Nakuelewa maana hiyo situation niliwahi kuipitia mwaka jana.
VPN ya ttcl ilipokuja nikatabiri neema lakini kama unavyojua kizuri hakidumu na adui wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe
Kweli baada ya muda mfupi wakushi wakakata nyaya na kila mtu akapoteana.
Sema nilikuja kugundua kuwa hii VPN mimi nilikuwa nimeipata kwa kuchelewa, wapo vibopa walioifaidi tangu inaanzishwa siku za mwishoni
Kuna raia way back walikuwa wameungwa halafu kuna time TTCL mtandao unakuwa slow mambo yao wanaona hayaendi halafu ukicheki na wao wamelipia hela.
Naskia walikuwa wanawapigia simu customer care, customer care akipokea tu jamaa anaanza direct "oya vipi wazee mbona VPN yenu inazingua na wakati nimeunga juzi tu"
Kwa hiyo naskia simu za namna hiyo zilikuwa nyingi na ndio zilizowasanua TTCL kuwa kuna mwanya ambao watu wanautumia kupata internet ya bure.