Selim bin Abakari, mtu mweusi wa kwanza kufika Siberia Watu wa kule wakadhani ni Mungu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,233
12,742
Kuna huyu Mngazija mmoja mwenye akili sana aliyeitwa Selim bin Abakari. Wakati Wajerumani ndiyo wanaanza kutawala Tanganyika huyu Selim Alikuwa akifahamu kijerumani, hivyo akaajiriwa na afisa mmoja wa serikali ya Ujerumani kama mfanyakazi wake. walisafiri naye sana.

Safari ya kwanza ilikuwa ni kupeleka meli ya mvuke ziwa Nyasa. Walisafiri kupitia mto Zambezi, mto Shire na kuingia Malawi. Huko walifunga boti yao na ikaanza safari ziwa Nyasa. Walifika Kyela, wakaenda Ukinga, Unyakyusani, Kwa Chifu Merere wa Usangu, wakaenda hadi Rukwa na Zambia kwa wawemba. Selim ameandika yote hayo. Ameelezea vizuri mambo mbalimbali waliyokutana nayo.

safari ya pili wameenda na bosi wake Berlin ujerumani kutokea Dar. Wako na meli, wakaenda Unguja, Tanga, Mombasa, Lamu, Somalia, Misri hadi Napoli Italia. hapo walipanda Treni hadi Berlin. Kaeleza vizuri na hali ya kila mji waliopita.

Kutoka Berlin wakasafiri kwenda Urusi. Walienda St Petersburg kwa treni. Wakaenda hadi Moscow. Baadaye wakapanda boti na kusafiri mto Volga, huko wakachukua magari ya farasi kuelekea Siberia. Safari yao ilikuwa kufika milima ya Altai iliyo mpakani mwa China, Urusi, Mongolia na Kazakhstan. Kaeleza vizuri sana safari yake. Anasema huko Siberia watu hawajawahi kuona mtu mweusi. Walivyomuona walimnyenyekea sana, walijua yeye ndiye bosi wa msafara, maana watu weupe wamezoea kuwaoana.

Pia kuna watu huko wanaabudu Mungu wao ambaye ni Mweusi, Walipomuona Selim wakaanza kama kumsujudia, kwamba Mungu wao amerudi. Sidhani kama kuna mswahili amewahi safiri kama huyu bwana.

silimu-en-russie1.jpg

silimu-21.jpg

fb-couvsilimu.jpg

Simulizi zake zinapatikana kwenye kitabu Safari za Wasuaheli(Waswahili) cha mwaka 1901.
 
Ilikuwaje utu wa mtu mweusi ukadhalilika na kudharaulika?
Hakuna kitu kama icho weusi ndo watu pekee waliacha Tamaduni zao na kukimbilia za wageni.

Ukitaka kujua ilo watu wanaoshikilia tamaduni zao mpaka leo wanakuwa na thamani ushawai kusikia Mmasai akiteswa na wazungu au waarabu?

Wamasai Wana thamani Africa hakuna maana Wana kitu kipya mbele ya macho ya wageni ila sisi kajamba8 manguo yanatoka huko ,elimu huko sasa una kitu gani kigeni mbele ya wageni.
 
Wamasai hawahawa wanaosuka dada zetu huko saluni na kulinda mageti(walinzi)?au Kuna wengine unaowaongelea?
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkoloni mzungubna mwarabu. Ingekuwa yuko na waarabu angekuwa na mshipi wa kuficha ub..o.o na angehasiwa.
 
😄😄 Zanzibar Ina wamasai wa kutosha arifu,tembea uje uone mambo yanayoendelea huku mkuu.

Watu hawajui tu Zenji Hadi wasukuma wapo wengi kichizi,wanapiga kazi ngumu ngumu.
Juzi kati nakatiza mitaa ya Chukwani hapa Unguja nakutana na Mmasai anauza fegi na ugolo...
 
Hakuna kitu kama icho weusi ndo watu pekee waliacha Tamaduni zao na kukimbilia za wageni.

Ukitaka kujua ilo watu wanaoshikilia tamaduni zao mpaka leo wanakuwa na thamani ushawai kusikia Mmasai akiteswa na wazungu au waarabu?

Wamasai Wana thamani Africa hakuna maana Wana kitu kipya mbele ya macho ya wageni ila sisi kajamba8 manguo yanatoka huko ,elimu huko sasa una kitu gani kigeni mbele ya wageni.
Masai ameanza kutengeneza vitu vyake lini?
Matairi anayovaa...migolole hadi shanga wananunua
 
Naona tumezingua wenyewe, maana Heshima siyo kitu cha bure, unaifanyia kazi kuipata. Mi hata ubaguzi wa rangi, yaani wa kumdharau mtu sababu ya rangi siamini kama upo. Ni vile tu watu wanahusianisha ishu zetu mbovumbovu na rangi yetu.
Yeah! Nisisi wenyewe tumejiweka ivo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom