Siwezi kuelezea au kufupisha ngoja nijaribu
Kuna town ndogo ambayo watu wa Marekani huwa wanapotelea katika njia isiyoeleweka na wanabaki kujiuliza wamefikaje, maana wengine walikuwa wanasafiri kusini mwa nchi wengine Kaskazini lakini wanajikuta wanapotelea kwenye mji huo huo.
Watu waliopotea hapo wameunda community yao na wanaishi ila wanatafuta njia ya kutoka kwenye mji huo ila kuna mambo ya kutatanisha yanawazuia kutoka nje ya huo mji. Mfano, ukiendesha gari kuelekea nje ya town baada ya muda unajikuta umerudi palepale, hamna internet ila kuna umeme ambao haueleweki umetoka wapi.
Mbaya zaidi kila inapofika usiku kuna viumbe vinakuja dirishani kukushawishi uwafungulie dirisha, wanaweza kuja katika mfano wa mtu anayempenda au unayemkumbuka ili kukushawishi uwafungulie. Na ukiwafungulia tu wanakutafuna, unakuwa chakula chao. So wanakula watu usiku ila mchana mji uko safe
As a result series inaacha maswali mengi kuliko majibu
View attachment 2700344