Epuka matumizi ya madawa ya kuongeza uume na nguvu za kiume

Bukoba Finest

JF-Expert Member
Jul 13, 2023
250
314
Boost homoni yako ya Testosterone kwa kutumia natural foods. Chukua Popcorn tushuke nayo taratibu:

•NDIZI MBIVU:
Ndizi ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja kiitwacho (Bromelain) ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa (Testosterone).

Pia ndizi zina Magnesium, vitamini B1 na vitamini C, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

•MBEGU ZA MABOGA:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya zinki ambayo ni muhimu katika kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya Testosteroni.

Pia mbegu za maboga zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni muhimu katika kuongeza idadi ya mbegu za kiume. Vile vile mbegu za maboga zina madini ya kalsiamu, Potasiamu, Phosphorasi na Niacin.

•CHOCOLATE NYEUSI.
Hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu.

•PARACHICHI:
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume, (Testosterone)

Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.

•TIKITI MAJI NA MBEGU ZAKE:
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume.

Tikiti linapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku usikose.

•VITUNGUU SWAUMU:
Kitunguu swaumu kina ‘Selenium’ na pia kinasaidia kuondoa sumu mwilini, mambo haya mawili muhimu yanasaidia kuongeza spidi ya mbegu za kiume.

Pia kitunguu swaumu kina "Allicin" ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenye uume.

NB: Unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

•PILIPILI KICHAA:
Hii husaidia mzunguko wa damu kuwa vizuri,hivyo kusaidia pia tatizo la uume unaolegea.

•TANGAWIZI:

Husisimua sana mzunguko wa damu, Sikuzote mzunguko mzuri wa damu huleta matokeo mazuri wakati wa tendo ndio maana imekuwa ikitumika sana katika maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.

•ASALI MBICHI:
Asali husaidia utengenezwaji wa homoni ya testosterone ambayo kazi yake ni kuimarisha mifupa, misuli na utengenezaji wa mbegu za kiume.
Pia hutumika kutengeneza Nitric Oxide (NO) ambayo hutumika kusaidia uume kusimama kwa kuongeza msukumo wa damu sehemu hiyo.

•SAMAKI AINA YA PWEZA NA KAMBA:

Zina madini aina ya zinc kwa wingii zaidi ambayo huzalisha vichocheo muhimu katika afya ya uzazi kwa wanaume Testosterone.

•TENDE:
Niielezee "TENDE" kwa undani zaidi, Katika kila gram (100) ndani ya tende kuna virutubisho kwa asilimia kama ifuatavyo.

•Nishati (energy) 317kcal.
•Wanga (cabohydrate) 78.8%.
•Chuma (iron). 5.50ppm.
•Hamirojo (protin)2.5%.
•Mafuta (fat).0.4%.
•Unyevu nyevu (moisture)15.3%.
•Madini zinc 2.1%.
•Grucose (Sukari) 35%.
•Kamba kamba (fiber)4%
•Fructose 27%

● FAIDA MUHIMU ZA TENDE.

•Huongeza damu ukichanganya na maziwa.
•Husaidia kuzalisha manii kwa wingi.
•Huongeza nguvu za kiume.
•Huzidisha hamu ya tendo la ndoa.

NB: hakikisha unakunywa maji mengi, hakikisha unakuwa na ratiba yakufanya mazoezi ya mwili hasa mazoezi ya "KEGEL" yana matokeo ya mara moja kuimarisha misuli ya nyonga, na kwa wanawake husaidia kubana uke.
 
Jambo moja ambalo nimegundua ni hili;

Wanaume wengi siyo kwamba hawana nguvu za kiume lah!, Wengi wanazo na kuna shida kubwa kwenye kutambua kama mtu anazo au hana na huwa ziko wapi?.

Maisha yamebadirika sana, yaani mfumo wa maisha umefanya mazingira yetu kuwa magumu hasa kwenye issue ya mahusiano.

Watu wanaoa na kuolewa, mwanzoni wanaume wanaonekana kuhimili tendo but kadiri siku zinavyosogea hali inakuwa ndivyo sivyo, ugumu wa kuahindwa kuendelea na kuishia kati.

Hii nimegundua ni kutokana na mfumo wa maisha na kuna ugonjwa unaohitaji uponyaji hasa kwenye vichwa vya wanaume ambao wakiingia kwenye hilo tendo mawazo yao hayasimami kqma awali anaingia akiwa mgonjwa tayari.
 
Jambo moja ambalo nimegundua ni hili;

Wanaume wengi siyo kwamba hawana nguvu za kiume lah!, Wengi wanazo na kuna shida kubwa kwenye kutambua kama mtu anazo au hana na huwa ziko wapi?.

Maisha yamebadirika sana, yaani mfumo wa maisha umefanya mazingira yetu kuwa magumu hasa kwenye issue ya mahusiano...
Nguvu za kiume kila mwanaume anazo, ni jinsi ya kuhufadhi hormones zako, lakini pia kwa kufanya mapenzi mara kwa mara husaidia misuli kukaza
 
kwa kufanya mapenzi mara kwa mara husaidia misuli kukaza
Kukaza au kusinyaa?.

Hapo unataka kunipa maswali mkuu, kuna wale wanaosema kufanya mara kwa mara kunadhoofisha misuli na kukufunya uwe dhaifu leo na wewe unaleta hili how?
 
Naam, inategemea na hormones za mtu lakini pia kufanya bila kutumia vyakula vya kuhimarisha hizo hormones udhohofisha na kinyume chake.
 
Boost homoni yako ya Testosterone kwa kutumia natural foods. Chukua Popcorn tushuke nayo taratibu:

•NDIZI MBIVU:
Ndizi ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja kiitwacho (Bromelain) ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa (Testosterone).

Pia ndizi zina Magnesium, vitamini B1 na vitamini C, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

•MBEGU ZA MABOGA:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya zinki ambayo ni muhimu katika kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya Testosteroni.

Pia mbegu za maboga zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni muhimu katika kuongeza idadi ya mbegu za kiume. Vile vile mbegu za maboga zina madini ya kalsiamu, Potasiamu, Phosphorasi na Niacin.

•CHOCOLATE NYEUSI.
Hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu.

•PARACHICHI:
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume, (Testosterone)

Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.

•TIKITI MAJI NA MBEGU ZAKE:
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume.

Tikiti linapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku usikose.

•VITUNGUU SWAUMU:
Kitunguu swaumu kina ‘Selenium’ na pia kinasaidia kuondoa sumu mwilini, mambo haya mawili muhimu yanasaidia kuongeza spidi ya mbegu za kiume.

Pia kitunguu swaumu kina "Allicin" ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenye uume.

NB: Unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

•PILIPILI KICHAA:
Hii husaidia mzunguko wa damu kuwa vizuri,hivyo kusaidia pia tatizo la uume unaolegea.

•TANGAWIZI:
Husisimua sana mzunguko wa damu, Sikuzote mzunguko mzuri wa damu huleta matokeo mazuri wakati wa tendo ndio maana imekuwa ikitumika sana katika maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.

•ASALI MBICHI:
Asali husaidia utengenezwaji wa homoni ya testosterone ambayo kazi yake ni kuimarisha mifupa, misuli na utengenezaji wa mbegu za kiume.
Pia hutumika kutengeneza Nitric Oxide (NO) ambayo hutumika kusaidia uume kusimama kwa kuongeza msukumo wa damu sehemu hiyo.

•SAMAKI AINA YA PWEZA NA KAMBA:

Zina madini aina ya zinc kwa wingii zaidi ambayo huzalisha vichocheo muhimu katika afya ya uzazi kwa wanaume Testosterone.

•TENDE:
Niielezee "TENDE" kwa undani zaidi, Katika kila gram (100) ndani ya tende kuna virutubisho kwa asilimia kama ifuatavyo.

•Nishati (energy) 317kcal.
•Wanga (cabohydrate) 78.8%.
•Chuma (iron). 5.50ppm.
•Hamirojo (protin)2.5%.
•Mafuta (fat).0.4%.
•Unyevu nyevu (moisture)15.3%.
•Madini zinc 2.1%.
•Grucose (Sukari) 35%.
•Kamba kamba (fiber)4%
•Fructose 27%

● FAIDA MUHIMU ZA TENDE.

•Huongeza damu ukichanganya na maziwa.
•Husaidia kuzalisha manii kwa wingi.
•Huongeza nguvu za kiume.
•Huzidisha hamu ya tendo la ndoa.

NB: hakikisha unakunywa maji mengi, hakikisha unakuwa na ratiba yakufanya mazoezi ya mwili hasa mazoezi ya "KEGEL" yana matokeo ya mara moja kuimarisha misuli ya nyonga, na kwa wanawake husaidia kubana uke.
Sawa Mkuu tumekupata.
 
Hiyo popcon inakiambata cha homoni za kike gestrojen( kama nimekosea kuiadika mnisahihishe) hivyo kushusha homoni ya kiume Na hatimae nguvu kupungua, bia aina zote lia hazifahi kwa afya ya uzazi wa mwanaume nimechunguza bia bia zote nimegundua zina kiungo kinaitwa Hops ambacho kina kiambata cha homoni za kike, kiambata hivi vimeandikwa ubavuni kwa Chupa someni, ushauri wanywaji bia punguzeni au acheni kabisa, pombe bora imethibitika ni Red wine, haina kiambata hicho, pia ina kings zidhi ya Kansa, Moyo, kupooza, kuongeza mzunguko wa Damu kwenye viungo cha uzazi hivyo ni nzuri kwa jinsia zote, zingatia kunywa kiasi, kea wasiotumia kilevi wale zabinu nyekundu au watengeneze fresh juisi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom