Sera za Ubepari hazitatusaidia kama nchi

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
932
Nafahamu kuwa Chadema kinaamini katika sera ya ubepari na kwamba kama chama wana uhusiano wa karibu na vyama vya kibepari duniani i.e. Conservative (UK) and Republican (US)

Ubepari kama sera na mtazamo wa chama ukitekelezwa hauna tija kwa mfanyakazi mnyonge au mkulima maskini. ubepari kazi yake ni kusimamia maslahi ya wenye mitaji ...i.e. wenye pesa

Je sera ya ubepari kwa chadema ni kwa ajili ya nani? au kwa faida ya nani?.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
932
Asije mtu akaukana upebari si sera ya chadema..akasome kwanza katiba yao.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Halafu ni kudandia sera bila hata kujua kwamba umma wa watanzania hawa maskini hawawezi kupata fursa ya kuishi chini ya mfumo huo halafu ukadai una uwezo wa kuwapa fursa sawa za kiuchumi wakati msingi wake ni kuwawezesha matajiri wachahce wamiliki njia kuu za uchumi na kuruhusu wawanyonye wasio nacho! Serious contradiciton and a big paradox!
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,938
1,427
Unachsoema ni kweli lakini Sijui kuna chama gani kisochocha kibepari Tanzania. Kifupi hakuna .Kama n ubeari wa chadema au hata CUFauNCCR mi naoa unaweza kuwa a faida na nafuu kuliko ubepari wa CCM huku wakijinadi ni wajamaa.i i

Kinachotakiwa Tanzania sio siasa za sera . ni utekelezaji wa sera kwa vitendo. Iwe seraayeyyeote atayeonyesha zinatekelezeka na zinaweza kuwa na amnufaa wa wananchi apewe nafasi.
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,506
Nafahamu kuwa Chadema kinaamini katika sera ya ubepari na kwamba kama chama wana uhusiano wa karibu na vyama vya kibepari duniani i.e. Conservative (UK) and Republican (US)

Ubepari kama sera na mtazamo wa chama ukitekelezwa hauna tija kwa mfanyakazi mnyonge au mkulima maskini. ubepari kazi yake ni kusimamia maslahi ya wenye mitaji ...i.e. wenye pesa

Je sera ya ubepari kwa chadema ni kwa ajili ya nani? au kwa faida ya nani?.

Halafu ni kudandia sera bila hata kujua kwamba umma wa watanzania hawa maskini hawawezi kupata fursa ya kuishi chini ya mfumo huo halafu ukadai una uwezo wa kuwapa fursa sawa za kiuchumi wakati msingi wake ni kuwawezesha matajiri wachahce wamiliki njia kuu za uchumi na kuruhusu wawanyonye wasio nacho! Serious contradiciton and a big paradox!
Kwa kuuliza maswali kama haya taratibu mnaanza kuikubali Chadema kuna mwingine ameanzisha thread anataka kuijua CDM kwa undani zaidi ni dalili nzuri kwa Chama. Kuwasaidia mnaweza kutembelea tovuti yao.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
5,375
Kinachochekesha CCM wana ubepari wa kudandia ambao hauna mpango wakati Chadema wana ubepari wa kupangwa. Kwa CCM mwekezaji ni mkombozi lakini Chadema wanataka Mtanzania awezeshwe. Kwa CCM madini ni mali ya mzungu wakati Chadema wanasema madini lazima yanufaishe taifa. Kwa CCM kilimo kwanza ni kugawa mapande makubwa ya ardhi kwa kampuni za kigeni zijilimie wenyewe chakula wakati wakulima wa Kitanzania wakifa njaa wakati Chadema inataka mkulima wa Kitanzania awezeshwe. Sasa sijui Topical na Mbopo ni ubepari gani mnaouzungumzia hapa.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
45,208
95,712
hili neno ubepari siku hizi halitumiki

inaaitwa uchumi huria...au uchumi wa soko....
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
45,208
95,712
Boss,
Najua ni mvinyo ule ule katika chupa mpya. Ubepari bado u hai.

mkuu
kuna ubepari wa aina nyingi mno
na sio wote mbaya.....
tatizo nyerere hakutaka kujifunza aina zingine

chukulia mfano nyerere alikuwa rafiki mkubwa wa waziri mkuu wa sweden
palme,na wote walikuwa wasoshalist....cha ajabu sweden ilkuwa nchi huru tena ya kibepari

ubepari aina ya sweden ungetusaidia kama nyerere angekuwa yuko tayari kujifunza...

ubepari wa marekani na sweden ni dunia mbili tofauti........sweden hakuna umasikini uliopo marekani...
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,626
Nafahamu kuwa Chadema kinaamini katika sera ya ubepari na kwamba kama chama wana uhusiano wa karibu na vyama vya kibepari duniani i.e. Conservative (UK) and Republican (US)

Ubepari kama sera na mtazamo wa chama ukitekelezwa hauna tija kwa mfanyakazi mnyonge au mkulima maskini. ubepari kazi yake ni kusimamia maslahi ya wenye mitaji ...i.e. wenye pesa

Je sera ya ubepari kwa chadema ni kwa ajili ya nani? au kwa faida ya nani?.
Kwanza inabidi kuondokana na hili neno Kibepari na badala yake kutumia maneno yanayoswihi kama Vile Ujamaa vs Uhafidhina..
Mkuu ukisoma vizuri sera za Chadema utagundua kwamba zimeelekeza nguvu zake ktk kuwatajirisha wananchi wenyewe. Chadema kama mrengo wa kati wanachukua mazuri kutoka pande zote mbili na kusema kweli ndivyo vyama vyote vya Tanzania vinafanya, hakuna chama cha Kijamaa (kushoto)wala cha kihafidhina (kulia) isipokuwa tunakwenda tu kama gari bovu kwa sababu ni wananchi wachache sana wanaopenda Ujamaa na wachache zaidi watapenda hifadhi ya mila na desturi zilizounda Utaifa wetu kuwa kioo (blueprint) cha ujenzi wa sera za chama. Na hao CCM duh, hata sijui niseme nini maanake hata Ubepari wao umepitiza yaani ni sawa na gari linalokwenda bila brakes!

Tunachokifanya sisi ni kuiga tu siasa za Ulaya na kuchukua yale yanayotufaa na kuachana na yale ambayo hayana maslahi kwetu kwa sababu maskini hata siku moja hana sauti. We can't make a call ndani ya dunia hii na hili muhimu zaidi kulitambua hivyo hizi siasa na demokrasia kwetu ni sawa na kumpelekea msukuma keki ama halua..Tutaweza vipi kuwa wajamaa bila kufuata siasa za Utengano hali hatuna uwezo wa hali na mali (Mtaji na elimu) ya kutuwezesha!..Maskini anaweza vipi kuweka mikakati ya kibiashara ikiwa hata mtaji wenyewe hana!...Na utaweza vipi kuwa mhafidhina ikiwa mila na desturi zako mwenyewe unazikataa kiasi kwamba hata lugha zetu zenyewe tunazipiga vita acha mbali kiswahili kinavyopotea!.. Hapa ndipo tunapojikuta tunakwamba na hizi siasa na demokrasia tofauti na wenztu waliotutangulia.

Ubepari sio sera na haitakuwa sera isipokuwa ni itikadi ambayo nchi nyingi za magharibi wameichukua na tofauti zipo ktk sera kama vile Wakristu au waislaam wanajulikana kwa imani zao lakini ndani yake kuna madhehebu tofauti..Haya madhehebu ndio unavyoona vyama vya Conservative na Democratic....
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Kinachochekesha CCM wana ubepari wa kudandia ambao hauna mpango wakati Chadema wana ubepari wa kupangwa. Kwa CCM mwekezaji ni mkombozi lakini Chadema wanataka Mtanzania awezeshwe. Kwa CCM madini ni mali ya mzungu wakati Chadema wanasema madini lazima yanufaishe taifa. Kwa CCM kilimo kwanza ni kugawa mapande makubwa ya ardhi kwa kampuni za kigeni zijilimie wenyewe chakula wakati wakulima wa Kitanzania wakifa njaa wakati Chadema inataka mkulima wa Kitanzania awezeshwe. Sasa sijui Topical na Mbopo ni ubepari gani mnaouzungumzia hapa.

This should not turn out to be a contest. Ukweli ni kwamba ubepari kwa nchi yetu hauwezi kuwa suluhisho la matatizo yetu, whether ubepari huo umepangwa au la. Misingi ya ubepari haibadiliki kwa kuzingatia boardroom zilizotumika kutengeneza katiba. Misingi ya ubepari, faida na hasara zake ni elimu basic ya sekondari, lakini tukiangalia yanayotokea kwa wenzetu, ni rahisi kuelewa kwa nini mfumo huo haufai na hauna manufaa kwa wananchi wanaodai kuwatetea. It remains to be a paradox
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
932
Kwanza inabidi kuondokana na hili neno Kibepari na badala yake kutumia maneno yanayoswihi kama Vile Ujamaa vs Uhafidhina..
Mkuu ukisoma vizuri sera za Chadema utagundua kwamba zimeelekeza nguvu zake ktk kuwatajirisha wananchi wenyewe. Chadema kama mrengo wa kati wanachukua mazuri kutoka pande zote mbili na kusema kweli ndivyo vyama vyote vya Tanzania vinafanya, hakuna chama cha Kijamaa (kushoto)wala cha kihafidhina (kulia) isipokuwa tunakwenda tu kama gari bovu kwa sababu ni wananchi wachache sana wanaopenda Ujamaa na wachache zaidi watapenda hifadhi ya mila na desturi zilizounda Utaifa wetu kuwa kioo (blueprint) cha ujenzi wa sera za chama. Na hao CCM duh, hata sijui niseme nini maanake hata Ubepari wao umepitiza yaani ni sawa na gari linalokwenda bila brakes!

Tunachokifanya sisi ni kuiga tu siasa za Ulaya na kuchukua yale yanayotufaa na kuachana na yale ambayo hayana maslahi kwetu kwa sababu maskini hata siku moja hana sauti. We can't make a call ndani ya dunia hii na hili muhimu zaidi kulitambua hivyo hizi siasa na demokrasia kwetu ni sawa na kumpelekea msukuma keki ama halua..Tutaweza vipi kuwa wajamaa bila kufuata siasa za Utengano hali hatuna uwezo wa hali na mali (Mtaji na elimu) ya kutuwezesha!..Maskini anaweza vipi kuweka mikakati ya kibiashara ikiwa hata mtaji wenyewe hana!...Na utaweza vipi kuwa mhafidhina ikiwa mila na desturi zako mwenyewe unazikataa kiasi kwamba hata lugha zetu zenyewe tunazipiga vita acha mbali kiswahili kinavyopotea!.. Hapa ndipo tunapojikuta tunakwamba na hizi siasa na demokrasia tofauti na wenztu waliotutangulia.

Ubepari sio sera na haitakuwa sera isipokuwa ni itikadi ambayo nchi nyingi za magharibi wameichukua na tofauti zipo ktk sera kama vile Wakristu au waislaam wanajulikana kwa imani zao lakini ndani yake kuna madhehebu tofauti..Haya madhehebu ndio unavyoona vyama vya Conservative na Democratic....

Je hiyo kuwa kati kwa kati ndio ubepari au nini?
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
932
Kwa kuuliza maswali kama haya taratibu mnaanza kuikubali Chadema kuna mwingine ameanzisha thread anataka kuijua CDM kwa undani zaidi ni dalili nzuri kwa Chama. Kuwasaidia mnaweza kutembelea tovuti yao.

Inaweza kukubalika au kutokukubalika both ways are possible

Je ubepari kama sera kwa faida ya nani..
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
5,375
This should not turn out to be a contest. Ukweli ni kwamba ubepari kwa nchi yetu hauwezi kuwa suluhisho la matatizo yetu, whether ubepari huo umepangwa au la. Misingi ya ubepari haibadiliki kwa kuzingatia boardroom zilizotumika kutengeneza katiba. Misingi ya ubepari, faida na hasara zake ni elimu basic ya sekondari, lakini tukiangalia yanayotokea kwa wenzetu, ni rahisi kuelewa kwa nini mfumo huo haufai na hauna manufaa kwa wananchi wanaodai kuwatetea. It remains to be a paradox
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
932
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.

You might have a point, Ubepari ambao una faida kwa wananchi wa kawaida na sio wenye mitaji (matajiri) ni upi?

Naomba unisaidie ubeoari wa chadema na ccm una tofauti gani..? kwa ajili ya wananchi?
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
5,375
You might have a point, Ubepari ambao una faida kwa wananchi wa kawaida na sio wenye mitaji (matajiri) ni upi?

Naomba unisaidie ubeoari wa chadema na ccm una tofauti gani..? kwa ajili ya wananchi?

Kwa kuanza tu CCM inaamini kuwa mwekezaji ni mkombozi. Hata kama atawanyanyasa na kuwanyang'anya ardhi raia wazawa kama ambavyo
imetokea huko Mbarali. Chadema inaamini kumwezesha raia mzaliwa kuwa mwekezaji katika nchi yake mwenyewe. Chadema inaamini kuwa madini shurti yanufaishe nchi na hasa maeneo yanakochimbwa. CCM inaamini kuwa madini yamnufaishe mwekezaji kwani ameleta mitambo yake na asilipe kodi. Hayo ni mawili tu yanayoonyesha tofauti kubwa baina ya upebari wa CCM na vision ya Chadema. Ukitaka nitaendelea kumwaga somo.
 
Hizo si Imani ya CCM..inabidi ukasome sera za ccm ok tuache hayo maana unaongelea kishabiki zaidi

Nimesoma sera za chadema sijaona mahali kuna imani hizo ulizosema..

Unamwezeshaji raia mzaliwa .. i mean unafanyeje ki-sera..i.e. ubepari? ambao ndio sera mama ya chadema
 
Mlamoto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
351
135
Hizo si Imani ya CCM..inabidi ukasome sera za ccm ok tuache hayo maana unaongelea kishabiki zaidi<br />
<br />
Nimesoma sera za chadema sijaona mahali kuna imani hizo ulizosema..<br />
<br />
Unamwezeshaji raia mzaliwa .. i mean unafanyeje ki-sera..i.e. ubepari? ambao ndio sera mama ya chadema

Duh! Kumbe unaongelea usichokijua! Maajabu!. Debe tupu halikosi kutika.
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,542
5,870
hili neno ubepari siku hizi halitumiki

inaaitwa uchumi huria...au uchumi wa soko....

Nimelipenda jibu lako.
Free market economy ndio order of the day dunia nzima kwa sasa, hata hao wanaojiita wakomunisti/wajamaa (China, Russia, Cuba etc) nao wameingia kwenye soko huria.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
You are preaching to the wrong tree. Waambie CCM ambao wamejitumbukiza katika ubepari bila mpango na bila dira.

Hata hao walioweka kwenye katiba zao wamedandia kwa sababu mazingira ya nchi yetu hayako compartible na huo mfumo wanaoupendekeza. Labda kama shida yao ni kuangalia maslahi ya wenye uwezo na siyo watanzania.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom