Senzo ni bingwa wa Rege

Senzo ni bingwa wa Rege

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,916
Reaction score
15,974
Nipo nasikiliza playlist ya huyu mwamba,hakika huyu jamaa alikuwa anajua sana. Kwangu mimi nampa namba 2 baada ya Lucky Dube, shukrani Mwamba kwa kutuachia memory inayoishi

View attachment 1772305
Screenshot_20210503-172928_1620052215723.jpg
 
Oi natafuta ile ngoma yake kuna kibwagizo anaimba "oooh darasa darasa dara..." Kama unaijua plz nisababishie ntafurahi mno
 
Hahahaha kuna kitu alifyatua inaitwa IRENE acha kabisa, huyu Irene hana dogo! I have written so many letters begging you to come back to my house....you break my heart Iran oogh, you break my Soul, Irene ooggh dah
 
Naipenda
Great Counqerer Warrior
I'll be there
New love
Rast wake up n. k

Ila kumfikia Lucky Philip Dube bado sana
 
Yuko vizuri...

Ila hiyo 1. Dube
2. Senzo

Ni kwa africa si ndio!?
 
Hii ngoma ni kali sana, na album ya IRENE pia ni kali sana.
 
Yuko vizuri...

Ila hiyo 1. Dube
2. Senzo

Ni kwa africa si ndio!?
Najua utamsema Bob Marley, ni kweli ana ngoma kali nyingi na watu wengi wanaamini ndo mkali wa Rege kupata kutokea, ila kwangu mimi Senzo na Dube nyimbo zao huwa zinanitouch sana, nikisikiliza nyimbo za Dube na Senzo nakuwa na feelings fulani hivi ambayo siipati nikimsikiliza Bob
 
Senzo hajafa, he is alive sema alipata malaria Kali (sijui ikoje) ikamharibu sauti, wapo wanaodai amerogwa sauti ikapotea. Yupo Hai Mpwa
Mmh, kila mtu huwa anasema lake. Ila mimi kitu nilichokikamata mda mrefu ni kwamba alikufa
 
Naipenda
Great Counqerer Warrior
I'll be there
New love
Rast wake up n. k

Ila kumfikia Lucky Philip Dube bado sana
I'll be there ni mwisho wa matatizo ikifuatiwa na New Love, yaani nikiplay hiyo I'll be there naweza nisiibadilishe hata masaa mawili
 
Najua utamsema Bob Marley, ni kweli ana ngoma kali nyingi na watu wengi wanaamini ndo mkali wa Rege kupata kutokea, ila kwangu mimi Senzo na Dube nyimbo zao huwa zinanitouch sana, nikisikiliza nyimbo za Dube na Senzo nakuwa na feelings fulani hivi ambayo siipati nikimsikiliza Bob
Mkali ni Pita Toshi anafata Bob wengine wote kawaida
 
Mkali ni Pita Toshi anafata Bob wengine wote kawaida
Naomba unitajie nyimbo kali za Peter Tosh, maana nimejaribu kuzifatilia Boomplay ila nilizozisikiliza hazijanigusa
 
Back
Top Bottom