Sera ya Elimu yataka umri wa elimu lazima kuwa miaka 10

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imeunda timu ya kuanza kupitia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 ambayo miongoni mwa mambo yanayotajwa kwenye sera hiyo ni elimu ya lazima kuwa miaka 10 badala ya saba.

Hatua hiyo itakwenda sambamba na mabadiliko ya mitaala ya elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya walimu.

Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda, aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa dini na wamiliki wa shule binafsi, jijini Dodoma.

Alisema pamoja na kuendelea na mchakato wa kuboresha mitaala, ameona ni vyema kufanya mapitio ya sera ili kwenda sambamba na maboresho hayo na tayari ameshaunda timu ambayo imepewa jukumu la kupitia sera ambayo ni tofauti na ile inayosimamia maboresho ya mitaala.

Pia alisema sera hiyo imebainisha kuwa mtoto wa kitanzania mwenye miaka kati ya minne hadi sita, angalau asome elimu ya awali kwa pamoja na elimu ya msingi kwa miaka 10 ili kumwezesha kujua kusoma, kuandika na kupata ufahamu wa mambo yatakayompa maarifa.

“Baadhi ya maeneo hayajatekelezwa kwenye hii sera, hivyo nimeona tufanye mapitio na kama tuendelee kuutekeleza au kama tubadilishe basi tubadilishe nini. Tunapotekeleza elimu ya lazima basi tutatekelezaje bila kushusha kiwango. Tumeunda timu ya sera itakayoongezwa na profesa wa uchumi pamoja na mambo mengine waje na mapendekezo.

“Kama tunaenda nayo, tunaandika sera upya au tunaboresha katika maeneo yanayofaa au tuondoke kabisa. Pia wataangalia tunahitaji walimu wangapi, fedha kiasi gani, wataalamu wangapi na madarasa mangapi. Hatua hii inalenga kuwaandaa wanafunzi wa kitanzania katika kuakisi mazingira ya Tanzania na kimataifa,” alisema.

Awali, Kamishna wa Elimu, Dk. Lyabwene Mtahabwa alisema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Watanzania kutoa maoni ya kuboresha mitaala na mpaka sasa zaidi ya wadau 100,000 wameshajitokeza kutoa maoni yao.

Alisema katika maeneo ambayo Watanzania wameyatolea maoni ni pamoja na kupendekeza kuondolewa kwa wingi wa maudhui, kufundisha masomo ya ujuzi kulingana na mazingira, kuwapo na mikondo ya kubaini vipaji vya wanafunzi, lugha zote zitumike na kusisitiza kufundisha maadili kuanzia ngazi ya awali.

Dk. Mtahabwa alisema lengo la wizara ni kuhakikisha Januari, 2024 mtaala mpya uanze kutumika kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya walimu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Anneth Komba, alisema mapitio ya mitaala imepita hatua mbalimbali za maboresho na kuwa matarajio ni kuwa rasimu ya kwanza ya mtaala itakuwa tayari ifikapo Mei 30, mwaka huu na wadau wanataka fursa ya kupitia na kuboresha zaidi.

Chanzo: Nipashe
 
Miaka 10 mtoto yuko shule ile ile?
Inachosha sana akili hasa hizi shule zenye changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na viboko kutoka kwa walimu wenye stress.
 
Safi sana.
Tulisuburi hili kwa muda mrefu.
Natamani elimu ya tehama ifundishwe kwenye hiyo miaka 10 ya elimu ya msingi.
 
Back
Top Bottom