Sensa 2022: 17% ya kaya zimehesabiwa kwa siku moja

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,364
8,096
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema kuwa asilimia 17.13 ya kaya zote nchini zimehesabiwa ndani ya siku moja kwenye Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza jana Jumanne Agosti 23, 2022.

Makinda amesema hayo leo Jumatano Agosti 24 jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi.

Amesema lengo kwa siku ya kwanza lilikuwa kufikia asilimia 15 ya kaya lakini wamevuka hadi asilimia 17.13, akisema hayo ni mafanikio makubwa katika mchakato huo.

Amesema kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan alivyoeleza Agosti 23 sio watu wote wangeweza kuhesabiwa kwa siku moja ndio maana mchakato huo umepangwa kufanyika kwa siku saba.

Alisema anafahamu kuwa kila mwananchi angependa kuhesabiwa jana kwa sababu ilikuwa ni siku ya mapumziko lakini haikuwa rahisi.

Kutokana na hali hiyo, Makinda amewaomba wananchi wa kaya ambazo makarani hawajapita kuwa na subira katika kipindi cha siku sita zilizobaki.

Amebainishwa kuwa taarifa za wanakaya zinazohitajika ni zile waliolala eneo husika usiku wa kuamkia Agosti 23.

Mbali na hilo, Makinda amesema karani atapita katika kaya kuweka miadi na mkuu wa kaya na kuacha fomu maalum ambayo mkuu wa kaya atajaza taarifa muhimu za watu wote waliolala katika kaya yake usiku wa kuamkia siku ya Sensa yaani Agosti 22 kuamia Agosti 23.

"Fomu hii imeainisha taarifa hizo hivyo tunawasihi wakuu wa kaya kujaza fomu hizo ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa wakati karani wa Sensa atakapofika kufanya mahojiano. Natoa wito kwa waratibu wa Sensa wa Mikoa na wilaya kuhakikisha fomu hizo zinasambazwa katika kaya b ili kuharakisha mchakato huu," amesema Makinda.
 
Zoezi ni endelevu,hakika pesa ipo kwenye sensa,watu watatoka na mamilioni.Ningepata,daaah!
 
Amesema kama ambavyo Rais Samia Suluhu

Kutokana na hali hiyo, Makinda amewaomba wananchi wa kaya ambazo makarani hawajapita kuwa na subira katika kipindi cha siku sita zilizobaki.

A
Bado tunasubiri kuhesabiwa.
P
 
Bado tunasubiri kuhesabiwa.
P
😳😳
 
Ukweli ni kwamba hili zoezi naona limefeli kwa upande wangu.

Mosi; hiyo August 23 usiku mpaka jioni yake hatukuona mtu pamoja na kuacha milango wazi ili tusikie hodiiii...

Pili; tarehe 26 nilisafiri to mkoa mwingine na hii trh 28.8 alikuja karani wa sensa nikamweleza sijatoa taarifa zangu za sensa toka nilipokuwa na hata hapa nilipo, alichonijibu kinatosha kusema zoezi limeshindwa.

Kwa ufupi; watajaza maelezo fake fake kwa familia na watu wengi, ilimradi umpe jina tu.

Na wale wanasiasa wanaoingilia hili zoezi kwa kuwatisha wananchi wakidhani hii ni issue ya ccm wamefail sana.
 
Back
Top Bottom