Nafahamu kuwa Chadema kinaamini katika sera ya ubepari na kwamba kama chama wana uhusiano wa karibu na vyama vya kibepari duniani i.e. Conservative (UK) and Republican (US)
Ubepari kama sera na mtazamo wa chama ukitekelezwa hauna tija kwa mfanyakazi mnyonge au mkulima maskini. ubepari kazi yake ni kusimamia maslahi ya wenye mitaji ...i.e. wenye pesa
Je sera ya ubepari kwa chadema ni kwa ajili ya nani? au kwa faida ya nani?.
Kwa kuuliza maswali kama haya taratibu mnaanza kuikubali Chadema kuna mwingine ameanzisha thread anataka kuijua CDM kwa undani zaidi ni dalili nzuri kwa Chama. Kuwasaidia mnaweza kutembelea tovuti yao.Halafu ni kudandia sera bila hata kujua kwamba umma wa watanzania hawa maskini hawawezi kupata fursa ya kuishi chini ya mfumo huo halafu ukadai una uwezo wa kuwapa fursa sawa za kiuchumi wakati msingi wake ni kuwawezesha matajiri wachahce wamiliki njia kuu za uchumi na kuruhusu wawanyonye wasio nacho! Serious contradiciton and a big paradox!
Boss,hili neno ubepari siku hizi halitumiki
inaaitwa uchumi huria...au uchumi wa soko....
Boss,
Najua ni mvinyo ule ule katika chupa mpya. Ubepari bado u hai.
Kwanza inabidi kuondokana na hili neno Kibepari na badala yake kutumia maneno yanayoswihi kama Vile Ujamaa vs Uhafidhina..Nafahamu kuwa Chadema kinaamini katika sera ya ubepari na kwamba kama chama wana uhusiano wa karibu na vyama vya kibepari duniani i.e. Conservative (UK) and Republican (US)
Ubepari kama sera na mtazamo wa chama ukitekelezwa hauna tija kwa mfanyakazi mnyonge au mkulima maskini. ubepari kazi yake ni kusimamia maslahi ya wenye mitaji ...i.e. wenye pesa
Je sera ya ubepari kwa chadema ni kwa ajili ya nani? au kwa faida ya nani?.
Kinachochekesha CCM wana ubepari wa kudandia ambao hauna mpango wakati Chadema wana ubepari wa kupangwa. Kwa CCM mwekezaji ni mkombozi lakini Chadema wanataka Mtanzania awezeshwe. Kwa CCM madini ni mali ya mzungu wakati Chadema wanasema madini lazima yanufaishe taifa. Kwa CCM kilimo kwanza ni kugawa mapande makubwa ya ardhi kwa kampuni za kigeni zijilimie wenyewe chakula wakati wakulima wa Kitanzania wakifa njaa wakati Chadema inataka mkulima wa Kitanzania awezeshwe. Sasa sijui Topical na Mbopo ni ubepari gani mnaouzungumzia hapa.
Kwanza inabidi kuondokana na hili neno Kibepari na badala yake kutumia maneno yanayoswihi kama Vile Ujamaa vs Uhafidhina..
Mkuu ukisoma vizuri sera za Chadema utagundua kwamba zimeelekeza nguvu zake ktk kuwatajirisha wananchi wenyewe. Chadema kama mrengo wa kati wanachukua mazuri kutoka pande zote mbili na kusema kweli ndivyo vyama vyote vya Tanzania vinafanya, hakuna chama cha Kijamaa (kushoto)wala cha kihafidhina (kulia) isipokuwa tunakwenda tu kama gari bovu kwa sababu ni wananchi wachache sana wanaopenda Ujamaa na wachache zaidi watapenda hifadhi ya mila na desturi zilizounda Utaifa wetu kuwa kioo (blueprint) cha ujenzi wa sera za chama. Na hao CCM duh, hata sijui niseme nini maanake hata Ubepari wao umepitiza yaani ni sawa na gari linalokwenda bila brakes!
Tunachokifanya sisi ni kuiga tu siasa za Ulaya na kuchukua yale yanayotufaa na kuachana na yale ambayo hayana maslahi kwetu kwa sababu maskini hata siku moja hana sauti. We can't make a call ndani ya dunia hii na hili muhimu zaidi kulitambua hivyo hizi siasa na demokrasia kwetu ni sawa na kumpelekea msukuma keki ama halua..Tutaweza vipi kuwa wajamaa bila kufuata siasa za Utengano hali hatuna uwezo wa hali na mali (Mtaji na elimu) ya kutuwezesha!..Maskini anaweza vipi kuweka mikakati ya kibiashara ikiwa hata mtaji wenyewe hana!...Na utaweza vipi kuwa mhafidhina ikiwa mila na desturi zako mwenyewe unazikataa kiasi kwamba hata lugha zetu zenyewe tunazipiga vita acha mbali kiswahili kinavyopotea!.. Hapa ndipo tunapojikuta tunakwamba na hizi siasa na demokrasia tofauti na wenztu waliotutangulia.
Ubepari sio sera na haitakuwa sera isipokuwa ni itikadi ambayo nchi nyingi za magharibi wameichukua na tofauti zipo ktk sera kama vile Wakristu au waislaam wanajulikana kwa imani zao lakini ndani yake kuna madhehebu tofauti..Haya madhehebu ndio unavyoona vyama vya Conservative na Democratic....
Kwa kuuliza maswali kama haya taratibu mnaanza kuikubali Chadema kuna mwingine ameanzisha thread anataka kuijua CDM kwa undani zaidi ni dalili nzuri kwa Chama. Kuwasaidia mnaweza kutembelea tovuti yao.
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.This should not turn out to be a contest. Ukweli ni kwamba ubepari kwa nchi yetu hauwezi kuwa suluhisho la matatizo yetu, whether ubepari huo umepangwa au la. Misingi ya ubepari haibadiliki kwa kuzingatia boardroom zilizotumika kutengeneza katiba. Misingi ya ubepari, faida na hasara zake ni elimu basic ya sekondari, lakini tukiangalia yanayotokea kwa wenzetu, ni rahisi kuelewa kwa nini mfumo huo haufai na hauna manufaa kwa wananchi wanaodai kuwatetea. It remains to be a paradox
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.
You might have a point, Ubepari ambao una faida kwa wananchi wa kawaida na sio wenye mitaji (matajiri) ni upi?
Naomba unisaidie ubeoari wa chadema na ccm una tofauti gani..? kwa ajili ya wananchi?
Kwa kuanza tu CCM inaamini kuwa mwekezaji ni mkombozi. Hata kama atawanyanyasa na kuwanyang'anya ardhi raia wazawa kama ambavyo
imetokea huko Mbarali. Chadema inaamini kumwezesha raia mzaliwa kuwa mwekezaji katika nchi yake mwenyewe. Chadema inaamini kuwa madini shurti yanufaishe nchi na hasa maeneo yanakochimbwa. CCM inaamini kuwa madini yamnufaishe mwekezaji kwani ameleta mitambo yake na asilipe kodi. Hayo ni mawili tu yanayoonyesha tofauti kubwa baina ya upebari wa CCM na vision ya Chadema. Ukitaka nitaendelea kumwaga somo.
Hizo si Imani ya CCM..inabidi ukasome sera za ccm ok tuache hayo maana unaongelea kishabiki zaidi<br />
<br />
Nimesoma sera za chadema sijaona mahali kuna imani hizo ulizosema..<br />
<br />
Unamwezeshaji raia mzaliwa .. i mean unafanyeje ki-sera..i.e. ubepari? ambao ndio sera mama ya chadema
hili neno ubepari siku hizi halitumiki
inaaitwa uchumi huria...au uchumi wa soko....
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.