Seminal fluid analysis(sperm analysis) elimu na ushauri juu ya vipimo vya mbegu za kiume

Mr kenice

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
2,856
4,475
HABARINI WAKUU,

Leo nimewiwa na kuona ni vyema kutoa elimu japokua kidogo kuhusu upimaji wa mbegu za kiume na elimu juu ya uwezo wa kizalisha Kwa mwanaume(Fertility).

MANII (SEMINAL FLUID) ni mchanganyiko wa mbegu za kiume(sperm) na majimaji mengine kutoka kwenye Korodani (testis) na tezi zingine amabo huonekana pale mtu anapo jamiiana na mwanamke na kupandisha hisia zaidi (Orgasm) kufikia kurusha mbegu hizo(EJACULATION) kwenda kwenye uke.

MANII hufanyiwa majaribio au VIPIMO Kwa lengo la kutambua wingi, ubora, na muonekano wa mbegu(Spermatozoa) Ili kujiridhisha juu ya uwezo wa kutunga ujauzito.

Vijana wengi wa sasa wamekua na uwezo mdogo au wakubahatisha kutungisha ujauzto, hii imechagizwa na miasha yaliyopo saiv sio kama zamani.

MAABARA zetu walau Kwa sasa zimekua na uwezo wa kupima tatizo hili kwani vifaa vipo na wataalam huongeza kila kukichaa.

NINI HASA WATAALAMU HUPIMA KWENYE MANIII ZETU.

images.png

Kwanza kabisa wataalamu hujiridhisha Kwa macho yao ya nyama kutizama vitu vifutavyo.

1/ Muonekano ( appearence)
Wa MANII Kwa kawaida huonekana ikiwa na rangi ya kijivu hivi,( grey na kua na wingu kiac) muonekano tofauti na huo huleta tafasiri tofauti.

Mfano rangi ya kijivu yenye njano mpauko humaanisha uwepo wa bacteria, au manjano.

Ikitokea Kuna wekundu basi Kuna uwepo wa ERYTHROCYTES, na ikiwa Haina rangi kabisa hapo humaanisha mbegu ni chache.

2/ Ujazo ( volume) wataalamu HUPIMA Ujazo wa Manii Kwa Kwa kutumia vipima Ujazo kama graduated test tube. Ujazo wa kawaida Kwa kila kumwanga( ejaculation) ni kuanzia MLS 2 - 5.
Ujazo pungufu na huo inabaki kua hesabu za kubahatisha kutungisha mimba.

3/ Uyeyukaji ( Fluidfication) au liquefaction
MANII inapotoka kwenye uume hua nzito na kushikana kama Mucus (ukamasi) flan hivi ila huanza kuyeyuka na baada ya sekunde30 mpka dakika kadhaa hua nyepesi mfano wa mafua ya asubuhi.

Hii Hali husaidia kusafiri kirahisi iwapo ndani ya uke.
Ikaonekana nzito sana na Haina dalili za kuyeyuka basi hapo kutakua na shida kidogo itakayo pelekea uwezo mdogo wa mbegu kuogelea na kufika eneo na urutubishaji.

4/ pH, huu ni uzani wa alikalis na acidi ya Manii.
Kwa kawaida Manii hua ni Alkalinity na hivyo huwezesha safari yenye matumaini iwapo kwenye uke uliojaa Acidi na kuweka uwiano sawa wa PH( Neutralization) Ili kuhakikisha mbegu haidhuriki.

5/ Unato (viscosity) wa Manii.
MANII hupimwa namna inavoweza kunata.

Na 👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿 ni vipimo vya awali vya manii.

BAADA YA HAPO WATAALAMU HUPIMA VIPIMO VIFUAVYO.

*. KUJONGEA ( MOTILITY)
Hapa Manii hupimwa kama inauwezo wa kutoka uneo moja na kuelekea eneo jingine yaani kuogelea.
Na hapa tunatazama Aina pia ya uogeleaji Kuna aina kadhaa za uogeleaji kama. Kuogelea Kwa haraka, kuogelea Kwa polepole, na kutokuogelea kabisa.

** UHAI WA MBEGU( SPERMATOZOA)
SPERM VITALITY TESTING.
Hapa wataalamu hupima %ya mbegu zenye uhai na %ya mbegu mfu, Ili kuoanisha nikwa %ngapi mbegu hufaa na hubaki hai kwenye mzunguko wako.

MUONEKANO WA MBEGU (SPERM MORPHOLOGY TEST).

images (1).jpeg

Muonekano wa mbegu ni muhimu sana Katika kuwezesha urahisi wa kutungisha mimba. Hapa tutaona Kwa makini kua mbegu inatakiwa iwe na umbo sahihi.

Kichwa kiwe kimechongoka vyema, uwepo wa mitochondria Ili kuhuisha nishati Kwa ajili ya kuogelea, na mkia mmoja wenye sifa ya kuogelea straight.

Kuna mbegu hua na muonekano usío ridhisha mfano kichwa kua na umbo la duara, mkia kua mfupi, vichwa viwili vilivoungana, mikia miwili iloungana hii huweza kuhatarisha Usalama wa kutungisha mimba.
Aidha ukosefu wa acrosome mbele ya kichwa Cha mbegu(sperm) kwani hii ni kemikali ambayo husaidia kama driller inayo lainisha ukuta uliofunika gameti kike Ili mbegu iweze ingia kirahisi.

**** WINGI WA MBEGU ( SPERM CONCENTRATION TEST)
Hapa hupimwa idadi kwa namba, Kwa kila MLS je Kuna uwezekano kukawa na mbegu kiasi gani

images.jpeg


JE!? KIPI NI CHANZO CHA VIJANA KUPUNGUKIWA UWEZO WA KUZALISHA NA KUA WALENGAJI( KUBAHATISHA)

Mitondo yetu ya maisha ya kila siku imegarimu kabisa uwezo binafsi wa Vijana wengi.

Hizi ndizo sababu chache zinazopelekea ongezeko la Vijana hao.

Unywaji wa pombe, na vinywaji vikali kupindukia. Beee 🍻 nyingi zna sabibisha ongezeko la Estrogen mwilini ambapo Kwa Mwanaume hupunguza uzalishaji wa mbegu. Hivyo tutumie kistaarabu na ikiwezekana kuacha acha.

Vyakula vya kiwandani kama nyama za kiwandani, carbonated soft drink, sukari kupita kiasi, na vyakula vya mtindo huo, hupunguza uzalishaji, na ubora wa mbegu.

Baadhi ya madawa yatolewayo hospital, tumia dawa kama ishauriwavyo na daktari.

images (3).jpeg

Mazoezi makali Sanaa, hasa yanayo husisha KEGEL.
Kuna watu hugeuza mazoezi ni mlo hii itakuathiri kwani huleta mionekano isiyostaili kwenye mbegu.
Fanya mazoezi wastani.

Kula vyakula vyebye mafuta mengi.
Uzito mkubwa, na magonjwa mbalimbali.

KWA KUBORESHA AFYA YAKO YA UZAZI BASI.
Jitahidi kula vyakula vyenye utajiri wa Zinc, na Protein, kama Nyama, Mayai, main, maharage.
Ulaji wa matunda na mbogamboga, pia vyakuka vyenye vitamin C.

Fanya mazoezi kupungaza ongezeko la mafuta mwalini.
Ukihisi tatizo fika Kwa wataalamu Kwa USHAURI na huduma zaidi

Kwa watu waluopo KAHAMA HUFUMA HII YA VIPIMO NA USHAURI INAPATIKANA KWEMA HOSPITAL NA COMMUNITY HEALTH CENTER.

MWANZA , FIKA AGHA KHAN , HINDU MANDAL NA RAINBOW HOSPITAL.

MBEYA - CHUNYA FIKA ADONAI HEALTH CENTER KWA DR NGARA.


🖐🏿🖐🏿👆🏿👆🏿
 
Aiseee

KWA KUBORESHA AFYA YAKO YA UZAZI BASI.

Jitahidi kula vyakula vyenye utajiri wa Zinc, na Protein, kama Nyama, Mayai, main, maharage.

Ulaji wa matunda na mbogamboga, pia vyakuka vyenye vitamin C.
 
Aiseee

KWA KUBORESHA AFYA YAKO YA UZAZI BASI.

Jitahidi kula vyakula vyenye utajiri wa Zinc, na Protein, kama Nyama, Mayai, main, maharage.

Ulaji wa matunda na mbogamboga, pia vyakuka vyenye vitamin C.
Hii mbona kama sijaielewa hivi. Kiafya imekaaje?
 
Back
Top Bottom