Serengeti Girls mmetuheshimisha sana Watanzania, pokeeni pongezi za dhati kabisa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Serengeti Girls wanakwenda India kucheza kombe la dunia na ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.

Bravo sana makocha, bravo wachezaji wote mliopambana mpaka kupata ushindi wa kishindo wa magoli 5-1 tena ugenini dhidi ya timu yenye uzoefu mkubwa ya hadhi ya Cameroon,

Mmefuta aibu ya miaka na miaka ya ushiriki hafifu wa michuano ya hadhi ya kombe la dunia. Kaka zenu wameshazoea aibu ya kuishia hatua ya makundi kila wanaposhiriki michuano ya afrika tu sembuse hii ya dunia.

Mwaka 1980 wakaenda Lagos Nigeria na baada ya hapo ikapita miaka 39 ndio wakaenda tena Misri tena baada ya Uganda kucheza mpira wa 'kishkaji' ili tuwafunge na sisi tuweze kufurahi. Miaka 39 ni umri wa waheshimiwa wengi ndani ya ukumbi wa bunge na wengine ni mawaziri kabisa.

Hongereni sana kinadada wa Serengeti Girls, binafsi sitojali ni aina gani ya matokeo mtakayoyapata huko, kule kwenda tu na kuwa mojawapo ya nchi zenye kuwakilisha bara la afrika ni mafanikio tosha kabisa.

Sitojali mkikutana na wazoefu USA au Norway au Sweden wa soka la wanawake tutafungwa magoli mangapi, sitojali kwani kuweza kufika tu hapo ni mafanikio tosha kabisa kwa soka letu.

Wanaume na soka lao wanachojua ni majungu tu ndio maana Barbara Gonzalez dada mwenye akili chanya na za kisasa za kuendesha soka, anapigwa fitina na kundi la viongozi wa TFF na baadhi yao kutoka Simba na Yanga. Ni akili zile zile za kushindwa za miaka yote na ndio hizi zimejaa katika soka la wanaume.

Kinadada mnazidi kuwaonyesha wanaume kwa vitendo nini maana ya kuendesha soka kisasa, pongezi za dhati ziwafikie.

Tuswibeteke na kuanza kuzihusianisha sifa za serengeti boys na mafanikio ya kichama au ya mtu binafsi, siasa ipungue wakati wa michakato yote ya kuelekea India kushiriki kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17.
 
Tuliambiwa wanawake wanaweza kufanya mambo zaidi ya mawili kwa wakati mmoja, sisi tukijaribu tunachanganya madesa, sms ya Maimuna tunatuma kwa Zubeda
 

Attachments

  • male-and-female-brain-what-constitutes-the-gender-12-320.jpg
    male-and-female-brain-what-constitutes-the-gender-12-320.jpg
    13.7 KB · Views: 14
Kwa kumbukumbu yangu kama sijakosea serengeti boys walishawahi kufuzu kama si kombe la dunia basi ni copa cocacola(ya dunia) lakini pia timu ya watoto wa mitaani ishawahi kufuzu michuano ya dunia.
Inavyoonekana timu za watoto zinafanya vizuri lkn tunashindwa kuviendeleza vipaji hivyo
 
Kwa kumbukumbu yangu kama sijakosea serengeti boys walishawahi kufuzu kama si kombe la dunia basi ni copa cocacola(ya dunia) lakini pia timu ya watoto wa mitaani ishawahi kufuzu michuano ya dunia.
Inavyoonekana timu za watoto zinafanya vizuri lkn tunashindwa kuviendeleza vipaji hivyo
Copa ndio Walifuzu ambayo timu kutoka kigoma ndio ilienda licha ya kupoteza fainali ambayo walipata umaarufu kwa mashabiki wake kwenda uwanjani na chungu kinachotoa moshi

Kuna wachezaji watano walipata timu hukohuko Brazil mmoja wao alikuwa anaitwa Shabani mokah
 
Back
Top Bottom