Kwenye Ubepari siyo jukumu la Serikali kulinda maadili ya mtoto wako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
KWENYE UBEPARI SIO JUKUMU LA SERIKALI KULINDA MAADILI YA MTOTO WAKO.

Anaandika, Robert Heriel.

Akiwa teja shauri yako. Akiwa Shoga utajua mwenyewe na toto lako. Akiwa litoto lilevi na linaloshinda vijiweni haiwahusu serikali. Ilimradi serikali haidhuriki, na Yale mapapa na mabepari hawapata madhara yoyote, wao kwao hiyo haiwahusu.

Siasa za kibepari haziangalii Watu wajingawajinga na Maskini watakaobebwa na upepo wa mabadiliko ya kidunia(utandawazi), ubepari unahusu zaidi Watu wenye nguvu ya fedha, wasomi wenye Akili za juu, Watawala ambao wanauwezo kuwa kukabiliana na changamoto zozote za mabadiliko yoyote ya kimfumo.

Kwenye Ubepari ndio kuna ishu za Masingle mother's, Single mother Kwa wenye Pesa sio tatizo Kwa sababu Mama anapesa, Baba anapesa, mtoto anasoma shule nzuri, kila mzazi anajionyesha kuwa anauwezo wa Kulea Watoto pasipo Usaidizi wa Mwenzake. Lakini vipi Kwa Wale Maskini? Nchi Maskini haziwezi himili changamoto za Ubepari hasa katika kipengele cha Usingle mother. Mama bado ni Maskini, yeye mwenyewe hajiwezi, ili aweze kuishi itampasa awe na madanga, naam hiyo tayari ni biashara na ndio Ubepari wenyewe lakini wenye madhara.

Familia na koo Maskini hazitakubali mifumo ya kibepari kwani hazina uwezo wa kuzikabili changamoto zake.
Ubepari unaruhusu Uhuru uliopitiliza ili kutengeneza biashara nyingi zenye Pesa. Ili kuongeza kundi kubwa la Maskini na watu ambao wamechanganyikiwa.

Familia na koo tajiri kamwe hazitoruhusu mfumo wa kijamaa na kijima kwani mifumo hiyo haiwasapoti kuendelea kuwa matajiri. Ubepari ndio mbinu pekee ya kuongeza idadi ya kutisha ya Watu wajingawajinga na Maskini, Kwa gharama ndogo ya Uhuru uliopitiliza ambao ni upumbavu.

Kumuachia Uhuru MTU mjinga na Maskini ndio mbinu rahisi isiyo na gharama ya kumfanya azidi kuwa Maskini na mjinga kabisa. Kumdhibiti MTU na kumpunja Uhuru wake ni kumfanya MTU huyo awe na Akili hata kama angekuwa mjinga Kwa kiwango gani, MTU huyo kadiri unavyombana ndivyo polepole Kwa uhakika ataanza kufikiri kujikomboa.

Katika Ubepari itatolewa Elimu ili kumpa MTU Uhuru WA kifikra na kimawazo lakini Uhuru huo itamfanya MTU huyo kuwa mfungwa wa Matendo, Uhuru uliozidi WA kifikra utamuingiza MTU kwenye GEREZA la Mwili bila ya yeye kujua. Uhuru wa kidini, hupofusha Akili na macho,

Katika Ubepari, Uhuru wa kuabudu ni nyenzo muhimu na silaha ya kutegemewa katika kuwaumiza Watu wajingawajinga na maskini, wanasiasa na watu mashuhuri wa madhehebu watahubiri Uhuru wa kuabudu huku wakiwaambia waumini wao kuwa wawe tayari Kufa kupona kwaajili ya kupigania Uhuru wao wa kuabudu.
Lakini ni Uhuru huo ni uhuru kweli au ni jitihada za kuwafanya wao wawe watumwa?

Taikon natafakari, je MTU anayeabudu na Yule asiyeabudu ni Nani aliyehuru? Ubepari hautakulazimisha kuabudu katika dini Fulani Kwa mabavu lakini tayari ulishaandaa mfumo wa kimabavu indirect way WA kukufanya uwe mfungwa wa kiimani. Kadiri MTU anavyotaka kuwa huru ndivyo anavyojiingiza kwenye Utumwa.

Dini zinapohubiri kumkomboa mtu na kumfanya awe Free/ huru ni maneno kinyume kabisa, kwani tangazo hilo linamaanisha kumfanya MTU awe mtumwa katika dini Fulani. Ubepari ni mashindano, kugombea fursa. Fursa zipo nyingi na ili fursa zigombewe Kwa kile kiitwacho Usawa itabidi Uhuru utangazwe, Jambo Hilo ni nzuri. Lakini Nani Ajuaye na kupima Jambo hili ni huru au sio huru likifanyika au kufanyiwa. Hicho nacho ni kitendawili.
Kitendawili hiki kitateguliwa Baada ya Uhuru huo kupatikana, itadhihirika kuwa ni kweli upo huru au ilikuwa danganyatoto. Uhuru hautakuwa mdomoni bali nafsini. Kila MTU atakiri kuwa nipo Huru.

Nafikiri wanasiasa, Watawala na wale wasomi wanafahamu Ubepari ni silaha ambayo kwayo watazidi kustawi.

Lakini je ni kweli, Watawala wenyewe, na wanasiasa wakiwa na familia zao hutumia ubepari Kwa Wake/waume zao au Watoto wao. Jibu ni hapana. Wanajua Ubepari sio mzuri, sio furaha, na hakuna Raha katika Ubepari.
Ubepari wanajua ni Unyonyaji, naam Unyonyaji WA jasho, Akili, uzuri, furaha, Mali, na kila uwezo wa Watu wajinga na Maskini ili wao wazuri kustawi.

Ubepari ni kama swali ambalo utapewa Options nyingi za kuchagua majibu lakini katika hizo options hakuna jibu hata moja Sahihi. Ooh! Taikon unasema nini?

Taikon ninaamini katika Falsafa hii; Mnyama utamtawala Kwa kumnyima Uhuru wake. Wakati binadamu utamtawala Kwa kumpa Uhuru wake uliopitiliza.

Acha nipumzike SASA!
Ni Yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ila ujamaa na umaskini ni kama mwili na damu, vinakaa pamoja.
Ujamaa ni mzuri kinadharia, kiuhalisia hauna tija sana.
Nyerere mwenyewe ulimchosha!
 
Ujamaa unachukua long process kuleta utajiri wa Watu lakini unasaidia Watu wengi Kwa pamoja.
Ubepari unaleta Maendeleo Kwa haraka na utajiri lakini Kwa wachache.

Tusuke au tunyoe
 
Mkuu ujamaa hauwez leta utajiri hususan katika level ya taifa labda iwe level ya familia,
Kote ujamaa ulikojaribiwa umefeli vibaya sanaaaaa
N.Korea hadi leo bado anajaribu kuishi kijamaa na unaona maisha yake, China, USSR Tanzania kote ujamaa umefeli

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Ila ujamaa na umaskini ni kama mwili na damu, vinakaa pamoja.
Ujamaa ni mzuri kinadharia, kiuhalisia hauna tija sana.
Nyerere mwenyewe ulimchosha!
Jambo la kipuuzi katika ujamaa ni kutaka watu waishi pamoja, kufanya kazi pamoja na kugawana mapato sawa. Hili ni upuuzi maana watu hawana akili moja, nguvu sawa, nia moja nk. Kwa asili binadamu wanatofautian na hivyo ubepari hutoa fursa wenye uwezo zaidik kusonga mbele
 
Ndio maana Tz Mtu akifanikiwa tu basi kuna huwa kuna kauli mbili ya kwanza huitwa mwizi au muuza UNGA na ya pili alikuwa FISADI zamani ndio maana huwezi kukuta maendeleo ya maana sababu mtaji wa mwanasiasa kuwapigania wa WANYOGE ili hali wanajua sio kweli.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom