Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?

Hivi kwa nini lakini kuwe na upendeleo? Kwa nini kusiwe na fursa sawa kwa wote nikiwa na maana kila mtu awe na nafasi inayolingana na mwingine katika kufanikiwa kimaisha na akishindwa basi hana mwingine wa kumlaumu isipokuwa yeye mwenyewe....

Kwa maoni yangu mimi naona cha muhimu hapa ni kuwa au kujenga nidhamu ya kufuata utawala wa sheria na utungaji wa sheria nzuri zisizo za kibaguzi zitakazoenda sambamba na utawala huo. Tutakapoliweza hilo naamini kabisa tutakuwa tumejenga misingi ya usawa wa fursa kwa wote bila kuangalia uzaliwa, rangi, dini, jinsia ya mtu na mambo mengine kama hayo.

Does that make sense, common sense that is?
Nyani sikatai inabidi kufuata utawala wa sheria, lakini suala la kumuwezesha mzawa inabidi liwa la lazima. Sasa hivi tunaambiwa kwa South Africa ni wazalishaji wa tanzanite na wakati tanzanite inapatikana Tanzania, wanaondoka nazo na ndege moja kwa moja wewe unadhani hizo Tanzanite zinaijenga TZ au SA? I'm sorry lakini siwaamini white people (Niite rasist sitajali) wako very sneaky na haya mambo ya globalisation wameyaweka ili waweze kutunyonya tuu na sisi tuna-fall kwenye trap. yaani wanafanya mbinu nyingi sana watuweke tuamini hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo inavyotakiwa. Kwani hujaona Uchumi wao unaporomoka wanakimbilia kwenye serikali na wakati wao ni mabepari, ila mwingine unaonekana mjamaa (na hiyo ni sumu ya maendeleo).
Wengine ambao ni wahindi wana uraia wa nchi nyingi nyingi tuu na wamekaa kuibaiba tuu na ndio wanao-influence viongozi wetu wengi waibe (Of cource kila mtu lazima usingizie kitu) Lakini ndio hivyo, na wao wakiiba wanajenga huku ziliko familia zao. (Mfano Saddam alivyoiba alijenga wapi?) lakini kwa kweli inanisikitisha sana na jamaa hawana machungu kabisa na Bongo.
 
Fundi Mchundo kaandika:
Hizo ekari 50-100 kwa kila mchaga uchagani zitatoka wapi?

Pendekezo langu ni kwamba wale ambao kwao kuna ardhi, basi warasilimishwe hiyo mali. Warudishiwe mali ambayo tangu mwanzo ilikuwa halali yao.Uchagani hakuna ardhi. Wale ambao hawakuitika mwito wa Mwalimu wa kuhamia sehemu nyingine basi shauri yao. (Mimi nimewahi Bagamoyo). Sio kila mzawa atawezeshwa kwa njia hii. Nilisema hii ni njia mojawapo. Lazima zitatumika njia mbali mbali. Ukitaka nitataja njia nyingine tena.

Na kwa mtaji huu, huyo mchaga hataruhusiwa kwenda kuziomba Mahenge maana zitakuwa zimeishatengwa kwa wazawa wa kule

Zitabaki nyingine. Huoni tumependekeza kiwango?

Na jee, huyo mzawa mwenye hizo ekari, akitaka kumkatia mtu wa kutoka nje ya sehemu ile, ataruhusiwa?

Mali ikishakuwa yako na ukawa na haki miliki basi ni yako kweli kweli. Ni kama pesa tu. Unaweza kumpa au kumwuzia mtu yoyote.

Akiruhusiwa na baada ya muda mfupi tukikuta wageni kutoka sehemu nyingine ya nchi wanahodhi sehemu kubwa ya hiyo ardhi, tutawanyang'anya?

Wakikamata ardhi wakalima wao na fedha tukawa nazo sisi mfukoni kuna ubaya gani? Kama kuna mtu atauza na fedha akatafuna basi huyo ni goigoi. Kuna watu ambao haitawezekana kuwainua hata ungewapa nini. Ni wa kunyonywa tu!

Tukumbuke tulinyang'anya maghorofa yote ya uhindini, tukaanzisha msajili wa majumba, tukagawiana wenyewe na leo yako wapi?

Hatukugawiana wenyewe. Majumba yaliwekwa chini ya makampuni ambayo viongozi wake ni mashabiki wa chama. Kwa vile ni watu corrupt basi hali imekuwa kama ilivyo.

Kuwarasilimisha wazawa kwa kuwapa haki miliki ya ardhi yao ni kutenda tu haki. Si kuwapendelea. Ardhi ilipokonywa wakati wa Uhuru. Tusahihishe hilo kosa.
 
Hivi kwa nini lakini kuwe na upendeleo? Kwa nini kusiwe na fursa sawa kwa wote nikiwa na maana kila mtu awe na nafasi inayolingana na mwingine katika kufanikiwa kimaisha na akishindwa basi hana mwingine wa kumlaumu isipokuwa yeye mwenyewe....

Kwa maoni yangu mimi naona cha muhimu hapa ni kuwa au kujenga nidhamu ya kufuata utawala wa sheria na utungaji wa sheria nzuri zisizo za kibaguzi zitakazoenda sambamba na utawala huo. Tutakapoliweza hilo naamini kabisa tutakuwa tumejenga misingi ya usawa wa fursa kwa wote bila kuangalia uzaliwa, rangi, dini, jinsia ya mtu na mambo mengine kama hayo.

Does that make sense, common sense that is?
Nyani Ngabu. Kwanza heshima mbele, pili naomba nikupe mfano mdogo wa upendeleo n kukuonyesha kama upendeleo usingekuwepo hali ingekuwaje..
Wakati wa Ukoloni, ulifanyika mtihani mmoja tuu kwa Middle School zote za makoloni ya Mwingereza na ulitungwa Cambridge. Matokeo waliofaulu wengi walitoka baadhi ya maeneo tuu. Shule za Sekondari hata zilizokuwa vijijini, wazawa wa eneo lile waliziona kwa macho tuu. St. Francis (Pugu) na St. Andrews (Minaki) zilikuwa Uzaramoni na amini usiamini zilijaa makabila mengine tuu na hakukuwa na Wazaramo, na wachache waliobahatika ni wale waliolelewa na Mission. Sambamba na Mazengo huko Dodoma hakukuwa na Wagogo. Wagogo wa kwanza kupata elimu ya juu ni Mzee Malecela na nduguye Job Lusinde tena bahati yao walilelewa na Mission.

Baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere aliliona hili ndipo akaamua japo tutaendelea kufaya mtihani mmoja wa darasa la saba, kila mkoa utakuwa na passmark yake.
Passmark ya Kilimanjaro na Bukoba iko juu sana huwezi kulinganisha na ile ya Singgida na Dodoma. Hii ilisaidia
Kutoa fursa kwa makabila mengi zaidi kuingia sekondari.

Mimi nimesoma Ilboru High School, nimeshuhudia upendeleo maalum kwa watu kwa watoto wa makabila ya wafugaji toka Singida na Shinyanga na Wamasai wakiletwa Ilboru ili nao waelimike. Tena wengine walikuja wamezoea maziwa tuu, Mkuu wa Iliboru enzi hizo akiitwa Bino (Mlm Mushi), aliwaendelezea dose ya maziwa kwa miezi sita ya mwanzo huku wakizoeshwa kupiga Chui (uji usio na sukari) na ugali.

Miaka ya 80, serikali iliwachukua kwa nguvu watoto wanne wa kabila la Wabarbaig. Ikawasomesha msingi na kuwapasisha wote na kuwapeleka Pugu Sekondari
Wakafanya mtihani wa O-Level wakapata
F masomo yote na kutoka na Div.0. Serikali ikawarudisha Ubarbaig na walipotembelewa kuona kawa watawabadilisha wenzao, wakakutwa nguo wametupo, back kwenye ngozi and life as usual.

Hii ni mifano michache ya umuhimu wa upendeleo. Kama kusingefanyika upendeleo wa aina fulani kwenye Elimu, basi wasomi wote wangekuwa watu wa makabila fulani fulani na makabila mengine ungekuta hakuna!.

Vivyo hivyo kufuatia mfumo dume kutawala jamii zetu kwa miongo mingi nyuma, umefanyika upendeleo maalum kutoa fursa maalum kwa wanawake katika nyanja mbalimbali ili kutoa fursa sawa kwa wote.

Kuna tofauti kubwa ya I.Q kati ya mtu na mtu na makabila na makbila. Kama wenye I.Q ndogo hawatasaidiwa, kamwe hawawezi kupata maendeleo sawa na wenye I.Q kubwa.

Tunachosisitiza sio ubaguzi bali wazawa bado tuko nyuma katika biashara kubwa na uwekezaji. Kufanyike upendeleo kulazimisha kila mwekezaji lazima aingie ubia na mzawa ili tuendelee kwa pamoja.
 
Nimefuatilia huu mjadala sasa nimeconclude kwamba, sera inayofaa zaidi ni sera ya KUMUWEZESHA MTANZANIA. neno uzawa liko veiled, linasimama badala ya "watanzania weusi ", na kwa maana hii, hii sera inavunja misingi ya katiba yetu ya kwamba hakuna sheria yoyote itakayotungwa na kutekelezwa ambayo inabagua watanzania fulani dhidi ya wengine.hii itakuwa ni sera ya upendeleo.

Kuna mtu katoa mfano wa kuwagawia watu ardhi halafu wawekezaji wakija waingie ubia na wananchi, hili ni sawa lakini je kama tunafuata sera hii ya uzawa ni Mtanzania yupi atastahili kupewa hii ardhi?, aliyezaliwa Tanzania kisha akawa Mtanzania?, aliyeomba uraia na kwa hiyo akawa Mtanzania?, mweusi?, mweupe?.

kwa hiyo utagundua kwamba sera ya Uzawa hailengi kumkomboa Mtanzania bila ya kujali rangi yake, kwa hivyo basi hii itakuwa ni sera ya kibaguzi. kumbuka wananchi wanaolipa kodi Tanzania si wale wenye rangi nyeusi peke yake, bali Watanzania wote. kwa hivyo basi sera muafaka hapa ni SERA YA KUMUWEZESHA MTANZANIA NA SI KUMUWEZESHA MZAWA, tukitumia neno uzawa itakuwa ni contradiction isiyo ya lazima kwa sababu kuna Watanzania wamezaliwa London, au New York au sehemu nyingine nje ya Tanzania tena baadhi yao na Mzazi mmoja Mtanzania na mzazi mwingine si Mtanzania je hao nao ni Wazawa kwa vigezo vipi?
 
Mkuu hivi ktk akili yako unaamini kwamba mashirika haya ya Ford, GM yataondoka na kufa kifo cha nyani bila kupewa msaada!...U must be kidding! Mkuu wangu jaribu kusoma nyakati kwa sababu hizi ni siasa tupu zinatumika sasa hivi lakini by the end of all this, mashirika haya yatapewa kila msaada yaweze kushindana. Focus ya Marekani ni kuiweka nchi yao ktk uwezo wa kushindana na wanaposema nchi yao ni muhimu uelewe kwamba wewe na mimi hatumo!

- Mkuu Bob, point yangu ni kwamba serikali haiwezi kujihusisha na siasa za uzawa tena maana time zimebadilika, Ford haijayumba kwa sababu ilishajiunga ubia na wageni longtime ago na kufuta dhana ya uzawa,

- Hayo mashirika mengine yaliomo kwenye ICU sasa hivi, mkuu wangu hayo ndio nitolee yameisha, si umesikia yamefunga viwanda vyake kila kona tayari hayawezi kurudi tena it is over, serikali haiwezi kuwasiadia wazawa as a sera, serikali inasaidia uchumi wake regardless nani anaumiliki katika sera za Free Markets maana hizi markerts hazijali mzawa wala mgeni na ndio sera za kisasa zile za kitikadi zilishindwa siku nyingi mkuu.
 
Nafikiri hapa watu wanachanganya mambo.
Tuseme sehemu zenye machimbo Tarime. Watu wanahamishwa na serikali kwa nguvu au kupewa PESA ili wahame kupisha uchmbaji wa dhahabu. Serikali yetu (hapa ndiyo inalalamikiwa kuwa haiendelezi Weusi) inatoa mfano wa ovyo kabisa. Wao kama Wasomi inatakiwa watoe mfano na kuwafundisha watu biashara. Kwangu mie ilitakiwa kufanya hivi kwamba, serikali kuwasaidia Wananchi kuingia mkataba na Wachimbaji. Wanahakikisha mikataba na Wachimbaji inafanyika na yenye faida kwa wananchi. Hayo maeneo yanabaki bado ya wenyeji, wageni wanayakodisha kwa hela nzuri tu. Serikali inakuwa inakusanya kodi tu na hizo pesa nyingine sijui wanaziitaje. Serikali kwa kufahamu UJINGA wa Weusi wengi, inaweka SHERIA kali kuwa Mgeni hawezi kununua ardhi. Sasa tuseme Barick akija na kusema kanunua hilo eneo, serikali iseme NO. Mwisho wa siku, wakulima hao wataanza kupata mwanga jinsi MAMBO yanavyokwenda. Watajua kuwa kumbe usiingie kichwa kichwa.
Kuna zile film za GOD MUST BE CRAZY. Yule Mzee nasikia film ya kwanza walivyomlipa pesa basi akaangalia yale makaratasi na akayutupa. Film ya tatu akawa kajua dola ni nini na akadai alipwe zaidi. Cha muhimu kwa watu hawa ni kwamba, wengi inabidi kuwafundisha nini maana ya kuwa na pesa kubwa. Kule kwetu walikuwa wakipata pesa za tumbaku, wanapata kichaa. Ukiwafundisha na kuanza kuwapata mwanga nini cha kufanyia hizo pesa, Duniani hakuna mtu mjinga.
Kwa kumalizia niseme kwamba, inaposemwa KUMSAIDIA MTANZANIA MWEUSI, sidhani ina maana ya kumpendelea tu. Kumuwezesha KIFIKRA hilo ndilo linatakiwa kwanza. Hawa watu wakiandaliwa na kupewa mwanga, watakuwa wazuri tu. Tatizo hata viongozi wetu hili hawalijui. Hata kama wakilijua bado wanalifanya bila MAANDALIZI. Hela za Kikwete si zimeliwa tu na wajanja? Hata kama zisingeliwa, huko kijijini, mjomba akizipata tu anaongeza mke wa pili.
Ukisikiliza history za Wayahudi, hawa kwa kutumia ma RABIN, huandaa watu wao mapema sana kibiashara. Wana nyimbo, funy story, misemo nk mingi tu inayomfumbua macho Myahudi katika dunia hii. Je Mtanzana anaambiwa nini? KWenye Dini ndiyo tunapotezwa kabisa. Methali zetu ndiyo hizo, Haraka haraka haina...., kawia ufike, mtaka cha uvunguni........ Kazi ipo.
 
Nadhani kila mahali kuna kaubaguzi, ndio maana sijaona shwahili kule jamatini ambako kuswali ni asilimia 25% tu ya shughuli zinazofanyika huko ikiwa ni pamoja nani apewe mchango wa biashara. Na ukifanya utafiti utagundua kuwa hata marekani kuna maeneo yaliyotengwa kwa wamarekani tu. Tusiyaogope sana hayo.
 
Huko Nyuma, Mzee Iddi Simba alikuja na hoja kuwa kama kweli Tanzania inataka ipige hatua kubwa ya maendeleo hatuna budi kuja na sera za kujali wazawa(weusi...). CCM ilikataa maneno hayo kitu kilichochangia kuanguka kwa mzee Simba kwenye medazi za kisiasa. Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na makala ya kiingereza iliyoandika na Adam Lusekelo wa Daily News kuhusu kuwapa nguvu watu weusi!! Makala yenyewe hii hapa:

_____________________________________________________________
HEARD our prez, Jack Mrisho, say that given the empowerment, Tanzanians are quite good at doing business and making their bones in life.

I agree. But I would have liked the prez to add what would have touched the other word which Tanzanian political establishment have shied away from - B - word. Black Tanzanians. Black empowerment!

Because we have seen the much-played around word of people of Bongo. Tanzanians. It seems that some Tanzanians are more equal than other Tanzanians and that is based on colour.

It is just like in the colonial times. White Tanzanians come tops in everything, finances and opportunities. They come even tops in meeting the big potatoes. Which is understandable, bearing the latent inferiority complex of most of our leaders.

Then come in Tanzanians of Indian descent. They have been holding most of the money. Some people, including some leaders, want some of the dosh to go to build silly looking mansions (call them pyramids) somewhere. Presumably they will be buried in the mansions.

Then comes in the scandalous poverty amongst the black Tanzanians. If the prez meant empowerment, he should then talk about Black Tanzanian empowerment.

In Sausi, they talk openly about Black empowerment in a country where the mass of the population has been brutalised and raped over decades. Why shouldn't we?

In Mchuchuma I hear funny names. In all the mines I hear funny names, never heard before in my life. When the figures of income derived from the mines are read out it's from wa-zungu Tanzanians. Can't Black Tanzanians read? Should the so-called investors be white or, as the press put it, Tanzanians of Asian origin only?

Because, really, this is insulting to us, Blacks. I once heard a remark by some clownish minister (he still is a minister. Sad) that Black Tanzanians were not trained to do business.

Some ministry of education idlers even removed subjects like commerce from the curricula.

You simply wonder if those guys had something from their necks upwards. In history, we learnt that many Mediterannean countries had what they called city-states. They were powerful and lived on commerce. Look at Zanzibar when the rule of Seyyid Said Bin Sultan started. But he empowered fellow Arabs.

The politicians have been pooh-pooing what Mzee Iddi Simba has been saying about 'Uzawa'. He was simply talking about Black empowerment. He is not wrong. We want to see Black Tanzanian businessmen and women. We want them being millionaires. Privatising should not be 'whitening' of public corporations in Bongo!

* * *

Mawazo yangu kwanza baada ya kusoma makala hiyo ni kuwa huyo Lusekelo aachie ngazi, hawezi kusema maneno aliyoyasema hapo juu bila ya kuonekana mbaguzi!! Sijui kama kuna ulazima wa sera ya namna hii, na ni jinsi gani sera kama hii inaweza kutekelezwa bila kuleta athari za ubaguzi!! Hata hivyo bado najaribu kufikiri kwa kufuata mfano wa Afrika ya Kusini na Marekani!!!

tatizo langu siwezi ku download kijaruda cha cheche natumia dobe six
 
Nafikiri hapa watu wanachanganya mambo.
Tuseme sehemu zenye machimbo Tarime. Watu wanahamishwa na serikali kwa nguvu au kupewa PESA ili wahame kupisha uchmbaji wa dhahabu. Serikali yetu (hapa ndiyo inalalamikiwa kuwa haiendelezi Weusi) inatoa mfano wa ovyo kabisa. Wao kama Wasomi inatakiwa watoe mfano na kuwafundisha watu biashara. Kwangu mie ilitakiwa kufanya hivi kwamba, serikali kuwasaidia Wananchi kuingia mkataba na Wachimbaji. Wanahakikisha mikataba na Wachimbaji inafanyika na yenye faida kwa wananchi. Hayo maeneo yanabaki bado ya wenyeji, wageni wanayakodisha kwa hela nzuri tu. Serikali inakuwa inakusanya kodi tu na hizo pesa nyingine sijui wanaziitaje. Serikali kwa kufahamu UJINGA wa Weusi wengi, inaweka SHERIA kali kuwa Mgeni hawezi kununua ardhi. Sasa tuseme Barick akija na kusema kanunua hilo eneo, serikali iseme NO. Mwisho wa siku, wakulima hao wataanza kupata mwanga jinsi MAMBO yanavyokwenda. Watajua kuwa kumbe usiingie kichwa kichwa.
Kuna zile film za GOD MUST BE CRAZY. Yule Mzee nasikia film ya kwanza walivyomlipa pesa basi akaangalia yale makaratasi na akayutupa. Film ya tatu akawa kajua dola ni nini na akadai alipwe zaidi. Cha muhimu kwa watu hawa ni kwamba, wengi inabidi kuwafundisha nini maana ya kuwa na pesa kubwa. Kule kwetu walikuwa wakipata pesa za tumbaku, wanapata kichaa. Ukiwafundisha na kuanza kuwapata mwanga nini cha kufanyia hizo pesa, Duniani hakuna mtu mjinga.
Kwa kumalizia niseme kwamba, inaposemwa KUMSAIDIA MTANZANIA MWEUSI, sidhani ina maana ya kumpendelea tu. Kumuwezesha KIFIKRA hilo ndilo linatakiwa kwanza. Hawa watu wakiandaliwa na kupewa mwanga, watakuwa wazuri tu. Tatizo hata viongozi wetu hili hawalijui. Hata kama wakilijua bado wanalifanya bila MAANDALIZI. Hela za Kikwete si zimeliwa tu na wajanja? Hata kama zisingeliwa, huko kijijini, mjomba akizipata tu anaongeza mke wa pili.
Ukisikiliza history za Wayahudi, hawa kwa kutumia ma RABIN, huandaa watu wao mapema sana kibiashara. Wana nyimbo, funy story, misemo nk mingi tu inayomfumbua macho Myahudi katika dunia hii. Je Mtanzana anaambiwa nini? KWenye Dini ndiyo tunapotezwa kabisa. Methali zetu ndiyo hizo, Haraka haraka haina...., kawia ufike, mtaka cha uvunguni........ Kazi ipo.
Sikonge ninakubaliana na wewe, KUWAWEZESHA SI KUWAPENDELEA. Nakumbuka mwaka 2000 nilikuwa nchi fulani na hali ya uchumi ilikuwa inayumba. Serikali ya nchi ile ikaona kuna haja ya "kustimulate" uchumi lakini wafanye nini??? Ikaonekana ili mzunguko wa pesa uanze tena kwa kasi ni lazima ku"inject pesa za kuwafanya wananchi wanunue bidhaa, ili zikiisha wenye kuzalisha bidhaa hizo watatengeneza nyingine, lakini inahitaji watu kuajiri watu kuzalisha!!!!!!!!!!!
Hizi ni baadhi tu ya mbinu.
Nakumbuka mwaka 1995 nilikwenda musoma nikakuta MUTEX imefungwa. Mtaalamu mmoja akaniambia hali imekuwa mbaya sana toka kiwanda kile kufungwa, nikasema mbona ni kiwanda kimoja tu, akasema kile kiwanda kilikuwa kikilipa mishahara karibu shs million 18 kwa kukifunga maana yake millioni hizo ziliondoka kwenye mzunguko wa pesa Musoma, hivyo wauza samaki, watengeneza baisikeli, wapika vitumbua barabarani, wauza dawa, wauza 'gongo' (unajua wote wanafaidi) n.k. walipungukiwa wateja kwa hiyo nao uwezo wao wa kununua ulipungua............................
Sasa iko namna ya kuwawezesha baadhi ya wazawa ili kuwainua. Labda tusidhani wote kumi watakao wezeshwa basi wote watafanikiwa la hasha labda wanne tu, lakini bora kuliko kukosa kabisa.
 
Nafikiri hapa watu wanachanganya mambo.
Tuseme sehemu zenye machimbo Tarime. Watu wanahamishwa na serikali kwa nguvu au kupewa PESA ili wahame kupisha uchmbaji wa dhahabu. Serikali yetu (hapa ndiyo inalalamikiwa kuwa haiendelezi Weusi) inatoa mfano wa ovyo kabisa. Wao kama Wasomi inatakiwa watoe mfano na kuwafundisha watu biashara. Kwangu mie ilitakiwa kufanya hivi kwamba, serikali kuwasaidia Wananchi kuingia mkataba na Wachimbaji. Wanahakikisha mikataba na Wachimbaji inafanyika na yenye faida kwa wananchi. Hayo maeneo yanabaki bado ya wenyeji, wageni wanayakodisha kwa hela nzuri tu. Serikali inakuwa inakusanya kodi tu na hizo pesa nyingine sijui wanaziitaje. Serikali kwa kufahamu UJINGA wa Weusi wengi, inaweka SHERIA kali kuwa Mgeni hawezi kununua ardhi. Sasa tuseme Barick akija na kusema kanunua hilo eneo, serikali iseme NO. Mwisho wa siku, wakulima hao wataanza kupata mwanga jinsi MAMBO yanavyokwenda. Watajua kuwa kumbe usiingie kichwa kichwa.
Kuna zile film za GOD MUST BE CRAZY. Yule Mzee nasikia film ya kwanza walivyomlipa pesa basi akaangalia yale makaratasi na akayutupa. Film ya tatu akawa kajua dola ni nini na akadai alipwe zaidi. Cha muhimu kwa watu hawa ni kwamba, wengi inabidi kuwafundisha nini maana ya kuwa na pesa kubwa. Kule kwetu walikuwa wakipata pesa za tumbaku, wanapata kichaa. Ukiwafundisha na kuanza kuwapata mwanga nini cha kufanyia hizo pesa, Duniani hakuna mtu mjinga.
Kwa kumalizia niseme kwamba, inaposemwa KUMSAIDIA MTANZANIA MWEUSI, sidhani ina maana ya kumpendelea tu. Kumuwezesha KIFIKRA hilo ndilo linatakiwa kwanza. Hawa watu wakiandaliwa na kupewa mwanga, watakuwa wazuri tu. Tatizo hata viongozi wetu hili hawalijui. Hata kama wakilijua bado wanalifanya bila MAANDALIZI. Hela za Kikwete si zimeliwa tu na wajanja? Hata kama zisingeliwa, huko kijijini, mjomba akizipata tu anaongeza mke wa pili.
Ukisikiliza history za Wayahudi, hawa kwa kutumia ma RABIN, huandaa watu wao mapema sana kibiashara. Wana nyimbo, funy story, misemo nk mingi tu inayomfumbua macho Myahudi katika dunia hii. Je Mtanzana anaambiwa nini? KWenye Dini ndiyo tunapotezwa kabisa. Methali zetu ndiyo hizo, Haraka haraka haina...., kawia ufike, mtaka cha uvunguni........ Kazi ipo.

Heshima yako Sikonge,
tatizo kubwa miongoni mwetu ni kuchanganya mambo ama kutaka kupotosha ukweli wa mambo.Kama ulivyosema na wengine wamegusia, kinachotakiwa ni kuwawezesha WATANZANIA WEUSI. Ukweli ni kuwa watanzania weusi ndio wengi walio katika lindi la umaskini na ndio wanahitaji kuwezeshwa. Na kugeuza uwezeshwaji kuwa ni ubaguzi ni upotoshaji wa hali ya juu. Hivi kama sisi hatuwezi kujimudu tukiwa nchini kwetu, ni nani atakayetuwezesha kunyanyuka???Kwa sababu kila siku wanaingia nchini wageni kila sekta wamejaa wao tu.Na wanafanikiwa kwa sababu viongozi wa serikali na sekta zinazotakiwa kulinda maslahi yetu wazawa na nchi yetu ndio wamekuwa wakiwaachia wageni wafanye wanachotaka.Hawa wageni wakija nchini wanababaikiwa kuanzia TIC, UHAMIAJI, WIZARA YA KAZI,na kila ofisi wanayoingia wanasujudiwa kama miungo kwa sababu tu wao ni colored.
Jamani au mmesahau maneno ya hawa waporaji wanavyotamba??mara hii tumesahau maneno ya Nolan(rip) aliyetaka kuanzisha ufugaji wa kamba delta ya rufiji???Ukweli ni kwamba kuwawezesha wazawa weusi sio ubaguzi hata kidogo, kwani kama ni ubaguzi basi weusi wamebaguliwa sana tena kwa muda mrefu, na ni wakati muafaka kuwawezesha ili wanufaike na uhuru wa nchi yao.
sasahivi ukienda kariakoo utafikiri uko Beijing!!!wachina wanauza hadi karanga na cha kuchekesha zaidi mgambo wa jiji hawathubutu kuwakamata.Ngoja wakuone mmatumbi uone wanavyomparamia.
Namalizia kusema kuwa ni wakati muafaka kuwawezesha watanzania wazawa weusi.Na siwezi kuwa mbaguzi kwa jambo hili kwa kuwa wale wenzetu waliofanikiwa hatuhitaji kuwanyang'anya kile walichonacho, bali tunachohitaji ni kuwawezesha wazawa.
 
Kuna member hapo nyuma kazungumza kitu makini sana ambacho kusema kweli kimenigusa sana...
Hii habari ya kuwahamisha wananchi maeneo ya madini na kuwapa fidia ya eneo jingine ambalo kwanza halilingani na shamba la mkulima huyo ni adhabu ya maisha. Wasukuma wengui miji yao ni pamoja na sdshamba lake sasa unapomhamisha ili kupisha uchumbaji wa dhahabu ukasahau kwamba huyo msukuma ajira yake ni kilimo inakuwa kana kwamba umemsahau mzawa..
Ombi la Kumwezesha mzawa ni pamoja na kutazama vitu kama hivi, macho ya viongozi wetu yanatazama tu pato la dhahabu ambayo itaajiri asilimi 1 ya wakazi wa eneo hilo kisha unawaacha watafute maisha mapya ktk eneo dogo lililojengwa vibanda utafikiria mabweni ya shule...mtu huyu hana tena shamba la kulima ama eneo tosha la kufuga mifugo yake...Uzawa iwe kwa tafsiri yoyote ile, ni muhimu kwa wananchi na nakubaliana na mwalimu Augustine kuwa ardhi ndio urithi mkubwa wa Uhuru wetu na tunapofikia kuuza ardhi hizo basi ni sawa kabisa na kuuza Uhuru wetu....

FMES,
mashirika yote ya magari marekani yameingia Ubia na mashirika ya Ulaya kwa sababu yalikuwa yakianguka kiuchumi kama vile mashrika ya ndege, hivyo yalikuwa yakitafuta nguvu mpya kuweza kushindana ktk dunia hii sio swala la kusema ati ni Utandawazi..They were going down na kwa bahati mbaya bado yanakwenda chini pamoja na kuungana huko.. Tatizo bado lipo palepale na I bet my money within few years hao Ford watakuwa juu ya mawe..ama watahitaji msaada toka serikalini...

Nje ya yote haya mkuu wangu hizi ni nchi zilizoendelea tayari, zimejengwa na immingrants kama wanavyodai lakini tukumbuke tu wanapotumia neno immigrant ni ukweli kwamba wamezipora nchi hizi toka kwa wazawa..Ni sawa na South ilivyojengwa na wakoloni..
Kisha hakuna mfano ama historia yoyote duniani hapa inayoonyesha immigrants wameweza kuiendeleza nchi bila uwezo mkubwa wa kuipora isipokuwa nchi ambazo bado zinawawezesha raia wake kuweza kushindana na nguvu ya wahamiaji toka nje na mfanoi mzuri ni nchi za Ulaya.. Usipomwezesha mzawa kuna kila uwezekano mgeni kuipora nchi hiyo na mzawa kushuka chini na kuwa second class citizen. Ni hulka ya binadamu na mifano kibao ya tawala zilizotangulia imetuonyesha hivyo. Kwa hiyo tusijaribu kukimbia Ukweli ambao ni dhahiri, hata kama sisi tuna moyo wa kufikiria kwamba binadamu wote ni sawa basi kumbuka upande wa pili hawafikirii hivyo!...
 
Wahindi wanataka kuingiza hiyo Caste yao hapa Tanzania ndio maana wakatumiwa kwenye EPA na Richmond.Angalia bif ya Mengi na Manji/Rostam,lengo ni kuhamisha umiliki wa uchumi wa Nchi kwa wageni na kibaya zaidi wamewakuta viongozi wenye tamaa ya mali ya ajabu.Wahindi wanahamisha nje faida ya biashara zao,wamewafundisha viongozi nao wanaweka fedha zao nje.Watanzania tusikubali uhujumu huu wa uchumi wa nchi yetu Tanzania.
 
Tatizo linakuja tunapotumia neno mzawa kumaanisha mweusi. Si weusi wote wanaohitaji kuwezeshwa kama vile si watanzania wote wasio na rangi nyeusi wenye uwezo. Kwa nini tunang'ang'ania neno mzawa badala ya mtanzania kama hatumaanishi rangi? Ukweli ni kuwa wengi wetu ni wabaguzi ingawa hatutaki tuonekane hivyo!

Amandla.....

Sasa akina rangi mbili kama sisi ambao tuna damu za wajomba weusi na zile za wakuja tunawekwa kwenye kundi lipi? Mimi ni mweupe kama Salim Ahmed Salim lakini kuanzia mama na wandugu wengine kibao ni weusi.Kuhusu hali yangu ya maisha imekuwa ya kubangaiza na nimekuwa na struggle sana lakini mambo hayajanyooka.Katika mapambano ya kutaka kuinuka kiuchumi walio karibu nami ndiyo hao hao wajomba zangu.

Je tatizo la umaskini wangu limekuja sababu nimezaliwa ma mama mweusi au nini?Na hata baba yangu ambaye alikuwa mweupe alikufa akiwa hoi maskini wa kutupwa.Wenye kukazania sera ya uzawa kwa maana ya mtu mweusi wanaweza kuniweka kwenye kundi lao?
 
Je tatizo la umaskini wangu limekuja sababu nimezaliwa ma mama mweusi au nini?Na hata baba yangu ambaye alikuwa mweupe alikufa akiwa hoi maskini wa kutupwa.Wenye kukazania sera ya uzawa kwa maana ya mtu mweusi wanaweza kuniweka kwenye kundi lao?​

Inawezekana hujasoma au hujui kuchakalika.....
 
[/INDENT] Inawezekana hujasoma au hujui kuchakalika.....

Nyani,
Unafahamu kuwa kuna wahindi kibao wamejazana bongo ilihali hawana shule kabisa???ukipita kwenye viwanda vya wahindi bongo maana ndio wengi wenye viwanda, nenda migodini na kwenye makampuni mengi tu unakuta watu wameajiriwa kwa sababu mwenye mali ni mhindi mwenzake, kaburu mwenzake au mzungu mwenzake.
Tembea kwenye viwanda vya sukari uone kama wale makaburu waliojazana pale wamesoma, tembelea meli za uvuvi bahari ya hindi uone kama wale wahindi na wafilipino kama wamesoma, nenda migodini uone kama wale askari wa kinepali(nepalese) kama wamesoma kama unavyodai.Ukweli ni kuwa hawa wenzetu wanawezeshana, huku wabongo wakigeuka watumwa ndani ya nchi yao.Waulize watanzania waliojaribu kuwekeza nyumbani vikwazo walivyokumbana navyo, manake usije ukadhani wabongo-wazawa hawajui kuchakarika.
ndio maana tunasema ni muhimu mno kuwawezesha wazawa ili wafaidike na rasilimali za nchi yao.
kama kila siku watu wanahamishwa kutoka kwenye maeneo yao yanayowapatia rizki kwa kisingizio cha kupisha wawekezaji, mona huo uwekezaji wa wageni hususani migodi haina tija yeyote kwa serikali na kwa wananchi, fedha yote wanapeleka kwao, wasukuma, wakurya na wamasai wamebaki kutaabika tu huku wakwapuaji wakizidi kufaidi rasilimali madini za watanzania.
 
Kusoma kwa kiwango kipi ndiko kunakoleta nafuu ya maisha?Kuchakalika nachalika vibaya..si mchezo!

Kwa Tanzania ili kuweza kupata kazi ya maana ukiwa na elimu angalau ya digrii ya kwanza unaweza kuwa na hali nzuri kuliko kama ungekuwa na elimu ya sekondari tu. Kwa nchi kama Marekani haijalishi sana una elimu gani. Kuna watu walioishia high school tu ambao wanatengeneza hela nyingi kuliko waliosoma na wenye madigrii. Hii yote ni kwa sababu wao wenzetu dhana ya fursa sawa kwa wote wameitilia maanani na wanafanya kila wawezalo kuiweka dhana hiyo katika matendo..

Sasa sijui wewe una elimu ya kiwango gani. Ila endelea tu kuchakalika mjomba maana ukikata tamaa, kwa hali ya uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, utakuwa fukara bure.
 
Sasa akina rangi mbili kama sisi ambao tuna damu za wajomba weusi na zile za wakuja tunawekwa kwenye kundi lipi? Mimi ni mweupe kama Salim Ahmed Salim lakini kuanzia mama na wandugu wengine kibao ni weusi.Kuhusu hali yangu ya maisha imekuwa ya kubangaiza na nimekuwa na struggle sana lakini mambo hayajanyooka.Katika mapambano ya kutaka kuinuka kiuchumi walio karibu nami ndiyo hao hao wajomba zangu.

Je tatizo la umaskini wangu limekuja sababu nimezaliwa ma mama mweusi au nini?Na hata baba yangu ambaye alikuwa mweupe alikufa akiwa hoi maskini wa kutupwa.Wenye kukazania sera ya uzawa kwa maana ya mtu mweusi wanaweza kuniweka kwenye kundi lao?

Haswa, Mkuu Alnadaby. Kwa mtazamo wa wengi humu ndani, wewe utawekwa kwenye kundi la watu weupe kwa hiyo hauna mgao. Umeishapendelewa kwa rangi bsi inatosha.

Kuwezeshwa kunakozungumziwa humu ni kupewa upendeleo hata pale mtu asipo/qualify.

Wengi wanachosahau ni kuwa upendeleo huo umekuwa ukifanywa toka nchi yetu ipate uhuru. Kwa mfano, tulipopata uhuru tulianzisha National Housing ijenge nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wale wenye kipato kidogo. Na wale wasio na uwezo wapangishwe kwa bei nafuu.Wote tunajua nyumba hizi ziliishia wapi. Wale waliombiwa wanunue hawakufanya hivyo bali waliendelea kupanga kwa pango hiyo nafuu ambayo wengi hata kulipa walikuwa hawalipi. Serikali ilipoamua kuwapa nafasi ya kuzinunua tena, wengi wa hao wazawa waligeuka na kuwauzia wenye nazo.

Tulikuwa na Benki ya Nyumba ambayo lengo lake lilikuwa kuwapatia mikopo nafuu wananchi ili wajijengee nyumba. Wengi walichukua mikopo hiyo na badala ya kujenga, waliongeza wake, walinunua chenja (rekodi pleya), baiskeli na bling bling nyingine za enzi zile. Matokeo yake shirika lilikufa likiwadai.

Tulipopata uhuru tulinyang'anya shule zote zilizokuwa zinaendeshwa kwa misingi ya dini au rangi. Watanzania wote wakapewa haki sawa katika elimu. Sehemu zilizoonekana ziko nyuma zikawa zinapewa upendeleo. Matokeo yake ni hao waliokuwa wakipewa upendeleo waligeuka na kuwauzia nafasi zao za masomo watu kutuka makabila yaliyoonekana yana maendeleo. Wakati wetu ilikuwa si ajabu kukutana na wachaga wenye majina ya kabila nyingine. Matokeo yake, shule tumeshindwa kuziendesha na leo wenye nazo hawataki watoto wao wasome nchini.

Tulipopata uhuru, tulianzisha vijiji vya ujamaa. Mashamba ya wale tuliowaita makabaila mara nyingi yalinyang'anywa na kupewa wanakijiji. Wote tunajua matokeo yake.

Tulipopata uhuru, ndugu zetu wa nchi za scandinavia wakawekeza kwenye shule na vyuo vilivyolenga kumuinua mtanzania maskini. Shule kama Kibaha zililenga kwenye kilimo na ufugaji. Chuo cha Mbegani, Bagamoyo kwa uvuvi. Leo Mbegani zinapanga klabu za mpira.

Tulipopata uhuru, tulibinafsisha mabenki na kuyaweka mikononi mwetu. Tukaanzisha benki ya ushirika ili itoe mikopo nafuu kwa wananchi. Wote tunajua tulifanyia nini mikopo hiyo.

Tulianzisha viwanda sehemu mbalimbali ( Tabora Spinning, Mutex, Tanga Steel, Tancut, Morogoro Ceramics, Mbagala Glass, Kiltex, Ufi, n.k. n.k.) ili zitoe ajira kwa watanzania. Wote tunajua tulivifanya nini hivyo viwanda. Vingine tumeiba hadi bati.

Tuliwaruhusu wachimbaji wadogo wadogo. Wote tunajua Mererani palikuwa ni sehemu ya namna gani. Ujambazi na uchafu wa kila aina ulipatikana pale. Na tunajua hao wachimbaji wadogo walipozipata pesa walifanya nini? Ni wachache sana waliowekeza kwenye biashara iliyoweza kuwatoa katika umasikini. Pesa walipata, walitapanya na baada ya siki chache walirudi kwenye umaskini wao. Sehemu nyingine ni hao hao wanaomwaga Mercury kwenye mito yetu na hivyo kuua samaki wao. Ni hao hao wanaowinda viungo vya albino ili wapate utajiri wa chap chap.

Leo hii, miaka 47 baada ya kupata uhuru wetu, miaka zaidi ya 40 ya kushika sehemu muhimu zote za uchumi, hatuoni aibu kweli kudai kuwa tunahitaji upendeleo? Kwa sababu ya rangi yetu!

Mimi naamini wakati umefika wa kujiangalia wenyewe na kujikosoa. Tudai, level playing ground, ambayo haitaangalia kama huyu ni Patel au Mengi. Wote wapewe haki sawa na atakayekiuka taratibu achukuliwe hatua bila kujali rangi yake. Tukifanya hivyo, wakina Alnadaby hawata kuwa na sababu ya kujiuliza yeye ni nani maana atajua atapimwa kwa utanzania wake na si rangi ya mzazi wake!

Hii sera ya uzawa ndiyo iliyotufikisha mahali ambapo wakina Moshi wanaambiwa hawana nafasi pwani maana hawajui kula chapati. Hii ni pamoja na kwamba wamenunua na kuwekeza katika sehemu hizo.

Hapana, hii sera ya uzawa ni ya kibaguzi na hata siku moja haitatuondoa kwenye umaskini wetu!

Amandla........
 
Wajameni

Kutomiliki biashara kwa wazawa tanzania kunasababishwa na sababu zifuatazo.

1)Kukosa mwamko wa kibiashara kwa vijana wa kizawa.

Nenda chuo kikuu sasa hivi na uwaulize vijana wakigraduate wanataka kufanya nini.Asilimia kubwa watakuambia wanataka kufanya kazi kwenye hizi ngos ni wachache sana watakuambia wanataka kuanzisha biashara au viwanda vidogovidogo.Culture ya misaada imeshatudumaza.

2)Ujinga na wizi wa viongozi wetu.

Akija kijana mzawa mchapakazi akampa business plan waziri kama Karamagi bila kutoa ruswha atapewa vikwazo mia moja.Lakini akija mzungu na hongo yake ingawa plan yake sio nzuri kama ya mzawa atapewa tu kwa kuwa yuko tiyari kutoa kidogo.Ninayo mifano kadhaa hasa enzi za waziri mramba(alipokuwa waziri wa viwanda vidogovidogo) -watu wengi walinyimwa vibali vya kuanzisha viwanda bila sababu yoyote baadae kushitukia plan zao zimechukuliwa na mwanatribesman wa mramba.

Zaidi,Viongozi wetu wanaimiza sana misaada badala ya kusaidia kuendeleza ideas za wazawa, kama viwanda sayansi na teknologia.

Kwahiyo lawama ni sisi wenyewe hasa viongozi tuliowachagua ambao wako tiyari kutuuza kwa masilahi yao wenyewe.
 
Last edited:
Back
Top Bottom