Video: Mahakama ya Kisutu
yamzuia Davido kuperform katika
tamasha la Fiesta
posted 3 hours ago by admin
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es
Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji
Adelek maarufu kama Davido kuperform katika
tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na
Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu
mkazi wa mahakama ya kisutu , mheshimiwa D.
Kisoka kufuatia maombi ya dharura
yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times Fm
Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka
maombi ya dharura mahakamani hapo wakiitaka
mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika
tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza
La Sanaa Tanzania) kukataa kutoa kibali cha msanii
huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa
ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini
November 1 kwenye tamasha lililoandaliwa na
Times Fm Radio, Clouds Fm na Prime Times
Promotion waliendelea na taratibu zote bila kujali
zuio hilo la BASATA.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba
mahakama kuidhinisha madai yao dhidi ya Clouds
Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni
inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama
na usumbufu waliosababishiwa na walalamikiwa
kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo
amezuiwa kufanya onesho hilo October 18,2014
hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana
mhakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times
Fm Radio akieleza kuwa atakuja Tanzania
November 1 kwa ajili ya kufanya onesho
linaloandaliwa na kituo hicho cha radio lililopewa
jina la The Climax.