Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Serikali 2 ni ghali kuliko serikali 3, Ushahidi huu hapa

Sasa hiyo uliyoleta ni ya Serikali moja katika tatu, halafu tuwekee na gharama za hizo Serikali mbili ulizoacha kukokotoa.

ya Tanganyika, kwasababu haipo(?) in the first place. Mbaya ni kwamba Watanzania hatujiulizi haya maswali magumu, tumebakia na mipasho na light touch story hadi huko kwenye BMK. Lakini kwakuwa rasimu ya S3 tunayo, na pili kwa kuwa SMZ tayari ipo. Hii inaweza ikawa reference nzuri ya kufanya comparative analysis ya uendeshaji wa S2 v S3 kwa kutumia SMZ as a reference point. Wachambuzi watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani ya S2 zikoje. Na pia watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani S3 zitakuwaje kwa kutumia rasimu ya katiba. Hata kama sasa SMZ haichangii SMT is not excuse. To be fair kwa akili ya kawaida tu kwa mtu yeyote aliyesoma algebra. Kama tutakwenda kwenye S3, SMZ itagharamikia zaidi kuendesha serikali zake (SMZ na Serikali ya Shirikisho), but at the same time Tanganyika itagharamikia kidogo/itapunguza gharama za kuendesha serikali zake (Serikali ya Tanganyika na Shirikisho) in relative with S2. Kama tutaamua kuendelea S2, SMZ itagharamikia kidogo ni relative with S3 kuendesha serikali zake (SMZ na Muungano) kwasababu gharama zote za serikali ya Muungano anazibeba Tanganyika ambaye amejivisha KOTI la Muungano. Huo ndiyo UKWELI wenyewe.
 
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko serikali 2 unapatikana katika rasimu ya katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma, ambayo inapigwa vita na kundi la wengi kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2). Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama hizi:

USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki kinasomeka ifuatavyo:

“Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1), idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.

Idadi ya mawaziri na manaibu waziri katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding gharama za nyumba, gari, mafuta, safari na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).

Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka).

Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%. Haya, sasa wale mnaodai kwamba serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti muoneshe mnakokotoaje hizo gharama, sio watu wanakaririshwa majibu kwenye vikao halafu wanakuja kupayuka hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!

USHAHIDI WA PILI
Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya 113(1) na (2) idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye rasimu ni wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5 walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion.

Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka).
Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion.
Sasa hawa waongo wanaosema kwamba kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia kigezo kipi hawa vilaza?

KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za makatibu wakuu, makamishina, wakurugenzi na wakuu wa idara katika wizara husika. Ukijumlisha na gharama za kuwalipa viongozi hawa pesa zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu ushahidi unatosha kabisa kuonyesha kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali 2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa ili waendelee kukukandamizeni, kukumasikinisha na kukuchukulieni kama mazuzu wa kupandia ngazi za madaraka na kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.


TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2 ili wananchi waendelee kubebeshwa gharama za kuendesha serikali kwa manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania anapaswa kufunguka macho na kuhoji hizo gharama wanazodai wanazikokotoa kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania kutohoji mambo ndio unaosababisha wanasiasa waendelee kutudanganya na kutufanya ngazi za kupandia na kuning’inia madarakani kwa manufaa yao binafsi.


N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale waongo wanaowadanganya raia kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.

:yield:

Mkuu usisahau kujumlishia gharama za wakuu wa mikoa 25 na wakuu wa wilaya 130,ambao mishahara yao @ ni zaidi ya Tsh.2m/mwezi
 
Mnaangalia ghalama za pesa tuu, hamuangalii ghalama zitakazo tokea Muungano ukivunjika? Au mgongano wa kisiasa, hz sy ghalama? Embu acheni ufinyu wa mawazo.
 
Mkuu hapo cjakuelewa. Ila jua kitu kimoja hapo.kwamba Hao wabunge 70 ujue ni wa muungano so huwezi kulinganisha na wabunge399 kwa7bu hao wote ni mchanganyiko wa tz bara na visiwani.

acha u-mbwiga weyeee . huo ufafanuzi uliotolewa hapo kama hujauelewa basi ww utakuwa ni mb.....
umeambiwa ikiwa ni serikali 3 hao wabunge 399 hawatakuwepo tena kwa idadi hiyo unayosema. ni lazima watapungua kutokana na majukumu megi kugawanywa katika serikali zilizopo. hivyo huo uwingi wa wabunge hautokuwepo.
 
Mnaangalia ghalama za pesa tuu, hamuangalii ghalama zitakazo tokea Muungano ukivunjika? Au mgongano wa kisiasa, hz sy ghalama? Embu acheni ufinyu wa mawazo.

aliyekwambia muungano unavunjika ni nani? toa maelezo unavunjika vipi... acha kuchanganya watu weyee?
 
ya Tanganyika, kwasababu haipo(?) in the first place. Mbaya ni kwamba Watanzania hatujiulizi haya maswali magumu, tumebakia na mipasho na light touch story hadi huko kwenye BMK. Lakini kwakuwa rasimu ya S3 tunayo, na pili kwa kuwa SMZ tayari ipo. Hii inaweza ikawa reference nzuri ya kufanya comparative analysis ya uendeshaji wa S2 v S3 kwa kutumia SMZ as a reference point. Wachambuzi watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani ya S2 zikoje. Na pia watueleze gharama za kuendesha SMZ ndani S3 zitakuwaje kwa kutumia rasimu ya katiba. Hata kama sasa SMZ haichangii SMT is not excuse. To be fair kwa akili ya kawaida tu kwa mtu yeyote aliyesoma algebra. Kama tutakwenda kwenye S3, SMZ itagharamikia zaidi kuendesha serikali zake (SMZ na Serikali ya Shirikisho), but at the same time Tanganyika itagharamikia kidogo/itapunguza gharama za kuendesha serikali zake (Serikali ya Tanganyika na Shirikisho) in relative with S2. Kama tutaamua kuendelea S2, SMZ itagharamikia kidogo ni relative with S3 kuendesha serikali zake (SMZ na Muungano) kwasababu gharama zote za serikali ya Muungano anazibeba Tanganyika ambaye amejivisha KOTI la Muungano. Huo ndiyo UKWELI wenyewe.
kwahiyo tanganyika iendelee kuvaa koti la muungano??????
 
Sasa hiyo uliyoleta ni ya Serikali moja katika tatu, halafu tuwekee na gharama za hizo Serikali mbili ulizoacha kukokotoa.

Kila nchi ikiunda serikali yake itaondoka na gharama zake. Gharama zile za kuendesha Tanganyika (iliyovaa koti la Muungano na kujiita Tanzania), zitapungua kwa kuwa sasa itakuwa haiibebi Zanzibar ktk baadhi ya gharama. Wale wabunge 54 kutoka Zanzibar wataondoka na kurejea kwao, hivyo gharama zao zitatumika kwa ajili ya kuendeshea serikali ya Muungano.

Serikali ya Zanzibar ipo na inaweza kujiendesha. Hakuna haja ya kujadili gharama zake hapa.

Tanganyika itakayoundwa itakuwa na mawaziri 8 tofauti na 60 wa sasa. Zile gharama za mawaziri 52 watakaokuwa wamepungua zitaenda kuendesha serikali ya shirikisho. Na hiki ndicho kiini hasa kwanini CCM hawaipendi serikali ya Tanganyika kwa kuwa wanaogopa kupoteza vyeo 52 vya uwaziri walivyokuwa wamevizoea. Umeona eeh?
 
Mkuu hao mawaziri 60 ni wa muungano+Tanganyika na hao 15 wanaozungumziwa kwenye rasmu ni wa Muungano peke yake hizo gharama ulizokokotoa ni za kuendesha serikali ya muungano peke yake hapo hujaelezea gharama za kuendesha Serikali ya Tanganyika kama utaweza hebu jaribu kutuwekea idadi ya wabunge na mawaziri wa Tanganyika na pesa itayotumika kuwalipa usisahau kama kuna mahakama pia ya Tanganyika na ya Muungano


Kwa uelewa wako katiba ya Tanganyika ilishatebgenezwa? Je inasemaje katika muundo wa serikali?
Kama jibu ni bado basi ujue na hiyo itatengenezwa kulingana na uhitaji na uwezo wa kibajeti wa watanzania.

Amka na jitambue, Tizama jinsi maisha yako yanavyomuathiri jirani yako. Je ungefanyiwa wewe unfelikubali?
 
Acha kupotosha watu , usidhani wote waliopo humu ni mapoyoyo wa hesabu kama wewe. Hebu mtaje waziri ambae anaelipwa milioni 20 kwa sasa? waziri mkuu mwenyewe mshahara wake hauzidi hata milioni 6.

mshahara wa mbunge tu ni tsh milioni 11, waziri mkuu ndiye alipwe 6? acha ukasuku.

na je unajua kwamba waziri mkuu na familia yake wote wanatunzwa na serikali kwa kutumia fedha za umma? je, huyo waziri mkuu wako anajua bei ya chumvi, sabuni, mafuta ya gari, unga, nyama, mchicha, nk? hujiulizi gharama zote hizi zinalipwa na nani umeng'ang'ania mshahara tu? kama hufahamu jambo ni bora ukakaa kimya.
 
Mkuu hapo cjakuelewa. Ila jua kitu kimoja hapo.kwamba Hao wabunge 70 ujue ni wa muungano so huwezi kulinganisha na wabunge399 kwa7bu hao wote ni mchanganyiko wa tz bara na visiwani.


Nilivyomwelewa mimi hao wabunge 399 ni bunge la jmt tukijumlusha na baraza la wawakilishi kule zanzibar nafikiri bado serikali 2 ni mzigo ambao tumechoka kuubeba.
 
Mnaangalia ghalama za pesa tuu, hamuangalii ghalama zitakazo tokea Muungano ukivunjika? Au mgongano wa kisiasa, hz sy ghalama? Embu acheni ufinyu wa mawazo.

nani huyo tena anayetaka kuvunja muungano? yeye amependekeza kuwepo na serikali ngapi? usimsikilize huyo, mpuuze.
 
Mtu akiwa na akili kama za mbuni wa jangwani, ambaye huchimbia kichwa mchanagni akidhani amejificha, ni vigumu sana kuuona ukweli. Hebu jaribu kupitia michango yangu yote kabla ya kubisha.

Nimesema hivi: kwa sasa kuna wabunge 54 wa kutoka Zanzibar ndani ya JMT ambao hugharamiwa na serikali ya Tanganyika ( kwa kivuli cha Tanzania). Tukiingia kwenye shirikisho, hawa wabunge watapaswa warudi kwao. Hizi pesa tutakazookoa hapa tutazitumia kugharamia wabunge wetu 30 waliomo kwenye JMT ya Shirikisho. Pesa zitazosalia zitarudi serikali ya Tanganyika kwa ajili ya matumizi mengine.

Vyeo vya anasa kama vile wakuu mikoa, wakuu wa wilaya na wakuu wa tarafa vitafutwa. Tutabakiwa na wakurugenzi watendaji, makatibu tawala na maafisa utumishi wa majiji, manispaa na halmshauri. Hebu niambie tuna wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa wangapi katika nchi hii. Je, vyeo vyote hivi vikifutwa hatupati fedha za kuendesha nchi yetu ya Tanganyika na tukabakiwa na chenji ya kuchangia kwenye shirikisho?

Pamoja na haya yote, nchi ya Tanganyika itaongeza jitihada za kukusanya kodi, kupiga vita ufisadi na usafirishaji wa twiga kwenda uarabuni na ulaya. Hivyo nchi itakuwa na mapato ya kutosha kujiendesha. Hivi vyote ni vyanzao vya mapato. Sijui watu mnataka tuendelee kubebeshwa gharama za kipumbavu hadi lini. Serikali ikipunguza matumizi yake ya kipumbavu, kwa kutumia katiba mpya tutakayoitunga, nchi itapata pesa za kujiendesha na chenji itabaki.

Gharama za kuendesha serikali zitapunguzwa. Hakutakuwa na matumizi ya kipuuzi kama vile kununua samani na magari ya kifahari kutoka nje. Mawaziri watakuwa wanatumia magari ya kawaida kabisa—mashangingi na maV8 yatapigwa mnada wa hadhara na pesa zitakazopatikana zitatumika kununulia magari ya bei ndogo kwa ajili ya viongozi na chenji inayobaki tutaingiza kwenye matumizi mengine ya serikali.

Idadi ya wizara itapunguzwa hadi kufikia chini ya wizara 8 kutoka 29 za sasa na hakukutakuwa na uongezaji holela wa wizara kama ilivyo sasa. Mnadhani kwamba mawaziri kama Mwandosya wataendelea kuwepo katika serikali ya Tanganyika? Thubutu! Uongezaji wa kishikaji wa wizara kwa ajili ya kuwazawadia vyeo marafiki kwa gharama za wananchi utapigwa marufuku. Idadi ya wizara zinazotakiwa kuundwa zitaingizwa kwenye katiba. Kwa hiyo, rasi akiongeza wizara au akateua mawaziri zaidi ya wawili kusimamia wizara moja (kama ilivyo sasa) atakuwa wamevunja katiba. Marekani, pamoja na ukubwa wake wote ule, ina wizara 15 tu. Kwanini sisi tuwe na utitiri wa wizara wakati tungali masikini na ombaomba?

Haya makatazo yote yakiingia kwenye katiba, yatatusaidia kupata fedha za kutosha kuendesha nchi yetu hata bila kutegemea misaada ya masharti na masimango kutoka kwa wazungu. Tunapotafakari kuwa na serikali yetu ya Tanganyika inayojitegemea ni sharti tufikiri nje ya boksi. Tusikae tu kuimbishwa nyimbo za gharama bila kuchanganua mambo kwa kutumia vichwa vyetu wenyewe.
Kwa kweli kupanga ni kuchagua, serikali ya Tanganyika inaweza kuundwa ndogo yenye tija kwa kuondoa hivi vyeo vya asante kwa wana mitandao kama wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, kupunguza au kuondoa wabunge wa viti maalum, kuhakikisha wizara zinatamkwa na katiba na zitakuwa chache iwezekanavyo kuondoa uwezekano wa Rais kujitengenezea wizara zake etc. Mawaziri wathibitishwe na Bunge. Pia kwa kuwa mawaziri si watendaji wakuu wa wizara kuwe na waziri mmoja tu.
 
kwahiyo tanganyika iendelee kuvaa koti la muungano??????

On a neutral perspective mimi kama Mtanganyika ningependelea muundo wa S3 maana utanipunguzia gharama. Lakini kama mimi ningekuwa Mzanzibari ningependelea muungano wa S2, maana gharama za serikali ya muungano anazibeba Tanganyika aliyevaa koti la Muungano. Therefore it depends to which side of the fence you're standing.
 
serikali tatu za kwenye muvi zinawezekana wakina JB fastaa wanatoa muvi ndani ya wiki part 1 na part 2
 
On a neutral perspective mimi kama Mtanganyika ningependelea muundo wa S3 maana utanipunguzia gharama. Lakini kama mimi ningekuwa Mzanzibari ningependelea muungano wa S2, maana gharama za serikali ya muungano anazibeba Tanganyika aliyevaa koti la Muungano. Therefore it depends to which side of the fence you're standing.

Maajabu ni kuwa wazanzibar wanataka S3
 
Jana uongozi wa Mkoa wa DSM umeomba wilaya mbili mpya (Kigamboni na Ubungo).

Swali: Je kuongeza wilaya na mikoa kila wakati si gharama? Kuna tofauti gani kati ya hili na kuongeza serikali 3?

Tuache unafiki.
 
Back
Top Bottom