SENSA: Nini faida yake?

SENSA: Nini faida yake?

Vijisenti

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2011
Posts
544
Reaction score
330
Sensa ni zoezi ambalo halina faida kabisa kwa watanzania hususani sensa
hii itakayofanyika. Serikali isiyowajali wanchi wake itafanya nini baada ya
kuwahesabu zaidi ya kuwa ni zoezi au njia ya kutengeneza nafasi ya kufisadi
pesa zetu?

Nitakapokujibu sina kazi utaniajiri?
Nitakapokujibu sina mke utaniozesha?
Nikisema kuna mlemavu utanisaidia?
Watoto utawalea....................?

Ajabu! kwa serikali hii hii ambayo memba wengi tumekuwa
tukiilalamikia leo tunaiunga mkono katika zoezi la sensa kwa
faida ya nani?

Tuache unafiki hata kama tunawachukia waislamu ukweli unabaki
pale pale kuwa sensa haina faida kabisa kabisa kwa Watanzania.
Hakuna huduma yoyote itakayoboreshwa na serikali ya CCM eti kwa
sababu ya kuhesabiwa. Wangekuwa wameanza hapo kabla
tungeamini kuwa ni kweli wana nia nzuri.................

Labda hawa wanaounga mkono kuna manufaa wanayapata.

Serikali ya msumbiji inatoa huduma kwa wazee na kusaidia
mambo mbalimbali ya kijamii. Sensa yake inazingatia kuboresha
huduma hizo.

SENSA YETU IMELENGA KUSAIDIA JAMBO GANI?
 
Waathiika wa HIV wanapata dawa bure za kuongeza maisha
shule za kata ni bure hakuna ada....
elimu chuo kikuu wanafunzi wanakopeshwa

na mengineeyo meengi ambayo Sensa itasaidia sana
 
Mkuu uko sahihi, Ingawa sensa huanzia ngazi ya kaya. Mkuu wa kaya (awe baba au mama) lazima aelewe ana watoto wangapi, hata kama hana uwezo au anao. Kila mpango huenda na takwimu. sasa kama huoni faida za sensa, yawezekana hata huoni faida za kujua idadi ya watu katika kaya yako. (BE POSITIVE)
 
Waathiika wa HIV wanapata dawa bure za kuongeza maisha
shule za kata ni bure hakuna ada....
elimu chuo kikuu wanafunzi wanakopeshwa

na mengineeyo meengi ambayo Sensa itasaidia sana
Huwa sizipendi sana hoja za vijisenti kwa kuwa zimejaa udini lakini kwa leo na kwa muda wacha nimuunge mkono.

Sioni kama hii serikali ina nia ya dhati, pesa zetu za korosho tumenyanyasika
sanaaaaaaana, maduka yetu yamechomwa moto na polisi wakati tunadai haki zetu, malipo ya awamu ya tatu wanataka watulipe tsh 16 kwa kilo
Kuondoka kwa CCM ni muhimu kuliko sensa.

Hakuna siku shetani anamkuwa
mwema abadani.
 
aisee! sasa mtoa mada sijui unashaurije,tukatae kuhesabiwa au unalenga kuhamasisha nini hasa.
 
wajumbe wengi wa JF ni wakufuata upepo unapovumia hawatumii akili zao kufikiri wao wako kule wanakopelekwa ndiko huenda poleni sana leo munamsapoti kisha akija mtu na mada kama hiyo ya kusapoti sensa nae munamkubalia eee hii kali wapi misimamo yenu wakubwaa
 
aisee! sasa mtoa mada sijui unashaurije,tukatae kuhesabiwa au unalenga kuhamasisha nini hasa.
Ni we mwenyewe ndo utaamua kwani kuhesabiwa hakuna faida, hasara yake ni kupotezeana muda kama kuna shuguli zitasimama kwa sababu ya zoezi la sensa.

Kama muda upo na hakuna usumbufu
kwako unaweza kuhesabiwa lakini moyoni lichukulie zoezi hilo kama
mchezo wa BAO ambao mtu anakula nyjmba wakati katika hali halisi
hawezi kumeza hata kitasa.
 
Mkuu uko sahihi, Ingawa sensa huanzia ngazi ya kaya. Mkuu wa kaya (awe baba au mama) lazima aelewe ana watoto wangapi, hata kama hana uwezo au anao. Kila mpango huenda na takwimu. sasa kama huoni faida za sensa, yawezekana hata huoni faida za kujua idadi ya watu katika kaya yako. (BE POSITIVE)
Kuna faida gani ya kujua idadi ya watu kwenye nyumba yake
baba ambaye muda wote yu ashinda kilabuni huku kila kitu ndani ya
nyumba kikitokana na Juhudi binafsi za mama.

Hoja hapa si umaskini wa serikali, hoja ni nia ya dhati ya serikali
ya kuhakikisha kile kidogo kilichopo kinafika katika mikono ya
wananchi.
 
Hakuna faida ya sensa kwa watawaliwa labda
watawala!

Vijisenti, ajabu wewe unaendekeza unafiki!

Unaposema sensa haina faida, ulitegemea sensa ndio ikupe mke? Ulitegemea sensa ndio ikupe ajira?
Weka unafiki kando, sensa ina faida; kwetu wananchi, vyama vya siasa na watawala.

Takwimu zitakazopatikana zitawasaidia hata wananchi kuzitafsiri na hata kufanya maamuzi kuhusu hali za maisha yao. Mfano, ukijua mkoa fulani una watu wachache zaidi kwa km, ukitaka kulima patafaa.
 
Waathiika wa HIV wanapata dawa bure za kuongeza maisha
shule za kata ni bure hakuna ada....
elimu chuo kikuu wanafunzi wanakopeshwa

na mengineeyo meengi ambayo Sensa itasaidia sana
Ndio maana wanahimiza watu wakapime kwa hiyari ili wawe
na takwimu sahihi ya watu kama hao. Sensa haiulizi kama mtu
ameathirika au hajaathirika.
 
Vijisenti, ajabu wewe unaendekeza unafiki!
Unaposema sensa haina faida, ulitegemea sensa ndio ikupe mke? Ulitegemea sensa ndio ikupe ajira?
Weka unafiki kando, sensa ina faida; kwetu wananchi, vyama vya siasa na watawala.
Takwimu zitakazopatikana zitawasaidia hata wananchi kuzitafsiri na hata kufanya maamuzi kuhusu hali za maisha yao. Mfano, ukijua mkoa fulani una watu wachache zaidi kwa km, ukitaka kulima patafaa.
Halafu ukilima unapewa masharti ya jinsi ya kuuza mazao
yako..... Unadhulumiwa wakati hujasaidiwa pembejeo n.k
Waulize wakulima wakorosho..... huko watu wa sensa wakienda
huwa wanazomewa ktika baadhi ya maeneo.
SENSA NI MUHIMU LAKINI SI KWA SERIKALI YA CCM.
 
Mtoa mada umenifanya nitafakari upya, Serikali hii inashindwa kuboresha hata hospitali zetu, hili halihitaji sensa, Duuh.

Madaktari wanalalamika Hospitali hazina vifaa, Sidhani kama barabara mbovu nazo zinahitaji Sensa duh ipo kazi.
 
Halafu ukilima unapewa masharti ya jinsi ya kuuza mazao
yako..... Unadhulumiwa wakati hujasaidiwa pembejeo n.k
Waulize wakulima wakorosho..... huko watu wa sensa wakienda
huwa wanazomewa ktika baadhi ya maeneo.
SENSA NI MUHIMU LAKINI SI KWA SERIKALI YA CCM.
Sasa hapo kwenye kudhulumiwa sensa inahusika vipi? Huoni kuwa itakuwa imekusaidi kufanya maamuzi sahihi? Kukataa kuhesebiwa hasara yake inakurudia wewe mwenyewe.
 
Waathiika wa HIV wanapata dawa bure za kuongeza maisha
shule za kata ni bure hakuna ada....
elimu chuo kikuu wanafunzi wanakopeshwa

na mengineeyo meengi ambayo Sensa itasaidia sana

hapo kwenye blue,,,umesoma bure kwenye hizo shule au umehadithiwa,,,,,,,???????kama hujui kaa kimya,,,,,KARUME K£ng€ wewe usidanganye hapa
 
1. Nitakapokujibu sina kazi utaniajiri?
2. Nitakapokujibu sina mke utaniozesha?
3. Nikisema kuna mlemavu utanisaidia?
4. Watoto utawalea....................?

Tuache unafiki hata kama tunawachukia waislamu ukweli unabaki
pale pale kuwa sensa haina faida kabisa kabisa kwa Watanzania.

Kama waislamu wangekuja na hoja hizo nne kama zako, hata mie ningevaa kibandiko na makubazi kwenda kuwasikiliza. Lakini wao hoja yao ya msingi ni "sisi wengi" na "wao ni wachache"

Sasa kama wao ni wengi wanatakia nini kipengele cha dini?
1. Ili tuwaajiri.......?
2. Tuwatafutie wake.......?
3. Tuwasaidie waislamu tu walio walemavu........?
4. Tulee watoto wa waislamu tu.......?

Hatuwachukii waislamu isipokuwa tunasema sensa ya waislamu ifanyike misikitini wanakoswali.

KWELI SENSA HAINA MAANA VIJISENTI!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom