Series (Special thread)

‎ARRIVAL
‎ Ni movie inayoelezea mtazamo mwingine wa muda na kumbu kumbu tofauti na uhalisia

‎Louise ni professor wa lugha mbali mbali akifundisha jinsi lugha zilivyoundwa, sauti zake na utafuti wake, akiwa na kumbu kumbu za kumpoteza mwanae na mume wake ambaye kwenye data zikionyesha hajawahi kuwa na mume, siku moja akiwa anafundisha kuna taarifa inakuja kuwa kuna ndege za ajabu zimekuja na kuweka kambi kwenye baadhi ya miji hapa duniani, hivyo serikali ikamuita kwa ajili ya kuwasoma na kujua lugha zao ili kama kuna uwezakano wa kuwasiliana nao, ila kadri anavyosoma lugha zao anashangaa inakuwa ni vyepesi kwake kufahamu lugha zao, na hajui ni kwa nini.

Kama unapenda movie za science fiction nenda kaitafute ni nzuri ila kama ni mfuasi wa Mr Q hutaipenda sana maana ni story tu
 
‎Leo nikapita na movie ya kuitwa Custom Frontier toka huko Hong Kong. Picha linaanza tu! Nikaona bendera ya Tanzania, nikasema haa! Ina maana hii ngoma location yake ni TZ? Ila baadaye wakaitaja ile nchi ni Jamhuri ya Loklamoa.

‎Nkajiuliza, ina maana kuna nchi inaitwa Loklamoa na ina bendera inakaribia kufanana na ya TZ? Uvumilivu ukanishinda, nikastopisha muvi, nikaenda kugogo. Majibu yakaja kuwa hiyo ni nchi ya kubuni tu lakini kiundani walielezea nchi inayopatikana Afrika Mashariki. So, moja kwa moja nikajua wameamua kuitumia TZ lakini kama nchi ya kubuni tu. Sijui walikuwa hawana hela ya kuja huku au ndo vile tena, kile walichoigiza hakiendani na mazingira yetu.

‎Basi stori ya humu ni kama huu mgogoro wa Israel na Palestina tu. Nchi kama Israel ina silaha kali, inaipiga Palestina. Na Palestina sasa waamue kutafuta silaha kali kujibu mashambulizi. Basi na stori ipo hivyo. Jamhuri ya Loklamoa inapigwa na jirani yake nao wanatafuta silaha kujibu mashambulizi. Ndipo wanadondokea kwa mfanyabiashara wa Hong Kong ambaye anachukua almasi za Loklamoa halafu analeta silaha.

‎Sasa wale polisi wa Hong Kong ambao ndo hawa Custom Frontier, wanaingilia kati kuzuia usambazaji haramu wa silaha.

‎Nzuri kuitazama. Haina mbwembwe. Full nazi, full mijegejo.

nmeikuta sehemu nmeona nilete na humu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…