Sera ya kilimo kwa Serikali hii ni ipi?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF,

Ningependa kujua sera ya kilimo ya serikali hii ya Magufuli kama ipo?

Leo sijui mtalionaje hili wazo..au kama lishawahi kufanywa before?!

..ila ningependekeza serikali kuwa na Supermarkets zake:rolleyes::rolleyes:
😂😂😂

Watu wanunue na kuuza huko.

Iwe cheap compared na supermarket private.

Itawavuta wazalendo!

Kiasi fulani cha product yoyote inayouzwa na hizi supermarket, kiende kwenye Research

Kuwe na special Research commitee.

Kwa ajili ya ku identify masoko BOTH ndani ya nchi na nje.

Vipi???Nimezingua?
 
Hello JF,

Ningependa kujua sera ya kilimo ya serikali hii ya Magufuli kama ipo?

Leo sijui mtalionaje hili wazo..au kama lishawahi kufanywa before?!

..ila ningependekeza serikali kuwa na Supermarkets zake:rolleyes::rolleyes:

Watu wanunue na kuuza huko...

Iwe cheap compared na supermarket private...

Itawavuta wazalendo!!,

Kiasi fulani cha product yoyote inayouzwa na hizi supermarket, kiende kwenye Research

Kuwe na special Research commitee..

Kwa ajili ya ku identify masoko BOTH ndani ya nchi na nje..

Vipi???Nimezingua?
Jiamini dada.
 
Supermarket za serikali? Ndugu labda hauwajui vizuri watumishi wa umma.

Angalia huduma unayopata unapoenda kwenye ofisi za serikali basi ndio hiyohiyo utaipata huko supermarket.

Alafu biashara ikiwa mbaya kwa sababu ya huduma zao mbovu watakacho kifanya ni kuzifungia supermarket binafsi zote ili wabakie na monopoly kwenye soko.
 
sera ya kilimo au sera za kilimo zaweza kuwa kwenye makaratasi lakini kwenye utekelezaji bado kabisa, kilimo kina hitaji mabadiliko makubwa sana yapaswa tuwe na kilimo cha kisasa tuanze kwa kumtoa mkulima kwenye jembe la mkoni na kumuwezesha kumiliki trekta au kulima kwa trekta sambamba na kuweka mifumo ya umwagiliaji na upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa bei rafiki
tukishaweza kuzalisha mazao ya kutosha kitacho fata ni ni kuweka mifumo mizuri ya kuhifadhi ikiwa ni pamoja na kutoa mazao ghafi kuwa bidhaa kamili soko la mmazao sio tatizo endapo tutazalisha kwa wingi na kwa gharama za chini
sula la serikali kufanya biashara siliungi mkono tutaruudi kule kwa kina ugawaji na RTC
 
Serikali ikae mbali na biashara..
 
Serikali ikae mbali na biashara..

Sijui mnalionaje lakini mimi nawaza kama serikali itauza cheap products then private itabidi ipunguze bei na wenyewe..kwa hio advantages ni sisi wananchi ...

halafu nje ya nchi/ export strategically product/brand ikiwa ya serikali ina weigh more credibility than products za mtu mmoja ama kikundi,
 
Umeanza vizuri ila hapo ulipomalizia Mkuu enzi za ugawaji zilikua sio nzuri ila kila mwananchi alipata na kuwa happy...
 
ningependekeza serikali kuwa na Supermarkets zake:rolleyes::rolleyes:
😂😂😂
Kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya kilimo utagindua kuwa wadau wa kilimo hawataki mifumo ya serikali kuingilia trade in agricultural products. Hata humu kuna uzi mpya unaopinga mfumo wa TMX kwenye korosho
 
NFRA mahindi tuu wameshindwa kununu mara utasikia hawana magunia mara pesa Kama saa hizi hawana pesa wamesimamisha ununuzi huko kaskazini na rushwa imetamalaki huko kuchukua pesa kwa wakulima ili wakubaliwe kuuza mazao yao hapo...Mimi sijui wanaweza kufanya nini kwenye kilimo maana wao ndio wanadidimiza wakulima...
 
Sijui mnalionaje lakini mimi nawaza kama serikali itauza cheap products then private itabidi ipunguze bei na wenyewe..kwa hio advantages ni sisi wananchi ...

halafu nje ya nchi/ export strategically product/brand ikiwa ya serikali ina weigh more credibility than products za mtu mmoja ama kikundi,

Wazo lako zuri na inawezekana lakini sio
Serikali ifanye kila kitu
Serikali ianzishe shirika au mashirika Kwa kazi
Hiyo halafu iyamilikishe wananchi Kwa hisa..

Hata CRDB na Nmb na TBL zina hisa za serikali
Na bado sio kampuni za serikali lakini ni kampuni za umma Kwa kupitia hisa..
Serikali inaweza fanya hilo
 
Ni biashara gani serikali imewahi kufanya kwa ufanisi? Au ni shirika lipi la serikali limeendeshwa kwa ubora na kuleta faida?

Wazo lako zuri sana Rebeca 83 najua hii ni katika kuhangaika kupata namna bora ya kuinua kilimo kilete tija.

The Boss amejibu kifupi lakini jibu lake limeshiba "Serikali ikae mbali na biashara"
Yenyewe itengeneze mazingira rafiki na sera rafiki kwa wafanya biashara.

Watu watavutiwa na ubora wa bidhaa lakini sio nembo ya serikali.
 
Sijui mnalionaje lakini mimi nawaza kama serikali itauza cheap products then private itabidi ipunguze bei na wenyewe..kwa hio advantages ni sisi wananchi ...

halafu nje ya nchi/ export strategically product/brand ikiwa ya serikali ina weigh more credibility than products za mtu mmoja ama kikundi,
Mawazo ya kijinga kweli. Unaturudisha kwenye ujima wa awamu ya kwanza!
 
Niambie ubaya wa haya mawazo,?!? na ulikuwepo enzi za ujima kujua haya mawazo yalikuwepo enzi hizo?
Nimekuwepo toka enzi za mkoloni toka mwaka 1948. Awamu ya kwanza ilikuja na na NAFCO na wala bei za vyakula havikuwa rahisi. Kurudi tena kwenye mfumo ulioshindwa Ndiyo ujinga wenyewe
 
Back
Top Bottom