Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,422
39,670
Huko Nyuma, Mzee Iddi Simba alikuja na hoja kuwa kama kweli Tanzania inataka ipige hatua kubwa ya maendeleo hatuna budi kuja na sera za kujali wazawa(weusi...). CCM ilikataa maneno hayo kitu kilichochangia kuanguka kwa mzee Simba kwenye medazi za kisiasa. Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na makala ya kiingereza iliyoandika na Adam Lusekelo wa Daily News kuhusu kuwapa nguvu watu weusi!! Makala yenyewe hii hapa:

_____________________________________________________________
HEARD our prez, Jack Mrisho, say that given the empowerment, Tanzanians are quite good at doing business and making their bones in life.

I agree. But I would have liked the prez to add what would have touched the other word which Tanzanian political establishment have shied away from - B - word. Black Tanzanians. Black empowerment!

Because we have seen the much-played around word of people of Bongo. Tanzanians. It seems that some Tanzanians are more equal than other Tanzanians and that is based on colour.

It is just like in the colonial times. White Tanzanians come tops in everything, finances and opportunities. They come even tops in meeting the big potatoes. Which is understandable, bearing the latent inferiority complex of most of our leaders.

Then come in Tanzanians of Indian descent. They have been holding most of the money. Some people, including some leaders, want some of the dosh to go to build silly looking mansions (call them pyramids) somewhere. Presumably they will be buried in the mansions.

Then comes in the scandalous poverty amongst the black Tanzanians. If the prez meant empowerment, he should then talk about Black Tanzanian empowerment.

In Sausi, they talk openly about Black empowerment in a country where the mass of the population has been brutalised and raped over decades. Why shouldn't we?

In Mchuchuma I hear funny names. In all the mines I hear funny names, never heard before in my life. When the figures of income derived from the mines are read out it's from wa-zungu Tanzanians. Can't Black Tanzanians read? Should the so-called investors be white or, as the press put it, Tanzanians of Asian origin only?

Because, really, this is insulting to us, Blacks. I once heard a remark by some clownish minister (he still is a minister. Sad) that Black Tanzanians were not trained to do business.

Some ministry of education idlers even removed subjects like commerce from the curricula.

You simply wonder if those guys had something from their necks upwards. In history, we learnt that many Mediterannean countries had what they called city-states. They were powerful and lived on commerce. Look at Zanzibar when the rule of Seyyid Said Bin Sultan started. But he empowered fellow Arabs.

The politicians have been pooh-pooing what Mzee Iddi Simba has been saying about 'Uzawa'. He was simply talking about Black empowerment. He is not wrong. We want to see Black Tanzanian businessmen and women. We want them being millionaires. Privatising should not be 'whitening' of public corporations in Bongo!

* * *

Mawazo yangu kwanza baada ya kusoma makala hiyo ni kuwa huyo Lusekelo aachie ngazi, hawezi kusema maneno aliyoyasema hapo juu bila ya kuonekana mbaguzi!! Sijui kama kuna ulazima wa sera ya namna hii, na ni jinsi gani sera kama hii inaweza kutekelezwa bila kuleta athari za ubaguzi!! Hata hivyo bado najaribu kufikiri kwa kufuata mfano wa Afrika ya Kusini na Marekani!!!
 
Mkjj unaikumbuka sera ya Africanization ya Nyerere??????? ever heard of it? Jaribu kuitafuta na kuresearch the pro's and con's halafu tuendelee na mjadala!!!!!!!
 
MJJ tuweke elimu ubaguzi hausaidii hasa ukizingatia Tanzania ni nchi masikini Solution ya Tanzania ni Elimu siyo biashara. Elimu italeta biashara lakini biashara pekee haisaidii nchi.
 
MJJ you can not punish sucess, remeber you said before that Wachaga leaders should step down!. Tanzanians need postive enforcement we should tell people to step up and not some group to step down!.
 
Black Empowement is long due in Tanzania. Sera za uzawa sio ubaguzi bali kujenga mfumo kwa rasilimali zote zimilikiwe na wazawa halafu wawekezaji wote lazima waingie ubia na wazawa katika kila sekta ili baadhi ya net profit ya hii miradi ya uwekezaji ibakie nyumbani.

Niko hapa India, ardhi yote ni mali ya koo fulani fulani the rest ni landless. Kama umezaliwa kwenye landless family, kwa hakika utakufa landless. Hakuna namna yoyote ya mwekezaji toka nje ya India, anayeweza kuwekeza India bila kushirikisha wazawa. Tatizo la India wana Caste System ambao ni ubaguzi wa wazi wazi yaani kama umezaliwa ukoo wa hali ya chini wewe ni mtu duni maisha yako yote, na kama umezaliwa familia bora wewe ni bora. Hawa wahindi walioletwa Tanzania, walitoka low caste na walikuja kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati. Ndipo wakapata fedha na kukuta Bongo ardhi bure, ndio wakajitwalia na kujenga maghorofa karibu miji yote mikuu na hatimaye kulowea na kupata uzao wao Tanzania.

Tangu baada ya kutaifishwa kwa majengo yao, wahindi waliamua hawajengi tena, wameishia kupanga nyumba za Shirika la Nyumba, hawaweki tena vitega uchumi vya infrastrucure, kazi yao ni kuvuna tuu pesa na kuzihamishia India kuangalia namna ya kuinua hali za maisha ya low caste za jamaa zao walioko huku ambao kutokana na mfumo huo wa caste, hao jamaa zao huku ni masikini kweli kweli, hata wale ombaomba wa Dar ni afadhali!.

Umoja wa Falme za Kiarabu pia umeweka sheria kali za uwekezaji kwanza ardhi yote ni ya ukoo wa Kifalme, wananchi wanagaiwa bure ila haiuzwi, pili kila mwekezaji lazima aingie ubia na wazawa. Matokeo yake waarabu ni matajiri, kazi yao kula na kulala huku wakilipwa gawio la uwekezaji hivyo kubaki wakifanya ziara za utalii mwaka mzima na kuwinda wanyama
Baada ya burudani za kuua binadamu kupigwa marufuku.

Tanzania tunashindwa nini kumillikisha maeneo yenye madini kwa wazawa waliolizunguka. Wakina Barrick wakija, lazima waingie ubia na wamiliki ili hiyo dhahabu iwafaidie wote.
Maeneo yote yenye vivutio vya utalii kumilikiwa na waliopo. Ingawa lengo la Nyerere kukataamfumo huu lilikuwa zuri la kuzuia matabaka ya wenye nacho na wasionacho, lengo hili sasa limepitwa na wakati kwa sababu wenye nacho ni wageni na wasionacho ni wazawa, afadhali wazawa wa maeneo yenye nacho wamilikishwe na serikali iwatoze kodi kubwa hao wenyenacho na kuwagawia wasionacho.

Kariakoo wengi waliomiliki zile nyumba ni wanawake wa Kizaramo na Kimanyema baada ya waume zao waliokuwa makuli bandarini kufariki. Leo nyumba zote wameuza, wamehamia Tabata, wamiliki wapya ni Wahindi na Waarabu. Kama kungekuwa na sera ya uzawa, hawa wazawa wangeendelea kumiliki ardhi na mwekezaji angejenga kitega uchumi na kumiliki kwa ubia na wawekezaji.

Kilio cha kijana Nape kuhusu mkataba wa Jengo la Umoja wa Vijana-CCM, kimedondokea 'sikio la kufa' maana ule ni mkataba wa maisha!. Kwa lugha rahisi hilo jengo jipya linalojengwa litakuwa ni mali ya mwekezaji ila Umoja wa Vijana utapewa floor moja ua mbili, za kupangisha kupata tujisenti kidogo twa kiasi cha mbogana visenti vya kununulia soda za wakubwa ili wasipige kelele!.

Kwa waliiona movie ya 'Trading Places' watakubaliana na mimi kuwa wazawa weusi wana uwezo wa biashara kama wakiwezeshwa. Kuwezeshwa kwenyewe ni pamoja na kujengewe uwezo, capacity building ya kuja kuendesha hizi biashara kubwa kubwa ama- miradi mikubwa ya uwekezaji.

Ukiisoma vizuri ile sera ya Ubinafsishaji, utaona lengo lilikuwa tuuze yale mashirika na fedha zitakazo patikana ziwekwe kwenye mfuko maalum ambao ungetumiwa kuwagawiya wazawa mtaji katika ununuzi wa hisa mbalimbali. Sijui kama hilo lilitimizwa hivyo kwa lugha nyingine, zoezi lote la ubifsishaji pamoja na umasikini wetu, ni kile kidogo tulichonacho ndio tumekigawa bure kwa wenyenacho ili litimie lile neno, 'mwenenacho anaongezewa, na asiyenacho ananyang'anywa hata kile kidogo alichonacho.

Japo hayo yote yameshafanyika, thank God, Tanzania bado hatujachelewa kwa sababu japo mbele hatusongi, ila tumesimama hapa hapa tulipo na wakati mwingine tunapiga hatua kwa kurudi nyuma tungali tumesimama. Ushauri ni utekelezaji wa msemo huu 'anayejidhania amesimama, na aangalie usianguke'. Njia pekee ya kuzuia tusianguke ni kuwawezesha wazawa weusi kukamata usukani wa uchumi wetu.

Paskali
 
Tayari Serikali imeanzisha kitengo hicho na ofisi zake ziko pale karibu na ofisi ya mipango .Nimesha ingia humo ndani yet nimekuta ni wahindi na wachina wana jazana mle .Nimejaribu kutaka kuwa empowered mkuu wacha mchezo utasikia mambo ya ajabu.Kitengo na ofisi zipo na well equiped ila wanasema bado itawachukua muda kuwa in full operational sasa wanazunguka Duniani kujifunza .
 
Watanzania wazawa tukitaka utajiri kazi kwenda kwa waganga kisha wanatupa masharti tupate viungo vya albino!Malbino wamekuwa deal !wakati wenzetu wapo busy kufanya biashara sie tupo kwa waganga kutafuta utajiri!Tena ikiwekwa hiyo sera naona maalbino wote watakwisha !
 
Hawa wezi tunaowaita wawekezaji wanapokuja Ole Naiko anashughulikia vibali vyote vinavyowawezesha kutuibia ikiwa pamoja na msamaha wa kodi kwa miaka 5. Katika hali hii sera ya kuwawezesha wazawa si hisani, ni kitu ambacho hakiepukiki.
 
Samahani wakuu,hivi mwandishi Adam Lusekelo ndio yule mwandishi aliwahi kutimua tifu na wahindi pale Kisutu baada ya kufukuzwa asipaki mkweche wake mahali pao?, siku hiyo nakumbuka jamaa alipaka sana na ilibaki kidogo wazawa wafanye kweli lakini Wahindi wakawahi kufunga maduka yao
 
Adam Lusekelo ni mmoja tuu, hilo tifu la Kisutu silijui ila gari ya mwandishi usiite mkweche kwa sababu ni waandishi wachache sana wa bongo, wanaomiliki magari ya kununua kwa fedha zao, ukiondoa kundi la waandishi wakike na watangazaji ambao magari wamenunuliwa,na Adam Lusekelo ni mmoja wa wanaomiliki magari ya kununua wenyewe. Huyu ni mwandishi mkongwe oldtimer toka Dailynews ya enzi zile daily papers ni mbili tuu, yaani Dailynews na Uhuru. Kitu kizuri kuhusu Lusekelo maji anapiga sana na bado anaandika sense with a light touch.
 
Asante mkuu. lakini ulikuwa mkweche kwa wahindi, mie alichonifurahisha siku hiyo ni kutetea UUUUZZAAAAWAAAAAA, Kuna siku uzawa utashinda na Simba atarudi ulingoni,
 
Tuachane na lugha aliyotumia Adam Lusekelo, lakini ukweli utabakia kwamba kuna kila haja ya kuwawezesha Wazawa. Maelezo ya ndugu Pasco ni tosha kabisa kutufungua akili..

Swala la Uzawa sio kuwarudisha nyuma wahindi ama foreigners isipokuwa kuwawezesha wazawa - Kuna tofauti kubwa sana na kama alivyosema Kamundu Tanzanians need positive enforcement we should tell people to step up and not some group to step down!...
Nje ya hapo itatuuwia vigumu sana kuelewa nini malengo ya sera ya Uzawa.
 
- Sera za uzawa ni sera za kibaguzi period, miaka 47 ya uhuru kama wazawa hawajawa empowered, basi kuna kasoro kubwa na foundation ya uhuru wetu, nikiwa na maana kwamba huenda priorities zetu as a nation hazikuwa straight wakati tunadai na kupewa uhuru, na kama this is the case which I do not believe to be, then it is too late kwa sababu nafasi na time haipo tena ya ku-experience ishus za uzawa, na besides uzawa ni ubaguzi anyways!

- Idd Simba, ni opportunists politician aliyekuwa akijaribu ku-explore kila rogue political avenue kui-manipulate our political system ili afikie urais, kumbuka kwamba kwanza originally yeye ni Banyamulenge anyways, lakini akajipenyeza penyeza na kuwa among us, kwanza alijaribu kutumia U-Islam akashindwa kwa sababu CCM walishituka mapema, aliposhindwa akajaribu hii avenue ya uzawa nayo pia akakwama, sasa Simba angekua ni for real baada ya kutemwa ndio angeivalia njuga hii sera kama alikua anaiamini kwamba ni real deal kwa taifa letu ili tuamini kuwa ana hoja, lakini kimya anaendeleza mali alizopora akiwa serikalini hasa kutoka South Africa.

Wa-Tanzania tufike mahali tukubali kwamba tumechelewa sasa kilichobaki ni kujaribu kujifunza kwa kasi kubwa kutoka kwa waliowahi kama kasi ya wenzetu wa-China wanavyojifunza, leo US inashinda inakopa hela toka China kila leo, sera za uzawa ni nothing but ubaguzi na zisiruhusiwe katika taifa letu ambako tuna wazawa wanaoamini kuwa ukimuua Albino utapata utajiri, jana nilikuwa ninasoma gazeti moja bongo jinsi tajiri mmoja mzawa mwenye kampuni kubwa ya spare za magari na baiskeli huko Mbeya, sasa yuko Rumande kwa kutuma watu saba kumteka jirani yake Albino, ili akatwe viungo vya mwili na kuzikwa ndani ya nyumba yake ndio angekuwa tajiri zaidi, what a pathetic thinking za kizawa! maana ukianza ku-promote uzawa kwenye natiional level lazima iwe package na haya ya kuua wananchi wenzetu Albinos yakiwa ndani yake!
 
FMES,
Mkuu wangu wee hata marekani wenyewe hadi leo wana empower wazawa, trust me. Kuna tofauti kubwa ya kumrudisha mgeni chini na kumwezesha mzawa..hatuzungumzii kumrudisha mgeni chini bali focus ni kumwezesha mzawa. Ukielewa nia na madhumuni ya maneno haya utanipata vizuri. hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea haimweki mzawa mbele ya mgeni ila inamruhusu mgeni ku compete kwani uwanja wazi.. Empowering wazawa ni swala la lazima kwa nchi hizo isipokuwa nchi maskini tu.. na pengine ndio maana tunaendelea kuwa maskini.
 
Sasa mtu mweusi Tanzania apendelewe based on what? Kwa sababu ya rangi yake au? Maana South Africa Black Economic Empowerment ni kwa watu wote waliokua wanagandamizwa na policy ya apartheid yaani Black= watu weusi, cloured,wahindi na hata wachina.
Tukisema tujipendelee watu weusi kwa vile tu ni weusi tutakua tunajidhalilisha nadhani.
 
Mkuu wangu wee hata marekani wenyewe hadi leo wana empower wazawa,

- Mkuu wangu Bob, hili la ku-empower wazawa linakwama US ndio maana Republican Party wamegoma kutoa hela kwa Auto Industry yao maana wanajua tayari kwamba it is over, jawabu ni free market tu maana hizo big three auto zao hazitakuja ku-recover tena, no way!

- Hizo benki kubwa karibu zote zinazotumika kuwakopesha wazawa huko US ni za wageni, na sio siri tena sasa kwamba ili mzawa huko afanikiwe ni lazima ashirikiane na wageni ndio maana kampuni kama za Ford na Sartun, ziko sawa ni kwa sababu walishituka mapema sana na kuingia ubia na wageni in the 90s, jawabu ni free market ambayo ni careful na strickly regulated na federal gov.
 
Thank you Thank you Thank you Field Marshall ES:

Nchi yenye zaidi ya 98% ya wazawa, haiitaji sera ya wazawa hata kidogo. Kinachotakiwa ni sera ya kuinua standard of living kwa watu wote.

Matatizo makubwa tuliyonayo ilikuwa ni kuanza na mguu mbovu mara baada ya kupata uhuru.

Tuliweka sana nadharia mbele na maneno mengi bila ya kuwa pragmatic.
 
Black Empowement is long due in Tanzania. Sera za uzawa sio ubaguzi bali kujenga mfumo kwa rasilimali zote zimilikiwe na wazawa halafu wawekezaji wote lazima waingie ubia na wazawa katika kila sekta ili baadhi ya net profit ya hii miradi ya uwekezaji ibakie nyumbani.
Niko hapa India, Ardhi yote ni mali ya koo fulani fulani. Kama umezaliwa kwenye landless family, kwa hakika utakufa landless. Hakuna namna yoyote ya mwekezaji toka ndani ama nje anayeweza kuwekeza India bila kushirikisha wazawa. Tatizo la India wana Caste System ambao ni ubaguzi wa wazi wazi yaani kama umezaliwa ukoo wa hali ya chini wewe ni mtu duni maisha yako yote, na kama umezaliwa familia bora wewe ni bora. Hawa wahindi walioletwa Tanzania, walitoka low caste na walikuja kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati. Ndipo wakapata fedha na kukuta Bongo ardhi bure, ndio wakajitwalia na kujenga maghorofa karibu miji yote mikuu na hatimaye kulowea na kupata uzao wao hapa. Tangu baada ya kutaifishwa kwa majengo ya, wameishia kupanga nyumba za Shirika la Nyumba, hawaweki tena witegauchumi vya infrastrucure, kazi yao ni kuvuna pesa na kuzihamishia India kuangalia namna ya kuinua hali za maisha ya low caste za jamaa zao walioko huku ambao kutokana na mfumo huo wa caste, hao jamaa zao huku ni masikini kweli kweli, hata wale ombaomba wa Dar ni afadhali!.

Umoja wa Falme za Kiarabu pia umeweka sheria kali za uwekezaji kwanza ardhi yote ni ya ukoo wa Kifalme, wananchi wanagaiwa bure ila haiuzwi, pili kila mwekezaji lazima aingie ubia na wazawa. Matokeo yake waarabu ni matajiri, kazi yao kula na kulala huku wakilipwa gawio la uwekezaji hivyo kubaki wakifanya ziara za utalii mwaka mzima na kuwinda wanyama
Baada ya burudani za kuua binadamu kupigwa marufuku.

Tanzania tunashindwa nini kumillikisha maeneo yenye madini kwa wazawa waliolizunguka. Wakina Barrick wakija, lazima waingie ubia na wamiliki ili hiyo dhahabu iwafaidie wote.
Maeneo yote yenye vivutio vya utalii kumilikiwa na waliopo. Ingawa lengo la Nyerere kukataamfumo huu lilikuwa zuri la kuzuia matabaka ya wenye nacho na wasionacho, lengo hili sasa limepitwa na wakati kwa sababu wenye nacho ni wageni na wasionacho ni wazawa, afadhali wazawa wa maeneo yenye nacho wamilikishwe na serikali iwatoze kodi hao wenyenacho na kuwagawia wasionacho.

Kariakoo wengi waliomiliki zile nyumba ni wanawake wa Kizaramo na Kimanyema baada ya waume zao waliokuwa makuli bandarini kufariki. Leo nyumba zote wameuza, wamehamia Tabata, wamiliki wapya ni waarabu. Kama kungekuwa na sera ya uzawa, hawa wazawa wangeendelea kumiliki ardhi na mwekezaji angejenga kitega uchumi na kumiliki kwa ubia na wawekezaji.

Kilio cha kijana Nape kuhusu mkataba wa Jengo la Umoja wa Vijana-CCM, kimedondokea 'sikio la kufa' maana ule ni mkataba wa Maisha!.Kwa lugha rahili hilo jengo jipya linalojengwa litakuwa ni mali ya mwekezaji ila Umoja wa Vijana watakaa bure na tujisenti kidogo twa kununulia soda za wageni!.

Kwa waliiona movie ya 'Trading Places' watakubaliana na mimi kuwa wazawa weusi wana uwezo wa biashara kama wakiwezeshwa. Kuwezeshwa kwenyewe ni pamoja na kujengewe uwezo, capacity building ya kuja kuendesha hizi biashara kubwa kubwa ama- miradi mingi ya uwekezaji.

Ukiisoma vizuri ile sera ya Ubinafsishaji, utaona lengo lilikuwa tuuze yale mashirika na fedha zitakazo patikana ziwekwe kwenye mfuko maalum ambao ungetumiwa kuwagawiya wazawa mtaji katika ununuzi wa hisa mbalimbali. Sijui kama hilo lilitimizwa hivyo kwa lugha nyingine, zoezi lote la ubifsishaji pamoja na umasikini wetu, ni kile kidogo tulichonacho ndio tumekigawa bure kwa wenyenacho ili litimie lile neno, 'mwenenacho anaongezewa, na asiyenacho ananyang'anywa hata kile kidogo alichonacho.

Japo hayo yote yameshafanyika, thank God, Tanzania bado hatujachelewa kwa sababu japo mbele hatusongi, ila tumesimama hapa hapa tulipo na wakati mwingine tunapiga hatua kwa kurudi nyuma tungali tumesimama. Ushauri ni utekelezaji wa msemo huu 'anayejidhania amesimama, na aangalie usianguke'. Njia pekee ya kuzuia tusianguke ni kuwawezesha wazawa weusi kukamata usukani wa uchumi wetu.

Maelezo hayo hapo juu ya Pasco ni muhimu sana.
Wale wanaosema kuna ubaguzi kuhusu uzawa...Then niwaulize na hao wahindi na caste system si ubaguzi?
Mapungufu tuliyonayo ni makubwa kiasi cha kwamba tukifanya marekebisho bado tutakuwa fair na si ubaguzi hata chembe.
Kwamba mzawa anufaike na ardhi ya Taifa lake ni ubaguzi?
Kwa kulinganisha na wenzetu...Sisi bado sana tu...Tunahitaji marekebisho na nimeshangazwa na MKJJ kudai Lusekelo ajiuuzulu kwa hili...MKJJ una problrm na watu weusi? Kwanza ulisema ushabiki wa waafrika kwa Obama ni kwasababu ya weusi...Then weusi wakinufaika na ardhi yao ni ubaguzi...Vipi wakuu?
 
Sasa mtu mweusi Tanzania apendelewe based on what? Kwa sababu ya rangi yake au? Maana South Africa Black Economic Empowerment ni kwa watu wote waliokua wanagandamizwa na policy ya apartheid yaani Black= watu weusi, cloured,wahindi na hata wachina.
Tukisema tujipendelee watu weusi kwa vile tu ni weusi tutakua tunajidhalilisha nadhani.

Kuwawezesha wazawa kwenye nyanja muhimu za kiuchumi ni jambo la muhimu...Imagine mapesa yote yaliyohamishwa nje pamoja na za mafisadi wetu wazawa...Taifa lingekuwa wapi?
We huoni kwamba kuna uozo hapo na kunahitaji mabadiliko makubwa?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom