Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Kesho ukipita mitaa hii unijulishe mapema!
Bado nipo
20220216_172000.jpg
 
ndio mkuu, nimekazia 😀, so nazidi ku elewa na ku confirm, na kuheshimu kila raha ya mkulungwa😀 ,at the end of the day kila mtu a enjoy anachopenda bila shida.
Halafu unajua nini? Ukiwa bado mdogo sisi wanaume tunakuwa na hizi fantasies za ajabu ajabu. Mke wangu sijui lazima awe hivi, sijui vile. Utoto mwingi!

Tunasahau kwamba kwa kadri muda unavyokwenda mwili wa mwanamke hubadilika sana. Matokeo ya uzazi, mfumo wa maisha na umri. Hiyo pisi kali kimodo yenye kiuno kama nyigu na vititi mchongoko kifuani kama mkuki wa morani huenda huko mbele ya safari ikabadilika sana mpaka ukashangaa. Hapo ndipo kimbembe kinapoanza hasa kama sifa kuu ya mapenzi yenu yalikuwa ni ulimbwende wa mwili. Ooh mke wangu kabadilika. Ooh hana mvuto siku hizi na blah blah kibao.

Hao akina mama kwenye hiyo picha likely wako mid 40s au late 30s. Kwa kuwaangalia tu wakati wao ni wazi pengine walikuwa visu hatari hata kukidhi vigezo vyako...

Kwa sisi wazee tumeona mengi na haya yote nayaongea kutokana na experience. Msichague wake wa kuoa kwa kuangalia maumbo yao wakati wakiwa under 30. Tia akilini kuwa baada ya watoto watatu na miaka 20 huko mbele ya safari huyu mke wangu atakuwa na umbo gani? Wewe utakuwa na umbo gani? Kama ulimuoa kwa ajili eti kimbaumbau au bonge, vipi akibadilika na kuwa tofauti kabisa na ulivyompenda utafanyeje? Ndoa inakufa? Mapenzi yanakufa? Unatafuta mchepuko au unaoa mwingine?

Ukiweza kuyajua majibu ya maswali haya basi hutasumbuka na vigezo hivi bandia kama uzuri wa mwili - kwa sababu mapenzi yenu yatasimikwa katika vigezo vingine vya kudumu na muhimu zaidi kuliko tu uzuri wa mwili (japo nao ni muhimu pia)...

#Busarazawazee
 
Darasa safi kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom