Selfika na JF: Snap it. Show it


Athari za mfumuko wa bei, nakumbuka mara ya kwanza kwenda ughaibuni nilipotoka na mwenyeji wangu kununua mahitaji ya nyumbani (groceries), aliniachia nichukue vitu ntapenda kutumia na yeye ndo alilipa. Aiseeh nilipata tabu.... kila bidhaa kabla sijaiweka kwenye toroli nilikuwa napiga mahesabu ingekuwa bongo ningelipa shilingi ngapi, nikiona bei inazidi ya Tanzania nakiacha.
Akahisi namuonea aibu akaniambia ananiacha ntamkupa paying point... nilichukua muda akashangaa nimekwama wapi kumbe mwenzie kila bidhaa nashika calculator naweka exchange rate huyo narudisha bidhaa kwenye shelf.

Akanirudia kimya kimya akaona nnachofanya. Ilibidi anunue turudi nyumbani kisha akanikalisha kunipa darasa....😅😅😅.

Nikaacha hiyo tabia..... guess what....😆😆😁

Nilivyoona hiyo bei ya hizo flower vase nimechukua calculator chaap 😆😆😆😆

Sijui nina infobia ya bei....😁😁😄

Cheers for the pizza 🍕.

Najiuliza msukuma alivyokuwa anakula pizza, aliifinyanga kama ugali au alikiwa anainyofoa kama anavyonyofoa minofu ya sato 🤣🤣🤣🤣🤣🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Umenichekesha sana. Ukifanya hivyo huwezi kununua kitu aisee. Mara ya kwanza nimeenda London kwenye interview nikatakiwa kutafuta suti eti more presentable. Suti yenyewe eti inauzwa £170. Mi nikipiga mahesabu nakuta ni karibia laki 5. Nikawa najisemea kweli ninunue suti kwa laki 5? Nikakomaa tu na suti niliyokuwa nimekwenda nayo...na kazi sikupata


Pizza hii ni ya binti alikuwa ameagiza na marafiki zake. Na anajua mi wala siyo mpenzi wa mavyakula yao haya ya kiutopolo. Nikila kakipande kamoja tu basi kanatosha...halafu nakasukumizia na bonge la ugali kwisha habari





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…