “Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na Wizara kwa kuzingatia mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii.” Kwa maana nyingine ukubwa wa Serikali lazima uzingatie Mambo saba ya Muungano. Kwa sababu hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano haiwezi kuwa na mawaziri wengi kuliko Mambo saba ya Muungano;

c. Kwa mtazamo huo huo wa aya ya 93(3) na orodha ya Mambo ya Muungano kama kipimo cha ukubwa wa Serikali ya Muungano, haiwezekani Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu wanaopendekezwa katika aya za 98 na 99 za Rasimu kuwa zaidi ya wanne;

d. Kwa kuzingatia idadi ya Makatibu Wakuu wenyewe, Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu inayoelezwa katika aya ya 100 na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inayotajwa katika aya ya 101, hazina maana wala umuhimu wowote kikatiba;

e. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu kuhusu Bunge la Jamhuri ya Muungano katika aya ya 105, kwa idadi ya sasa ya mikoa ya Tanzania Bara na wilaya za Zanzibar, Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa na wabunge 75. Kwa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, endapo Bunge la Zanzibar litakuwa na Wabunge hamsini wa majimbo ya sasa ya uchaguzi, wakati bunge la Tanganyika litakuwa na wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi ya sasa. Kwa maana hiyo, muundo wa Muungano wa serikali tatu utakuwa na mabunge matatu yenye jumla ya wabunge 314;

f. Kwa kulinganisha, Bunge la Jamhuri ya Muungano la sasa lina idadi ya wabunge 399. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kuna jumla ya Wawakilishi 91. Kwa maana hiyo, kwa muundo wa sasa wa Muungano, mabunge mawili tuliyonayo yana idadi ya wabunge 490. Idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu kwa wabunge 124! Hapa kuna unafuu wa gharama za kulipa wabunge 366 (sawa na unafuu wa Tsh 5.9 bilion). Hizi pesa zinatosha kabisa kuendesha serikali ndogo ya muungano na tukabakiwa na chenji tukafanyia mambo mengine.

g. Taasisi nyingine za Muungano zinazopendekezwa kama vile Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali (aya ya 102); Tume ya Utumishi wa Mahakama (aya ya 172); na Tume ya Utumishi wa Umma (aya ya 178) haziwezi kuwa kubwa sana kwa kuzingatia ukubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Rasimu;

h. Taasisi nyingine kama vile Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji (aya ya 188) na Tume ya Haki za Binadamu (aya ya 194) hazipo kwenye orodha ya Mambo ya Muungano na uwepo wao kwenye Rasimu unakinzana na matakwa ya aya za 59(1) na 60 za Rasimu. Kama majukumu ya taasisi hizo hayahusu Mambo ya Muungano, Tume hizo haziwezi kugharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

i. Majukumu ya utekelezaji wa Mambo mengine ya Muungano kama uchaguzi na usajili wa vyama vya siasa yanaweza kutekelezwa na taasisi husika za Washirika wa Muungano kwa makubaliano na masharti maalumu chini ya aya ya 59(3) ya Rasimu. Hii nayo itapunguza gharama za kuendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
View attachment 153735

Mkuu na cement kidogo, kama tukiamua kutumia mfumo wa kupata wabunge ulivyopendekzwa n tume basi kwenye bunge la Tanganyika tutafuta vitu maalumu na kuruhusu kuwa na wagombea wawili kila jimbo yaani baba na mama, hivyo kwa majimbo ya sasa 189 tutakuwa na wabunge 378. Hivyo jumla ya wabunge wote Tanganyika na muungano kwenye mabunge yote mawili watakuwa (378+75)=453. Kama kwa wale wa serikali mbili wakiamua kutumia pia mfumo huu wa uwakilishi wa baba na mama kila jimbo nao utakuwa na wabunge 378 kutoka bara na 100 kutoka visiwani na kuwa 478.Hapa tunaona serikali tatu ina idadi ndogo ya jumla kuliko mbili Sijui mgawanyiko wa sasa wa kutumia vitu maalumu ulivyo kama kuna anayefahamu aweke hapa mchanganuo wake pia
 
Rasimu imeainisha ukubwa wa serkali na bunge la Muungano.
Kweli ni remarkably ndogo.
Ya Zanzibar tunajua ipo na ukubwa wake unajulikana.
Ya Tanganyika imeainisha kwenye Rasimu?

Serikali ya Tanganyika kuna oportnity ya kuipunguza kwa mfano kuondoa wakuu wa wilaya na kutumia mameya badala yake. Pia wakurugenzi wa wilaya wanaweza kuajiliwa na ya serikali za mitaa hivyo wanaondoka kwenye serikali kuu ya Tanganyika. Bunge la Tanganyika litakuwa na wawakilishi wawili kila jimbo yaani baba na mama na kuondoa vitu maalumu vya sasa. Hivyo kwa majimbo 189 kama sikosei ya sasa tunakuwa na wabunge 378 ukiongeza labda 10 kwa walemavu. Na kama tukiamua hwakilishi wa baba na mama basi majimbo yanaweza kupunguzwa na kutumia wilaya kama majimbo badala ya sasa wilaya moja inakuwa na majimbo zaidi ya moja.
 
Mkuu hao mawaziri 60 ni wa muungano+Tanganyika na hao 15 wanaozungumziwa kwenye rasmu ni wa Muungano peke yake hizo gharama ulizokokotoa ni za kuendesha serikali ya muungano peke yake hapo hujaelezea gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika kama utaweza hebu jaribu kutuwekea idadi ya wabunge na mawaziri wa Tanganyika na pesa itayotumika kuwalipa usisahau kama kuna mahakama pia ya Tanganyika na ya Muungano

Hii idadi ya wabunge na mawazir ni kwa pande zote mbili( tanganyika & zanzibar)
 
Kila nchi ikiunda serikali yake itaondoka na gharama zake. Gharama zile za kuendesha Tanganyika (iliyovaa koti la Muungano na kujiita Tanzania), zitapungua kwa kuwa sasa itakuwa haiibebi Zanzibar ktk baadhi ya gharama. Wale wabunge 54 kutoka Zanzibar wataondoka na kurejea kwao, hivyo gharama zao zitatumika kwa ajili ya kuendeshea serikali ya Muungano.

Serikali ya Zanzibar ipo na inaweza kujiendesha. Hakuna haja ya kujadili gharama zake hapa.

Tanganyika itakayoundwa itakuwa na mawaziri 8 tofauti na 60 wa sasa. Zile gharama za mawaziri 52 watakaokuwa wamepungua zitaenda kuendesha serikali ya shirikisho. Na hiki ndicho kiini hasa kwanini CCM hawaipendi serikali ya Tanganyika kwa kuwa wanaogopa kupoteza vyeo 52 vya uwaziri walivyokuwa wamevizoea. Umeona eeh?

Well, i catch u..
 
Back
Top Bottom