Tupo kwenye Ubepari

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,184
6,593
Nchi yetu ilianza kama nchi ya kijamaa chini ya Rais Julius K Nyerere. Tuliamini katika mfumo wa kijamaa na tulijua kuwa mfumo huu ndio pekee unaoweza kutuletea maendeleo.

Katika mfumo wa kijamaa kila kitu ni cha jamii. Mambo kama shule na afya ni huduma za bure kabisa. Kwenye mfumo huu tofauti za kimatabaka ya uchumi ni ndogo sana kwenye jamii. Kwani kila kinachopatikana kinagawanywa kwa usawa, iwe ulijituma zaidi au la.

Ni mfumo mzuri ulituweka pamoja tukawa kama ndugu lakini ukatuletea umasikini.
Kwa kuwa kipato kilikuwa sawa na kuna mashamba ya vijiji pakazaliwa jamii ya wazembe wasiotaka kufanya kazi wakiamini kitakachopatikana kitagawanywa sawa.

Ufanye kazi usifanye, utatibiwa bure na watoto wako watasoma bure kwa kutegemea juhudi za wenzako.

Kipindi cha Rais Mwinyi tukaanza kuingia kwenye ubepari baada ya ujamaa kushindwa. Pakaanza kuwa na biashara za shule binafsi na viwanda na gap la kiuchumi likaanza kati ya walio nacho na wasio nacho.

Hakuna nchi duniani ipo kwenye ubepari kamili. Maana nchi nyingi za kibepari bado zina baadhi ya tabia za ki jamaa kama kusoma bure na huduma za afya. Na serikali bado inaendelea kusimamia baadhi ya vitu ili wenye nacho wasiwanyonye wasionacho.

Raia kwa kutokuelewa kuwa tulishaachana na ujamaa bado wanaendelea kutegemea serikali na jamii kwenye kila kitu.

Akipatikana mtu ana fedha kuwazidi wanalalamika, akija mwekezaji wanalalamika wanataka usawa wasijue kwenye ubepari hakuna usawa.

Kwenye ubepari hakuna kutegeana kwenye kazi ukitegea ni hasara yako. Kwenye ubepari usikubali kuwa mnyonge pambana kwa njia zote za halali utoke huko maana hakuna utegemezi wa jamiii kukuokoa.

Ubepari ni mzuri kuliko ujamaa maana maendeleo tunayaona. Lakini ubepari mzuri ni ambao serikali bado inanguvu ya kuregulate biashara binafsi.
 

inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
12,330
10,638
Watu huchanganya ubepari na soko huria'..soko huria' lipo tangu enzi za yesu,akichonga stuli na kuuza,ubepari ni pale mabepari(capitalists/wenye mitaji) wanapoilekeza serikali wapi pa kwenda..mfano Vita Vietnam,Iraq,Syria,Afghanistan nk
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom