Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Kwa kukusaidia ili uelewe watu wanakuambia nini, chambua haraka za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na gharama zitakazokuwepo za kuendesha serikali 3

Ubishi upo kwenye serikali ya 3 (Muungano) ambayo watu wanabisha kwamba hakutakuwa na fedha za kuiendesha. Nimekuwekea takwimu zinazoonyesha namna gani uendeshaji wake utakuwa rahisi baada ya structure ya government kubadilika. Tulia usome kwa makini taarifa yangu utailewa. Serikali ya Tanganyika na Zanzibar hazitupi shida sana kwa kuwa kila nchi itajiendesha kwa kutumia rasilimali zake.
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Kaka hapa umesahahu kuweka gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika ambayo Bunge lake litakuwa pungufu kwa kuwaondoa wale wabunge wa kutoka Nchi Jirani,na pia itawatowa Mawaziri ambao wanashika Wizara za Muungano.

Ukifanyia mahesabu na hawa ukawaweka pamoja unaweza kupata kitu cha maana zaidi kwa kujadili.

Ukumbuke wale Mawaziri wa Tanganyika hawataruhusiwa kuingia Bungeni na hivyo kupunguza zile POSHO na sitting allowances,pia kuna uhakika wa kupunguza mawaziri kutoka 60 kufika 30 au 20 tu kama ilivyokuwa zamani.

Bado pia haujakokotoa zile pesa za cha juu na rushwa pamoja na wafanyakazi hewa wa wizara mbalimbali,matumizi mabaya ya fedha za Umma,maana Katiba yake itakuwa inawashika pabaya wale wapenda vya Kunyonga (wezi wa mali na raslimali za Taifa).

Hongera kwa kuanza kukokotoa gharama hizi.
 
Hapo Mkuu bado hujakamilisha kazi ya kushawishi watu kuwa serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2. Kumbuka kuwa umepigia serikali ya Muungano tu bado hujazungumzia Tanganyika na Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka kamili kama nchi washirika kwenye shirikisho. Kila nchi itakuwa na bunge lake ambao majimbo huenda yakabaki kama yalivyo kwa sasa. Hivyo basi, kama hivyo ndivyo, tutakuwa tumeongeza gharama za wabunge 75 ambao mwanzoni hawakuwapo. Labda kwa upande wa mawaziri hapo tutakuwa tumewahamisha waliokuwa wakihudumia kwenye serikali ya sasa ya muungano na hivyo baadhi ya wizara hazitakuwapo kwenye nchi washirika (zile zitakazoshughulikia mambo ya muungano), mfano wizara ya mambo ya nchi za nje; Ulinzi na JKT; Fedha, uchumi na mipango; Elimu na mafunzo ya ufundi; Afrika Mashariki, n.k.

Suala hapa ni kusema fedha ya kugharamia hao wabunge wapya 75 zitatoka wapi? Hapo ndipo wachumi wanatakiwa wapafanyie kazi maana magamba ndipo yaliposimamia! Ila ukiyasikiliza haya majamaa ni kama mataahira fulani vile, kuna moja liliibuka mle bungeni eti linahoji, ardhi ya kujenga hizo ikulu 3 (serikali ya muungano, Tanganyika na Zanzibar) itatoka wapi?

Hivyo tusikimbilie kusema tu serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2 bali tuainishe gharama zote na vyanzo vya mapato vya kugharamia hizo serikali (iwe 2 au 3), hapo ndiposa tutakuwa tumeweza kushawishiana!! Lakini kwa hili bandiko lako mheshimiwa, bado hujanishawishi (ingawa mimi naitaka Tanganyika yangu!!)

Nami naungana na wewe, jamaa akichambua vizuri itaweka huru na kifua mbele ukisema 3 useme kweli kwa uchambuzi kihesabu. Bila shaka atarusha tupate somo na maamuzi sahihi.
 
Hizo takwimu zina kasoro. Rudi shule kidogo. Hapo Tanganyika haijawekwa.

Hizi gharama za serikali mbili zilizotajwa hapo juu kwa sasa zinalipwa kwa kodi ya watanganyika(aka Tanzania bara).Zanzibar wanakusanya mapato yao kupitia ZRA na yanatumika kwa SMZ pekee.Hapo ndipo umuhimu wa Tanganyika unapokuja.
 
Hapo Mkuu bado hujakamilisha kazi ya kushawishi watu kuwa serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2. Kumbuka kuwa umepigia serikali ya Muungano tu bado hujazungumzia Tanganyika na Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka kamili kama nchi washirika kwenye shirikisho. Kila nchi itakuwa na bunge lake ambao majimbo huenda yakabaki kama yalivyo kwa sasa. Hivyo basi, kama hivyo ndivyo, tutakuwa tumeongeza gharama za wabunge 75 ambao mwanzoni hawakuwapo. Labda kwa upande wa mawaziri hapo tutakuwa tumewahamisha waliokuwa wakihudumia kwenye serikali ya sasa ya muungano na hivyo baadhi ya wizara hazitakuwapo kwenye nchi washirika (zile zitakazoshughulikia mambo ya muungano), mfano wizara ya mambo ya nchi za nje; Ulinzi na JKT; Fedha, uchumi na mipango; Elimu na mafunzo ya ufundi; Afrika Mashariki, n.k.

Suala hapa ni kusema fedha ya kugharamia hao wabunge wapya 75 zitatoka wapi? Hapo ndipo wachumi wanatakiwa wapafanyie kazi maana magamba ndipo yaliposimamia! Ila ukiyasikiliza haya majamaa ni kama mataahira fulani vile, kuna moja liliibuka mle bungeni eti linahoji, ardhi ya kujenga hizo ikulu 3 (serikali ya muungano, Tanganyika na Zanzibar) itatoka wapi?

Hivyo tusikimbilie kusema tu serikali 3 ni nafuu kuliko serikali 2 bali tuainishe gharama zote na vyanzo vya mapato vya kugharamia hizo serikali (iwe 2 au 3), hapo ndiposa tutakuwa tumeweza kushawishiana!! Lakini kwa hili bandiko lako mheshimiwa, bado hujanishawishi (ingawa mimi naitaka Tanganyika yangu!!)

Mkuu, hizo gharama zakuendesha wabunge 75 zitachangiwa na nchi washirika. Kumbuka kwamba kila ushirika (hasa huu ambao tunataka sasa tuufanye uwe wa kiuchumi) una gharama zake. Sio kwamba hakutakuwa na gharama kabisa ila ninachotaka kuonyesha ni kwamba gharama zake zinamudika. Kama ingekuwa tuanaogopa gharama basi tusingejiunga na SADC, AU, EAC, UN na mashirika mengine ya kimataifa. Demokrasia ni gharama. Ndio maana tunatumia pesa nyingi kwenye matukio kama vile chaguzi za kisiasa kwa sababu ni muhimu kwa ustawi wa wananchi.

Kwa sasa hivi wabunge wa kutoka zanzibar waliopo kwenye bunge la JMT wanagharamiwa na serikali ya Tanganyika (kwa jina feki la Tanzania). Zile gharama ambazo tulikuwa tukizitumia kuwagharamia hawa watu sasa tutazielekeza kwa wabunge wetu wa kutoka Tanganyika ndani ya bunge la muungano. Kama Tanganyika inaweza kuwahudumia wabunge 54 wa kutoka Zanzibar itashindwaje kuwahudumia wabunge wake 50 tu? Tatizo sio gharama, ila ni uwoga tu wa wanasiasa wanaoogopa kupoteza vyeo ndani ya muundo wa serikali 3 (kama nilivyogusia kwenye hoja yangu ya msingi).
 
Ungetuwekewa na uchambuzi wa serikali ya Tanzanyika na Zanzibar ili tupate unganisha gharama za serikali tatu na ilivyo sasa serikali mbili.

Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu
Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa ymwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:
 
sio muanze kuprint tu vitu msivyo vijua hizo gharama alizo kokotoa hapo ni za serikali ya muungano yaani hao wabunge ni additional ya hao 399 waliopo sasa kwahio hizo gharama zote unazichanganya kwa pamoja ndio unapata serikali tatu
 
Ki msingi hilo ndilo kosa wanalolifanya baadhi ya wachambuzi wetu. Serikali ya muungano ni nyongeza katika serikali mbili, hivyo inakuwa ya tatu. Kwa maana kuwa inaongezeka katika serikali ya Tangayika iliyovua koti la muungano na ya Zanzibar ambayo ipo na itandelea kuwepo. Kwa hiyo mkokotoji wa gharama za serkali tatu ajipange upya na ataona hoja yake haina mashiko ya kimantiki.
 
Kwa ukokotozi huo ni.shayiri serikali 3 ni nafuu.

kwa watu wajinga kama ninyi ndo mnadanganyika kirahisi sana. Ukweli ni kwamba hao mawaziri 15 na wabunge 70 waliotajwa ni gharama za ziada kuliko hizi za sasa. Ukweli ni kwamba Tanganyika itaendelea kuwa na mawaziri hawa hawa tulionao sasa na wabunge hawa hawa tulionao sasa. Hapo ni wazi kwamba serikali ya tatu itabeba gharama ambazo hatuzioni kwenye mfumo wa serikali mbili
 
Ki msingi hilo ndilo kosa wanalolifanya baadhi ya wachambuzi wetu. Serikali ya muungano ni nyongeza katika serikali mbili, hivyo inakuwa ya tatu. Kwa maana kuwa inaongezeka katika serikali ya Tangayika iliyovua koti la muungano na ya Zanzibar ambayo ipo na itandelea kuwepo. Kwa hiyo mkokotoji wa gharama za serkali tatu ajipange upya na ataona hoja yake haina mashiko ya kimantiki.

mkuu, kama mwenyekiti wa chama chao hata shule hajaenda, unategemea wafuasi wake watakuwa na akili gani? Wao ni copy and paste
 
Mkuu, hizo gharama zakuendesha wabunge 75 zitachangiwa na nchi washirika. Kumbuka kwamba kila ushirika (hasa huu ambao tunataka sasa tuufanye uwe wa kiuchumi) una gharama zake. Sio kwamba hakutakuwa na gharama kabisa ila ninachotaka kuonyesha ni kwamba gharama zake zinamudika. Kama ingekuwa tuanaogopa gharama basi tusingejiunga na SADC, AU, EAC, UN na mashirika mengine ya kimataifa. Demokrasia ni gharama. Ndio maana tunatumia pesa nyingi kwenye matukio kama vile chaguzi za kisiasa kwa sababu ni muhimu kwa ustawi wa wananchi.

Kwa sasa hivi wabunge wa kutoka zanzibar waliopo kwenye bunge la JMT wanagharamiwa na serikali ya Tanganyika (kwa jina feki la Tanzania). Zile gharama ambazo tulikuwa tukizitumia kuwagharamia hawa watu sasa tutazielekeza kwa wabunge wetu wa kutoka Tanganyika ndani ya bunge la muungano. Kama Tanganyika inaweza kuwahudumia wabunge 54 wa kutoka Zanzibar itashindwaje kuwahudumia wabunge wake 50 tu? Tatizo sio gharama, ila ni uwoga tu wa wanasiasa wanaoogopa kupoteza vyeo ndani ya muundo wa serikali 3 (kama nilivyogusia kwenye hoja yangu ya msingi).
Mkuu nafikri bado hujatuelewa tunachokipinga katika uchambuzi wako, na bado unafanya kosa lile lile la kuonesha kwamba upande wa Tanganyika hakutakuwa na wabunge kabisa! Hapa tukubaliane kwanza kuwa serikali 3 inaongeza gharama ya kuhudumia wabunge 75 ambao hawakuwapo kabisa katika bunge la sasa la muungano. Ili kujua kama hawa wabunge walikuwapo au hawakuwapo hapo mwanzo lazima ujue majimbo ya muungano yamekaaje? Kwa mujibu wa rasmu ya katiba mpya, majimbo ya bunge la muungano ni mikoa yote ya Tanganyika (25) na Zanzibar (5), hivyo kila mkoa utatoa wabunge wawili (kwa uwiano wa 1:1 - me:ke). Kwa upande wa serikali ya Tanganyika majimbo yatabaki yale yale yaliyopo sasa hivi, maana hapo mwanzo hatukuwa na majimbo ya mikoa. Mtu mvivu kufikiria anaweza kusema sasa kama mkoa umetoa mbunge kuna haja gani tena kwa wilaya ile ile ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa (mfano Geita, Shinyanga, Arusha, Singida, Tabora n.k.) kutoa mbunge wa Tanganyika? Hii itakuwa ni upotoshaji, mbunge wa muungano ni wa jimbo la mkoa na atapigiwa kura na wakazi wote wa mkoa husika, wakati yule wa Tanganyika atapigiwa kura na wakazi wa jimbo husika. Hivyo sisi wapenzi wa serikali 3 tusikurupuke kusema itakuwa nafuu kuliko serikali 2, huu utakuwa upotishaji, bali tukubali kwamba kuna gharama mpya zitazaliwa lakini tutaweza kuzimudu (je! utatumia mbinu gani kuzikabili?). Hata UKAWA walipaswa kutengeneza partial budget ambayo ingeonesha mchanganuo wote wa gharama mpya na zile zinazojifuta, hapo wa-TZ wengi wangewaelewa, lakini sasa hivi wanapiga kelele kwa maelezo ya kufikirika kuliko uhalisia wake.

BADO TUNA KAZI YA KUFANYA WAKUU!!!
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.

TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Dar imeomba kuongeza wilaya 2 n miyaa 213, imeomba bajeti ya sh360 bn sawa na mishahara ya wabunge 350 wa sasa.
 
Mkuu hao mawaziri 60 ni wa muungano+Tanganyika na hao 15 wanaozungumziwa kwenye rasmu ni wa Muungano peke yake hizo gharama ulizokokotoa ni za kuendesha serikali ya muungano peke yake hapo hujaelezea gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika kama utaweza hebu jaribu kutuwekea idadi ya wabunge na mawaziri wa Tanganyika na pesa itayotumika kuwalipa usisahau kama kuna mahakama pia ya Tanganyika na ya Muungano

pia hapo amezungumzia 60 wa muungano na koti lake, hajaongeza nadhano 30 wa zanzibar
 
kwa watu wajinga kama ninyi ndo mnadanganyika kirahisi sana. Ukweli ni kwamba hao mawaziri 15 na wabunge 70 waliotajwa ni gharama za ziada kuliko hizi za sasa. Ukweli ni kwamba Tanganyika itaendelea kuwa na mawaziri hawa hawa tulionao sasa na wabunge hawa hawa tulionao sasa. Hapo ni wazi kwamba serikali ya tatu itabeba gharama ambazo hatuzioni kwenye mfumo wa serikali mbili

Kwa mengine umesema kweli, ila hapo kwenye red napingana na wewe. Serikali ya Tanganyika haitakuwa na mawaziri kwa idadi kama hii tuliyo nayo maana wizara za muungano zitahama na mawaziri wake, hivyo nchi washirika hazitakuwa na mawaziri kama wale wa wizara za muungano. Mfano, wizara ya mambo ya nchi za nje; wizara ya ulinzi na JKT n.k nchi washirika hawatakuwa na wizara ya mambo ya nchi za nje n.k. Hivyo nchi washirika watapunguza idadi ya mawaziri. Upotoshaji mwingine unaofanywa na wale waumini wa serikali 2 ni kuhusu majeshi, kwamba serikali ya muungano itapata wapi fedha za kuwalipa? Ukweli ni kwamba majeshi yote yatakuwa chini ya serikali ya muungano na nchi washirika hazitakuwa na majeshi yake, bali kazi ya ulinzi na usalama itafanywa na majeshi ambayo yatakuwa chini ya muungano.

Sawa ukweli ni kuwa serikali 3 zitakuwa na gharama za ziada lakini zinaweza kukabilika!!!
 
Mkuu hapo cjakuelewa. Ila jua kitu kimoja hapo.kwamba Hao wabunge 70 ujue ni wa muungano so huwezi kulinganisha na wabunge399 kwa7bu hao wote ni mchanganyiko wa tz bara na visiwani.

Mchanganyiko wa Tz bara na visiwani ndo muungano wenyewe. Wewe zuzu kweli
 
Nipinge kwa kutumia facts and figures kama ambavyo mimi nimeweka figures. Vinginevyo hutaeleweka. Ubishi wa kizombi na usiokuwa na mantiki kama huu wako ndio unapelekea mnaitwa majina ya ajabu ajabu kama vile Intarahamwe, nk.
Haujaweka facts na figures za Serikali 3, hauwezi kuja hapa kusema Serikali tatu ni nafuu kuliko Serikali mbili halafu unaishia kutoa gharama za serikali moja tu, ndio maana nikakwambia uchambuzi wako ni Goigoi na uliojaa pumba na hata hao wanaokushangilia nao wako kama wewe. Weka gharama za Serikali zote tatu halafu ndio tutajua mfumo upi wa Serikali ni nafuu.
 
Mkuu hao mawaziri 60 ni wa muungano+Tanganyika na hao 15 wanaozungumziwa kwenye rasmu ni wa Muungano peke yake hizo gharama ulizokokotoa ni za kuendesha serikali ya muungano peke yake hapo hujaelezea gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika kama utaweza hebu jaribu kutuwekea idadi ya wabunge na mawaziri wa Tanganyika na pesa itayotumika kuwalipa usisahau kama kuna mahakama pia ya Tanganyika na ya Muungano
hili watu hawalionagi.
 
Back
Top Bottom