Ukiwa kiongozi kama hujaacha legency yeyote ile tambua kuwa hukustahili kuwa kiongozi na huna akili

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,546
2,989
Uongozi ni ushawishi wa fikra wenye kuleta mabadiliko katika jamii unayoiongoza impact ya uongozi huonekana pale kiongozi ataanzisha mifumo ya kipekee katika wakati wake wa kuongoza mfano mdogo tu,waafrika tunaongelea wazungu sababu wametengeneza impact kwetu ambazo ziliathiri jamii kwa kiasi kikubwa jambo kama vile destruction, creation na preservation ni mambo ya msingi ambayo yalifanywa kwetu katika kuendelea kututawala na mpaka leo tumebakiwa kuendeleza misingi ya hao wazungu kuendeleza jamii zetu.

Tanzania kuna baadhi ya viongozi wachache tu,ambao watabakia katika vichwa vya wananchi ila wengi kati yao wanayeyuka kama moshi angani, miongoni mwao ni ;

RAIS WA AWAMU YA KWANZA

Mwalim J Nyerere ataendelea kukumbukwa sababu ya historia ya Tanzania na mapinduzi ya uchumi kwa kutumia itikadi ya ujamaa ambayo imezalisha chama tawala cha Tanzania bila kusahau muungano wa jamhuri ya TANZANIA na yeyote atakayevunja muungano atabakia kuwa katika kumbukizi.

RAIS WA AWAMU YA PILI

Alhaj Hassani Mwinyi vitabu vya historia vinamtaja kama mwanzilishi wa ubepari katika nchi ya TANZANIA

RAIS WA AWAMU YA TANO

John Joseph Pombe Magufuli huyu atakauwa ni miongomi mwa maraisi watakaobakiwa kuwa katika historia ya nchi kwakuwa aliweza kuanzisha mfumo tofauti wa uchumi katika zama za ubepari,sera ya uwajibikaji na mageuzi ya kiuchumi kwa mfumo wa kijamaa ambao ni mfumo sahihi wa chama cha mapinduzi.

Marais wengine bado hawajaweza kuandika historia kwa sababu wamebase katika kufanya presarvation na destruction ya effect za wenzi wao.
 
Back
Top Bottom