Sera ya kilimo kwa Serikali hii ni ipi?

Sera ya kilimo kwa Serikali hii ni ipi?

Sijui mnalionaje lakini mimi nawaza kama serikali itauza cheap products then private itabidi ipunguze bei na wenyewe..kwa hio advantages ni sisi wananchi ...

halafu nje ya nchi/ export strategically product/brand ikiwa ya serikali ina weigh more credibility than products za mtu mmoja ama kikundi,
Cheap price haiji kwa serikali kuuza cheap products, cheap price inatokea endapo supply ikiizidi demand
 
Serikali hii haina habari kabisa na kilimo wala viwanda, kipaumbele chake ni miundombinu
 
Ni biashara gani serikali imewahi kufanya kwa ufanisi? Au ni shirika lipi la serikali limeendeshwa kwa ubora na kuleta faida?

Wazo lako zuri sana Rebeca 83 najua hii ni katika kuhangaika kupata namna bora ya kuinua kilimo kilete tija.

The Boss amejibu kifupi lakini jibu lake limeshiba "Serikali ikae mbali na biashara"
Yenyewe itengeneze mazingira rafiki na sera rafiki kwa wafanya biashara.

Watu watavutiwa na ubora wa bidhaa lakini sio nembo ya serikali.

Asante mkuu.....

Ningependa kujua history,.. ina maana hili wazo la serikali kununua na kuuza bidhaa za watu lishawahi kufanyika before???

Kama jibu ni NO,nini kimepelekea watu/wakulima wa JF 😉 😉 kukataa hii idea ya serikali kuwa involved...??? fear of unknown?? kwa nini serikali ikae mbali na biashara??

Bidhaa za serikali i still think its good idea; wewe leo ukipewa option, ya kununua product kutoka kwa mfanya biashara USA,au Kikundi kinachouza hio product ambacho kipo USA au product hio hio inauzwa na serikali ya USA, be honest utachagua muuzaji gani you put trust on???

Ubora nadhani ni kitu kinachoweza kuangaliwa na serikali...hasa pale inapoona wakivulunda inatu cost wote...

Hata diaspora mkiona papai from Mkuranga Tanzania hamtanunua kweli?????

There is Pride and Uzalendo..moja ya sababu za watu kununua brand fulani...
 
Cheap price haiji kwa serikali kuuza cheap products, cheap price inatokea endapo supply ikiizidi demand

Ohhh my bad!, naomba msingize hii mada kwenye deep uchumi, sielewi hayo mambo mimi...
 
Serikali hii haina habari kabisa na kilimo wala viwanda, kipaumbele chake ni miundombinu

Jiandae na shamba mkuu,Magufuli next term ni Kilimo, keshajenga miundo mbinu, i just predict Kilimo will be his next move,so kale ka shamba usikauze...😉😉
 
Nimekuwepo toka enzi za mkoloni toka mwaka 1948. Awamu ya kwanza ilikuja na na NAFCO na wala bei za vyakula havikuwa rahisi. Kurudi tena kwenye mfumo ulioshindwa Ndiyo ujinga wenyewe

Tatizo lilikua nini kama vyakula havikua rahisi...lazima kutakua kulikua na sababu..
 
Ohhh my bad!, naomba msingize hii mada kwenye deep uchumi, sielewi hayo mambo mimi...
Not deep hii ipo hata ktk maisha ya kawaida angalia kwenye sukari serikali ilitumia regulations zake za price control kwa set minimum price lkn mpaka Leo madukani bei imegoma kushuka na hiyo ni sababu uzalishaji wa sukari nchini upo chini kuliko mahitaji ya sukari nchi nzima
 
Ni biashara gani serikali imewahi kufanya kwa ufanisi? Au ni shirika lipi la serikali limeendeshwa kwa ubora na kuleta faida?

Wazo lako zuri sana Rebeca 83 najua hii ni katika kuhangaika kupata namna bora ya kuinua kilimo kilete tija.

The Boss amejibu kifupi lakini jibu lake limeshiba "Serikali ikae mbali na biashara"
Yenyewe itengeneze mazingira rafiki na sera rafiki kwa wafanya biashara.

Watu watavutiwa na ubora wa bidhaa lakini sio nembo ya serikali.
Biashara pekee ambayo serikali inaweza ikafanya na ikapata faida ni financial business
 
Jiandae na shamba mkuu,Magufuli next term ni Kilimo, keshajenga miundo mbinu i just predict it will be his next move,so kale ka shamba usikauze...😉😉
Mabilioni anayopoteza kujenga uwanja chato angeyatumia kujenga irrigation scheme kama ya Kapunga pale chimala mbeya hakika serikali ingepiga hela ndefu balaa!
 
Serikali isithubutu kabisa kuingilia kufanya biashara ya kilimo bali ifanye mabadiriko katika sera za kilimo.

Sera hizo zielekeze serikali kupanga bajeti kubwa katika sekta ya kilimo kwa ajili ya kutafuta masoko.

Tuanze ndani tu kwanza kuna unequal distribution of agricultural produce, unakuta mahindi upande fulani wa nchi bei ndogo na kwingine kubwa. Soko la nje ndilo usiseme, lipo wakati wote, ni wajibu tu wa viongozi wa serikali husika kufanya mazungumzo ya kibiashara. Kwa ufupi tu, soko ndio mchawi mkubwa wa kilimo nchini achana na mitaji, machines, pembejeo n. k. Wakulima wenye mitaji wapo ila wamefirisika kwa kushindwa kupata soko zuri.

Mabadiriko ya ki-sera pia yalazimishe serikali kupanga bajeti ya kuboresha miundombinu ya kilimo. Tuna uhaba wa cold warehouses wakati huohuo tuna tuna soko lililo tayari la kitunguu kwa nchi za Zambia, DRC, Kenya, Uganda na Sudan kusini. Shida ni kuwa kuna wakati masoko haya huwa yanafurika kwa kitunguu na kuna wakati yanakuwa tupu, hapa ndipo cold facilities zinapokuja kufanya kazi ili kuimarisha bei angalau kwa 100,000 kwa gunia mwaka mzima bila kushuka. Hizi chanja za kienyeji kuhifadhi kwa muda mrefu ni changamoto. Wakulima walipie wanapohifadhi kwa gunia na serikali ifaidike, chanzo cha mapato.

Bajeti nyingine ielekezwe kwenye miundombinu ya kisasa mikubwa ya umwagiliaji. Yale maji ya ziwa Tanganyika mfano yanaweza kufanya mikoa ya Rukwa, Dodoma, Tabora, Singida izalishe mara kumi zaidi ya mikoa ya nyanda za juu kusini ya mvua nyingi kwa mwaka mzima. Watumwe watu waende mfano Australia wakajifunze kuhusu murrambidge irrigation project n. k na sehemu nyingine zilizoendelea duniani kwa kilimo.

Nina mengi sana ya kuandika labda niandae uzi maalumu siku moja. Kilimo kina pesa endapo kitachukuliwa serious, Australia kwa mfano inaingiza wastani wa usd bilioni 62 kupitia kilimo, USA wastani wa usd 200+ bilioni kwa mwaka. Wakati huohuo benki ya dunia inakadiria kuwa thamani ya kilimo na shughuli za uzalishaji wa bidhaa za kilimo barani afrika itafikia dola trilioni 2 za kimarekani mwaka 2030 kutoka usd 400 bilioni kwa sasa. Kwa hio utaona ni jinsi gani soko la afrika tu lilivyo endapo tutajipanga vyema.
 
Hili hata mkuu Red Giant alishawahi kulisema,sijui akipewa next term atafanya nini, ila i wish angekua anasoma na kutelekeza ushauri anaopewa humu.
 
Mkuu nakwambia hivi wizara ya kilimo kama itaweza kujenga project za mfano wa kapunga irrigation kila mkoa baada ya miaka kumi wizara inaanza kujiendesha bila kutegemea hata senti moja kutoka bajeti ya serikali, pale kapunga mkaburu anapiga hela ya maana bila jasho kwa kukodisha mashamba tu,
 
Serikali isithubutu kabisa kuingilia kufanya biashara ya kilimo bali ifanye mabadiriko katika sera za kilimo.

Sera hizo zielekeze serikali kupanga bajeti kubwa katika sekta ya kilimo kwa ajili ya kutafuta masoko.

Tuanze ndani tu kwanza kuna unequal distribution of agricultural produce, unakuta mahindi upande fulani wa nchi bei ndogo na kwingine kubwa. Soko la nje ndilo usiseme, lipo wakati wote, ni wajibu tu wa viongozi wa serikali husika kufanya mazungumzo ya kibiashara. Kwa ufupi tu, soko ndio mchawi mkubwa wa kilimo nchini achana na mitaji, machines, pembejeo n. k. Wakulima wenye mitaji wapo ila wamefirisika kwa kushindwa kupata soko zuri.

Mabadiriko ya ki-sera pia yalazimishe serikali kupanga bajeti ya kuboresha miundombinu ya kilimo. Tuna uhaba wa cold warehouses wakati huohuo tuna tuna soko lililo tayari la kitunguu kwa nchi za Zambia, DRC, Kenya, Uganda na Sudan kusini. Shida ni kuwa kuna wakati masoko haya huwa yanafurika kwa kitunguu na kuna wakati yanakuwa tupu, hapa ndipo cold facilities zinapokuja kufanya kazi ili kuimarisha bei angalau kwa 100,000 kwa gunia mwaka mzima bila kushuka. Hizi chanja za kienyeji kuhifadhi kwa muda mrefu ni changamoto. Wakulima walipie wanapohifadhi kwa gunia na serikali ifaidike, chanzo cha mapato.

Bajeti nyingine ielekezwe kwenye miundombinu ya kisasa mikubwa ya umwagiliaji. Yale maji ya ziwa Tanganyika mfano yanaweza kufanya mikoa ya Rukwa, Dodoma, Tabora, Singida izalishe mara kumi zaidi ya mikoa ya nyanda za juu kusini ya mvua nyingi kwa mwaka mzima. Watumwe watu waende mfano Australia wakajifunze kuhusu murrambidge irrigation project n. k na sehemu nyingine zilizoendelea duniani kwa kilimo.

Nina mengi sana ya kuandika labda niandae uzi maalumu siku moja. Kilimo kina pesa endapo kitachukuliwa serious, Australia kwa mfano inaingiza wastani wa usd bilioni 62 kupitia kilimo, USA wastani wa usd 200+ bilioni kwa mwaka. Wakati huohuo benki ya dunia inakadiria kuwa thamani ya kilimo na shughuli za uzalishaji wa bidhaa za kilimo barani afrika itafikia dola trilioni 2 za kimarekani mwaka 2030 kutoka usd 400 bilioni kwa sasa. Kwa hio utaona ni jinsi gani soko la afrika tu lilivyo endapo tutajipanga vyema.

Mkuu mimi sijui sielewi kama tatizo la sasa ni soko,huoni serikali ikianzisha supermarket zake itakua platform nzuri na reliable kwa wakulima kuuza vitu vyao???

Nimependa wazo lako la kuwa na cold facilities kwa ajili ya mazao,hili la muhimu sana,Kingine ninachoweza ku add ni Machines za Kusindika mazao,..mfano nyanya kuna wakati zilizalishwa nyingi sana zikaoza na kuna wakati bei ya nyanya ilikua haishikiki...hizo zilizoachwa mpka zikaharibika zingeweza kusindikwa na kuuzwa kwenye makopo kwa muda mrefu
 
Hello JF,

Ningependa kujua sera ya kilimo ya serikali hii ya Magufuli kama ipo?

Leo sijui mtalionaje hili wazo..au kama lishawahi kufanywa before?!

..ila ningependekeza serikali kuwa na Supermarkets zake🙄🙄

Watu wanunue na kuuza huko.

Iwe cheap compared na supermarket private.

Itawavuta wazalendo!

Kiasi fulani cha product yoyote inayouzwa na hizi supermarket, kiende kwenye Research

Kuwe na special Research commitee.

Kwa ajili ya ku identify masoko BOTH ndani ya nchi na nje.

Vipi???Nimezingua?
Supermarkets za serikali? Hapo umezingua rafiki yangu kipenzi (kidding)
 
Mkuu mimi sijui sielewi kama tatizo la sasa ni soko,huoni serikali ikianzisha supermarket zake itakua platform nzuri na reliable kwa wakulima kuuza vitu vyao???

Nimependa wazo lako la kuwa na cold facilities kwa ajili ya mazao,hili la muhimu sana,Kingine ninachoweza ku add ni Machines za Kusindika mazao,..mfano nyanya kuna wakati zilizalishwa nyingi sana zikaoza na kuna wakati bei ya nyanya ilikua haishikiki...hizo zilizoachwa mpka zikaharibika zingeweza kusindikwa na kuuzwa kwenye makopo kwa muda mrefu
Wazo lako la serikali kuwa na supermarket au maduka ni haliwezekani, litaua vibaya mno sekta binafsi yaani regulator wewe halafu uingie tena sokoni kushindina na sector binafsi magoli yote si utafunga wewe.
 
Sijui mnalionaje lakini mimi nawaza kama serikali itauza cheap products then private itabidi ipunguze bei na wenyewe..kwa hio advantages ni sisi wananchi ...

halafu nje ya nchi/ export strategically product/brand ikiwa ya serikali ina weigh more credibility than products za mtu mmoja ama kikundi,

Serikali itapata wapi hizo products za kuuza?
 
Mkuu mimi sijui sielewi kama tatizo la sasa ni soko,huoni serikali ikianzisha supermarket zake itakua platform nzuri na reliable kwa wakulima kuuza vitu vyao???

Nimependa wazo lako la kuwa na cold facilities kwa ajili ya mazao,hili la muhimu sana,Kingine ninachoweza ku add ni Machines za Kusindika mazao,..mfano nyanya kuna wakati zilizalishwa nyingi sana zikaoza na kuna wakati bei ya nyanya ilikua haishikiki...hizo zilizoachwa mpka zikaharibika zingeweza kusindikwa na kuuzwa kwenye makopo kwa muda mrefu
Kwanza fahamu kuwa watanzania hatuna utaratibu wa kununua bidhaa supermarkets pia supermarkets zinauza bidhaa nyingi si za vyakula tu. Watanzania wengi wanapata bidhaa za vyakula kupitia masoko ya umma ambapo serikali kupitia halmashauri husika inajenga soko, huyu mdau wa kwanza, mdau wa pili ni wafanyabiashara wadogo wauzao bidhaa hapo sokoni ambao hulipia ushuru serikalini.

Hivyo supermarkets za vyakula zitaua masoko ya umma ambayo ni mengi na ajira nyingi zitapotea kwa serikali kuhodhi soko na bidhaa zinazouzwa. Wazo lako halina ufanisi kiuchumi, litaharibu badala ya kutengeneza.

Hiyo aya ya pili ni nzuri. Mwanzoni mwa mwaka huu mimi mwenyewe ingawa nafanya kilimo cha nyanya ila nililazimika kununua nyanya za kwenye pakiti ya plastiki kutoka China, vilikuwa ni vi-gramu kadhaa tu kwa sh 500. Si jambo zuri la kufurahia bidhaa kama nyanya kuagiza kutoka nje.
 
Back
Top Bottom